Riwaya: penzi la mfungwa 14
"Ni kweli,lakini ujue hata tusipouza ni sawa na bure tu. Hizi ni nyanya Zabroni hazichelewi kuoza, Kwahiyo kuliko tupate hasara ni bora tuuze tukagange yajayo", alisema jamaa huyo. Zabroni alijikita katika mambo ya kilimo baada kuona kumaliza kisasi chake. Hivyo siku hiyo yeye na rafiki walikuwa mji mdogo kwa niaba ya kuuza mazao yao.
Walikubalina wakawa wameuza mazao ya kwa hiyo hiyo bei waliyoikuta gulioni,na mara baada kupokea ujira wao walianza safari ya kurejea kijijini ambapo huko hukukuwa na mtu hata mmoja aliyemfahamu Zabroni. Aliishi kwa amani pasipo kuwa na shaka.
Lakini kipindi wanatoka gulioni mara ghafla Zabroni akakutana tena Veronica, wote kwa pamoja waliachia tabasamu hasa Zabroni baada kukumbuka kwamba kuna muda aliyekanyagwa na huyo binti akawa amemuomba radhi.
Safari hiyo Veronica alikuwa anafungua mlango wa gari teksi,kabla hajaingia ndani alimuuliza Zabroni wapi wanapo elekea,Zabroni akataja na hapo ndipo Veronica alipowataka wapande kwa madai kwamba naye anaelekea huko. Zabroni na rafiki yake walifurahi sana kupata lifti,Veronica akamwambia dereva wake afungue buti nyuma ili waweke tenga ambalo walibebea nyanya. Safari ikaanza kuelekea kijijini,wakiwa ndani ya gari walipiga zogo mpaka mwisho wa safari ya safari ya Zabroni na rafiki yake ambapo walishuka kisha wakatoa shukrani zao.
Kabla hawajaondoka Veronica alimuita Zabroni ndani ya gari huku nje akibakia rafiki yake akiwa amesimama...Ndani ya gari Veronica alimwambia Zabroni "Smahani kama hutojali nilikuwa naomba kesho uje mjini tukale pamoja chakula cha mchana,usistuke nimevutiwa sana na ukarimu wako unaonekana kijana mpole,kiukweli kaa ukijua tu kwamba umenivutia sana na pia nitafurahi endapo kama utanikubalia", alisema Veronica kwa sauti nyororo huku uso wake ukionyesha haibu. Zabroni aliposikia maneno ya huyo dada,moyo wake ulistuka.
Ndani ya nafsi yake akajiuliza "Bahati gani hii inanitokea? Hili ni zali la mintali siwezi kulipuuzia " kwisha kuwaza hayo alijibu "sawa nipo tayari usijali. Je, tukutane wapi?",Veronica alimuelekeza mahali pakukutana,Zabroni akawa amemuelewa ambapo alisisitiza kutokukosa.
Baada ya hapo waliagana,Veronica akaondoka zake lakini pia Zabroni naye akajua hamsini zake huku kila mmoja akijanasibu kiana yake. Mtukutu Zabroni akijigamba kwamba huwenda akawa amepata zali la mentali kwa Veronica, ilihali Veronica naye akiamini kuwa yule ndege mtutundu anakaribia kunasa kwenye tundu bovu!
Inaendelea..
Comments
Post a Comment