MADAM WA TUTION - Sehemu ya 11 na 12.





Page Bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
Basi nikafanya yangu pale na baada ya hapo nikawa namuwaza madam dhahara, yaan nilikuwa ni mtu ambae nipo busy sana kutokana na majukum yangu ambayo nilikuwa nafanya na course ninayoisomea ila nilikuwa nina hisia sana na madam dhahara, kiasi kwamba kila ninapopata nafasi mtu wa kwanza kuwasiliana nae alikuwa ni yeye, kwa maana sikuwa nawasiliana na mtu mwingineb yoyote Yule zaidi yake……
Tukajikuta urafiki wetu umekuwa mkubwa sana, hapo hajawah kuniona na kila siku nilikuwa nawaza ikitokea siku akiniomba picha itakuwa je, kwa maana hata kwenye profile yangu sikuwa nimeweka picha yoyote ile, so tukawa tunaongea sana na kuchart sana, kiasi kana kwamba muda wetu ukifika wa kuwasiliana kila mmoja anammiss mwenzake…
Urafiki wetu ukaenda kwa takriban mwaka mzima, hapo hakuna kuambiana mambo ya mapenzi, ila kuna muda nilikuwa Napata shida sana na ile sauti yake, yaan haswa haswa tukiongea usiku, mimi hoi taaban, yaan sina hali kabisa, sikuwa najiweza kwa chochote kile juu yake, nikawa nataman sana niwe nae kila wakat, nikawa nataman kila dakika awe na mimi, kuna muda nisipomkuta online nilikuwa nateseka mno, hakuwa anajua ni namna gani nataman kila ninapopata nafasi awe karibu yangu, ila ndio hivyo alikuwa ni mama na muda mwingi anakuwa na majukum kama mzaz…….
Basi maisha yetu yakaanza kwenda, nikawa namtumia zawad, anaenda anazipokea, yaan kwanza sikuwa nataka ateseke na kitu chochote kile, yaan nilitaman kumpa kila anachokitaka, ikiwezekana nimpe kila kitu , na hata asifanye kazi, yaan muda wote awe na mimi tu….
Siku moja ikaona nivunje ukimya, maana niliamin hata yeye aliona namna ambavyo nilikuwa mstaamilivu kwake, kwa maana nilikuwa nampenda kwa muda mrefu a nahisi alishaanza kuhisi hilo, ila nilikuwa namuheshimu sana, so hata mara moja sikuwah kumtongoza, so hata nilipomtongoza hakunisumbua, alikuwa ni kama anasubiri tu ni mtongoze kwa maana yeye alikuwa tayar ameshanipenda, kwa maana hakuwa anasikia au anaona lolote lile kuhusu mimi……………….
Alinikubali kisha mahusiano yakaanza wahindi huwa anaenda kufundisha usiku, ambapo akanitajia mpaka jina la mdogo wangu Sandra, alikuwa anasifia sana familia yangu kuwa ina roho nzuri, nikawa namfatilia mpaka anafika pale nyumban kwetu saa ngapi na anaondoka saa ngapi, nikawa namuuliza mlinzi, maana nilijua nikianza kumuuliza Sandra ataanza kunihoji hoji maswali na sikuwa nataka kabisa hicho kitu, na niliamin ningekuwa namuhoji sana Sandra na vile anapatana sana na madam dhahara basi kuna muda atamsimulia na huenda dhahara akanijua na nlitaka kama ni ukweli basi nimuambie mimi mwenyewe na sio asimuliwe na mtu…., alikuwa ananisimulia maisha yake yote, kuwa kuna nyumba moja y siku moja nikiwa naongea nae, yale maongezi y mapenzi, kwa maana nilikuwa nataman sana kupga nae hizo story kwa muda mrefu sana, ila nilikuwa naogopa, so aliponikubali niliona kama ndio mwanya huo, na ikiwezekana ndio niutumie huo huo kuendelea kujimaliza, so vile m vimaswali na zile story za mahaba ambazo tulikuwa tunapiga zikawa zinanipeleka kabisa kwenye dunia nyingine, yaan hakuwa anajua tu namna ambavyo nilikuwa najichukulia sharia mkononi kwa kutumia sauti yake tu……….
Mapenzi yakawa moto moto, nilikuwa nimetoka kwenye familia ambayo kidogo ilikuwa inajiweza, so kumpa mahitaji na kutekeleza majukum yangu haikuwa tatizo kabisa kwetu, kwa maana nilikuwa napambana sana kufanya kila kitu kwaajili yake, na nilishaapa kuwa nitahakikisha ananipenda sana na ikiwezekana kuliko hata ninavyompenda mm………………………
NAKUJA…
MADAM WA TUTION 12
Page bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
Siku moja tukiwa kwenye story zetu akaanza kucheka, ikabidi nimuulize kuwa anacheka nini..
