MADAM WA TUTION - Sehemuya 01 na 02

Simulizi master
0

 



Page Bahari yasimulizi
WhatsApp 0755090082
SSehemuya 01 na 02

KKITUKKIPYA..... TTUANZENNAYOSijui kwanini wanawake wengi huwa wakiona mwanaume mdogo wanamdharau licha ya kwamba umri ni namba tu na sio mapenzi, hata sisi wanaume wadogo huwa tuna haki ya kupanda na kupenwa kama watu wengine….

Dada husqer embu ipostie, sijui kama ndio wananicheka kuwa nimependa lishangazi, au ndio watanipongeza kwa ujasiri wangu, maana nimepambana sana , mpaka mwenyewe nilikuwa najishangaa nilipata wapi ujasiri, sijui nilipata wapi nguvu ya kupambania penzi la mwanamke ambae alikuwa ananidharau sana, na kuniuona kama mtoto , utadhan anakadi langu la clinic…
Naitwa Shakti, baba yangu ni muhindi na mama yangu ni chotara wa kihindi na mshirazi, ila ukiniona ni lazima utaamin kuwa mimi ni mhindi pure, kwa sasa nina miaka 27, ila nimeteseka sana, kwa maana nilitokea kumpenda mdada ambae alikuwa ananifundisha tution nilipokuwa mtoto, nilikuwa kijana mdogo sana, na yule dada alikuwa mweusi tu, kwa maana kwa namna ambavyo sisi tulikuwa na yeye, ni dhahiri tulikuwa watu wa aina mbili tofauti, ila nikiwa mtoto mdogo wa miaka 12 nilikuwa najishangaa kwa maana , kwanza sikuwah kutaka kukosa vipindi vyake, kwa maana nilikuwa nikijua kuwa anakaribia kuja, basi ninitashinda ndani siku nzima, akija, nilikuwa namfata namkumbatia…

Na kwakuwa nilikuwa mdogo akawa anakubali kunikumbatia, na wakat huo mimi nina miaka kumi na mbili, ila yeye ndio alikuwa amemaliza form six, alikuwa anakuja kutrufundisha kile kipindi cha kusubiri matokeo ya form six, nilikuwa nasisimka sana akinikumbatia, alikuwa ana pafyumu flani hivi, yaan mpaka nilienda kununua hio pafymu, nilikuwa naweza kupulizia nguo nikashinda nimeikumbatia, nilikuwa nampenda sana, na kwakuwa nilikuwa nampenda, nilikuwa napambana sana kumfanya ajisikie vzr, so nilikuwa nasoma sana, ili walau anisifie kuwa nina juhudi…

“ nilikuwa mdogo sana, sasa sikuwa najua kama yanayonisumbua ni mapenzi au ni nini, kwa maana kijana wa miaka 12, kuanza kumuwaza bint kama Yule madam wangu, nilikuwa naona kama ni kitub cha ajabu, ila nilikuwa nashindwa kabisa kujizuia, na siku ambazo alikuwa haji kunifundisha, nilikuwa nataman kumfata huko alipokuwa anaishi, walau nimuone tu…

Maendeleo yangu yalikuwa mazuri sana, kwa maana hata shule nilikuwa nasifika sana kwa juhudi zangu, bila kujua hizo juhudi ni kwasababu nataka kumfurahisha madam wangu…

Basi muda ulienda na hatimae madam wangu wa tution, akawa amefaulu na akatakiwa kwenda chuo, hiki ndio kilikuwa kipindi kigumu zaidi kwenye maisha yangu, kwa maana sikuwa na raha, nilikuwa naumia kana kwamba nilikuwa na mawazo, kana kwamba nilikuwa na nimeachwa, tena ghafla, nikawa ni mtu wa kujifungia chumban na kuchukua ile pafyumu ya madam, ambayo nilikuwa napulizia kwenye nguo, kisha naanza kuinusa, nilikuwa nikifanya hivyo Napata kabisa hisia, na nilikuwa mtoto, hapo nitalala vzr, na nikawa ni mtu wa kusoma tu, nikimalia kusoma naenda kupulizia ile pafyumu kenye nguo naikumbatia kisha nitainusa mpaka napitiwa na usingizi…

Maisha yangu yakawa yanaendelea hivyo…
Nikamaliza darasa la saba, ila kuanzia nimemaliza shule, sikuwah tena kukutana na Yule madam, alikuwa anaitwa dhahara, wala sikuwa kujua nitampata wapi, ila nikawa najipa moyo kuwa, kwanza ni mkubwa so inawezekana kabisa anamahusiano yake, na kingine nilikuwa najua hata iweje hawezi kunipenda, na niliamin kuwa nitamsahau tu..

