Kazi ya mochuari-02
KAZI YA MOCHUARI
EPISODE 2
0699286085
Nilipokuwa nyumbani niliwaza kweli sisi wakufanya kazi mochuari na kama stori zenyewe ni hizo za mzee komba kweli tutakaa muda mrefu pale "
Nilijiuliza ila mwisho wa siku nikasema " mwanaume hachaguwi kazi lakini naogopa mimi tusije tukateseka au kupoteza maisha basi tulilala vizuri nakumbuka hiyo ndo siku ambayo ilikuwa ni mara ya mwisho kulala usingizi wa kuenjoy lakini tulipoanza kazi yaliyoyukuta shahidi ni mungu tu πππππππππππndiyo duniani kuna kazi ila kuchagua kazi ya mochuari haikua kazi nzuri kwetu ukichukulia watu tumesoma na tumefaulu vizuri tu lakini haya ndo tuliyoyavuna kufanya kazi mochuari nilijikuta nikilia kama mtoto mdogo "
Kesho yake jioni, tulifika kazini tukiwa na ari na furaha ya kufanya kazi kwa nguvu zote. Moyo wetu ulikuwa na matumaini makubwa ya kuanza maisha mapya katika mkoa wa Njombe. Tulijua kuwa kazi yetu katika mochuari ingekuwa ni changamoto, lakini hatukuwa tayari kwa kile ambacho kingetokea usiku wa kwanza.
mida ya saa moja hadi saa sita kazi ilikuwa supa sana hadi tukawa tunajadili walisema ma oooooooh kuna tisha oooooh majini oooooob maiti kiko wapi tena tukaanza kusema walisema hatuajiliwi hapa ni wapi π π§️π π π π π π π huku tunagongesha tochi zetu na kucheka sana ujuwe mi na rashidi ni marafiki wakubwa sana ko utani kwetu ni furaha kwanza maisha mafupi haya
LAKINI Ilipofika saa 7 usiku, hali ilianza kubadilika upepo ulivuma kana kwamba kuna mvua . Tulikuwa tumeketi katika ofisi ndogo ya mochuari, tukitafakari mambo yote tuliyokutana nayo wakati wa mahojiano yetu. Kelvin, akiwa na wasiwasi, alichungulia dirishani, akitazama giza lililojaa giza la kutisha. "Rashid, unadhani kuna mtu atakuja hapa usiku huu?" aliuliza, sauti yake ikiwa na mtetemo.
Nilimkatisha, nikimwambia, "Tujiandae kwa lolote. Hii ni kazi yetu, na hatuna budi kuikubali." Hata hivyo, sikujua jinsi hali ingekuwa mbaya. Giza lilipofika, tulianza kusikia sauti za vicheko, lakini si vicheko vya kawaida. Vicheko hivyo vilikuwa vya maiti, π π π π π π π π π π π π π€£π€£π€£π€£π€£π€£ππ€£ππππππ€π€ππππ€π€ππππ€£π€£π€£π€£ Kila sauti ilikuwa inakuja kwa mawimbi, kama vile maiti zikiwa zinaangalia matendo yetu.
nikajaribu kumuuliza kelvina " unasikia hiyo"
akanijibu "naisikia kwa ubora wa HD "
Yaanππππππππi kelvin acha masihara nilimwambia kelvin akajibu nasikia kaka nilijua nawewe hujasikia
Tulijaribu kujizuia na kuangalia kila kona ya mochuari, lakini vicheko vilionekana kuja kutoka sehemu tofauti. Kelvin alijikuta akitetemeka, akijaribu kujificha nyuma yangu, maana sasa sauti zilikuwa nyingi na nzito za kutisha sana .
macho yake yakiwa na woga wa wazi. "Rashid, siyo vicheko vya kawaida hivi," alizungumza kwa sauti ya chini, akionekana kama mtu aliyejawa na hofu.
Mimi pia nilihisi mwili wangu ukitetemeka; aise, huwezi kuamini, nilijikojolea. Jasho lilianza kumwagika kama mvua, na kila sauti ilionekana kuwa na uzito wa kutisha. Nilihisi kama dunia yangu ilikuwa inakumbwa na giza la kutisha, na kutokuwa na uwezo wa kujua ni nini kinaendelea.
"Ni vicheko vya maiti," nilimwambia Kelvin, nikijaribu kujitunza. Tulijua kuwa hatukuwa peke yetu; sauti hizo zilionekana kuwa zinatoka kwa maiti za ndani ya mochuari Kila sauti ilionekana kuwa inatuambia kwamba, ndani ya giza hili, hatukuwa salama.
Tuliposogea karibu zaidi na mlango wa mochuari tukasikia watu wakisema " kwani hao walinzi wapya hawajalala tu tuanze mizunguko " mara tukasikia mtoto analia mama yake akasema wewe mpe nyama mwenzio "
hali ya wasiwasi ilitukumba na nilijihisi kama vile napoteza maisha. kwa upande wa kelvin yeye naye alizidi kunisisitiza tukimbie lakini hata tungekimbia isingesaidia kitu
Tulipofika karibu na eneo liliposikika vicheko, tuliona mwanga wa taa hii ni baada ya kuofungua ile mochwari kulikuwa kimya kana kwamba kulikuwa hakuna sauti ya vicheko tena .kelvin akasema si tumesikia watu wakicheka humu ndani au yalikuwa marue marue.mara tukiwa tunabishana maiti moja ikapita pale ikiwa imevaa sanda inayovuja damu mmmmmmmh weeee tulifunga mlango.
mapigo ya moyo puuuuh puuuh puuuuuh puuuuh puuuuuh yaaani nguvu ziliniisha baada ya hapo kulikuwa kimya sana muda huo tumeshachanganyikiwa basi hatimaye asubuhi ilifika tulishukuru mungu na tulirudi nyumbani na kupumzika
hakika ule usiku ulikuwa ni wa moto sana maishani mwetu lakini tulisema tutapigana mpaka mkataba uishe ila yakitushinda tutaacha kazi kwani shi ngapi ???
USIKOSE SEHEMU YA TATU
KUPATA FULL NI 1500
0699286085
Comments
Post a Comment