Simulizi: ndoa yangu inanitesa 15

Inawezekana huyu mshenzi akamkataa mke wangu. Midomo yake imejaa dharau”nilijisemea kimoyomoyo huku nikibonyeza kitufe cha geti. Getruda Kimario alifika getini na kufungua, mtu wa kwanza kuingia akiwa Mzee Jophu.Shauku yake haikufichika ,alimtupia Getruda jicho la lilo jaa ubembe.Ni hapo ndipo nilipohisi Mzee Jophu kumkubali mke wangu. Alikuwa na shauku ya kumbusu Getruda, nikipindi kirefu toka wapoteane pale ofisini kwake, na Getruda alimkumbuka kuwa yule alikuwa yule aliyempa mama yake mzazi shilingi laki tano za kitanzania iliamuowe yeye. Walitupiana macho yaliyojaa furaha macho ya matamanio ya Getruda yalizidi kumchanganya Jophu. Aliyekuwa na shauku kuupitisha usiku mwanana na binti aliyemlipia shilingi laki tano. Aliamini alikuwa na haki yakujivinjari jasho lake. Mwanzoni nilihisi hawakumbukani,kumbe kumbukumbu alikuwa nazo na alishuhudia mama yake akipokea hizo hela. Ulifikia muda muafaka wakuweka mambo hadharani ili nitatuliwe shidayangu. Kabla sijazungumza chochote nilipandisha...