Riwaya: penzi la mfungwa 17
Kwahiyo Bruno alipofika Dar es salaam alibadilisha jina na muonekano wake,ambapo alijiita Mr Rasi. Hakuwa na rasta lakini alijitahidi kuzifuga nywere,zilipokuwa ndefu ndipo akasokota rasta.
Na hapo ndipo rasmi kijana Bruno akawa Rasta man,jina ambalo liliendana na muonekano wake. Nitaishije ndani hili jiji? Ndilo swali alilojiuliza kijana Bruno ama Mr Rasi.
Kwani baada kujificha kwa kipindi kirefu nje ya kidogo ya Dar akingojea nywere zake zikue zimuweke katika muonekano mwingine ambao utamfanya mtu asimtambue,hatimaye akawa ameingia mjini sasa ambapo hilo ndilo swali alilojiuliza huku akiwa amesimama moja ya eneo ya kinondoni saa za usiku.
Muda ambao jiji la Dar es salaam linaonekana kuwa na mishe mishe nyingi utaweza sema mchana ndio usiku na usiku ndio mchana,watu hawalali wanatafuta salali.
Mr Rasi akiwa haelewi jinsi atakavyoishi ndani ya hilo jiji,mara ghafla kando yake alipo simama alionekana binti mmoja wa makamo akingojea daladala. Lakini punde si punde yule binti akasikika akipiga mayowe "Mwizi mwizi mwizii jamani kanikwapulia mkoba wangu",Mr Rasi aliposikia sauti hiyo akatoka kwenye dimbwi la mawazo,akatazama upande ule alio simama huyo binti kisha akautazama ule uma wa watu uliokuwa bize kugombania daladala huku wengine wakiendelea na mambo yao bila kumsaidia dada huyo aliyekuwa akilalama kuibiwa. "Kwanini hawajishughilishi na hili lililotokea?..",alijiuliza Mr Rasi.
Papo hapo akapotea kama upepo kumfukuzia yule mwizi, punde si punde akasimama mbele yake. Kibaka alistuka wakati huo huo Bruno ambaye ndio Mr Rasi akamwambia
"Dondosha mkoba chini kisha utimue mbio",kauli hiyo ukilinganisha na namna alivyomtokea,ilimuogopesha yule kibaka ambapo alifanya kama alivyo amrishwa kisha akatimua mbio. Mr Rasi akuchukuwa mkoba huo upesi akamkabidhi yule binti huku akimsihi awe makini.
Binti alishukuru sana lakini pia alihitaji kumjua jina sababu amemsaudia kwa kiasi kikubwa mno. Ni mgoba ambao ulikuwa na vitu kadhaa vya thamani "Naitwa Mr Rasi",alisema Bruno huku uso wake akiwa ameinamisha chini, kofia aina ya kepu aliyovaa ukiuficha vema uso wake.
"Naitwa Tina, ahsante sana Rasi kwa msaada", alijibu binti huyo. Ni yule Tina mpenzi wa Zabroni,siku hiyo anakutana na mbaya wa mpenzi wake pasipo kujua.
INAENDELEA

Comments
Post a Comment