Simulizi : Miss Tanzania Sehemu Ya Kwanza (1)

ADMIN
0


 IMEANDIKWA NA : PATRICK C.K

*********************************************************************************


“Patrick amka darling inakaribia saa nne sasa”Alisema Veronika kwa sauti laini ya kubembeleza.


‘Mmmmhhh”Akaguna Patrick ,akajigeuza upande wa pili na kulivuta zaidi shuka.


“Amka ukaoge”Alizidi kubembeleza Veronika.Kwa uvivu Patrick akaamka na kuelekea bafuni kuoga.Dakika chache baadae alitoka akiwa amechangamka.


"Kweli maji ni dawa nzuri ya uchovu.Sasa najisikia safi kabisa.Nadhani kwa sasa itabidi nipunguze muda wa kufanya kazi .Nimekuwa nikifanya kazi kwa masaa mengi sana kwa siku kiasi kwamba nakosa hata muda wa kupumzika.Naogopa tukija kuoana nisije kushindwa kutimiza majukumu yangu kama mume kwa sababu ya uchovu” akasema Patrick na kumfanya Vero atabasamu halafu akatoa kicheko cha chini chini na kusema


“Kweli mpenzi jitahidi kwa sasa kupata muda wa kutosha wa kupumzika.”


“Nitajitahidi baby”


Baada ya kuhakikisha sasa yuko safi Vero akamshika mkono Patrick na kumpeleka sebuleni kupata stafstahi.


“Patrick dear nataka unisindikize Supermarket nikafanye manunuzi ya vitu vya ndani .Si unajua kesho Andrew na vicktoria wameahidi kututembelea”Akasema Veronika wakati wakiendelea kupata chai.


“Mhh ! Vero nenda mwenyewe mimi niache nipumzike ”Patrick akajibu


“jamani dear usifanye hivyo naomba unisindikize ,mimi naona uvivu kwenda peke yangu”


‘haya mama ,tumalize chai twende ili tuwahi kurudi”


“Nashukuru dear”


Katika vitu ambavyo Veronika alibarikiwa kuwa navyo ni uwezo wake mkubwa wa kushawishi.


* * * *CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Veronika Rugi alikuwa ni msichana mrembo mwenye mvuto wa aina yake.Binti huyu licha ya kujaliwa kichwa kizuri chenye nywele laini ,nyingi na ndefu ,alikuwa na uso mpana wa mviringo ulionakshiwa na macho mapana yenye kurembua muda wote.Midomo mizuri ,laini ambayo akikupiga busu hutatamani abanduke mdomoni .Mtoto huyu alijaliwa shingo murua ambayo iliungana na kiwiliwili kilichokuwa na kifua chenye kupendeza kilichobeba chuchu changa zenye kusisimua,zenye kuwatoa udenda wakware.Kimwana huyu mwenye uzuri usiopimika alijaliwa umbo la utatanishi kuanzia kiunoni kushuka chini.Ni wasichana wachache sana waliopewa upendeleo wa namna hii na manani..


Pamoja na sifa hizo zote za nje lakini bado alikuwa na sifa lukuki za ndani.Kikubwa zaidi kinachomfanya apendwe na kila mtu ni uwezo wake mkubwa wa kuelewa mambo.Ni binti mwenye roho nzuri ya huruma na upendo asiyependa kujivuna wala kujikweza licha ya uwezo mkubwa familia yake ilionao.Ni binti mwenye heshima kwa watu wa rika zote ,mcheshi,asiyependa ubinafsi na zaidi ya yote ni mtu anayejua kupenda.


Veronika ambaye bado anaishi na mama yake mzazi baada ya baba yake kufariki miaka kadhaa iliyopita ,alikuwa ni mtoto wa tatu na wa mwisho katika familia ambayo haikubahatika kuwa na mtoto wa kiume.Dada mkubwa wa Veronika aliyeitwa Loniki hivi sasa anafanya kazi katika shirika la ndege la British airways ,ameolewa na anaishi nchini Uingereza.Mtoto wa pili kuzaliwa katika familia hii ni binti mrembo sana Sarah ambaye aliwahi kushika nafasi ya tatu katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa.naye amekwishaolewa na ni afisa mahusiano wa benki moja mpya kabisa nchini iitwayo African meckat bank.Mtoto wa tatu na wa mwisho ni Veronika ambaye bado hajaolewa ,ila alikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha maandalizi ya ndoa yake na mchumba wake Patrick.Ni hivi karibuni tu amehitimu shahada yake ya kwanza ya biashara katika chuo kikuu cha dar es salaam.Yeye ndiye msimamizi mkuu wa miradi yote ya familia kwa sasa.


* * *


“Patrick mpenzi nilisahau kukwambia toka mapema kuwa dada Loniki alifurahi sana kusikia tunataka tukafanye shopping ya harusi yetu nchini Uingrereza.Ameahidi kuwa yeye na mumewe watagharamia safari nzima ya kwenda na kurudi na gharama zote za manunuzi.Amesisitiza kuwa tusitumie hata shilingi yetu.Kwa maana hiyo wiki hii nataka niende tena kufuatilia yale maombi yetu ya viza pale ubalozini.Nadhani kama Mungu akijaalia basi ndani ya wiki mbili zijazo tutakuwa tumeshakamilisha taratibu zote zinazotakiwa.”


Alisema Vero huku akijiegemeza karibu zaidi na kifua cha Patrick.Muda huo ilipata saa mbili za usiku , bado walikuwa wakipunga hewa safi baada ya mlo wa jioni.


“Wow! Hongera sana Vero kwa kuwa na ndugu wakarimu na wenye upendo wa hali ya juu sana kama ulivyo wewe.Tena umeongea kuhusu Loniki nimekumbuka zile CD alizonitumia wiki iliyopita.Unajua sijatazama hata moja.Hebu twende ndani nikaitazame ile filamu mpya ya Jack bauer.”


Akasema Patrick huku akijiinua toka pale walipokuwa wameketi na kuelekea sebuleni .Vero naye akakusanya vitu vyote vilivyokuwapo chini naye akaingia ndani.


“Vero mbona ile CD ya Jack bauer siioni hapa au Andrew aliichukua?Akauliza Patrick baada ya kuitafuta CD ile bila kuiona.


“Yawezekana Andrew aliichukua kwa sababu siku ile aliing’ang'ania sana.Nakumbuka kuna CD alizichukua hapo nadhani na hiyo nayo ilikuwapo.”Akasema Vero


Patrick akalifunga kabati ,akaelekea katika friji akafungua na kujimimia Juice katika glasi .Vero alikuwa ameketi sofani akitazama Luninga.


“ Patrick ,Miss Tanzania mwaka huu itakuwa na ushindani mkubwa sana kwa sababu mabinti ni warembo kupita maelezo.Mhh………..”


Alkasema Vero huku amekodoa macho yake katika Luninga kubwa iliyokuwamo humo sebuleni.


“kwani fainali za miss Tanzania ni lini?”Patrick akauliza


“Ni jumamosi ijayo na itafanyikia pale Diamond Jubilee.Kutapambwa na onyesho kali la Malaika band,vile vile wana Fm academia na wasanii wengine kibao watakuwepo.Nataka kesho nikakate tiketi zetu za V.I P ili tusikose nafasi siku hiyo”Alisema Vero


Akiwa na juice yake mkononi Patrick akajisogeza taratibu kuelekea mahali alipokaa Veronika .Kabla hajafika sofani alisimama akapiga funda la juice kisha akaelekeza macho yake katika luninga


“Naitwa Neema ni mrembo toka kanda ya kaskazini.Ni miss Arusha.Napendelea sana muziki wa dini,kusoma na michezo mbali mbali.Nategemea kuwa mwanamitindo wa kimataifa.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitajikita zaidi katika kuwasaidia watoto yatima kwani naelewa mateso na machungu wanayoyapata kwa kutokuwa na wazazi wao.Naombeni kura zenu namba yangu ya ushiriki ni ishirini.”Alikuwa ni mrembo wa Arusha akijinadi katika kipindi maalum cha kuwatambulisha washiriki wa kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Tanzania kilichorushwa moja kwa moja na televisheni ya Taifa.


“Du! Si mchezo”Aliguna Patrick huku akiisogelea zaidi Luninga


“nimekwambia Patrick warembo wa mwaka huu si mchezo .Hebu kaa uangalie jinsi watoto walivyo wazuri ”Akasema Vero


“Naitwa Happy kibaho.Ni mrembo wa wilaya ya Ilala .Napendelea sana muziki laini,kusoma hadithi ,magazeti,kutazama luninga,na wanyama.Nategemea kuwa mwanasheria.Iwapo nitachaguliwa kuwa miss Tanzania nitaelekeza nguvu zangu zote katika kuwasadia vijana wajasiria mali ikiwa ni pamoja na kuwatafutia wafadhili,nitaitumia kofia yangu kuiomba serikali ielekeze nguvu zake zaidi katika kuwasaidia vijana hawa katika kuwapatia mitaji na kuwatafutia masoko ya bidhaa zao wanazozizalisha ili kupambana na ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira.Ninaomba kura zenu ili niweze kulitwaa taji hili la miss Tanzania kwani nina vigezo vyote vya kulitwaa taji hili .Namba yangu ya ushiriki ni 6.”


“Whaaaat!!!!!!!!!!!!!!........................”Patrick Akapiga ukelele mkubwa


“Nooooooooooo!!!!!!!!..I cant bel……………………”ghafla glasi aliyoishika ikamponyoka ikaanguka na kuvunjika .Taratibu nguvu zikaanza kumwishia akadondokea sofani kisha akapoteza fahamu.


“Patrick ,Patrick what’s wrong....!!!!!!!!!!!...”


Alihamaki Veronika huku akimsogelea Patrick pale sofani na kumtingisha.


“Patrick darling what’s wrong with you?CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Alizidi kuuliza Vero huku akimtingisha.


“Ooh ! Nooo...!!!!...Wake up Patrick”Alipiga ukelele baada ya kugundua kuwa Patrick hakuwa na fahamu.Vero akataharuki asijue afanye nini.Hakukuwa na mtu yoyote wa karibu ambaye angeweza kumsaidia .Alitoka kutaka kwenda kuwaita majirani ,akafika mlangoni na kurudi tena ndani mpaka sofani alipolala Patrick.


“Patrick ! Patrick dear what’s wrong with you.Whats’s wrong Patrick!!!!!!!!!”Vero aliongea peke yake huku machozi yakimtiririka.Pale pale akapata wazo la kumpeleka Patrick hospitali.Kwa nguvu zake zote akamuinua Patrick na kumpakia garini ,akakimbia kufungua geti kisha akaingia garini na kuondoka kwa kasi ya ajabu pasi na kufunga mlango wowote wa nyumba.Kwa kasi ya ajabu Vero aliendesha gari hadi hospitali ya karibu maarufu kama Dr Heneriko hospital.Si mbali sana na makazi ya Patrick.Huku akilia akapaki gari na kuingia ndani ,akawaomba msaada wauguzi .Haraka haraka wauguzi wakamchukua Patrick na kumuwahisha katika chumba maalum kwa ajili ya kumpatia huduma ya haraka.


“Hurry up !.hurry up.! Ooh Patrick what’s wrong with you?”Alilalamika Vero huku akiwaomba manesi waharakishe.Muda wote huo machozi hayakumkauka.


Veronika alizuiliwa asiingie katika chumba cha huduma ya kwanza akaachwa hapo nje na mmoja kati ya manesi akiendelea kumfariji.


“Jipe moyo dada yangu Patrick atapona tu.Mtumaini Mungu.”Nesi yule alimbembeleza Vero kwa upole.


Dakika kama 20 hivi baadae dokta Heneriko alimwita Vero ofisini kwake na kumuomba awe mvumilivu wakati wakiendelea kuishughulikia hali ya Patrick.Dokta alitaka kufahamu nini hasa kilichopelekea Patrick kupoteza fahamu.


“Unajua dokta ,Patrick ni mpenzi wangu na tuko katika maandalizi ya harusi yetu.Mimi siishi naye kwa sasa ila huja kwake kila mwisho wa wiki .Leo hii toka asubuhi alikuwa akilalamika kuwa alihisi uchovu mwingi .Tulitoka kidogo kisha tukarudi na akaendelea kupumzika.Usiku tukiwa sebuleni tukiangalia Tv nikaona mwenzangu akipiga ukelele akaishiwa nguvu na kuangukia sofani akapoteza fahamu.kwa kweli sina hakika mpaka sasa ni kitu gani hasa kilichopelekea hali ile kutokea.Naomba Dokta ufanye kila linalowezekana ili Patrick apone.Niko tayari kutoa kiasi chochote cha pesa ili mradi apone.”


Vero alishindwa kujizuia akaangua kilio.


“Nyamaza Vero,Hali ya Patrick inaendelea vizuri. nina hakika muda si mrefu atazinduka.Kwa hiyo yawezekana kuwa kuna habari yoyote aliyoitazama ambayo ilimpelekea Patrick kupata mstuko ?


“Sidhani dokta kwa sababu wakati tunaangalia Tv hakukuwa na taarifa yoyote ya kutisha au kustusha inayoweza kupelekea mtu kupata mstuko hadi kupoteza fahamu.Tulikuwa tukiangalia washiriki wa miss Tanzania wakijinadi.Ni hilo tu”Vero akajibu


Dokta Heneriko akanyamaza kimya kwa sekunde kadhaa kisha akasema


“Kwa kumbukumbu zako toka umekuwa naye kuna siku yoyote tukio kama hili limewahi kumtokea zaidi ya leo?