Basi maisha yakaenda, nikaanza kumsahau, nikafanikiwa kujiunga na elimu ya secondary, na kwakuwa familia yangu inajiweza kidogo nikawa nasoma pale Arusha boys Islamic secondary school, hii shule niliichagua mm, kwa maana nilikuwa napenda sana maswala ya dini, so nikawa nataka kusoma shule ya dini…

Basi maisha yangu yakawa yanaendelea, na kwakua shule niliokuwa nasoma hakukuwa na wanawake, so hata ile balehe iliponikuta, mwanamke pekee ambae naweza kusema kuwa nimempenda ni Yule madam wa tution, maisha yakaenda, na hatimae nikahitimu elimu yangu ya secondary, nilifaulu vzr, ila wazaz wangu hawakutaka nisome Tanzania, kwa maana nilipomaliza kidato cha nne, nikaenda kusoma sudan , nilienda kusomea udaktar, nilisoma miaka mitatu bila kurudi nyumban, siku hio narudi nyumban,nikashangaa namkuta Yule madam anamfundisha mdogo wangu, ambae kwa wakat huo alikuwa yupo kidato cha kwanza, alikuwa ni mdogo wangu wa mwisho,…….

Nilipomuona moyo wangu ulishtuka sana, nay eye alitabasamu kisha akasema “ Shakti, umekuwa sana mpaka umeanza kuota vi ndevu, ama kweli nimeshazeeka, akasema madam dhahara akiwa anshika ndevu zangu, nilikuwa najisikia vzr sana, nikawa natama hata anikumbatie, kwa maana nilikuwa naona kama kwa wakat ule nilikuwa nina uwezo wa kummiliki, maana nimeshakuwa sasa…

Ila hakuwa anaonekana kabisa kuvutiwa na mimi kimapenzi, nikaingia ndani na kuanza kujitengeneza, nikapiga mapigo yangu, nilikuwa najua madam dhahara, anapenda mwanaume ambae anadini, kwa maana alikuwa anatufundisha mambo ya madrasa na shule, nikatoka, hapo nanukia, na ile pafyumu yake ndio ilikuwa pafyumu yangu…

Nilitoka nikijua kuwa hata atauliza kuwa anasikia harufu ya pafymu yake, ila hakuuliza kitu, na alikuwa busy kumfundisha mdogo wangu, na hakuwa na muda kabisa na mimi, mpaka nikawa nahisi kama ananipuuza, ila nikawa najiambia kuwa natakiwa kuwa mtulivu tu, wakat wangu utafika…

Nikawa namuangalia, alikuwa na macho makubwa, na lips pana kidogo, na anakarangi katamu, yaan nikawa namuangalia tu, hapo namuwazia ujinga, kwa maana nilikuja kujigundua kuwa zile hisia zangu za utoto hazijawah kuondoka juu ya madam dhahara, licha ya kwamba muda ulipita, na nilikuwa nimeshaanzisha mahusiano na muhindi mwenzangu, ila sikuwa na hisia near ki hivyo, ni kwa kuwa sikuwa najua naweza kumpata vipi madam, na niliamin kuwa sitakaa kumuona tena, ila nimemuona sasa, so sikuwa na haja ya kumpenda mwanamke mwingine yoyote, ila Yule madam hakuwa na muda kabisa na mimi…

Basi akamfundisha mdogo wangu pale, alipomaliza akasimama na kusema “ sasa Shakti, mimi naenda nyumban, nimefurah kukuona umekuwa mbaba sasa, kwa maana sitaki kuamin kuwa wewe ndio kale katoto ambacho kalikuwa kanalia lia, akasema madam, nikatabasamu, ila sikuwa napenda akiniita mtoto, kwa maana sikuwa mtoto tena, na nilikuwa na miaka 22 kwa wakat huo, kwani alishawah kuona mtoto mwenye miaka 22, ila nikawa najiambia kuwa nitapambana na nitahakikisha kuwa hanichukulii kama mtoto….

Wakat huo nilikuwa najua kudrive, nikaomba nimpeleke nyumban, hakukataa, na lengo loa kutaka kumpeleka nyumban, nilitaka kujua anapoishi tu, ili hata siku nikimmiss niende tu kukaa nae, au niende nikamuone…

Basi tukaenda kwenye gari nay eye akakakaa nyuma, yaan kila dakika nilikuwa namuangalia kupitia side mirrore alafu nikawa natabasamu, kwa maana nilikuwa najisikia vzr sana kuwa karibu na madam, hapo madam hajui kama kijana wake huku nimeshachanganyikiwa juu yake……

