TAMU YA MASISTA
*SEHEMU YA 16---20(MWISHO)* "Cosmas?!" Mwanamama sist Berina alipigwa na butwaa na wawili hao, sista Matilda pamoja na mwenzake sista Tekla waliacha kupigana wakiwa tayari wameshaniponza na kunifanya nijulikane kwa mama yao huyo mlezi. "Naam" nilijibu huku nikijikuna kichwa. "Kulikoni kwenye mavazi hayo tena na umefuata nini huku?" "Aaamh nimekuja tu kutembea" nilimjibu akawageukia Tekla na Matilda. "Ninyi ndiyo mmemshawishi aje huku?" "Ni Matilda siyo mimi" "We koma, ni huyu Tekla wala siyo mimi mama" kila mmoja alikanusha akimnyooshea kidole mwenzake. "Kwahiyo mnanifanya mimi ni mdogo wenu?" "Hapana mama" walijibu na mwanamama huyo akanigeukia mimi. "Nimekuja mimi mwenyewe tu kwa mapenzi yangu wala hakuna kati yao aliyeniita" niliwatetea, "Oooh sawa haya nendeni huko kwa wenzenu nakuja, nina mazungumzo na huyu kidogo" aliwafukuza wakaanza kuondoka taratibu huku wakinong'...