Posts

Showing posts from March, 2025

INATOSHA - 5

Image
  Ilipoishia jana.. Nilishangaa kwa mara nyingine tena Gervas akimfuata Jammy nakumkumbatia kisha bada ya pale Gervas alinifuata na mi nakunikumbatia, "Levina...? Nakupenda na Jammy nawapenda sana" "hata sisi Gervas tunakupenda...!" Songa nayo sasa… Maisha yaliendelea kupendeza zaidi kwani kwa sasa tulikuwa tukiishi kama wanandugu tena wale wa damu na siyo wachumba tena,niliishi mi Gervas na Jammy huku mfanyakazi wa ndani alitusaidia kwa kupika chakula,hata inapofka muda wa kulala huwa kila mmoja anachumba chake, Nakumbuka siku moja ambayo ilikuwa ni sikukuu tulitengeneza chakula kizuri nakuwaalika marafiki,hivyo tulisherekea vizuri kwa kunywa nakucheza muziki na hata ilipofika muda wakulala kila mmoja alilala kwake,kwa upande wangu nilikuwa nimelewa sana kiasi chakuamua niwahi kulala,lakini mkojo ndio tatizo kubwa nilikuwa nalo hivyo kila baada ya muda nilikuwa ni mtu wa kwenda chooni kukojoa na kwa kipindi hiki nikasahau njia ya kuingia chumbani kwangu nakujikuta ...

Simulizi : Inatosha Sehemu Ya Nne (4)

Image
Ilipoishia juzi.. "Gervas..., Gervas..., Jammy nimekukosea nini jamani...? Gervas kakukosea nini...?" "embu nyamaza huko...?" Aliongea jammy kwa ukali huku akiondoka kwa mwendo wa makogo nakuniacha nikipiga makelele kwa kulia huku kwikwi ikinibana. Songa nayo sasa… Niliendelea kulia huku nikitoka nje kwa kutoamini kwamba kweli Gervas ametoka mikononi mwangu kweliau la...! Umati mkubwa wa watu waliokuwa wanachota maji hapa nje kwangu na wengine majirani walijaa kushuhudia ni kitu gani kimetokea hapa,niliendelea kulia tena kwa sauti ya juu huku wakimpakiza Gervas kwenye gari lao nakuondoka naye, niliendelea kuumia zaidi pale Gervas aliponyanyua mikono yake nakuniaga kwa kupitia dirisha la lile gari huku Jammy akiwa pembeni yake akioneshwa kufurahishwa na alichokitenda. "...mi ndio Levina a.k.a mamaa Sammy, nitahakikisha Gervas anarudi kwenye himaya yangu..." Nilijisemea kimoyo moyo huku nikirudishia geti nakurudi ndani, "mama...! Mama...." Ilikuwa ...