Tumefika kwenye mtaa mmoja huko sakina arusha, akanambia kuwa ameshafika anapoishi, na aliposhuka tu kwenye gari, kakaja kabint, ambacho kalikuwa kana kama miaka mitano na kusema ‘ mama umerudi…
Sijui kwa nini niulijisikia vibaya sana, niliona kama Yule bint hatakiwi kumuita dhahara mama yake, na wakat sio bint yangu, moyo wangu uliamin kuwa mimi pekee ndio natakiwa kuzaa na dhahara na sio mwanaume mwingine yoyote Yule, nilihisi atakuwa anaishi na mwanaume, nilishindwa kuendelea kukaa pale, kwa maana nilihisi kama sikuwa na ujasiri wa kumjua mwanaume ambae anamiliki dhahara wangu….
ITAENDELEA

MADAM WA TUTION
Sehemu ya 02.
Page Bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082

Basi nikaondoka zangu ila sikuwa na raha, nikataman kujua kila ambacho kinamuhusu madam dhahara, nilitaka kujua kama ana mume au laa, nilitaka kujua kama alikuwa ameolewa au alikuwa anaishi na mwanaume, nilikuwa nataman Yule mtoto angekuwa ndio mwanangu, kuna muda nilikuwa najifariji kuwa huenda huyo mtoto sio wake, labda ni wadada yaken ndio amezoea kumuita mama, siujui hata huu wivu nilikuwa naupata wapi, na wakat hata sikuwa na uhakika kama tanikubakli au laa, sikuwa na uhakika kama atanipenda au ndio ataniona katoto kama anavyonionaga, na wakat nilikuwa nampenda sana tena kwa muda mrefu, na kuna muda huwa nahis labda kwakuwa ndio first lover wangu, basi ndio maana siwez kumsahau, kwa maana hata kama nilianzisha mahusiano, ila sikuwa nayafurahia kabisa, kwa maana nilikuwa naamin kuwa ipo siku madam dhahara atakubali kuwa mke wangu…

Kuna muda nilikuwa najiambia kuwa niachane na ndoto zangu za abunuwasi, za kuwaza mambo yasio wezekana, ila kuna muda nilikuwa najipa nguvu na kujipa moyo kuwa hakuna kitu kinachoshindikana cha msingi ni juhudi zako na kumuomba mungu, nilikuwa naomba sana madam dhahara asiolewe, kuna muda hata sikuwa najua kuwa nilikuwa nampenda vile kwa sababu gani na wakat amenizidi umri na ni dhahiri kuwa kwa umr aliokuwa nao ni lazima anaweza akawa na mpenzi…

Niliporudi nyumban nilimfata mdogfo wangu Sandra na kumuuliza kama madam wake ameolewa au laa…
“ wewe unataka kujua maisha ya madam wa watu ya nini? Akaniuliza Sandra ..
“ wewe jibu swali na wewe, hayo mambo ya maswali yako utaniuliza ukishanijibu maswali yangu, nikajibu…

Sandra akacheka kisha akasema “ au unampenda nn, kwa maana naona hadi uliamuaga kutumia pafymu yake, maana nyie vijana huwa hamchelewi kabisa, akasema Sandra ..
“ kwani kumpenda ni kosa, maana yeye nin binaadamu na mimi ni binaadamu piua, na sion kosa hapo, so naomba unijibu swali langu, na kama hujui pia useme ili usinipotezee muda wangu wa kukaa na kukusikiliza, nikajibu…

“ well alishawah kuolewa, ila sijui ilikuwaje kwani mume wake inasemekana alipoteaga, kwa maana alikuwa ni miongoni mwa watu ambao alikuwa anafanya kazi Kenya, kwa maana alikuwa anaenda Kenya anakaa hata mwezi alafu anarudi kukaa na familia yake, ila ni miaka miwili sasa, mumewe hajawah kurudi na wamefuatilia sana , mpaka sasa hajulikan yuko wapi, akajibu Sandra, kisha akasema “ kuna muda hata mimi namuoneaga huruma sana, kwa maana naonaga kama ni mpweke sana, akamalizia kusema…

Sikutaka hata kuendelea kuhoji, nikasimama zangu na kuelekea chumban kwangu kisha nikajifungia mlango, nikawa naanza kujifarijin kuwa huenda madam dhahara atanipenda tu kwa maana mumewe hayupo, na huenda Mungu ana makusudio yake, kwa kumpoteza mume wake, huenda ni kwasababu yangu, kuwa nimerudi ili niishi na mwanamke ambae amekuwa akiutesa moyo wangu kwa namna ya kipekee sana…

Basi siku hio ikapita na hatimae kesho yake ikafika, nilijua nin lazima mdogo wangu Sandra akitoka shule basi madam atakuja nyumban, so siku hio nilienda kumfata mdogo wangu shule ila tuliporudi nyumban tukamkuta madam Sandra ameshafika na anamsubiri Sandra, nilipomuona nikajikuta naanza kutabasamu…
“ za sahizi madam, nikasema nikashangaa namuona madam shahara anatabasamu kisha akasema “ wewe ni mdogo kwangu so unatakiwa uniamkie na sio kusema za sa hizi, kwa maana hatulingani, akasema madam, nikaonan hapan dharau zakeb zimeanza..