“ yaan unajua mimi ni mwenda wazimu lakin, akasema ..
“ kwanini unasema hivyo?, ikabidi nimuulize, kwa maana my wangu hawez kuwa mwenda wazimu bana….
“ yaa nimemkubali mwanaume ambae sijawah hata kumuona, yaan kiufupi kitu pekee ninachokijua ni sauti yake na namba yake ya simu, akasema dhahara ikabidi na mimi nicheke…
“ ninauhakika kuwa ukiniona utanipenda tu dhahara, naomba usiwe na wasiwasi na hilo, nikaanza kujipamba pale…
“ embu nambie hupendi mwanaume wa aina gani, yaan kwa mfano nikiwa na kuonekano gani hauwezi kunikubali? Ikabidi na mimi nimuulize ….
“ kiukweli kwa namna ninavyokupenda, hata uwe kipofu au kiziwi, basi mimi nipo tayar kuwa na wewe, kwa maana nakupenda nakupenda sana na nipo tayar kuwa na wewe kwa vyovyote vile utakavyokuwa akasema dhahara mpaka nikajikuta nimetabasamu, hapo nikawa najihakikishia kuwa ameshanipenda, so hata akijua mimi ndio Yule mwanafunzi wake aliempiota miaka nane basi atanikubali tu……
Maisha yakaenda siku moja kale ka mwanamke changu cha mchongo kakaja kunitembelea, kwa maana kwao pesa kidogo ipo, na alikuwa nay eye anasoma huku sudan ambapo na mimi nasoma, ila ni kama alikuwa anaforce mambo, hakuwa na akili ya kusomea udaktar hata kidogo, na wakat wote alikuwa anawaza mapenzi tu na sio kusoma, kutwa alikuwa anagombana na wanawake ambao hata walikuwa wanajaribu kunisalimia, kwake ilikuwa ni ugomvi mbaya sana, yaan chuo kizima alikuwa anajulikana kwa ukorofi wake…..
Sasa alikuja sudan kunitembelea, hapo mimi sijiwez kwa dhahara, na hivi tunapata muda mwingi wa kuwasiliana, nahisi ndio nilizidi kuchanganyikiwa juu yake, kakaja kale kabint, kalikuwa kanaitwa suleiyah, nilikuwa nimepanga nje, nilikuwa nakaa kama kwenye apppartment karibu na chuo, kakaja, na kakijaga ni matumizi, hakajui hata kuchemsha chai, mimi ni mwanaume tena rijal, alafu nimeishi kwa muda mrefu na taswira ya dhahara na sijawah hata kumgusa, sasa kakanitega tega pale nikalala nacho, baada ya hapo kakajipost kila mahali, sijui hata nilipitiwa na nini, kwa maana simu yangu haina hata password, na nilikuwa najiamin kwa sababu nilikuwa naishi pekee yangu, yaan alijipost kwenye mtandao yote ya kijamii, kuwa Shakti ‘s wife to be…
Hapo mimi nimechoka kitokana na shoo, na vile nilikua kama nimekamia, nikalala zangu, asubuh naamka kila mtu ananiambia congratulation mpaka dhahara, nikawa najiuliza congratulation mbona zimekuwa nyingi, si ndio mtu akasema ila jamaa unajua kuchagua, umetuficha ficha kumbe demu wako muhindi mwenzako, na kila siku ulikuwa unatuambia unataka kuoa kitu cheusi, haya sasa tumemuona shemeji si ndio nikasema niangalie status, nilihisi kuchoka kwa maana kajipost facebook, whatassp status, insta, yaan kwenye social media zangu zote ….
Nilitaman kukaweka vibao, kwa maana nimemtesekea sana dhahara, na najua kwa alichokifanya ni dhahir kuwa dhaharahataweza kunitaka hata iweje, nilijiona kama nina mkosi, niliona kama ni adhabu yangu hio kwa kumsaliti kipenzi cha moyo wangu, kwa maana lait kama nisingelala na huyu bint basi hayo yote yasiongeweza kutokea, ila ni ngumu, hasa kwa sisi wanaume ambao tupo mbali na wapendwa wetu, ila hata kama ningekuwa karibu na madam dhahara basi ni gumu sana mimi kulala nae, na vile alivyo na misingi mingi………
Nikajkuta nachanganyikiwa, kwa maana ndio kwanza penzi langu na dhahara lilikuwa jipya alafu aje mpuuzi mmoja ajipost kila mahala, nilijua tu dhahara hawez kunielewa hata iweje, nikaona mimi ndio fungu la kukosa tena na ndio nimeshaumbiwa kuumia tu sasa, kwa maana juhudi zangu za miaka yote ile ambayo nilikuwa napambana kumuweka madam dhahara upande wangu ni sawa na bure…..
……JE NINI KITAENDELEAAA!! "
FULL SEASON 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082
Comments
Post a Comment