“Hapana dokta tangu mimi nimekuwa naye halijawahi tokea tukio kama hili Patrick kupoteza fahamu.”


“Ok Vero hivi sasa waweza kwenda kupumzika na kutuacha sisi tuendelee kumuhudumia mgonjwa wako.Iwapo kutakuwa na mabadiliko yoyote tutakupigia simu kukutaarifu.Na kama itahijika kumuhamisha kumpeleka katika hospitali kubwa zaidi tutakutaarifu pia.Lakini kwa sasa hali yake inaendelea vizuri,mapigo ya moyo wake yako sawa na kila kitu kinaonekana kufanya kazi vizuri.Huu ulikuwa ni mstuko wa kawaida tu ambao unaweza kumtokea mtu yeyote na hasa akiwa na msongo wa mawazo.”Akasema Doctor Henry.


“No Dokta ,siwezi kwenda nyumbani bila kujua hali ya mpenzi wangu iko vipi.Nitalala hapa hapa .Nataka niwe wa kwanza kuniona pindi atakapofumbua macho.Samahani dokta naweza kuitumia simu yako kuongea na mama yangu na kumtaarifu juu ya ugonjwa wa Patrick”


Dokta Heneriko hakuwa na kipingamizi akamruhusu Vero aitumie simu yake.


Vero akampigia simu mama yake na kumtaarifu juu ya tukio lile ,halafu akawapigia simu ndugu zake wote bila kumsahau Andrew rafiki mkubwa wa Patrick pamoja na Alois kaka yake Patrick.Wazazi wa Patrick walikuwa safarini nje ya nchi.




Ilichukua kama nusu saa hivi toka Andrew apate taarifa ya ugonjwa wa patrick,kuwasili pale hospitali.Akiwa na mpenzi wake Vick walishuka garini na kukimbia kuelekea mapokezi.Mara tu baada ya kuingia hapo mapokezi walilakiwa na sura yenye kusawajika ya Vero.Alipowaona Andrew na Vick wakiingia humo hospitali Vero aliangua kilio ambacho kiliwachanganya zaidi


“Where is Patrick??”Andrew akauliza huku akijikaza lakini ni wazi alikuwa akitetemeka


“Calm down Vero tuambie Patrick yuko wapi?”Aliuliza tena Andrew .Vick akamkumbatia Vero huku naye machozi yakimtoka.


Andrew alimfuata nesi aliyekuwa mapokezi na kumuuliza juu ya hali ya Patrick.Hakuridhika na jibu alilolipata ,kwa kasi akakimbia hadi katika ofisi ya Dokta Heneriko lakini hakumkuta.Taratibu akatoka humo ofisini jaso likimtiririka na kurudi mapokezi.tayari Aloicy kaka yake Patrick alikwisha wasili hapo hospitali akiwa ameongozana na mke wake nao wote waliungana na Vick katika kumbembeleza Vero.


Andrew akawasalimia kisha akamvuta mkono alois wakasogea pembeni kidogo.


“Hebu niambie Andrew kitu gani kinachoendelea hapa na Patrick yuko wapi ?


Aliuliza Alocyhuku naye jasho likimtiririka


“Brother Aloic hata mimi mpaka muda huu sielewe chochote kwani toka nimefika hapa muda mfupi uliopita sijaweza kuongea lolote na Vero.Ila kwa maelezo niliyoyapata toka kwa nesi ni kwamba Patrick yuko katika chumba cha huduma ya kwanza akipatiwa matibabu.Nasikia ni mstuko ndio uliopelekea akapoteza fahamu”


Mara dokta Heneriko akatokea.Nesi aliyekuwapo mapokezi akamtambulisha kwa akina Andrew.


“Dokta hawa ni ndugu zake na Patrick wamefika saa hivi na walikuwa wakitaka kupata taarifa juu ya maendeleo ya mgonjwa wao’


Dr henry akawasalimu wote halafu akawaomba Alois na Andrew wamfuate ofisini kwake..


“Vijana wangu kwanza poleni sana kwa matatizo ‘


“Ahsante sana dokta tumeshapoa”Walijibu kwa pamoja


“sasa vijana wangu nimewaiteni hapa ili tuongelee zaidi suala la ndugu yenu..Patrick aliletwa hapa kwangu usiku huu akiwa amepoteza fahamu.Kwa haraka nikisaidiana na madokta wenzangu tumejitahidi kumpatia huduma ya kwanza na mpaka sasa maendelo yake ni mazuri.Tumejitahidi kurekebisha mapigo ya moyoyaliyokuwa juu sana na kwa sasa yako kawaida.Taratibu anaanza kurejewa na fahamu zake ingawa bado anahitaji kupumzika zaidi kwani bado fahamu hizarejea vizuri.Maendeleo yake ni mazuri na baada ya muda mfupi ujao basi atarejea na fahamu zake zote.”


Alois alishusha pumzi nzito kwa kusikia taarifa ile ya dokta.akatoa leso na kujifuta jasho lililokuwa likimtirirka kwa kasi muda huo.


“Thanks God”Alisema Alois huku ameinua mikono juu ishara ya kumshukuru Mungu


“kwa hivi sasa bado ataendelea kuwapo katika uangalizi maalum mpaka hapo hali yake itakapokuwa nzuri kabisa.Tatizo lililompata ni mstuko wa moyo.Ni tatizo la kawaida kutokea.Ila hali yake itakapokuwa nzuri tutamshauri aonane na daktari bingwa wa magonjwa ya moyo ili aweze kumfanyia uchunguzi zaidi katika moyo wake ”


Baada ya kupata maelezo ya kutosha toka kwa dokta,Aloicy na andrew waliridhika kabisa na dokta akawa shauri waende kupumzika mpaka kesho .aloicy alikubaliana na wazo hilo lakini akashauri andrew awarudishe Vero na Vick nyumbani wakapumzike.Yeye atabaki pale kuangalia hali ya Patrick inavyokwenda.


Wakati wakiendelea kujadili mama yake Vero akatokea.Akawasalimu wote aliowakuta hapo kisha kwa wasiwasi akataka kujua juu ya hali ya Patrick.alipewa maelezo na mafupi ya hali ya mgonjwa halafu akaomba aonane na dokta Heneriko,akaongea naye na kupewa kwa muhtasari juu ya hali ya Patrick na maendeleo yake na akahakikishiwa uangalizi wa hali ya juu.


“Ok jamani sasa utaratibu gani unaoendelea hapa?


Aliuliza Bi stella Rugi mama yake na Vero.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


“Tumepanga kuwa Andrew awarudishe nyumbani Vero na vick wakapumzike ,mimi nitaendelea kubaki hapa hapa na kufuatilia hali ya mgonjwa”Alisema aloicy


“Vizuri ,basi msipate shida ,Vero na Vick nitaondoka nao mimi,halafu Andrew nenda kule kwa Patrick ukahakikishe usalama .Aloicy utaendelea kubaki hapa kumwangalia mgonjwa .Nitakuwa nakupigia simu mara kwa mara ili kujua maendeleao ya mgonjwa sawa baba eenh”Alisema mama yake Vero


“sawa mama tumekuelewa .”Andrew na aloicy waliitika kisha wote wakatawanyika na kumwacha Aloicy hapo hospitali


Saa saba usiku Patrick akarejewa na fahamu zake kamili.Kitu cha kwanza kuhisi ni harufu kali ya dawa.akageuza shingo kutazama pande zote akatambua kuwa pale alikuwa hospitali.Taratibu akavuta kumbukumbu za nyuma na mara akakumbuka kitu kilichopelekea yeye kuwepo pale.


“I saw her.Real I saw her.she’s alive”Alijikuta akitamka maneno haya huku jasho likikimtiririka na mapigo yake ya moyo kwenda kasi .


* * *


Muuguzi aliyekuwa akimuangalia Patrick aliingia ndani na kumkuta tayari Patrick amerejewa na fahamu na amekaa kitandani.Haraka akaenda kumwita daktari.Dk heneriko alikuja kwa kasi na kumpima akagundua kuwa bado mapigo ya moyo wa Patrick yalikuwa juu sana.


‘Lazima kuna kitu kinamsumbua huyu si bure”Aliwaza dokta Heneriko.


“Patrick “Dokta akamwita baada ya kumaliza kumfanyia vipimo.


“naam dokta”Aliitika Patrick kwa sauti yenye kukwaruza.


“Pole sana “


“Ahsante sana dokta”


“Patrick kijana wangu usijali utapona tu hali yako inaendelea vizuri .Unahitaji kupumzika sasa mpaka hapo asubuhi tutakapochukua tena vipimo vingine”


“Sawa dokta.”


“Ok pumzika Patrick na iwapo utahitaji kitu chochote nesi yuko hapo nje na atakuwa akija hapa mara kwa mara kukuangalia.Tena nimekumbuka kaka yako yuko nje muda sijui kama ungependa kumwona?”Akasema dokta heneriko.


“Yes dokta naomba uniitie..”


Dokta Heneriko akafungua mlango na kutoka.


Aloicy muda huo alikuwa amesinzia katika sofa lililoko mapokeziMara akastuliwa na sauti ya Dokta Heneriko.


“Aloicy ,Patrick amekwisha rejewa na fahamu zake kamili kwa hiyo unaweza kwenda kumwona.Ila tafadhali usijaribu kumuuliza chochote kuhusiana na kilichopelekea yeye kupoteza fahamu.Ongea naye maongezi mengine ya kawaida.sawa?”


“sawa dokta”Alijibu Patrick huku akifikicha macho yaliyojaa usingizi.Nesi aliyekuwepo mapokezi akampeleka hadi katika chumba laimokuwa amelazwa Patrick.


“Vipi brother unajisikiaje kwa sasa?Alisema Aloicy


“Sasa hivi sijambo brother najisikia vizuri.nashukuru kwa kuja kuniona”


“Usijali Patrick kwa sasa endelea kupumzika.bado unahitaji mapumziko ya kutosha.Mimi niko hapo mapokezi tutaonana asubuhi”


“Ok brother”


* * *


Baada ya kulia sana hatimaye kiusingizi kikaanza kumchukua na taratibu akajikuta akianza kulala.Hazikupita hata dakika kumi toka aanze kusinzia simu yak ikaanza kuita na kumstua toka usingizini.Alipoiangalia simu yake ilikuwa imeandika jina Aloicy.Aliogopa kuipokea simu ile akabaki akiiangalia ikiiendelea kuita.Mikono ilikuwa ikimtetemeka .Alihofia pengine simu ile inaweza kuwa imebeba ujumbe mbaya kuhusu Patrick.Simu iliita ikakatika ,ikaanza kuita tena.Akaamua kuipokea.


“Haloo”Aliita Vero


“Haloo shemeji vipi?Ilkuwa ni sauti ya upande wa pili wa simu ambayo Vero aliitambua moja kwa moja kuwa ilikuwa ya Aloicy.


“safi shemeji vipi kwema huko?Alisema vero huku mapigo yake ya moyo yakienda kwakasi isiyo ya kawaida.


“Huku kwema tu shemeji.Nataka nikufahamishe tu kuwa Patrick tayari amekwisha rejewa na fahamu zake na nimetoka kuongea naye muda si mrefu.Kwa hivi sasa anaendela kupumzika.kwa hiyo shemeji yangu unaweza ukalala kwa amani sasa.”


Vero akashusha pumzi ndefu akakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha akamuaga Aloicy na kukata simu.Alipokata simu akaanza tena kulia kwa kwikwi..Vick ambaye alikuwa katia usingizi mzito akaamka baada ya kustushwa na kilio cha Vero.


“Vero nini tena?


“Patrick anaendelea vizuri.aloicy amenipigia simu sasa hivi na kunifahamisha.”


“sasa kama hajambo unalia nini?


“Huwezi jua Vick ni jinsi gani nisivyopenda kumuona Patrick akiumwa kwa jinsi ninavyompenda..Ninalia kwa mateso ninayoyapata juu yake.”


Vick alimbembeleza vero hadi akanyamaza kisha akajilaza kitandani na kuanza kutafakari.juu ya tukio zima..Alikumbuka qwalikuwa sebuleni wakiangalia luninga ambapo warembo wanaotarajia kuwania taji al miss Tanzania walikuwa wakijinadi .alivuta picha na kumuona Patrick akiwa katka friji akijimiminia maji katika glasi ambapo muda huo Miss arusha neema japheti aliikuwa akijinadi.Alikumbuka kumuona Patrick alivyovutiwa ghafla na kipindi hicho cha warembo.Toka Neema hakumbuki ni mrembo gani aliyefuatia kujinadi ila anachokumbuka ni kwamba Patrick alipiga ukelele mkubwa wa kama anashangaa kitu halafu akaanguka.


“Ni dhahiri ni mstuko ndio uliomfanya Patrick aanguke na kupoteza fahamu .Lakini je ni kitu gani hasa ambacho kilimstua Patrick kiasi cha kupoteza fahamu?Je mstuko huu una uhusiano wowote na kipindi kile tulichokuwa tukiona?Lakini hapana Patrick nimekuwa naye muda kwa mua mrefu sasa na tabia yake ninaifahamu vizuri.Kuhusu wanawake siwezi kumsemea vibaya hana tabia hiyo ya kuwa na wanawake wengine nje ya mahusiano yetu.Nina uhakika na hilo.Sasa ni kitu gani alistuka ?any way siwezi kupata jibu kwa sasa mpaka hapo atakaponiambia yeye mwenyewe kwani nina hakika hawezi kunificha kitu chochote.”


Alikuwa akiwaza Vero na taratibu usingizi ukamchukua akalala.