Basi Sandra akamsalimia madam, kisha akaingia ndani na kwenda kubadilisha nguo ilia je kusoma, mm sikutoka kabisa pale ukumbin kwa maana nilikuwa najisikia vzr sana kumuona madam Sandra pemben yangu…
“ mwanao anaitwa nani madam? Nikauliza…
“ anaitwa aisha, akajibu huku akiwan anaendelea kutafuta kalamu kwaajili ya kuja kumfundisha Sandra, nilikuwa nataman hata aniangalie ila hakuwa kabisa na muda na mimi, itu ambacho kilikuwa kinanifanya nijisikie vibaya sana…………………

Basi Sandra akaja na wakaanza kusoma, mimi sasa nikawa kama mwehu, kama kawaida yangu nikaingia ndani, na kubadilisha nguo , na wakat nilikuwa msafi, nilikuwa nataman sana kumuona madam dhahara akiwa amevutiwa na mimi, simulizi hii imeandikwa na husqer baltazar,so nikaanza kushinda na mimi kwenye kioo kama mtoto wa kike, kila nilivyikuwa najitengeneza nikawa naona kama sivutii, nabadilisha muonekano, nilishunda nabadilisha nguo na mtindo wa nywe kwa karibu nusu saa, ili tu nikitoka madam dhahara avutiwe na mimi…

Basi nikatoka na kwenda kukaa ukumbin, nikawa najifanya kama nachezea chezea simu, alafu namkata kajicho cha pemben, yaan namna ambavyo alikuwa anatabasamu mm sina hali, najikuta natabasamu nae, nilikuwa kama nimevurugwa hivi, ila wakat wote ambao nilikuwa pale ukumbin, madam dhahara hakuwa hata anashughulika na mimi hata kidogo, nikawa nafanya kazi ya kujikohoza kohoza, lakin wapi, yaan ilikuwa ni sawa na bure, kwa maana kila ambacho nilikuwa nakifanya hakikuwa na matokeo yoyote yale……

Basi madam akamaliza kumfundisha mdogo wangu Sandra akawa anataka kuondoka, sasa kwa akili zangu nikawa nataman sana kumzuia, ila sikuwa najua naweza kumzuia vipi, yaan akae kae ili niendelee kumuona ona, ila sikuwa na chakumuambia, zaidi sana nikaomba nimsindikize…

“ oww samahan sana Shakti, kuna mtu naenda kuonana nae, so sidhan kama itawezekana mm na wewe kuongozana, akasema ..
Sijui kwann nilijisikia wivu mara baada ya madam kunambia kuwa kuna mtu anataka akamuone, kwa mawazo yangu nikajua lazima atakuwa mwanaume, niliamin kwakuwa mume wake kapotea muda mrefu kwenye mazingira ya kutatanisha, basi ni lazima atakuwa anataman kuanzisha mahusiano mapya….

“ kwani siwez kukupeleka sehemu ambayo unataka kwenda? Nikauliza…
“ owww naona kama nitakuwa nakusumbua, akasema madam…
“ wewe hauwez kunisumbua bana, naomba nikupeleke tu kama hautajal, nikaendelea kusisitiza…
Akakubali, nikampeleka moaka kwenye mgahawa mmoja, na akafika akakaa , na mm nikawa nimekaa pemben, ndipo nikamuona mwanaume wamakamo anaingia, kisha akaenda kukaa na madam dhahara, sio siri nilijisikia vibaya sana, kwa maana nilianza kuona wivu, nikawa najipitisha pitisha tu, nataman kumfatav Yule mwanaume na kumkunja kisha nimuulize kwann anakaa na mwanamke wangu, ila hata sikuwa najua naanzia wapi, sasa wakawa wameagiza chakula wanakula, huku wanapiga story wakiwa wanacheka, kwa akii zangu nikajua kuwa Yule mwanaume anamtongoza madam, na madfam anavyocheka basi atakuwa amekubali….

Nikaona usinitanie, nikaenda mpaka alipo madam kisha nikasema “ mume wako alikuwa ananipigia simu na anauliza mbona hakupati, maneno yangu ni kama yaliwaacha wote wawili kwenye mshangao, kumbe nilikuwa nataka tu nimkatishe tamaa Yule mwanaume na ikiwezekana asiwe karibu na madam Dhahara wangu…….

JE NINI KITAENDELEAAA!! "
FULL SEASON 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082
Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top