Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)
"Niulize tu mama angu" "We naweee...kila muda mama, mama! Kwani mi mama yako?" "Nisamehe bibi yangu" "We nitakufukuza kwenye hii nyumba...mimi ni bibi?" "Basi shangazi...anti" "Lione....mi nilidhani una akili timamu, kumbe zimepungua. Alafu ndo umekuja mbeya mjini kutafuta maisha kwa akili hizo?" "Mbona zinanitosha" Alinitazama kwa hasira nisura anilambe kibao cha utosi, alimeza mate kisha aliniacha. Alitazama godoro, alitazama mlangoni kisha alinitazama mimi. "Unataka kulala kwenye kitanda cha chuma?" "Ndiyo jamani nikilala hata kwa sekunde 2 nitashukuru sana" "Haya panda hapo kitandani ulale kidogo" "Mi naogopa" "Unamuogopa nani?" "Namuogopa mumeo" "Ameenda kazini. We si unalala kidogo tu kisha unaamka...ebu lala uonje ladha yake" Nilitetemeka kwa hofu, ndo mara yangu ya kwanza kulala kwenye kitanda cha chuma. Kabla.sijapanda, nilitazama miguu y...
Comments
Post a Comment