Posts

Showing posts from June, 2025

Simulizi: Penzi la mfungwa 02

Image
Zabroni alirudi nyumbani baada kutoka kumsindikiza mzee Maboso,akiwa njiani aliwaza kipi afanye nini sasa baada kumtambua mbaya wake. Je, aendelea kuchoma nyumba ama adili na mbaya wake? Akili ya fasta ikamjia kwamba bora aendelea kuchoma nyumba ikiamini kuwa maumivu aliyonayo moyoni mwake huwenda yakatulia kama sio kupotea kabisa. Yote hayo kijana Zabroni alikuwa akiyawaza huku akirejea nyumbani mikono nyuma kichwa chini,alipo fika nyumbani alikuta karatasi ndogo kwenye meza iliyokuwepo sebuleni. Zabroni alionekana kustuka huku moyo wake ukihitaji kufahamu kilicho andikwa kwenye karatasi hiyo,hatimaye aliichukuwa akakuta maneno yaliyoandikwa "Kijana Zabroni, mjukuu wangu mwanangu pia. Nimekupa dawa hii ili uweze kulipa kisasi juu ya kile ulicho fanyiwa,hakuna ubishi mzee Fungafunga ndio muhusika mkuu wa vifo vya wazazi wako. Alifanya kitendo kile baada kuona baba yako anamzungusha kumlipa deni lake alilokuwa akimdai. Zabroni Zabroni lipa kisasi kijana unyama huo kamwe huwezi kuup...

Sumulizi: Penzi la Mfungwa 01.

Image
  IMEANDIKWA NA : ALEXIS WAMILLAZO *********************************************************************************  Ilikuwa muda wa saa nane usiku zilisikika sauti za wanakijiji wakipiga mayowe.."mwizi mwizii mwizii..", sauti hizo zilitambaa kwa kasi ya ajabu usiku ule kitendo ambacho kiliwafanya wanakijiji waliokuwa wamelala wakaamka ili kumkimbiza mwizi huyo ambaye kimuonekano alionekana kuwa shapu na kasi ya ajabu,alifanikiwa kuruka vigingi mbali mbali akatoka kijijini akakimbilia nje ya kijiji akatokomea kunako mashamba yaliyokuwa kando ya kijiji hicho. Hapo mwizi huyo akawa amefanikiwa kuwatoka hao wanakijiji walioonekana kuwa na hasira kali kwani baada kutokemea nje ya kijiji,walibaki kujilaumu huku kila mmoja akiwa na hamu ya kumkata ili wamuadabishe jambo ambalo lilienda kinyume na malengo yao. Mwizi aliwapotea. Baada mwizi kufanikiwa kuwatoka,wanakijiji waliamua kurudi majumbani kwao. Kesho yake asubuhi palipo pambazuka mwenyekiti wa kijiji alimtaka mjumbe wake api...

Chombezo: Sharobaro wa Tandale 05 MWISHOOO

Image
Kama unavyofahamu joto linapopanda kwa watu ambao wapo sehemu ambayo ni salama kwao kufanya chochote bila kubughudhiwa na mtu zaidi ya kumchukiza tu mola wao, Dullah na Atu si wakajikuta wapo kama walivyokuja duniani. Dullah alipomtazama binti wa watu akiwa kalegea na kamtumbulia macho huku akihema, akaona akimchelewesha bila kumpa mkomboti itakuwa dhambi kubwa, sijui alimbinuaje bwana, Atu akaanza kutoa ushirikiano huku akilia kwa raha. Rigwaride lilichezwa kwa kila mmoja kuhakikisha anamfaruhisha mwenzake,wa kwanza kupeperusha bendera ya ushindi alikuwa Atu ndipo mzee mzima akalishusha kombora lake lenye ujazo wa kutosha lililomlegeza kabisa Atu. Baada ya wawili hao kumaliza awamu hiyo ya kwanza walipeana asante na kwenda kuoga ndipo Dullah alimwagizia Atu kilevi alichotumia, akamwita mtu wa jikoni na kuagiza michemsho ya kuku miwili ili warudishe damu. Dullah na Atu walikunywa bia na walipomaliza kula mchemsho wa kuku, si wakaanza tena vimichezo vyao vya chumbani zaidi,miili yao ili...

Chombezo: Sharobaro wa Tandale 04

Image
Alipoambiwa hivyo, si akakumbuka kwamba Doreen alimpatia simu ambayo mpaka muda huo hakumuonesha fundi Yassin akajikuta akiachia tabasamu lililoonwa na fundi. “Vipi naona umefurahi!” fundi Yassin alimwambia. Kutokana na kauli hiyo, kumzuga fundi wake, Dullah alimwambia alimfurahisha sana alipomwambia atakapoanza kwenda kwenye site nyingine wataenda wote. “Ndiyo hivyo, siwezi kukutupa mdogo wangu,” fundi Yassin alimwambia Dullah bila kujua mwenzake alifurahi kukumbuka alikuwa kapewa simu ambayo ingemsaidia kuwasiliana na mpenzi wake Doreen. Wawili hao walipotosheka kwa kinywaji waliondoka na kuelekea nyumbani, walipokaribia Dullah alimwambia fundi wake kwamba anakwenda kumsalimia rafiki yake Ipyana ambaye hakuonana naye kama siku nne hivi. “Dogo ukiwa na hela hutulii, au unakwenda kuongeza mbili za kulalia nini?” fundi alimwuliza. “Hapana, naenda tu kumwona mshkaji wangu huenda atanipa mchongo wa kazi maana kuanza kushinda nyumbani bila kazi kwa mtoto wa kiume haipendezi,” Dullah alimwa...