MADAM WA TUTION - Sehemu ya 13

Simulizi master
0



😘😘😜🥰😍
Page Bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082


Siku hio nzima nilikuwa namawazo, na nilikuwa na practical ya upasuaji pale chuoni nikabidi niombe udhuru, nisije nikafanya mambo ya ajabu, kwa maana kichwa hakikuwa sawa, mpaka wakat huo sikuwa najua nitamuambia nn dhahara mpaka anielewe, niliwaza sana, sasa nina rafiki yangu mmoja ambae alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana, alikuwa anaona hustle zangu kwa madam dhahara, nikaenda kumuomba ushauri, wa nini nifanye kwa maana nilikuwa nahisi nimechanganyikiwa, alianza kunicheka kisha akanambia mbona kazi rahisi sana hio na wewe ….

Ikabidi nimuulize rahisi ki vipi, kwa maana nilikuwa kama nimevurugwa wakat huo, na hakuna kitu hata kimoja ambacho nilikuwa naweza kukifanya….
Akianambia mtafute demu mmoja mwambie arecord whatsap voice kwenye simu yako, kisha tengeneza nae charts ikiwezekana sasa hivi fanya hivyo, alafu profile mwambie aweke picha ya Yule dada uwe unamlau sana kwanini kafanya vile, na wakat yeye ni rafiki au binamu yako, kisha Yule dada ajibu kuwa hatujawah kukuona na mwanamke so tulkuwa tunataka kumjua wifi, mlaumu sana kisha muambie kuwa nimeshaachwa sasa na mwanamke wangu, anajua kuwa nilikuwa namsaliti, lalamika mno, mpaka mtu akiona hizo charts zenu ajue kuwa alichokufanyia sio kizuri, alafu akuulize kuwa nifanye nn mpaka niyatengeneze mahusiano yako, maana sikuwa najua kama nina wifi, ndio muambie kuwa amuambie kila mtu kuwa wewe sio mpenzi wangu, na ataje jina la mpenzi wangu ambae ni dhahara na aombe msamaha kumuomba huyo mwanamke wako, alafu post alafu mpigie huyo mwanamke wako jilize na jiombeshe msamaha mpaka uhakikishe amekuelewa, aisee niliona kama nimepewa bonge moja la wazo, kwa maana nilishakata tamaa na sikuwa najua nitamrudisha vipi tena dhahara upande wangu…

Kweli nikamtafuta dada mmoja alikuwa ni mtanzania pale chuoni, alikuwa ni rafiki yangu sana, nikampa mchongo, tukatengeneza charts na voice nikapost kwenye mitandao yangu yote ya kijamii, na kwenye post zangu zote nilikuwa naonesha ni kiasi gani nampenda dhahara, alafu nikawa namtafuta sana dhahara, ila hakuwa anapokea simu zangu wala kujibu sms zangu…

Siku hio nililala kwa tabu sana, kwa maana sikuwa nimezoea kabisa kulala bila kusikia sauti ya mrembo wangu hata mara moja, nlikuwa najisikia vibaya, ila asubuh ile nashika simu nikakuta sms ya dhahara, na kabla hata sijaifungua nikajikuta natabasamu, na hapo sijui ndio ametuma sms ya tuachane au laa, nikawa mpaka naogopa kuifungua, ila nilipofungua nikakuta ameandika asalam aleykum bilal umeamka je? Yaan nikajikuta natabasamu mwenyewe bila kutaka ……..

“ waaleykum musalam dhahara wangu, embu nambie unaendelea je mrembo wangu? Nikauliza…

Akatuma viemoj vya kucheka kisha akasema ‘ ety mrembo wako, mwanamke anaitwa mrembo kama yupo chini ya miaka 25, na sisi wengine ni mashangazi tu….
“ ni kweli ni shangazi ambae umeubeba moyo wangu, au kuna shida? Nikauliza…
‘ akatuma tena viemoj vya kucheka kisha akasema , “ ni mimi au Yule mwanamke wako wa kihindi, kwanza nilisikia kuwa wanaume wanapenda wanawake weupe, na sisi wanawake weusi tukauwawe, akasema dhahara…

“ no mama mimi siwez kuoa mwanamke mweupe kwanza, kwa sababu mimi mwenyewe ni mweupe, so naomba uniamin kuwa sio kila mwanaume anapenda wanawake weupe, sisi wengine tunapenda mablack beuty kama wewe, na usije ukawaza kabisa kuharibu ramgi yako kwa maana sisi wengine tunapenda wanawake weusi na ndio maana sion aibu hata kwa bahat mbaya kukutagaza kwa ulimwengu mzima kuwa nakupenda sana dhahara, nikasema…
………JE NINI KITAENDELEAAA!! "
FULL SEASON 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082
Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top