Posts

Showing posts from June, 2024

Simulizi : Muafaka Sehemu Ya Tatu (3)

Image
“Ni kwa sababu nina kupenda Lulu… I love you…I really do …dear!” Lulu aligeuka na kutaka kuondoka, bali Onespot alimshika mkono na kumgeuza amuangalie yeye. “Unataka nini?!” Lulu alisema kwa ukali. “Sema wewe unataka nini, nifanye, hata kama ni kukupigia magoti mbele ya watu mimi niko tayari.” Lulu alikuwa karibu chozi limtoke, alisema kwa taratibu kwa sauti ya kubembeleza. “Tafadhali Onespot niache usinibughudhi…ndilo ninalolitaka, please, leave me alone… Hebu niache niwe huru.” Onespot nae alijifanya mnyonge ajabu na kumuulizia Lulu pasipo kumuangalia usoni, kwa sauti ya masikitiko. “Ina maana… Lulu… Wewe ni mtumwa kwangu?!” “La hasha… Mimi si mtumwa kwako, bali vitendo vyako kwangu, vinanifanya nikose uhuru ninaostahiki.” “Ni vitendo gani hivyo Lulu? Unaweza kuniambia?!” Lulu alisimama hapa aliposimama huku akihema hema kwa chuki, kichwani mwake alifikiri aondoke au amuambie, mwisho aliona dawa ni kumwambia, alimtamka kwa haraka haraka, “Vitendo vyako, kama ulinyofanya muda mchache ...