************************************************


Saa kumi na mbili asubuhi iliwakuta Vero ,Vick na mama yake vero hospitali.Hali ya Patrick ilikuwa ikiendelea vizuri .alfajiri hiyo tayari alikwisha hamishwa toka katika chumba cha uangalizi maalum na kuwekwa katika chumba cha mapumziko ya kawaida.


Wakiongozwa na aloicy ambaye alilala hapo hospitali walielekea moja kwa moja chumbani na kumkuta Patrick tayari amekwishaamka.Bila kupoteza muda Vero akamkumbatia na kumpiga mabusu mfululizo.


“Pole sana my dear.Unajisiaje kwa sasa?


“Najisikia vizuri sana”


alijibu Patrick huku akijinyoosha nyoosha pale kitandani.baada ya kusalimiana kilifuata kipindi cha vicheko na utani wa hapa na pale kisha Vick na mama yake Vero wkaomba waondoke kwa ajili ya kwenda kujiandaa na mishughuliko ya siku.


Vero alimwinua Patrick na kumpeleka bafuni ambako alimwogesha na kumrudisha tena chumbani ,akamwandalia kifungua kinywa .Patrick alijisikia faraja kubwa kwa jisni binti huyu alivyokuwa


akimuhudumia.


************************************************


“Andrew kwa kipindi kirefu sasa umekuwa ni msiri wangu mkubwa.Mambo yangu mengi ambayo sihitaji mtu mwingine kufahamu wewe wayajua.Urafiki wetu ni zaidi ya undugu.Naomba sana kile nitakachokuambia hapa usimwambie mtu yeyote yule.Itabaki kuwa siri yako mpaka pale muda muafaka utakapofika.”


Patrick aliongea taratibu huku akijiweka vizuri sofani.Ni siku ya kwanza tangu ameruhusiwa kutoka hospitali kwa sababu ya mstuko uliopelekea apoteze fahamu.Andrew rafiki mkubwa wa Patrick alikuwa kimya akiwa na shauku kubwa ya kutaka kulisikia lile ambalo rafiki yake alikuwa tayari kumwambia.


“I saw Happy ”alisema Patrick kisha akatulia na kuyaacha maneno yale yamwingie Andrew.


“what” aliuliza Andrew kwa mshangao


“I saw Happy ”


Patrick alirudia tena kisha akainamisha kichwa chini na kuzama katika mawazo mazito.andrew aliinuka na kuanza kuzunguka zunguka mle chumbani huku akionekana dhahiri alikuwa meshtushwa mno na kauli ile ya Patrick.




“Umemuona wapi?”andrew akauliza huku amejishika kichwa.


‘Nimemuona kwenye Luninga .Kulikuwa na kipindi cha kuwanadi warembo wanaoshiriki kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa Taifa .Happy ni miss Ilala.”


“are you sure” Andrew akahoji


“yes I’m sure na ndio kitu kilichonifanya nikapata mstuko na kupoteza fahamu”


Andrew alivuta pumzi ndefu ,akainuka akaanza kuzunguka zunguka humo ndani kisha akakaa.Vijana hawa wote kwa sasa walikuwa katika wakati mgumu sana.Ni Andrew pekee aliyefahamu kilichokuwa kikiendelea kati ya Patrick na Happy na ndio maana alichanganyikiwa asijue afanye nini.Alimuonea huruma sana Patrick kwa wakati huu mgumu alionao.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


“Vero aligundua chochote “Andrew akauliza tena


“sidhani kama aligundua kitu chochote.sidhani kama alihisi chochote kwa wakati ule”


“Ok kwa hiyo tufanye nini sasa” Andrew alihoji.


Patrick akainuka na kwenda katika friji akjimiminia maji baridi kwenye glasi akapiga fuda kubwa kisha akavuta pumzi ndefu na kusema.


“Nataka kuonana na Happy ”


Kimya cha sekunde kadhaa kikapita hapo sebuleni kisha Patrick akaendelea


“Nataka kabla ya kuonana naye kwanza tumfanyie uchunguzi anaishi wapi, anafanya kazi gani,ana mchumba au hana,na chochote kile tunachoweza kukifahamu kuhusu yeye.Uchunguzi huu nataka uwe wa siri na yeye Happy asiweze kufahamu kuwa anachunguzwa.Ikiwezekana tunaweza hata kuajiri mtu wa kuifanya kazi hii niko tayari kumlipa kiasi chochote cha pesa anachohitaji.Nakukabidhi kazi hii Andrew nina imani itafanyika ipasavyo.Tuko pamoja?


“Nimekuelewa Patrick lakini suala hili haliwezi kuathiri maandalizi ya harusi yako ambayo tayari yamekwishaanza?”


“Hahahahaa usihofu kuhusu hilo my friend.I know what I’m doing ,ok?”


“Una maana gani Patrick unaposema unajua unachokifanya ?Ninafahamu kuwa ndoto zako za siku nyingi ni kuwa na Happy katika maisha yako na kwa sasa umekwisha kuwa na uhakika kuwa yupo na kwa wakati wowote unaweza kumuona .Nina wasiwasi sana na huu ujio wa Happy katikati ya maandalizi ya Harusi yako unaweza kutibua kila kitu.


“Kwa ajili ya Happy niko tayari kwa lolote linaloweza kutokea.I must fight for her.all these years I’ve been hurting myself thinking about her na mpaka sasa nimeshindwa kabisa kuifuta kumbukumbu ya Happy moyoni mwangu.Siwezi kuendelea kuutesa moyo wangu Andrew.I have to face her.” Akasema Patrick


“Patrick nafikiri unahitaji kufikiri zaidi kuhusu suala hili, si suala jepesi kama unavyolifikiri.Ni suala ambalo linagusa hisia za watu wengi .Hi…..”


Andrew hakuendela Patrick akadakia.


“Andrew no body’s gonna change my mind.That’s my decision and its final.Nilivyoamua nimeamua.Nitapambana kadiri ninavyoweza ili kumpata Happy .I love her and I know that she loves me too.”


“Patrick miaka mingi imepita tangu mpotezane na Happy na kwa sasa bado kama mwezi mmoja na nusu hivi ufunge ndoa na Vero ,ndoa ambayo sehemu kubwa ya maandalizi yake yamekamilika.Huoni kuwa utakuwa unamyima haki zake Vero kama ukihamishia mawazao yako yote kwa Happy .?Nina imani Vero anakupenda kwa dhati ya moyo wake na nina imani vile vile hata wewe unampenda Vero sasa kwa nini utake kumtesa hivi mtoto wa watu?


“Andrew unayasema haya yote kwa sababu huwezi kuingia katika viatu vyangu na kuona nini kilichomo ndani.Nina imani kubwa hata wewe ungekuwa mahala pangu kwa sasa basi ungeweza kufanya kama mimi ninavyofanya.Please Andrew naomba msaada wako katika hili.Ni lazima nionane na Happy hivi karibuni.”


“Nimekuelewa Patrick lakini bado moyo wangu una wasiwasi sana juu ya kinachoweza kutokea.hapo mbeleni.nafahamu kuwa endapo utaingia matatizoni basi ni sote tutakuwa tuko katika matatizo.Tatizo langu ni lako na lako langu ndio maana tunahitaji sana kushauriana kwa kina kabla ya kufanya jambo.”


“Andrew najua una wasiwasi mwingi kuhusu mimi na Vero.Hilo ni kubwa linalokuumiza kichwa.Hata mimi sijisikii vizuri kumtesa Vero binti aliyeyatoa maisha yake kwangu.Binti anayenipenda kwa dhati ya moyo wake.Ni vero huyu huyu ndiye aliyeirudisha tena furaha ndani ya moyo wangu na kuliondoa wingu zito la ukiwa lililokuwa limenifunika.Nampenda Vero lakini sina jinsi ni lazima nionane na Happy .”


Andrew aliinuka kitini akaiendea friji na kujimiminia mvinyo baridi akanywa mafunda kadhaa kisha akamgeukia Patrick.


“Ok Patrick kwa sababu umekwishaamua basi hatuna budi kufanya hivyo.Mimi nitaianza kazi hiyo kesho.Nitamtafuta mtu ambaye ataifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa.Usijali kuhusu hili rafiki yangu”


Patrick alifurahi akainuka na kumkumbatia rafiki yake


.


*********************************


Saa kumi na mbili za jioni Veronika alirejea katika shughuli zake na kumuaga mama yake kuwa alikuwa akaienda kumwangalia Patrick anaendelaje.Ni siku ya tatu sasa toka Patrick atoke hospitali.Hali yake haikuwa ikiendelea vizuri sana.Muda mwingi alikuwa akionekana ni mtu mwenye mawazo mengi sana.Hali hii ilimpa wasiwasi mwingi Vero kiasi cha kumfanya awe karibu naye kila wakai ili kujaribu kumchangamsha na kumrudisha katika hali yake ya kawaida.


Ingawa Patrick alijitahidi kwa kila jinsi ili Vero asione hali hii ya unyonge lakini mara nyingi alishindwa na kujikuta akitoa machozi.Vero aliigundua hali hii na kwa kiasi kikubwa ikamuongezea udadisi juu ya kinachoendelea .alijua ni lazima liko jambo ambalo linamchanganya Patrick .


‘Haloo sweetie”Alisema Vero baada ya kuingia ndani kwa Patrick


“Haloo vero, you are back”akasema Patrick


Vero akamfuata Patrick kitandani akamkumbatia na kumpiga busu zito.


‘Unaendeleaje mpenzi”


“Naendelea vizuriMungu ananisaidia sana.Muda si mrefu nitapona kabisa”


Baada ya kujuliana hali Vero alimwandalia Patrick Juice kisha yeye akaelekea jikoni kufanya maandalizi ya chakula cha jioni.Patrick alipata faraja kubwa baada ya Vero kuwasili Ni wazi Patrick husikia furaha kubwa moyoni awapo na Vero.


Ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa bado alimpenda sana Vero lakini kwa ghafla Happy ametokea na kuanza taratibu kuzihamisha hisia zake.


Chakula kiilpokuwa tayari kikawekwa mezani,wakala kisha wakapumzika na baadae wakaelekea kulala.


“Vero dear tayari umekwisha kata tiketi za kuingia Miss Tanzania Jumamosi?Patrick akauliza


“Tayari mpenzi Nimekwishaziandaa .Je utaweza kweli kwenda na hali hii?Naona kama hali yako inazidi kudhoofika siku hadi siku”


“Usijali mpenzi wangu lazima nihudhurie hata iweje.Nina imani ndani ya siku mbili tatu zijazo hali yangu itakuwa shwari”


Vero akanyamaza kimya akajaribu kuvuta kumbukumbu nyuma siku ile Patrick alipoanguka na kupoteza fahamu alikuwa akitazama kipindi cha wagombea wa miss Tanzania .Hakutaka kukubaliana kuwa kuna kitu chochote kinachoendelea baina ya Patrick na mashindano yale.Alijitahidi kuilazimisha akili yake ikubaliane na taarifa ya daktari kuwa Patrick alipoteza fahamu kwa sababu ya uchovu mwingi uliokuwa ukimkabili kiasi cha kuufanya ubongo wake ushindwe kufanya vizuri kazi yake.


‘Lakini pamoja na taarifa ile ya daktari lakini kuna kitu kiko moyoni mwa Patrick ambacho kinamyima raha na na kuisumbua akili yake namna hii.Ni kwa sababu hiyo tu ndiyo maana amepoteza furaha yote aliyokuwa nayo kabla.Chakula chenyewe mpaka abembelezwe.mara kadhaa nimemfuma mwenyewe kwa macho yangu akilia.Ingawa anajitahidi sana kuificha hali hii lakini nimekwishafahamu .Anyway nitajitahidi kumuuliza ili anieleze kama kuna jambo lolote linalomsibu.”


Veronika alizama ghafla katika mawazo.


“Unawaza nini mpenzi wangu”Patrick akauliza


“Nothing.Siwazi chochote zaidi yako.Unajua Patrick hali yako kwa sasa inanipa wasiwasi sana.Tangu umetoka hospitali umebadilika.Ni kitu gani kinakusumbua mpenzi hebu niambie.Hali hii inanifanya hata mimi nihisi kama vile ninaumwa pia.Au kama kuna kitu nimekukosea niambie Patrick ili nijirekebishe.Tangu tumeanza mapenzi yetu sijawahi hata siku moja kukuona katika hali hii”


Vero akashindwa kujizuia akaanza kulia kwa kwikwi.


Patrick akamvutia Vero kwae akambusu na kumwambia


“Usihofu kitu baby hakuna kitu kingine kinachonisumbua .Kama daktari alivyosema kuwa natakiwa kupumzika sana .Uchovu ndio uliopelekea tatizo lile kutokea.”


Alisema Patrick huku akizichezea nywele laini za Vero.


‘Hapana dear najua lazima kuna kitu kinachokusumbua akili na hutaki kuniambia”


“Wow my dear angel ,wewe ndiye maisha yangu.Wewe ndiye uliyeyashika maisha yangu.Nimekukabidhi funguo za moyo wangu.Wewe ndie mfariji wangu,wewe ndiye furaha yangu,wewe ndiye kila kitu kwangu sasa kwa nini nikufiche kitu?Hakuna kitu nimewahi kukuficha wewe mpenzi wangu na haitakuja tokea nikawa na tatizo nikashindwa kukwambia.Sasa nisipokwambia wewe nitamwambia nani tena?”


Patrick alijitahidi kumtoa Vero wasiwasi aliokuwa ameanza kuwa nao juu yake na mara moja akaazimia moyoni kubadilika kitabia ili Vero asije akaendelea kumdadisi.Taratibu akaanza kurudi katika hali yake ya kawida ya ucheshi na uchangamfu mkubwa kitu ambacho Vero alikifurahia sana.


