mtu alionekana kuwa bize na mambo yake, kuanzia Mama, Baba na watoto, muda mwingi nilibaki peke yangu nyumbani.
Mzee Gidion aliitumia nafasi hiyo kuwa fursa ya kuwa karibu na mimi. Aliamua kuninunulia simu kwa lengo la mawasiliano, alihitaji kuwasiliana na mimi zaidi na zaidi.
Siku ziliendelea kukatika huku penzi kati yangu na Mzee Gidion likizidi kupamba moto. Alipanga kuninunulia nyumba pamoja na gari la kifahari kwa dhumuni la kunihamisha nyumbani hapo, hakutaka kuona mapenzi yetu yakiendelea kuwa siri, alinogewa na utamu wa penzi langu.
Nilijisikia furaha sana kusikia hivyo, niliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kusahau umasikini niliyotoka nao nyumbani kwetu Mtwara.
Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kiliniweka katika wakati wa furaha sana, nilizidi kumpenda Mzee Gidion, nilisahau kama alikuwa ni mume wa mwanamke aliyenitoa kijijini na kunileta mjini kwa lengo la kufanya kazi, ahadi nilizowaahidi wazazi wangu pamoja na kiapo nilichokiapa mbele yao kwa wakati huo nilikuwa nipo kinyume kabisa.
INAENDELEAAA......
