Riwaya:penzi la mfungwa 05

Zabroni alirudi nyumbani baada kutoka kumsindikiza mzee Maboso,akiwa njiani aliwaza kipi afanye nini sasa baada kumtambua mbaya wake. Je, aendelea kuchoma nyumba ama adili na mbaya wake? Akili ya fasta ikamjia kwamba bora aendelea kuchoma nyumba ikiamini kuwa maumivu aliyonayo moyoni mwake huwenda yakatulia kama sio kupotea kabisa. Yote hayo kijana Zabroni alikuwa akiyawaza huku akirejea nyumbani mikono nyuma kichwa chini,alipo fika nyumbani alikuta karatasi ndogo kwenye meza iliyokuwepo sebuleni. Zabroni alionekana kustuka huku moyo wake ukihitaji kufahamu kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo,hatimaye aliichukuwa akakuta maneno yaliyoandikwa "Kijana Zabroni, mjukuu wangu mwanangu pia. Nimekupa dawa hii ili uweze kulipa kisasi juu ya kile ulicho fanyiwa,hakuna ubishi mzee Fungafunga ndio muhusika mkuu wa vifo vya wazazi wako. Alifanya kitendo kile baada kuona baba yako anamzungusha kumlipa deni lake alilokuwa akimdai. Zabroni Zabroni lipa kisasi kijana unyama huo kamwe huwe...