Posts

Showing posts from May, 2025

Simulizi : Je Haya Ni Mapenzi!! Sehemu Ya Kwanza (1)

Image
Mimba yake ndio iliyosumbua wengi sababu alijikuta akimchukia kila mtu aliyemuona mbele yake, hata mume wake alimchukia kasoro binti mmoja mdogo ambaye ni mtoto wa mwenye nyumba anayoishi Sakina. Alimpenda sana huyu binti aliyekuwa na umri wa miaka kumi kwa kipindi hicho na alijulikana kwa jina la Sabrina. Kila kitu ambacho Sakina alikitaka alipenda achaguliwe na Sabrina. Kitendo cha Sakina kuwa karibu sana na Sabrina kilikuwa kinamkera sana mzazi wa Sabrina aliyeitwa Joyce, hakupenda kabisa mwanae awe karibu vile na Sakina kwani alijua wazi kuwa Sakina atamfanya mwanae kama mtumwa wake ila hakutaka kusema sana kwavile alimuhurumia Sakina kwa ule ujauzito aliokuwa nao kwani mimba zingine huwa zinafanya mtu awe vile kama alivyo Sakina. Mume wa Sakina nae alikerwa sana na tabia ya mkewe kwani kila alichokifanya yeye mkewe hakukitaka, hata kama akimletea kitu alikuwa anakikataa hadi amuite Sabrina na kumuomba amkabidhi hiko kitu kwa niaba yake, kwakweli hii hali ilimkera na kumfanya aombe...