********************************


Ni jumamosi angavu ndani ya jiji la Dar es salaam,jiji lililojaa kila aina ya pilika na purukushani.Jua lilikuwa likielekea magharibi na kulipisha giza lichukue nafasi yake.Jioni hii iliwakuta Patrick na Veronika wakiwa katika pilika pilika za kujiandaa kuelekea katika kinyang’anyiro cha kumsaka mrembo wa taifa katika ukumbi wa Diamong jubilee.


Patrick ndiye aliyekuwa katika pilika pilika nyingi zaidi jioni hiyo.Siku hii ilikuwa ni moja kati ya siku zake kubwa kabisa katika maisha yake.Ni siku ambayo aliamini ingemkutanisha tena na kiumbe ampendaye kwa dhati ya moyo wake.Alikuwa ndani ya suti nzuri ya gharama kubwa.Suti hii huwa anaivaa kwa nyakati maalum kama hizi.Hakika alikuwa amependeza vilivyo kijana huyu.Wakiwa katika harakati z a kumalizia kujiandaa simu yake ikaita.Alkuwa ni Andrew.


“Haloo Andrew”


“Hallo Patrick vipi mko tayari?aliuliza Andrew huku akicheka kichinichini.


“Tupo tayari Andrew na muda wowote toka sasa tunaweza kuanza safari ya kuelekea ukumbini”


“Ok Patrick sisi tayari tumekwishajiandaa na muda wowote tutakuwa njiani kuelekea huko na tutawasubiri nje ya ukumbi ili tuingie pamoja.Ila ndugu yangu nakuomba kitu kimoja katu usihamaki.Wala usionyeshe aina yoyote ya mstuko pindi utakapomuona Happy .Najua tu lazima kunaweza kutokea na kitu kama mstuko flani hivi ila tafadhali naomba ujaribu kujizuia kwa sababu pale tutakuwa tuko na Vero na Vick kwa hiyo wanatakiwa wasihisi kitu chochote.Mimi nitakuwa macho kuhakikisha kuwa hakuna kitu chochote kitakachoharibika “


“Usihofu Andrew nalifahamui hilo na niko makini nalo sana.naelewa leo ni siku ya kipekee maishani mwangu.Ni siku ya kihistoria katika maisha yangu hivyo siwezi kuiharibu.”


Baada ya kumaliza kujiandaa na kuhakikisha kuwa wako safi wakaingia garini na kueleka Diamond Jubilee.


********************************


Ukumbiwa Diamond jubilee ulikuwa umefurika watu pasi mfano.Pamoja na ukumbi kufurika watu bado watu walikuwa wakimiminika ukumbini hap kwa lengo la kushuhudia mchuano wa kumtafuta mrembo wa Taifa atakayeliwakilisha Taifa katika mashindano ya dunia.


Patrick,Vero,Andrew na Vick waliwahi sana kuingia ukumbini na kuchukua moja kati ya meza za mbele kabisa.Patrick moyo ulikuwa ukimdunda sana usiku huo,.Andrew alilifahamu hilo na hivyo akawa makini sana katika kuakikisha kuwa hakuna kitu kitakachoharibika .Toka wameingia ukumbini Patrick alikuwa kimya .


“Patrick are you ok?Vero liuliza baada ya kuona Patrick yuko kimya sana.


“Yes I’m ok Vero usihofu.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Mara muongoza shughuli akatokea jukwaani na kuanza kutangaza.


“Mabibi na mabwana mliohudhuria mashindano haya makubwa ya urembo nchini napenda kuwakaribisha sana katika usiku huu wa pekee kabisa kwetu sote.Ni usiku wa pekee kwa sababu leo tutaandika historia mpya kabisa katika mashindano ya urembo hapa nchini na ulimwengu kwa ujumla.Kwa mwaka huu kamati nzima ya Miss Tanzania imeazimia kufanya mabadiliko makubwa sana na nyie wote mlioko hapa ndio mtakaokuwa mashahidi wa kile kitakachotokea usiku wa leo.Nasema karibuni sana katika usiku huu na tujumuike sote mimi naitwa Mc Thora kwa wale ambao hawanifahamu..


“Mabibi na mabwana kabla hatujaendelea mbele na ratiba yetu ningependa kwanza kumkaribisha jukwaani mkurugenzi mkuu wa Masimulizi entertainments ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu Mabibi na mabwana makofi kwa Mr Petit.s Woris”


Petit woris mkurugenzi wa Masimulizi entertainments akapanda jukwaani akiwa amevalia nadhifu sana.


“viongozi mbali mbali mliohudhuria mashindano haya usiku huu, ndugu watazamaji mabibi na mabwana asalaam aleikhum.Ni furaha ilioje kwetu sisi kama Masimulizi entertainments kudhamini mashindano makubwa kama haya ya urembo hapa nchini.Kama wote mnavyoshuhudia mashindano ya mwaka huu yamekuwa na utofauti mkubwa mkilinganisha na mengine yaliyopita hukonyuma..Kwa mwaka huu nathubutu kusema maandalizi yake yamekuwa mazuri ,zawadi zimeboreshwa na ushindani miongoni mwa washiriki umeongezeka mara dufu.Kwa kuwa ni mara yetu ya kwanza kudhamini mashindano makubwa kama haya bado kunaweza kuwa na kasoro kadhaa ambazo nina imani kwa kushirikiana na wadau wote wa urembo hapa nchini tutasaidiana kuzitatua.Nina imani bado tutaendelea kudhamini na kuandaa matamasha mengi na makubwa zaidi hapa nchini ili kuzidi kuukuza wigo wa burudani hususani sanaa hii ya urembo.Mwisho kwa niaba ya uongozi na wafanya kazi wote wa Masimulizi entertainments napenda kuwatakia wote utazamaji mzuri wa mashindano haya usiku huu.Ahsanteni sana.”


Baada ya kumaliza akarudisha kipaza sauti kwa muongoza shughuli kisha akashuka jukwaani.


“mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mkurugenzi wa Masimulizi entertainment ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano haya kwa mwaka huu..Mabibi na mabwana kwa mujibu wa ratiba yetu kinachofuta kwa sasa ni kuwatambulisha majaji ambao ndio watakaofanya kazi kubwa na ngumu ya kutuchagulia mrembo mwenye sifa ya kuwa mrembo wa taifa kwa usiku huu.Majaji tulionao usiku huu ni saba.Ningeomba jaji utakaposiia jina lako likitajwa usimame ili watu wakufahamu.Wa kwanza ni Mr Ernest Namesha,wa pili ni ndugu Mecky ,tunaye pia Mr Boniventure Gregory,anayefuatia ni Mr Samweli Nathaniel,tunaye pia dada yetu mpendwa usiku huu naye ni dada Esther msethi,pia tunaye Mrs Coletha brown,tunaye vile vile bi Susan Abrahams na wa mwisho ni ndugu Jacob Lyimo.Hawa ndio majaji wetu ambao watakuwa wakifanya kazi ngumu ya kumchagua mrembo wa Taifa usiku huu wa leo.”


“mabibi na mabwana baada ya kuwafahamu majaji wa mchuano huu wa leo sasa naomba niwalete kwenu warembo wote 26 katika show maalum waliyoiandaa “


wimbo ukaanza kupigwa na warembo wakaanza kutoka huku wakicheza kwa staili yenye kuvutia sana.makofi nderemo na vifijo vikatawala ukumbini.Patrick alielekeza macho na akili yake yote jukwaani na bila kukosea alimuona Happy ambaye alikuwa amependeza kupindukia Jasho likaanza kumtiririka akatoa kitambaa na kujifuta.Alikuwa kimya kabisa.


Baada ya show ya warembo kumalizika ziliendelea burudani mbili tatu toka kwa wasanii mbali mbali kisha muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.


“Mabibi na mabwana baada ya kupata burudani hizo za kukata na shoka sasa naomba niwalete kwenu warembo wote 26 ili muwatambue.Watapita hapa jukwaani mmoja mmoja .”


Warembo wakaanza kutoka nyuma ya jukwaa na kuanza kupita mbele ya watazamaji.Kidogo Patrick atamke kitu baada ya kusikia jina la Happy likitajwa .Happy akapita jukwaani huku kelele za shangwe zikisikika.Happy alikuwa akionekana kama malaika usiku huu.alikuwa amependeza vilivyo.Kila mtu aliustaajabia uzuri wa binti huyu mwenye kila sifa ya kuwa mrembo wa Taifa na dunia.Kelele zile za mashabiki zilizidi kumchanganya Patrick na kumfanya ahisi kuchanganyikiwa.Andrew alikuwa makini sana kwa lolote ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani kati yao.


Baada ya kupita jukwaani kujitambulisha kwa mashabiki zikafuata burudani za aina yake toka kwa wanamuziki.Kisha Muongoza shughuli akarejea tena jukwaani.


“mabibi na mabwana mambo yanazidi kupamba moto.Mambo ni bam bam na kama nilivyowaeleza toka mwanzo kuwa Masimulizi entertainment wameleta mageuzi makubwa katika mashidano ya mwaka huu .Kwa sasa napenda kuwaleta kwenu warembo wote 26 wakiwa katika vazi la ufukweni.Mhh hapa pana kazi kweli kweli .mabibi na mabwana hebu tuwashangilie hawa warembo wetu watakapokuwa wakipita jukwaani katika vazi la ufukweni.”


Warembo wakaanza kupita jukwaani wakiwa katika vazi la ufukweni.Siyo siri walikuwa wamependeza vilivyo.Baada ya kumaliza kupita na vazi la ufukweni zikafuata tena burudani halafu warembo wote wakapita tena kwa mara nyingine na vazi la ubunifu.Kelele zilikuwa kubwa sana kila walipopita warembo Neema wa Arusha na Happy wa Ilala.Warembo hawa walionekana kuchuana vilivyo.Kisha pita na vazi la ubunifu muongoza shughuli akapanda jukwaani.


“mabibi na mabwana tayari tumewashudia warembo wetu 26 wakipita hapa mbele yetu wakiwa katika mavazi tofauti tofauti.Kwa sasa ule wakati mliokuwa mkiusubiri kwa hamu kubwa unaelekea kuwadia.Kwa hivi sasa tutakwenda kuwafahamu warembo 10 bora ambao wameonekana kufanya vizuri zaidi .Naomba sasa nimkaribishe Mrs Coletha brown ili aje atutangazie wale warembo wetu kumi waliofanya vizuri zaidi.Karibu sana mama.”


Mrs Coletha brown akapanda jukwaani akiwa na karatasi yenye majina ya warembo kumi waliofanya vizuri na ambao wataendelea na mchuano.


“mabibi na mabwana napenda kuchukua nafasi hii kwanza kuwapongea waandaaji wa mashindano haya ambayo kwa mwaka huu yameboreshwa kwa kiwango cha juu kabisa.


Mabibi na mabwana kazi yetu usiku wa leo imekuwa ni ngumu sana .Warembo wote wako katika hali ya ushindani wa hali ya juu mno.Lakini tumeweza kuwapata wale kumi ambao ni bora zaidi na ambao nitawataja hivi punde.Nambari 12 Nelea shulo,nambari 9Saida abdi,nambari 4 Upendo timelo,Nambari 20 Neema i,Nambari 11 Esther stevens,Nambari 6 Happy ,nambari 22 Elimeena kimuo,nambari 26 bahati udhoka,nambari 16 Winifrida mwasajuki,na mwisho ni namba 13 genevieve alphonse.”


Kelele za kushangilia zikasikika ukumbini.Warembo waliofika hatua ya kumi bora wakajipanga mstari.wakapiga picha ya pamoja kisha zikafuata burudani .baada ya burudani mc akapanda tena jukwaani.


“Mabibi na mabwana bado tunaendelea na mchakato wetu wa kuifikia ili hatua kubwa kabisa ambayo kila mmoja wetu aliyeko hapa ana hamu ya kuishuhudia.Kila mmoja anatamani amfahamu mrembo wetu mpya wa Taifa.Kwa sasa tutaenda kuwatafuta wale watano bora ambao kutoka kwao tutampata mrembo wetu.Atapanda tena Mrs Coletha kuja kututangazia warembo watano bora .”


mrs Coletha akapanda tena jukwaani akiwa ameongozana na watu wawili wa miraba minne wanaomlinda.




“mabibi na mabwana kama nilivyowaambia kuwa kazi yetu leo imekuwa ngumu sana hasa kutokana na jinsi warembo wote walivyo na vigezo vya juu mno kiushindani.Lakini pamoja na wote kuwa na ushindani wa juu tumeweza kufanikiwa kuwachuja na kupata wale watano ambao wameonekana kuwa ni bora zaidi.


Warembo waliopita hatua ya tano bora ni mrembo nambari 16 Winifrida mwasajuki,nambari 20 Neema i,nambari 13 Genevieve alphonse,nambari 26 Bahati udhoka na mwisho ni nambari 6 Happy .”


Kelele kubwa zikasikika zikishangilia.Kila mtu pale ukumbini alikuwa ameridhika na kazi waliyoifanya majaji.Hakukuwa na aina yoyote ya upendeleo.Baada ya kuwatambua warembo wote waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora hatimaye kikafuata kipindi cha maswali.Ni Happy kibaho tena ndiye aliyejibu swali vizuri zaidi na kuwafanya watu wote ukumbini kumshangilia kwa nguvu.Kila mtu alikuwa akiamini kuwa Happy ni lazima angeibuka kuwa mrembo wa Taifa.Patrick jasho lilikuwa likimtiririka mwilini.alijitahidi kwa kila alivyoweza ili asiweze kuonyesha hali yoyote ya utofauti pale mezani.Baada ya kipindi cha maswali kumalizika ikafuata burudani moja kisha muongoza shughuli akapanda jukwaani.


“mabibi na mabwana ule wakati uliokuwa ukisubiriwa na kila mtu hapa ukumbini naona sasa umewadia.huu ni wakati wa kumtambua mrembo wetu mpya wa Taifa.Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru sana majaji kwa kazi ngumu waliyoifanya usiku huu kwa kutuchagulia mrembo mpya wa Taifa.Kabla sijamkaribisha jaji mkuu kuja kutangaza mshindi wa shindano hili napenda kumkaribisha mrembo anayemaliza muda wake ili aweze kuongea machache na kuwaaga rasmi kabla hajalivua taji la Miss Tanzania.”


Helen Daudi mrembo anayemaliza muda wake alipanda jukwaani huku akishangiliwa vilivyo.Alipewa kipaza sauti na kusogea mbele.


“mabibi na mabwana ,wageni waalikwa,waheshimiwa majaji ,waandaaji na wadhamini wote wa mashindano haya habari za usiku.Napenda kwanza kabisa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha mimi kutimiza moja ya ndoto zangu nayo ni kuwa mrembo wa Tanzania.Nawashukuru vile vile wazazi wangu na ndugu zangu kwa kunipa moyo toka katika hatua za awali za kinyang’anyiro hiki hadi nilipobahatika kuchukua taji.Mabibi na mabwana kulivaa taji la Miss Tanzania ni mzigo mkubwa.Nimeshuhudia mimi mwenyewe uzito wa taji hili kubwa la urembo hapa nchini.Yapo mengi ambayo unapaswa kulifanyia taifa hili ukiwa kama mrembo wa Taifa.Kuna mazuri na magumu yake.Zipo changamoto nyingi ambazo yakubidi upambane kufa na kupona ili uweze kushinda.Napenda kuishukuru kamati nzima ya Miss Tanzaina kwa ushirikiano mkubwa walionipa katika kipindi chote nilichokuwa nimevaa taji hili.Sintaweza kumtaja mmoja mmoja lakini napenda niwashukuru wote kwa ujumla.Napenda niwashukuru vile vile wadau wote wa sanaa hii ya urembo hapa nchini kwa sapoti yao kubwa waliyonipa.Wamenisaidia sana kuifahamu sanaa hii ya urembo vizuri.Nawashukuru pia wananchi wote wa Tanzania kwa kunikubali Nawapenda wote na ninaahidi kushirikiana na mrembo atakayevaa taji hili usiku huu katika yale yote mazuri niliyokuwa nimeyafanya kwani kulivua taji hili si mwisho wa kuendeleza yale yote niliyokwisha yafanya wakati niko na taji.Mwisho kama binadamu kuna wakati naweza kuwa nimemkosea huyu na yule kwa namna moja au nyingine.Napenda kuchukua nafasi hi kwa dhati kabisa kuwaomba msamaha wale wote niliowakosea.Tusameheane na kuanzia usiku huu tuanze maisha mapya.Ahsanteni sana.”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Alimaliza kutoa machache mrembo huyu akarudi katika kiti chake cha heshima huku akishangiliwa na watu.’


“naam mabibi na mabwana huyo alikuwa ni mrembo anayemaliza muda wake.Na sasa ule wakati tuliokuwa tukiusubiri kwa hamu kubwa ndio umewadia.Ni hivi punde tutaenda kumfahamu mrembo wetu mpya.Naomba sasa nimwite Mr Jackob ili aweze kututajia washindi wetu.”


Mr jacob akapanda jukwaani.


“Mabibi na mabwana kama alivyotangulia kusema Mrs Coletha brown kuwa mchuano wa leo ulikuwa mgumu sana.Tunamshukuru Mungu kuwa tumeweza kumpata mrembo wa taifa licha ya kuwa na wakati mgumu hasa kutokana na kila mrembo alivyokuwa amejiandaa.Mabibi na mabwana nitaanza kuitangaza nafasi ya tatu hadi moja.”


Alitulia kidogo kisha akaendelea.


“Nafasi ya tatu imekwenda kwa mrembo nambari 16 winifrida mwasajuki”


alitulia kwanza na kumpisha mrembo huyu apite mbele huku akishangiliwa.


“nafasi ya pili imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 20 Neema Jaffa”


Kelele za shangwe zikasikika.Neema binti mwenye ngozi nyeusi yenye kung’aa akapita jukwaani akiwa ndani ya tabasamu kubwa.


“Na sasa mabibi na mabwana ni nafasi yakwanza.Nafasi ya kwanza imekwenda kwa mrembo mwenye nambari 6 Happy Kibaho .”


Tangu ukumbi wa Diamond jubilee ujengwe hakujawahi kutokea shangwe kubwa kama hii ya usiku huu ya kuushangilia ushindi wa Happy .Mrembo huyu alifanikiwa kuzikonga nyoyo za watu vwengi.


Patrick alishindwa kujizuia hisia zake akainuka na kushangilia kwa nguvu sana.


Jukwaani Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakuamini kama ni yeye ndiye aliyetangazwa mshindi wa shindano hili hasa kutokana na upinzani mkubwa uliokuwepo miongoni mwa washiriki.Watu walikumbatiana na kupeana mikono ya hongera kuashiria kukubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji ya kumchagua Happy kuwa mrembo wa Taifa.Kila mmoja aliamini kuwa Happy alistahili kulitwaa taji lile.


Baada ya kama dakika kumi hivi za hoi hoi na nderemo muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.


“mabibi na mabwana nafikiri hoi hoi hoi na nderemo hizi zote ni kuonyesha jinsi gani wote kwa pamoja tunavyokubaliana moja kwa moja na maamuzi ya majaji.Happy kibaho ndiye miss Tanzania wetu mpya.sasa kinachofuata ni mrembo anayemaliza muda wake kulivua taji na kumvisha mrembo mpya.”


Zoezi hili likafanyika huku likishangiliwa kwa nguvu sana.na baada ya zoezi hili kukamilika muongoza shughuli akapanda tena jukwaani.


“mabibi na mabwana tukio linalofuata sasa ni la kumkabidhi Miss Tanzania funguo za gari lake.Tunamuomba mkurugenzi mkuu wa Masimulizi entertainment ambao ndio wadhamini wakuu apande jukwaani na kumkabidhi Miss Tanzania funguo hizo.”


Petty woris mkurugenzi wa Masimulizi entertainment akapanda jukwaani na bila kupoteza muda akamkabidhi Happy funguo za gari ambalo ni zawadi ya mshindi wa kwanza.Akiwa katika tabasamu pana sana alipita jukwaani huku akizipunga funguo hewani .Kelele za kushangilia zilisikika.


Baada ya zoezi hilo zikafuata burudani mbili kisha mashindano yakafungwa rasmi na taratibu umati wa watu ukaanza kuondoka maeneo hayo ya Diamond jubilee kila mmoja akiwa amesuuzika vilivyo na ushindi wa Happy kibaho.


Happy sasa alikuwa akipiga picha na watu mbali mbali huku akisongwa na waandishi wa habari wakitaka kufahamu mawili matatu ingawa mkurugenzi wa Miss Tanzania alijitahidi kuwazuia kwani Happy angefanya mkutano na waandishi wa habari hapo kesho lakini haikusaidia kitu.


Patrick ambaye alionekana kuchanganyikiwa kadiri muda unavyosonga alitoa simu yake na kuanza kubonyeza namba kisha akajitenga na akina Andrew ambao kwa sasa walikuwa wamesimama wakijiandaa kuondoka.Patrick aliitumia njia ile ya kujifanya anapiga simu ili aweze kuondoka mahala pale bila kutiliwa mashaka kwani lengo lake kuu lilikuwa kujaribu kupata nafasi ya kuonana na Happy .Andrew alielewa mara moja nini kilichokuwa kikiendelea akawaomba akina Vero na Vick waondoke mahala pale waelekee katika magari.Lengo lilikuwa kuwatoa wasiwasi akina Vero.


Patrick sasa alikuwa akipigana vikumbo na waandishi wa habari ambao walikuwa wakichukua picha na kumuuliza Happy maswali mawili matatu.Alijitahidi sana kupenya na hatimaye akajikuta yuko mahala ambako anaweza kumuona Happy kwa ukaribu.Jasho lilikuwa likimtiririka na moyoni alikuwa na wasi wasi mwingi lakini hii haikukumkatisha tamaa ya kuonana na Happy .Alikwisha azimia hivyo.Alijisogeza taratibu na hakuna mtu yeyote aliyeweza kuwa na shaka naye kuwa si mwandishi wa habari tena toka katika chombo cha habari kikubwa hapa nchi au nje ya nchi kutokana na muonekano wake.


“Hongera sana Happy madame Tanzanie”Alisema Patrick wakati huo akiwa uso kwa uso na Happy .Happy kwa wakati huo hakujua aliyekuwa akiongea naye .Alijua wote ni waandishi wa habari.Lakini neno lile “Madame Tanzanie”linamstua na kumfanya ainue uso wake na kumtazama vizuri mtu yule aliye mpa salamu ile.Kwanza alihisi sauti ile ni kama si ngeni masikioni mwake .mbele yake alikuwa amesimama kijana nadhifu akiwa ndani ya tabasamu lenye kuonyesha aina Fulani ya wasi wasi.macho yake yakakutana na macho ya Patrick na kwa kasi ya umeme kumbukumbu ya ghafla ikamjia kichwani


“Noooooo!!!!!!!!!!! Pa………..t…………….”


Akaanguka na kupoteza fahamu.


Kizaa zaa cha ghafla kikatanda hapo ukumbini.Kwa sekunde kadhaa ikatokea taharuki kubwa.Kila mtu akapatwa mstuko kwa kitendo cha Miss Tanzania kupoteza fahamu ghafla.


Haraka haraka walinda usalama wakamwinua na kumkimbiza katika gari la wagonjwa ambalo lilikuwa nje tayari kabisa kwa dharura kama hii.Kwa kasi ya ajabu gari lile likaondoka kuelekea Hospitali.


Watu waliokuwa bado wako ukumbini hawakuamini kilichotokea ghafla vile .Waandishi wa habari wakalichukua tukio lile kama lilivyotokea.


Patrick nusura akili imruke kwa kitendo cha Happy kupoteza fahamu.Taratibu alihisi kuishiwa nguvu lakini tayari Andrew alikuwa ameshafika ,akamshika mkono na kumtoa nje ya ukumbi .




Saa kumi na moja asubuhi miss Tanzania Happy alizinduka.akaangaza huku na huku akatambua kuwa alikuwa hospitali.Taratibu akaanza kukumbuka kilichotokea na kumfanya awepo pale hospitali mida ile.Akalikumbuka tukio zima lililotokea usiku wa jana.


“ that’s him…I saw him..” Happy akajikuta akiongea mwenyewe kwa sauti na kuwastua watu waliokuwemo mle chumbani.Miongoni mwa watu waliokuwa wakifuatilia kwa karibu hali ya Happy ni mdogo wake Margreth .Alikuwepo pia mkurugenzi wa Miss Tanzania pamoja na watu wengine kadhaa.Mara tu waliposikia kuwa ameamka mkurugenzi wa Miss Tanzania alimwita daktari ambaye alikuja na kumpima.Baada ya vipimo vyote kuonyesha hakuna tatizo zaidi ya mstuko wa kawaida daktari alimuomba Happy aendelee kupumzika na asibughudhiwe.Daktari akawaomba wote waliokuwa pale Hospitali kwa ajili ya Happy waende kupumzika na kumwacha mgonjwa apumzike kwani bado alihitaji mapumziko ya kutosha.Ni margreth pekee ndiye aliyebaki ili kumsaidia dada yake.Baada ya watu wote kutawanyika Happy akageuza kichwa na kumwita margreth.


“my sister Pole sana”akasema Margreth


“I’m ok magie.” Akasema Happy


“happy what real happened? Akauliza tena Margreth.happy akanymaza akafikiri kidogo akasema


“ Magie I saw Patrick yesterday”


“Whaaaaat!!!!!!!!!!!!!!!!”akauliza margreth kwa mshangao mkubwa.


“ Patrick huyu huyu ambaye wote tunaamini amekufa..” akasema Happy


“ Parick is dead..yawezekana uliona mzuka wake” akasema margerth.


“Hapana Margreth haukuwa mzuka..Nilikuwa na akili zangu timamu wakati ninamuona patrick” akasema Happy.Margreth akainuka pale alipokuwa amekaa akamtazama dada yake na kusema


“ Happy hebu jaribu kumsahau Patrick..he’ll never come back..he’s gone forever” akasema margreth..akamtazamatena dada yake na kumuuliza


“Sister are you ok?...CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


“Sina tatizo magie ni kweli nilimuona Patrick jana wakati nikiongea na waandishi wa habari alikuja mbele yangu na kunisalimu .Alitaja maneno Fulani ambayo yalinifanya nistuke na nilipomtazama vizuri alikuwa ni yeye.Nina hakika ni yeye kwani ni mtu ambaye yuko moyoni mwangu kwa miaka mingi na kila siku ninaangalia picha yake hivyo siwezi kuwa nilimfananisha.Ninaamini nilimuona Patrick na ndio maana nikastuka hadi kupoteza fahamu.I’m confused Maggie .Totaly confused.”


Kimya kikatanda mle chumbani .


“Margreth tafadhali usije mweleza mtu yeyote juu ya habari hii.”


“Usijali sister siwezi sema”


“Sasa magie naomba unisaidie.”Akasema Happy .


