⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
uchovu,,akaangaza macho yake huku na kule kutafuta mti wenye kivuli,angalau ajipumzishe,,,
akafanikiwa kuona mti mkubwa akaamua kuufuata mti huo,,akajipumzisha....Laula akajikuta anazama kwenye dimbwi la mawazo mazito akanyanyua uso wake kutazama kando,,,akashtuka kuona eneo hilo kama alishawahi kuliona,,na sio mara ya kwanza,,alipojaribu kuvuta kumbukumbu,,,akastaajabu sehemu hiyo ni eneo la makaburi aliyoyaona ndotoni usiku wa jana! akanyanyuka harakaharaka....akazipiga hatua kuelekea katikati ya makaburi...huenda akaliona lile kaburi laliloliona kwenye ndoto...punde si punde akasikia sauti ya vishindo vya mtu akitembea nyuma yake!!!!
TAHARUKI!!!!!
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
hofu ikazidi kuongezeka,,akaogopa kugeuza shingo yake,,hakutamani hata kushuhudia, mtu aliyekuwa nyuma yake,,mapigo ya moyo yakaanza kupiga kwa kasi ya ajabu,,jasho likaanza kumtoka! mwili wa Laula ukaonyesha kutetemeka....punde si punde vile vishindo hakuvisikia tena..akaamua kugeuza shingo yake,lakini hakuona mtu yeyote! akaangaza angaza macho yake huku na kule,kwa mbali akahisi kama kamuona mtu anaishilizia mtu huyo alionekana ni mzee kikongwe! akamtambua mtu huyo kutokana na mavazi aliyoyavaa kikongwe huyo,,si mwingine ni yule babu yake!
Upande mwingine kule kijijini,,alionekana mkuu wa kijiji ,akiwa tayari kamuita mganga mchawi apige tunguri,,kujua chanzo cha miujiza iliyoonekana kijijini hapo!
mganga huyo ni moto wa kuotea mbali,,,aliaminika kuwa hakuna jambo aliloshindwa kulifanya! mganga akasema,,"nahitaji muda niachwe peke yangu, naweza kupata chumba?
mkuu wa kijiji akasema,," chumba kipo...aliongea maneno hayo huku akiongozana na mganga,kuifuata nyumba iliyokuwa jirani na shamba,,,akafungua mlango kisha akauliza,,"nadhani chumba hiki kitakufaa.
mganga akajibu,,"bila shaka.
mkuu wa kijiji akazipiga hatua akaondoka na kumuacha mganga akiwa peke yake! mganga huyo akavua nguo zake zote akabaki mtupu kama alivyozaliwa! kisha akatoa zana zake za kichawi tayari kuianza kazi yake ya uganga! akachukua pembe la ng'ombe,,,akanyunyizia dawa ya kichawi ndani ya pembe hilo....kisha akaanza kuongea lugha ya kichawi huku akazunguka ndani ya chumba hicho...alifanya hivyo kwa mara kadhaa....kisha akatabasamu,,akavaa nguo zake,,na kutoka nje ya chumba hicho.
wakati huo wazee wa kijiji pamoja na baadhi ya wanakijiji,,wakiambatana na mkuu wa kijiji,,walikuwa wamesimama nje wakisubiri majibu ya mganga huyo....wakamuona anatoka ndani ya chumba hicho...
mganga akazipiga hatua kuwafuata kisha akasema,,"msiwe na wasiwasi mimi ndiye SAGALI wa SAGALI...nimeshaweka mtego wa hatua ya kwanza,,mtego huo ni maalumu....kwa yeyote aliyehusika na mambo hayo lazima apatwe na maumivu makali kwenye mwili wake, pia atakuja mpaka hapa yeye mwenyewe na kuongea kila kitu alichowahi kukifanya ndani ya kijiji hiki.
wakati huo huo,,kule makaburini alionekana Laula akiwa bado kwenye taharuki, akatafakari nini cha kufanya,,ghafla wazo likamjia,akageuza shingo yake kutazama tena,ule upande aliomuna babu yake, Laula aliendelea kukodoa macho yake huenda akamuona babu yake,,lakini hakufanikiwa kumuona..akajisemea moyo,,"lakini hili kaburi lililopo mbele yangu ndio lile ninililoliona jana kwenye ndoto..alijisemea maneno hayo huku akilisogelea kaburi hilo,,akajiuli,,"hili kaburi ni la nani?
punde si punde akaanza kuhisi maumivu makali tumboni! Laula akashindwa kuvumilia,,akaamua kuketi juu ya kaburi hilo,,huku akiwa ameweka mikono yake tumboni!
kadri dakika zilivyozidi kusongo ndivyo maumivu yalizidi kumuandama....akanyanyuka na kuvua suruali,,ni ile suruali aliyoitoa kwenye sanduku la nguo za baba yake...
wakati Laula anachuchumaa lile jino likadondoka pale juu ya kaburi! lakini Laula hakuona kitendo hicho,kutokana na maumivu makali aliyokuwanayo!
punde si punde,,maumivu yakatoweka,,na tumbo lake likarudi katika hali yake ya kawaida! akanyanyuka na kuvaa suruali..akaifunga vyema kwa kamba kiunoni.....ghafla ikasikika sauti ya mingurumo ya ajabu,,,matawi ya miti iliyokuwa imeota kulizunguka eneno la makaburi,,yakaanza kutikisikika,,ukavuma upepo mkali,,,nuru ikaanza kutoweka taratibu na giza likatanda..
punde si punde lile kaburi lililokuwa mbele ya Laula likaanza kutikisika,Laula akalitazama kaburi hilo,,akashtuka kuona jino juu ya kaburi hilo! akaingiza haraka mkono wake ndani ya mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa, akajisemea moyoni,,"hilo jino limetokaje humu kwenye mfuko?
wakati anajiuliza maswali hayo,,ghafla ardhi ikaanza kutikisika na lile jino likatoweka kimiujiza Laula akaingiwa na hofu akaamua kutimua mbio,,kutoka eneo hilo la makaburi.
wakati huo huo,,kule kijijini,,waliendelea kusubiri,,punde si punde mganga akashtuka!akahisi harufu isiyoyakawaida akaingiwa na wasiwasi!!! akatimua mbio kukifuata kile chumba akachukua zana zake za kichawi,,akaziweka kando yake kisha akachukua kioo maalumu cha kichawi...akakipaka dawa ili aweze kuona nini kinachoendelea..
wakati huohuo kule upande wa nje,,wanakijiji hawakuwa na mashaka,,,ghafla ikasikika sauti ya mganga akipiga kelele.kule chumbani,,punde si punde mganga akaonekana akitokea ndani ya chumba hicho huku akitimua mbio....wanakijiji wakaingiwa na hofu...mara ghafla giza likatanda!!
PATASHIKA!!!!
↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔
