Simulizi : Mama’ke Mama Sehemu Ya Nne (4)

Sasa maji yale mithiri ya damu yalikuwa yamenifikia magotini ndipo yule kikongwe akazungumza. “Jitahidi sana uogelee kwa bidii zako, ukithubutu kuyameza haya maji utakuwa ni mwisho wako, utakufa kwa uchungu sana kwa sababu umeitwa kwa hiari yako unaleta ujanja ujanja....” alizungumza vile na kama kawaida yake aliendelea kunicheka. Mvua ilizidi kuongezeka, nilikuwa nimeuziba mdomo wangu ili nisije kumeza yale maji kama alivyonionya yule kikongwe. Hayawi hayawi hatimaye maji yalikuwa shingoni, sasa nikalazimika kuogelea katika lile dimbwi la maji, nilikata maji kwa kutapatapa lakini yule kikongwe yeye alikuwa amesimama tu.. yaani ni kama alikuwa anazidi kurefuka kadri maji yale yalivyokuwa yanaongezeka. Nilipiga mbizi mpaka nikaisikia mikono ikiwa imeshika ganzi na hapo nikasalimu amri nikijisemea na liwalo na liwe. Nikaacha kupiga mbizi nikasubiri kifo kama alivyokuwa ameniahidi. Kifo cha uchungu mkali. Nilipoacha kupiga mbizi maji yale yakakauka na nikajikuta katika ardhi kavu kabisa i...