Riwaya: penzi la mfungwa 12
kiona kule mstuni. Watu wote waliokuwepo pale kwenye maombolezo walimtazama yeye,naye alipo jihakikishia kuwa tayari yupo sawa alisema "Zabroni....",watu wote kasoro Bruno walistuka kulisikia hilo jina,Ghafla mmoja mmoja aliinuka na kisha kuondoka zake wakiogopa kwamba huwenda Zabroni yupo nyuma,ndio aliyekuwa anamkimbiza kijana huyo muwendaji aliyekuja mbio mbio.
Upande wa Bruno yeye hakuwa na hofu kwa sababu aliamini kuwa tayari huyo kijana atakuwa ameona maiti ya Zabroni na hivyo atakuwa amekuja kutoa taarifa rasmi hapo kijijini kuhusu kifo cha huyo mtukutu,kitu ambacho ndicho alikuwa akikitamani na ndio maana alimtundika eneo lile la wazi ili mpita njia ama muwindaji yoyote atakae katiza eneo lile aweze kuishuhudia.
Hivyo hofu ilitanda hapo,mama mmoja alisikika akiitikia kwa kusema "Heeh Zabroni? Aawapi jamani nilikuwepo nitarudi baadae", aliongea huku akiambaa na njia kutafuta mahali pa kujibanza ili kama Zabroni atafika pale yeye asiwepo. Lakini kabla hajafika mbali alisikia sauti zikisema "Mmmh jamani kweli ? "
"Aah sidhani,mzee Baluguza mtalamu. Mganga kati ya waganga kamshindwa eti leo hii ndio afe. Tena kirahisi rahisi tu? Teh teh teh..hiyo ndoto ya mchana "
"Sio bure huyu jamaa anakuwa kajambiwa na ndezi wake huko polini,anakuja kutueleza ujinga wake"
"Teh teh teh teh..Ni rahisi sana panya kubeba mimba ya paka kuliko mtu wa kawaida kumuua Zabroni, acheni kudanganyana bwana", zote hizo zilikuwa ni sauti moja ya maongezi yaliyosikika kwa fujo maeneo hayo,yote kutoka na kijana yule muwindaji kusimulia kile alicho kiona huku akisisitiza kuwa Zabroni kafa. Fujo ilisikika huku baadhi ya watu wakidiriki kumtukana,lakini baada Bruno kuona utata unazidi ndipo alipotaka kukata mzizi wa futina ili kuwaweka wanakijiji katika hali ya amani.
Alifikinya kiganja chake kwa kutumia mkono wa kulia alifikanya kiganja cha mkono wa kushoto,kisha akafumbua kiganja hicho ambapo ulionekana ule mpambano aliopigana naye mpaka tamati.
Hakika wanakijiji walishusha pumzi kila mmoja akimtazama Bruno kwa jicho la tatu na kumuona ni shujaa wa kukumbukwa katika hicho kijiji,yule mzee aliyemuuliza swali hapo awali alipata jibu la swali lake . Ambapo Bruno alipo mtazama,naye akamuonyeshea dole gumba kuonyesha kuwa tayari jibu analo. Furaha ilitawala sasa,hata wale walio kimbia mwanzo walirudi kuungana na wenzao kufurahia kifo cha Zabroni.
Baada ya hapo msafara wa wanakijiji ukiambatana na shujaa wao Bruno huku kiongozi akiwa Mwenyekiti,ulijikusanya ukaenda kuufuata mwili wa Zabroni ili wauchome moto. Lakini walipo fika eneo hilo hawakuuta mwili huo,walitaharuki wakamtazama Bruno ilihali Bruno naye akionekana kushindwa kujua kilicho tokea. Hofu kwa mara nyingine tena ilitanda mioyoni mwao,kila mmoja akionekana kuwa na sintofahamu kuhusu mtukutu.
Na wakati wote wakiwa katika hali hiyo mara ghafla ilisikika sauti ikisema huku ikijirudia mara mbili mbili. Sauti hiyo ilisema "Mimi ndio Zabroni. Nimerudi ",sauti hiyo ikamaliza kwa kicheko kikali. Punde baada kusema hivyo ghafla....!
ITAENDELEA
Comments
Post a Comment