“Nikusaidie nini Happy”


‘nataka kuonana na Patrick”Akasema Happy huku macho yake yamefunikwa na machozi.


“Pumzika kwanza sister ukitoka Hospitali tutaongea kwa undani juu ya suala hili.Kwa sasa bado unahitaji mapumziko ya kutosha na huhitaji kuwaza sana juu ya suala hili.”


“Thanks Maggie I understand “ Akajibu Happy.


mara mlango wa chumba alimolazwa Happy ukafunguliwa wakaingia wazazi wa Happy ambao walikuwa safarini lakini kutokana na matatizo aliyoyapata mtoto wao ikawabidi waahirishe safari yao na kurudi Tanzania haraka.mama yake akamkumbatia huku machozi yakiwatoka wote .baada ya kusalimiana Happy akawahakikishia kuwa kwa sasa alikuwa akijisikia mzima kabisa na pengine mchana wa siku hiyo angeruhusiwa kurudi nyumbani.


Wakiwa katika maongezi akaingia muuguzi akiwa na sinia la dawa.akawaomba radhi wote waliokuwa mle ndani kuwa alihitaji kumuhudumia mgonjwa hivyo akawaomba watoke nje kwa dakika kadhaa.Alipohakikisha wote wametoka akamkaribia Happy .


“Samahani dada Happy nina ujumbe wako ambao nimeambiwa ni wa muhimu na nyeti sana .Aliyenipa ujumbe huu amenionya kwamba nisikupe mahala penye watu .”


“Nani aliyekupa ujumbe huu?


“simfahamu ila ni kijana mmoja alikuwa amevaa suti nyeusi na hakujitambulisha jina lake .yeye alisema ukishausoma tu utakuwa umefahamu.”


Yule muuguzi akatoa bahasha toka katika mfuko wake wa koti na kumpatia.baada ya kumpatia dawa muuguzi yule alitoka na kumwacha Happy jasho likimtiririka.Hakujua ni nani aliyeleta ujumbe ule.


Aliishika bahasha ile na kuifungua taratibu.Ilikuwa ni kadi nzuri iliyomtakia uponaji wa haraka.Ndani ya kadi ile kikaanguka kikadi kidogo .Akakiokota na kukisoma.Nusura apatwe na wazimu baada ya kuisoma kadi ile.Margreth akaingia na akastuka sana kwa uso wa furaha aliokuwa nao Happy.


“Happy kuna nini?Mbona umefurahi namna hiyo? akauliza margreth kwa mshangao.


“Its Patrick”


“Patrick !!!!!!!!!!!!!!!”


“Yes .Look at this” akasema Happy akimuonyesha Margreth ile bussines card


“Mhhh”margreth akaguna


Wakati margreth akiisoma ile kadi mlango ukagongwa na likaingia kundi la warembo.wote wakafurahi baada ya kumkuta Happy ni mwenye furaha namna ile.


************************************************


MISS TANZANIA AZIMIA JUKWAANI,HAPPY KIBAHO MISS TANZANIA MPYA,ZENGWE LATAWALA UKUMBINI MISS TANZANIA AZIRAI,Hivyo vilikuwa ni baadhi ya vichwa vya habari vilivyotanda katika magazeti mengi kwa siku hiyo.Karibu magazeti yote yalijaribu kuandika kwa kina juu ya tukio la kupoteza fahamu kwa miss Tanzania ukumbini,lakini hakuna hata gazeti moja lililoweza kuandika au kuufahamu ukweli juu ya tukio lile.


Akiwa katika kibanda cha kuuzia magazeti asubuhi hiyo Andrew alinunua karibu kila gazeti lililotoka siku hiyo na kupitia habari ya Happy .Lengo lake kubwa ni kutaka kufahamu kama kuna mtu yeyote aliyeweza kumtilia shaka Patrick kuwa ndiye aliyekuwa chanzo cha tukio lile la kuanguka Happy ukumbini.katika magazeti yote hakukuta habari yoyote iliyomuhusisha Patrick na tukio lile.


Akatoa simu yake na kumpigia Patrick na simu ikapokelewa na Vero.


“Hallo shemeji” Akasema Andrew .


“Shemeji mambo vipi?habari za toka jana ?Andrew akauliza


“Habari nzuri tu shemeji”


“Vipi jamaa bado kalala?


“Ameingia maliwatoni kidogo anakuja sasa hivi”


Muda huo huo Patrick akatokea Vero akampa simu na kumwambia Andrew anahitaji kuongea naye.


“Hallow Andrew habari za asubuhi ndugu yangu” Akasema Patrick


“Poa Patrick vipi maendeleo yako?


“Nashukuru Mungu Andrew naendelea vizuri.Hebu nipe habari’


“Habari ni ndefu kidogo lakini kwa ufupi tu ni kwamba leo sijalala kabisa.baada ya kuachana pale ukumbini nikamrudisha Vick kwake halafu nikaanza kufuatilia Happy alipelekwa hospitali gani.Kwa msaada wa rafiki yangu mmoja nilifanikiwa kujua mahala Happy alikopelekwa.Unajua walificha juu ya hospitali alikopelekwa kwa sababu ya kuwakwepa waandishi wa habari.Alikuwa amepelekwa katika hospitali moja ya kanisa maeneo ya msasani.Mpaka saa kumi na mbili nilikuwa pale hospitali na ndipo nilipopata taarifa kuwa tayari Happy alikuwa amezinduka.Kuna muuguzi mmoja anafahamiana na Vick pale na ndiye huyo aliyenipa msaada mkubwa sana.Nilimpa kiasi Fulani cha pesa yule muuguzi na kumuomba aipeleke business card yako kwa Happy na kumwambia apige namba zile zilizoandikwa katika business card hasa muda wa mchana.Yule muuguzi akajitahidi na kuifikisha kadi ile .Baada ya kuhakikisha tayari ameipata mimi nikaondoka.Kabla sijafika nyumbani nikaona nipite kwanza katika kibanda cha magazeti ili nione magazeti yanasema nini lakini hakuna chochote kibaya.Kwa hiyo Patrick nina imani muda wowote Happy anaweza akakupigia simu.Mimi kwa sasa nakwenda nyumbani kupumzika tutaonana baadae ila be carefull brother’


Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akasema


“Sijui hata nikushukuruje Andrew kwa kitu ulichokifanya ila nasema thanks a lot.Dont worry I’ll be careful.Bye see you later”


Patrick akakata simu kisha akaelekea jikoni ambako Vero alikuwa akiandaa stafstahi .alianza kumsaidia Vero kuandaa mlo wa asubuhi kitendo ambacho Vero alikifurahia sana nakuamini tayari Patrick alikuwa amerudia hali yake ya kawaida.


*******************************


Saa sita kamili mchana Happy akaruhusiwa kutoka hospitali.akiwa na furaha isiyokifani huku ameongozana na mama yake pamoja na mdogo wake kipenzi Margreth bila kumsahau mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania akiwa na wajumbe kadhaa wa kamati hiyo pamoja na ujumbe wa watu toka sean woris entertainment ambao ndio wadhamini wakuu wa mashindano hayo walilakiwa na kundi kubwa la warembo waliokuwa wakisubiri atoke kwani walikwisha taarifiwa kuwa angeruhusiwa mchana.Walitumia kama robo saa kusalimiana na kupongezana vile vile kupeana pole kwa yaliyotokea. Kisha akapanda gari na kuelekea nyumbani kwao.Happy alikuwa ni mwenye furaha sana mchana huo.Ni margreth pekee ndiye aliyefahamu siri ya furaha ile aliyokuwa nayo dada yake.akiwa garini Happy akafumba macho kana kwamba amelala lakini alikuwa amezama katika mawazo na mara akajikuta akitamka kwa sauti.


‘Thanks God I found him’CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


mama yake aliyekaa kiti cha mbele aligeuka na kumuangalia mwanae bila kusema kitu.


Margreth yeye alikuwa katika lindi la mawazo na hasa akijaribu kuvuta taswira ya kinachoenda kutokea huko mbeleni.Anafahamu wazi kuwa katika dunia hii Patrick ndiye mwanaume pekee ambaye Happy anampenda .Licha ya kupotezana kwa muda mrefu lakini bado taswira ya Patrick haikufutika moyoni mwake.Kwa sasa Happy tayari ana pete ya uchumba ambayo amevishwa na mchumba wake ambaye ni mmarekani mweusi aitwaye Mike cambel anayefanya kazi katika ubalozi wa Marekani hapa nchini.Mike ni kijana anayependwa sana na kila mtu katika familia ya akina Happy .Pamoja na kuwa na pete ya uchumba kidoleni bado Happy ameshindwa kuifuta kabisa kumbukumbu ya Patrick moyoni mwake.Kuonekana kwa Patrick ni wazi kunaweza kusababisha mvurugano mkubwa ambao ni ngumu kujua hatma yake.Ni wazi Mike alikuwa akimpenda Happy kupita maelezo.Hiki ni kitu kilichomuumiza sana kichwa Margreth.


Baada ya mzunguko mrefu hatimaye wakawasili nyumbani ambako walilakiwa na kundi jingine la warembo,ndugu jamaa marafiki na waandishi wa habari wote walifika kumpongeza na kumpa pole Happy .Kisha salimiana na kupongezana Happy akaomba aachwe kidogo apumzike.


Happy akaoga na kupata chakula kisha akaingia chumbani kwake kupumzika.Kitu cha kwanza kabisa ambacho alikifanya ni kuitazama tena ile business card kwa makini .akaichukua simu yake na kuandika namba zile zilizoandikwa pale juu kisha akapiga.Mapigo ya moyo wake yalikuwa yakienda kwa kasi ya aina yake.Mikono ilianza kuloa jasho kwa wasi wasi.Hakujua angeongea nini baada ya kuisikia sauti ya Patrick.Hakujua Patrick angekuwa katika hali gani mara atakapoisikia sauti yake.Wakati akisuburi kujibiwa na sauti ambayo aliamini moja kwa moja ingekuwa ni ya Patrick akasikia kitu ambacho hakukitarajia.Ilikuwa ni sauti ya mwanamke ndiye aliyepokea simu ile ya Parick.


“hallow”Ilita sauti ya upande wa pili.


Happy mikono ilimtetemeka,akapatwa na kigugumizi cha ghafla kilichomfanya ashindwe kuongea.


“hallow nakusikia”Iliuliza tena ile sauti ya mwanamke.


Happy akashindwa ajibu nini akabaki ameiweka simu sikioni.


“Haloo nani mwenzangu?Iliuliza tena..Tayari Happy chozi lilikuwa likimtoka.Mara akasikia simu ikikatwa.Kitendo kile kikamuuma akajitupa kitandani machozi yakimtoka.


“Oooh Lord why me???Why me God?I love Patrick .Yes ni yeye tu ndiye mwanaume ninayempenda kwa dhati ya moyo wangu .Nimetengana naye muda mrefu sana na sielewi maisha yake kwa sasa.nadhani anaweza kuwa na mke au girlfriend.Sielewi kama ninaweza vumilia nikisikia Patrick anamke.I’m her only girl.Yes I know that.I know he loves me very much.’


Happy alikuwa kijisemea peke yake kwa sauti ndogo


“Patrick I’ll fight for you and I must win you back.You are mine Patrick .I lost you once and now I’ve found you I’ll never loose you again”


Happy alikuwa akiongea peke yake maneno haya huku machozi yakimchuruzika.


Patrick leo huamki?alisema Vero huku akimtingisha Patrick ambaye alikuwa amelala tangu alipokula chakula cha mchana.Patrick akajigeuza na kuangalia saa kubwa ya ukutani.Ilionyesha ni saa kumi na moja jioni.


“Oh nimelala sana”


“Ni vizuri hata hivyo ukipata mapumziko ya kutosha”


Happy akaelekea jikoni akaleta juice na kummiminia Patrick katika glasi.


“Halafu nimekumbuka kuna mtu alikupigia simu nikaipokea lakini cha ajabu hakutaka kuongea kitu chochote .Nimemuuliza zaidi ya mara mbili yeye ni nani lakini hakunijibu.”


Patrick moyo ukamruka.Kijasho kikaanza kumtoka .akaichukua simu na kuziangalia namba zilikuwa ni ngeni kabisa kwake.Hakufahamu zilikuwa ni namba za nani lakini akahisi huenda Happy ndiye aliyepiga.Kwa mujibu wa maelezo ya Andrew ni kwamba alimuelekeza Happy apige mida ya mchana.Bila kukawia akaipiga ile namba.Simu ikailiita sana bila kupokelewa,ikakatika.Akapiga tena mambo yakawa ni yale yale.Akapiga kwa mara ya tatu simu ikapokelewa.


“Hallow”Ilikuwa ni sauti tamu sana ya mtoto wa kike.kabla Patrick hajaongea lolote simu ikakatika.Patrick akaipiga tena na safari hii akaambiwa kuwa simu anayopiga haipatikani.


Patrick akaitupa simu kitandani kwa hasira .Hakuelewa sababu ya kukatiwa simu na mwanamke yule na mbaya zaidi kuizima kabisa.alisimama na kuzunguka zunguka humo chumbani huku Vero akimwangalia.Alisahau kama Vero alikuwa karibu yake .Vero ambaye muda wote alikuwa akimtazama alipatwa na wasiwasi.


“Patrick dear kuna kitu gani kibaya mbona umebadilika hivyo?


Patrick akastuka na kujilaumu sana kwa kuonyesha hali ile mbele ya Happy .


“Ah No darling hata mimi nashangaa huyu mtu sijui ni nani ananipigia simu haongei,mimi nikimpigia anakata simu na kuizima kabisa.Mbona ananipa wasiwasi?


“Basi usijali darl unajua kuna wakati mtu anaweza akakosea namba na akajikuta akimpigia mtu mwingine bila ya yeye kujua.Nadhani hata huyu alikosea namba na ndio maana akaona hakuna sababu ya kuongea na wewe kwani hauna umuhimu kwake.”


“hata mimi nafikiri hivyo”akajibu Patrick.


“Relax my dear achana naye huyo asikusuumize akili bure .kaa bwana tupange mipango ya harusi yetu.”


Patrick akastuka kwa ndani baada ya kuiskia habari ile ya harusi.lakini alijitahidi ili Vero asiweze kuuona mstuko ule.Jasho lilikuwa likimtoka.




MALANGALI SECONDARI -IRINGA


Ni ijumaa iliyotawaliwa na kiubaridi cha asubuhi.Hakukuwa na dalili zozote za kuchomoza kwa jua ingawa mida hiyo ilipata saa nne za asubuhi.Anga lote lilikuwa limefunkwa na mawingu.Pamoja na hali hii lakini shughuli ziliendelea kama kawaida.Kwa watu wa eneo hili hali hii walikwisha izoea.


Saa nne na dakika kumi basi moja linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Iringa lilifunga breki katika kijiji cha Mbalamaziwa.Dakika kama mbili hivi tangu basi lile lisimame kijana mmoja akashuka akiwa na mabegi matatu.Ilionyesha dhahiri kuwa kijana yule alikuwa mwanafunzi.Baada ya kuhakikisha kuwa mizigo yake yote iko salama basi likaondoka na kumwacha kijana yule akiangaza angaza macho kana kwamba kuna kitu alikuwa akikitafuta.Muda ule ule jamaa mmmoja akamfuata.


“Vipi dogo unaelekea Malangali?


“Yes brother “


“Ok gari ile pale ya kuondoka .Tunaondoka sasa hivi likijaa.”


Jamaa yule kumbe alikuwa ni dereva.Akamsaidia kubeba mizigo yake hadi katika gari dogo aina ya Toyota pick up.Kutoka hapo Mabalamaziwa hadi kijiji cha Malangali usafiri unaotumika ni huu wa gari ndogo.Gari lile halikuwa na abiria yeyote ndani zaidi ya mizigo.


“ mbona hakuna abiria yeyote humu?”Akauliza kijana yule


“Usijali dogo watu wapo si unaona mizigo yao hiyo hapo.We utaona nikipiga honi tu watakuja.Si unawaona wale wote ni abiria wengine wanakunywa chai kule na muda wa kuondoka ukifika basi watakuja..Unaweza kwenda kupumzika pale kwa yule dada naye ni mwanafunzi anaelekea huko huko Malangali wakati tunasubiri watu wawili watatu”


Katika kibanda kimoja kilichokuwa hakitumiki msichana mmoja alikuwa amekaa akisoma kitabu chake cha hadithi.Alikuwa amekiinamia kitabu hali iliyoonyesha kuwa alikuwa amenogewa sana na kilichoandikwa kitabuni.


“Dada habari yako” Dada yule alistuliwa na sauti ya kijana yule .Kwa sekunde kadhaa alikaa kimya akimtazama yule kaka .Sijui ni kwa nini alifanya vile lakini ni wazi alionyesha mstuko Fulani.


“Nzuri habari yako?akajibu kwa sauti laini na y a taratibu sana.Sauti ile ilionyesha kuwa dada yule hakuhitaji sana kusumbuliwa kwa wakati ule kwani baada tu ya kuitikia salamu ile akainama na kuendelea kusoma kitabu chake.Akiwa pembeni yake alimtazama yule dada kwa sekunde kadhaa na kugundua ni kwa nini alikuwa vile.Dada yule alikuwa na uzuri wa kipekee.Alikuwa mweupe ,mwenye nywele ndefu zilizorudishwa nyuma vizuri na kumfanya avutie zaidi.Alikuwa ni mwembamba na mrefu wastani.Binti huyu alijaaliwa sura nzuri yenye uzuri wa kipekee.


“Mhh basi hii shule ninayoenda kusoma si mchezo.Kama kuna watoto wazuri kama huyu.halafu ana nyodo kweli lakini ngoja nimuulize maswali mawili matatu akikataa kunijibu basi nitaachana naye .”akawaza yule kijana


“dada samahani nimeambiwa na yule dereva wa lile gari kuwa na wewe unaelekea malangali .Na wewe ni mwanafunzi pale?


Dada yule akainua uso wake na kumtazama yule kijana kama alivyofanya mwanzo.


“Ndiyo kwani vipi?akauliza


“ nilitaka tu kufahamu kwa sababu mimi ni mgeni pale ndio mara yangu ya kwanza nafika huku hivyo nilikuwa nahitaji kuyafahamu mazingira ya shule yenyewe kabla hata sijafika”


dada yule akamtazama tena .Macho ya binti huyu yalikuwa meupe na makali kiasi kwamba unaweza ukakwepesha macho yako asikuangalie.


“Wewe unatokea wapi?


“Natokea Mazwi secondary Sumbawanga”


“Uko kidato cha ngapi?Akauliza tena yule binti


“Kidato cha tatu”akajibu yule kijana


“hata mimi niko kidato cha tatu”Akajibu yule dada.


“Kumbe tuko kidato kimoja?”


“Yeah .Ila pale kuna michepuo.Mimi niko arts na wewe?


“hata mimi niko arts.Vipi unaonaje ufundishaji wao? Akauliza kijana yule nadhifu


“wanajitahidi kufundisha.Kumetulia na ni sehemu nzuri kwa kusoma.Mi napapenda sana”akajibu yule binti


“aisee kumbe nilifanya chaguo zuri”


‘hata mimi mwanzoni nilidhani kuwa nilikosea kuhamia shule hii .Mwanzoni nilipata shida sana kuzoea lakini mpaka sasa nimeshazoea”Akajibu yule dada


“Kumbe hata wewe ulihamia?Yule kijana akauliza


“Yes .Nilikuwa nasoma Mbeya secondary nikahamia huku.Sikutaka kusoma mjini nilitaka kusoma mahala tulivu kama huku”


“Umehamia mwaka huu?


“Hapana toka mwaka jana”


Walikwisha anza kuzoeana.Binti yle kumbe alikuwa mcheshi na muongeaji mzuri.Kwa upande wake alifurahia sana uchangamfu wa yule kijana.


“lakini kwa ujumla unaniambiaje kuhusu mazingira ?kijana yule akauliza.


“mazingira siyo mabaya.Mabweni yapo mazuri kwa ajili ya wavulana .Sisi wasichana tunalala hosteli.Ni hosteli nzuri ya kanisa.Wale wasiopenda kulala hosteli wanapanga vyumba kijijini.Maisha ni mazuri ukisha zoea ila kwa wewe nadhani utapata shida kidogo mwanzoni.” Akasema huku akicheka.


“kwa nini nipate shida?akauliza kijana yule.


“hahhahaha! Basi tu kwa muonekano wako unaonekana hujazoea shida”akasema huku akicheka.


Kijana yule naye akacheka sana kisha akasema


“sasa mimi na wewe nani anayeonekana hajazoea shida?


“hahahaha ! hata mimi mwanzoni nilipata shida sana lakini kwa kiasi Fulani kwa sasa nimeshaanza kuizoea hali halisi ya mazingira”


Kimya kikapita cha kama dakika mbili hivi kila mmoja akiwaza lake.Yule kijana akauvunja ukimya.


“Kwani wewe dada waitwa nani?


Binti yule akatabasamu kisha kama anajishauri vile aseme au asiseme akajikuta akitamka


“naitwa Happy .Wewe je waitwa nani?


“Mimi naitwa Patrick ”


“Happy nimefurahi sana kukufahamu.Na kama hutajali nitafurahi ikiwa utakuwa mwenyeji wangu”


“Hilo tu usijali.Nitakufundisha jinsi ya kunywa uji na maandazi ya ulanzi”


Wote wakacheka.


“Ulanzi upi”Mbona nasikia ulanzi ni pombe?


“Yes ni pombe tena kule iko nyingi sana ”


“aisee kumbe maisha mazuri huko”


“hahaha “Happy akacheka.


“Kwani Happy sasa hivi umetoka wapi? Patrick akauliza.


“Nilikuwa na ruhusa ya wiki moja.Nilikuwa nimeenda nyumbani mara moja nilikuwa na matatizo kidogo na leo ndio narudi shuleni.Twende pale kibandani tukapate chai unajua niliondoka asubuhi bila hata kunywa chai” Happy akasemaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Wakainuka pale kibandani walikokuwa wamekaa na kuelekea katika moja ya vibanda vinavyouza chai .


*********************************


“Haya wale wanafunzi wa Malangali tumefika.”


Alisema utingo wa lile gari walimokuwa wamepanda akina Patrick.Yeye na Happy wallikuwa wanafunzi pekee katika ile gari.


Mida hiyo ilipata saa saba za mchana.safari ilikuwa ni ndefu kidogo hasa kutokana na barabara .


‘Patrick tushuke”Akasema Happy akiwa wa kwanza kushuka kisha akaanza kupokea mizigo ya Patrick. Happy akatoa pesa na kumlipa yule utingo .


“kata nauli ya watu wawili”


“No Happy nina nauli yangu hapa”akasema Patrick


“Usijali Patrick just keep it”akasema Happy huu akitabasamu.


Abiria wote waliokuwamo katika ile gari macho yao yote yalikuwa kwa binti huyu mrembo.Kwa muonekano wake alionyesha dhahiri kuwa alitoka katika familia yenye uwezo mkubwa kimaisha.wote walistaajabia uzuri wa binti huyu.


“Poa mrembo karibu tena siku nyingine”


alisema utingo huku akimminyia Happy jicho moja.


Baada ya gari ile kutimua vumbi na kuondoka Patrick akageuza shingo na kutazama majengo ya shule.Idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa katika mapumziko ya mchana walikuwa wamesimama wakiwaangalia .Patrick alishangaa kidogo kwa namna walivyokuwa wakiangaliwa.Taratibu akaanza kujiuliza maswali juu ya kuangaliwa kule.Je ni kwa sababu alikuwa na Happy ?Au ni kawaida kwa mwanafunzi mgeni kuangaliwa namna ile?


“Patrick beba begi hilo mimi ngoja nikusaidie hili hapa.”akasema Happy na kumstua Patrick


“Wow thanks Happy lakini utaweza kulibeba hilo ni zito sana.Beba hili dogo.”


Wakabeba mabegi yale na kuanza kuelekea katika ofisi za shule.Ili kufika ofisini ni lazima upite katikati ya shule.Bado wanafunzi walikuwa wakiwaangalia na wengine wakisemezana.Kitendo hiki cha wanafunzi kuwaangalia kisha kuanza kusemezana wao kwa wao kilimzidishia Patrick ushawishi wa kutaka kufahamu kulikoni.


“Happy mbona wanafunzi wanatuangalia sana ?


“Just ignore them”akasema Happy kwa kifupi.


Wakafika katika ofisi za shule mizigo ikawekwa chini.


“Hapa ndio ofisi ya mkuu wa shule msaidizi .Ingia ndani ye ndiye atakayekusajili na kukupa maelekezo yote.Bye tutaonana baadae pengine tunaweza kuwa darasa moja’akasema Happy huku akichanua tabasamu pana na kuyaonyesha meno yake meupe na mwanya wa kupendeza katika meno ya juu.


“Nashukuru sana Happy tutaonana baadae”


Happy akaondoka .Patrick akagonga mlango na kuruhusiwa kuingia.


“Welcome gentleman.where are you from?Ilikuwa ni sauti ya ukakamavu ya mtu ambaye Patrick aliamini moja kwa moja kuwa ndiye alikuwa mkuu wa shule msaidizi.


“From Mazwi secondary school”Patrick akajibu.


“Ohh Mazwi!How is Mr Yamsebo?


“He’s ok”


Patrick akasajiliwa kisha mwali yule akatoka nje na kumwita mwanafunzi mmoja na kumuomba ampeleke Patrick katika bweni la Shaaban Robert.Mwanafunzi yule akamsaidia mizigo na kuelekea katika bweni hilo lililo upande wa juu kabisa wa shule hii.


Pale bwenini akapata kitanda kilichokuwa wazi akaweka mizigo yake.alijilaza kitandani huku akijaribu kuwaza jinsi atakavyoweza kuyakabili maisha mapya ya shuleni pale..Hakuwahi kusoma katika shule ya bweni na hii ilikuwa mara yake ya kwanza.


“lakini Happy yupo atanisaidia kuyazoea.Kama yeye mtoto wa kike amezoea sembuse mimi ?Ntazoea tu.Halafu shule hii inaonekana ina wanafunzi washamba sana kwa nini walikuwa wakituangalia vile wakati tumeshuka mchana.Au mimi ninaonekana mtu wa ajabu sana?”


Mawazo haya yakastuliwa na sauti ya mwanafunzi mmoja aliyeingia bwenini humo kwa kelele.Akamsogelea Patrick na kumsalimu kisha akaelekea katika kitanda chake kupumzika.


***************************


Mida ya kama saa kumi na moja jioni Patrick akaamua kuzunguka zunguka maeneo ya hapo shuleni.Ilikuwa ni mwishoni mwa wiki hivyo kulikuwa na pilika pilika nyingi.Ni wanafunzi wachache tu waliokuwamo madarasani jioni hii wakijisomea.


Alipofika katika bwalo la chakula akamuuliza mwanafunzi mmoja yalipo madarasa ya kidato cha tatu .alitaka kwenda kuyatembelea na kuangalia mahala atakapo kuwa akisomea.


Yalikuwa ni madarsa yaliyofuatana.Yaani kidato cha tatu A B na C.Yeye alikuwa amepangiwa kusoma kidato cha tatu C.Akayapita madarasa ya A na B akAelekea katika darasa la C .Mlango haukuwa umefungwa akingia ndani na mara macho yake yakagongana na macho ya Happy .


“Happy ”akaita Patrick


“Patrick!Naona umeshaanza kukata mitaa”


Patrick akacheka.


“Enhee hebu niambie unaendelaje?Vipi umeshaanza kuzoea?Umepangiwa bweni gani?”


Happy akauliza maswali mfululizo huku akifunika vitabu vyake.


“Nimepangiwa bweni la ShaAbani Robert na darasa ni hili hili C”


Happy akatoa tabasamu pana sana.


“karibu sana hata mimi ninasoma humu humu.”


“nafurahi sana kufahamu kuwa tutakuwa wote darasani.Vipi mbona uko hapa peke yako?


“Nimeamua tu kuja kukaa huku kwa sababu kule hosteli ninaboreka sana.Mara nyingi hupenda kuja huku kujisomea mwenyewe.sipendi kelele.”


“nimeambiwa kuwa kuna maktaba huku “Patrick akauliza.


“Yes ipo lakini mimi sipendi kwenda mara nyingi huwa nakuja huku darasani.Sipendi kusoma na watu wengi.Patrick naomba tuwe tukisoma wote”


Patrick akatabasamu kisha akasema.


“Usijali Happy tutasoma wote tena nimekuja na materials ya kutosha”


waliongea mpaka ikafika mida ya saa kumi na mbili Happy akaomba Patrick amsindikize kurudi hosteli kwao.Bila hiyana Patrick akakubali.wakatoka wote darasani wakaanza kupanda kilima kuelekea hosteli ya akina Happy .Kila mwanafunzi waliyekutana naye alikuwa akiwatazama.Patrick akaamua kumuuliza Happy


“Happy mbona kila mtu tukikutana naye anatuangalia sana kwa nini?Toka tumefika mchana naona watu wakitushangaa mno !!


Happy akatabasamu kisha akajibu


“Achana nao hao.Patrick ,Jali mambo yako.Kamwe usiwasikilize wanafunzi wa hapa wana mambo ya kipuuzi sana.Unajua wakiona mtu mgeni sijui wanakuwaje.wewe ukitaka kuishi kwa amani mahala hapa jitahidi kufuata kilie kilichokuleta yaani masomo”


Happy akajibu kwa sauti ambayo haikuwa ile yake ya kawaida.Patrick hakutaka kuuliza tena kuhusu suala hilo.


“Patrick kesho jumamosi kuna mnada hapo kijiji cha mbele vipi ungependa kwenda?


“Yes ni vizuri kama nikienda ili nianze kuyazoea mazingira”


“Ok nitakupitia basi mida ya saa tano ili tukashinde huko mpaka jioni huwa ni pazuri sana.Unajua weekend hapa shuleni panakuwa kimya mno.Halafu kama utapenda jumapili tutaenda sehemu moja inaitwa stone beach.Ni pazuri pia.Mi huwa napenda kwenda kutulia kule siku kama hizi za weekend.”


“Wow usijali Happy tutakwenda”CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Hatua chache mbele yao wakaliona geti la kuelekea hosteli ya wasichana wakaagana na Patrick akarejea bwenini.


Saa nne na nusu asubuhi siku iliyofuata alikuja mpishi katika bweni alilokuwa akilala Patrick na kuanza kumuulizia.


“wewe ndio Patrick? akauliza mzee yule wa makamo baada ya Patrick kujitokeza.


“Yes ndio mimi”Ptrick akajibu


“Nimeagiziwa na binti mmoja anaitwa Happy kuwa anahitaji kukuona sasa hivi .Panda na barabara utamkuta pale mbele karibu na kanisa anakusubiri.”


“Ok mzee nashukuru”


Mzee yule akaondoka kisha Patrick akavaa viatu vyake akaondoka kuelekea mahala alipoagiziwa na Happy .siku hii alikuwa amependeza vilivyo.alikuwa amevaa kaptura ya jeans rangi nyeupe,juu akavaa fulana nzuri yenye mistari ya kijani na nyeupe halafu akavaa na mkufu wake wa dhahabu uliomfanya avutie zaidi.Chini akavaa raba nzuri nyeupe na soksi nzuri .Mwisho kabisa akajipulizia uturi wenye harufu nzuri .Kwa ujumla alikuwa amependeza sana kijana huyu.Wakati akitoka alisikia baadhi ya wanafunzi waliokuwa hapo bwenini wakifanya usafi wakinong’onezana.


“alaaa kumbe ndo huyu”


“Du ! bonge la brother lakini maskini .haelewi “akadakia mwingine.


Patrick hakutilia maanani sana minong’ono ile akawapuuza na kuondoka zake.Alitamani sana kuonana na Happy kwani aliamini ni yeye tu ndiye anayeweza kumfanya akazoea mazingira yale magumu.Tangu amewasili bado hajapata rafiki wa karibu kama Happy .


Kwa mbali alimuona Happy amekaa chini ya mti amejiinamia.Moyo ukafurahi baada ya kumuona tena binti yule mrembo.Kwa mbali tu aliweza kutambua utofauti katika muonekano wa Happy .


“Hi Happy mambo vipi ”


“Poa tu Patrick Vipi mzima? Akasema Happy halafu akainua macho


Patrick akastuka kisha akauliza


“Happy kulikoni mbona macho mekundu na inaonyesha ulikuwa ukilia.Unaumwa?


Happy akanyamaza na kuanza kulia kwa kwikwi.Patrick akajua lazima kuna kitu kimemsibu binti yule.akatoa kitambaa na kumpatia


“Chukua hii futa machozi”


Happy akachukua kitambaa kile na kufuta machozi.


“Niambie Happy kitu gani kimekusibu mpaka ukawa katika hali hii?


“Patrick naona nitashindwa.”


“kwani kuna nini Happy ?.Niambie kama una tatizo ili tuone kama tunaweza kulitatua.”


“Patrick nakwambia hapa shuleni mimi nina matatizo makubwa.Yaani wenzangu wananichukia sana sijui hata nimewakosea kitu gani.Mara waseme eti mimi ninaringa ,wanasema eti ninajifanya nina pesa nyingi,eti ninajifanya mtoto wa tajiri,ndio maana wamenitenga na hakuna mtu anayetaka hata kushirikiana nami kitu chochote.Hata kusoma huwa nasoma peke yangu.Kwa hivi sasa shule nzima wanajua eti mimi nina ukimwi.Habari hizo zimesambaa kila mahala na hii ndio imenifanya nikose hata rafiki.Mimi silijali hilo kwa sababu ninafahamu mimi mwenyewe kuwa mambo hayo si ya kweli.Hata baadhi ya walimu wanaamini hivyo .Kuna siku walikuja watu wa afya na kuwataka watu wapime afya zao na karibu wanafunzi wote wakapima kasoro mimi.Nilikataa kupima kwa sababu nimekwisha pima toka huko nilikotoka na zaidi ya yote ninajiamini mimi mwenyewe kuwa sina.Kwa kipindi hicho walichokuja kupima watu nilikuwa ninasumbuliwa na kifua basi baada ya kukataa kupima afya , ikawadhihirishia watu kuwa ni kweli nina ugonjwa huo.Mimi sioni ajabu kwa sababu hata huko nilikotokea mambo haya yalinikuta na ndiyo sababu kubwa iliyonifanya nihame.Huku nako nikakuta mambo ni kama yale yale .Nilipata taabu mwanzoni lakini ikafika mahala nikazoea.Nimejaribu kuwa wazi kuwa mimi sisumbuliwi na ugonjwa huo wanaodai ninao lakini hakuna anayeniamini na hasa ukichukulia huu mwili wangu jinsi ulivyo basi kila mtu anajua ninaumwa.Namshukuru Mungu kwa sababu kwa sasa nimekwisha pona lakini hakuna mtu anayetaka hata kuchangamana nami.Pale tulipokutana nilikuwa nimetoka tena kufanya vipimo ili kujua kama ugonjwa ule wa kifua ulionisumbua kwa muda mrefu umekwisha kabisa au vipi.na kwa bahati nzuri madaktari wakanithibitishia kuwa tayari nimepona .Wewe mwenyewe jana uliona wanafunzi walivyokuwa wakituangalia wakati nakusindikiza kule ofisini.wote walikuwa wanakusikitikia wewe.”


Happy akanyamaza na kufuta machozi yaliyokuwa yakitoka.Patrick akawa kimya kabisa kumsikiliza.Kijasho kilikuwa kikimtiririka.


“Kibaya zaidi ni leo asubuhi.Nilikuwa nimeenda kuoga nikasahau kufunga sanduku langu .Niliporudi nikakuta pesa zangu zote karibu laki moja na ishirini na tatu elfu hazipo.Nimejaribu kuuliza lakini hakuna mtu yeyote anayejua zimeenda wapi.Ninaelewa hizi ni njama za wazi za watu wasionipenda.”


Patrick akavuta pumzi ndefu na kumwangalia Happy kwa makini .alimuonea huruma sana binti yule kwa matatizo anayoyapata.Sasa alipata jibu kwa nini wale wanafunzi walikuwa wakimwangalia sana na hata kusemezana wao kwa wao kila walipomuona yuko na Happy .Roho ikamuuma kumuona binti mrembo kama yule akitoa machozi.Ni wazi hakustahili kufanywa vile hata kama angekuwa ameathirika kama wanafunzi hao wanavyodai..


“Hawa watu wa namna gani ambao wanawafanya wenzao namna hii?Hivi ndio tunavyofundishwa kuhusu mapendo kwa wenzetu?no !! kama wao wako hivi mimi sijafundishwa namna hii.Wazazi wangu wamenifundisha kuwa na upendo kwa watu wote.Lazima nionyeshe mfano kwa watu hawa na nitaanzia kwa Happy ”Aliwaza Patrick akiwa na fundo la hasira moyoni.


Taratibu akamuinamia Happy na kumshika mikono.akamwangalia usoni kwa sekunde kadhaa kisha akasema.


“Happy usijali ,nyamaza kulia I’m here for you.I’ll be on your side.Hutalia tena.Hata kama dunia nzima itakutenga na kusimama mbali nawe I’ll be there for you.Hata kama ungekuwa na maradhi hayo wanayosema unayo nisingeweza kukutenga.”


Happy akapatwa na furaha ya ghafla baada ya kuambiwa maneno yale akainuka na kumkumbatia Patrick kwa nguvu.


“Thanks very much Patrick.Nadhani ni Mungu kakuleta ili uweze kunipa faraja.baba alitaka kunihamisha na kunipeleka mbali lakini nilikataa kwa sababu nayapenda mazingira haya ya huku.Napenda sana kuwa katika sehemu tulivu kama hii.sikujua kumbe kuna mtu ana kuja ambaye atakuwa ni faraja yangu.”


Alisema Happy huku machozi yakimtoka.hakuamini kwa mazingira yale kama kuna mtu angeweza kumtamkia maneno ya faraja kama yale.


“Usijali Happy .Hutalia tena.Usijali kuhusu pesa zako kupotea.kama ilikuwa ni njama zao basi wameshindwa.Mimi bado nina kiasi cha kutosha cha pesa nitakugawia na kiasi kitakachobaki tutaendelea kukitumia taratibu.Usijali you are more than a friend to me.To me you are like my sister.”


“Thanks Patrick.You are more than a brother to me”akasema Happy


‘Thanks. vipi kuhusu ile safari yetu ya mnadani bado ipo au ndio umeshaifuta? Patrick akauliza


“Mimi nilikuwa nimeshaifuta kwa sababu hata kama ningeenda huko ningenunua vitu na nini?wamechukua pesa zote.”


“Pole sana.sasa hebu nisubiri kidogo hapa nakuja sasa hivi”


Patrick akamwacha Happy pale na kutembea kwa kasi kurudi bwenini..akafungua sanduku lake kubwa na kutoa bahasha Fulani aliyokuwa ameificha .akaiweka mfukoni akafunga sanduku lake na kuondoka kurudi kule alikomwacha Happy .


“Happy chukua hii ni laki moja na nusu itakusaidia ila kuwa makini sana wasije wakakuibia tena siku nyingine.”akasema Patrick wakati akihesabu pesa toka katika ile bahasha aliyokwenda kuichukua kule bwenini.Happy hakuamini macho yake.hakuamini kama katika dunia hii bado kuna watu wenye moyo wa huruma kama wa Patrick.


“wow jamani Patrick Naomba kidogo tu sasa ukinipa hizi zote na wewe je utabakiwa na nini?


“Usijali Happy bado nina akiba ya kutosha”Patrick akajibu


“No Patrick siwezi kuchukua zote.”


“Happy kumbuka ulikuwa ukilia kwa kuibiwa na sasa narudisha kiasi kile kilichokuwa kimeibiwa ili ufute kabisa suala hilo moyoni mwako”


Happy akapokea pesa zile.


“nashindwa hata kupata neno la kukukushukuru litakalokufaa Patrick.Thanks very much “


“It’s nothing”Patrick akasema kisha kikapita kimya kifupi.


“Patrick thanks again unajua nilikuwa nawaza sana jinsi ya kumwambia daddy kuwa nimeibiwa kwa sababu si mara ya kwanza na mwambia hivyo ananitumia pesa Ila kwa sasa sijui ningesemaje.You are my angel.”

INAENDELEA....
Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top