Riwaya: penzi la mfungwa 20



 kipindi Tina anafika hapo Mr Rasi alikuwa anachezea ngumi za kila sehemu ya mwili wake kana kwamba jamaa aliyekuwa akipigana nae alionekana kumzidi ubavu,lakini baada Mr Rasi kusikia sauti ya Tina ikisema "Rasi,sijapenda mimi" ,Hapo mr Rasi alijihisi kupata nguvu mara mbili ya awali. 


Alipigana ipasavyo mpaka akaibuka mshindi,ikawa furaha isiyo kifani kwa Karani lakini pia kwa mrembo Tina baada kuona yeye kuwa moja ya chachu ya ushindi.



Makubaliano sehemu ya kukutana yalifanyika baina ya matajiri hao,Karani na na mwenzake. Ilihari kwingineko upande ule aliosimama Zabroni alijikuta akivuta kumbukumbu siku za nyuma kipindi alipokuwa akipigana na Bruno,aliona mapigo aliyoyaona hapo ulingoni kutoka kwa Mr Rasi na yale ya Bruno yalifanana fika. 


Jambo hilo kidogo lilimtatiza Zabroni,lakini yote kwa yote hakutaka kutilia maanani na hivyo aliamuwa kuondoka zake kwani tayari mpambano ulikuwa umeshamalizika. 


Zabroni alizipiga hatua kutoka mahali hapo akazunguka upande ule ziliposimama gari za matajiri pia na gari aliyokuja nayo Tina,kabla hajazikaribia hizo gari alimuona binti aliyefanana na Tina akifunguliwa mlango na Mr Rasi. 


Zabroni alistuka,kwa sauti kuu akasema "Tinaaaaa",Tina aliposikia sauti hiyo aligeuka kutazama kule ilipotokea,hakujua mtu aliyemuita kwa maana watu walikuwa wengi sehemu hiyo. Zabroni baada kuona Tina hajamuona alinyoosha mikono,hapo Tina akawa amemuona. Haraka sana Zabroni alizipiga hatua kumsogelea. Alipo mfikia alimsalimia lakini Tina hakumjibu salamu yake,alishangaa sana Zabroni. 


Kwa taharuki akasema "Ni mimi mpenzi wako uliyeniacha kijijini", akacheka kidogo kisha akaendelea kusema "Tina inaama umenisahau? Au kwa sababu nimechafuka hivi ndio maana umeshindwa kunitambua? Amini Tina kwa sasa nipo mjini,niliamua kuachana na yale mambo niliyokuwa nikiyafanya. 


Ndio maana sikuhizi nimejikita kwenye kazi hii niliamua kukimbia kijijini baada kuona naogopwa sana",alisema Zabroni huku akiwa na tabasamu bashasha,wakati huo Tina alikuwa kimya akimsikiliza huku machozi yakimtoka. Aliyafuta kisha akamjibu "Sawa,yote tisa. Kumi. Mimi sio mpenzi wako tena. Nimepata mwingine anayejua nini maana ya mapenzi,na sio wewe mwanaume katili usiyekuwa na hata chembe ya huruma.


 Wako wapi wazazi wangu? Wewe ndio muhusika wa vifo vyao. Je, unadhani kwa jereha hili unaweza kuniponya? Hebu achana na mimi bwana." aliongea Tina huku machozi yakimtoka. Muda huo huo Mr Rasi alitoka ndani ya gari akazunguka ule upande aliosimama Tina akiwa anaongea na Zabroni. 


Alipofika alitaharuki kisha akamuuliza Tina "Tina,kulikoni kwani kuna nini?..",Tina hakujibu aliishia kumtazama Zabroni kwa hasira kali. Ukweli ni kwamba hata Mr Rasi hakuweza kumtambua Zabroni kwani wakati Rasi anamuuliza Tina swali hilo,Zabroni yeye aliinamisha uso wake. Ni kitendo ambacho kilimuwe ngumu Mr Rasi kumjua yule mtu anayezungumza na Tina.



"Hapana mpenzi hakuna kitu ila..",kabla Tina hajamalizia jibu lake, mara ghafla Mr Rasi alimkatisha kwa kusema "Ila nini? Unajua tunasubiliwa sisi? Wenzangu wote wapo tayari,sasa naona wewe umesimama nje muda mrefu tu hata unachokifanya hekieleweki", alifoka Mr Rasi kwa hasira. 


Tina alijua kuwa mpenzi wake kakasirika,hivyo alimsogelea kisha akamkumbatia mbele ya Zabroni halafu akasema "Tazama we mwenda wazimu, Tina sio mali yako tena. Huyu ndio mpenzi wangu kwa sasa,kwahiyo itapendeza kama utaniita shemeji popote pale utakapo niona. 


Lakini tofauti na hivyo utahatarisha maisha yako mwanahidhaya mkubwa wewe ", aliongeza kusema hivyo Tina kisha akaingia ndani ya gari,gari likawashwa wakaondoka zao huku nyuma wakimuacha Zabroni asiamini kile kilicho tokea. Moyoni akawa anajiuliza "Hivi ni kweli au ni fikra zangu tu?.." wakati Zabroni akiwa katika hali hiyo ya kutoamini kile alichokiona,upande mwingine nako ndani ya gari Mr Rasi akiwa na Tina walikuwa wakipiga zogo huku Tina akimsifu mpenzi wake kwa kuibuka kidedea. 


Lakini baada ya sifa hizo,Mr Rasi alimuuliza Tina juu ya mtu yule aliyekuwa akiongea naye "Tina kwani yule nani uliyekuwa ukiongea naye?" ,Tina mara baada kuulizwa swali hilo alikaa kimya ila baadaye kidogo alijibu "Nadhani unakumbuka sikuile nilipokwambia kuhusu matendo machafu aliyokuwa akiyafanya mpenzi wangu wa kwanza"


"Nani yule aliyekuwa anachoma nyumba hovyo? ..",alirudia kuhoji Mr Rasi huku akionekana kustuka. Tina akajibu "Huyo huyo,anaitwa Zabroni. Ndio nilikuwa naongea naye,hivyo ilikudhihilisha kwamba simtaki tena nikaamua kukutambulisha kwake kwamba wewe ndio mpenzi wangu. 


Ukweli Rasi,namchukia sana yule mwanaume kwani nafahamu yeye ndiye aliyewaua wazazi wangu. Sitaki na sitotaka kumuona tena mbele yangu" Tina alilia, wakati huo huo Mr Rasi alikanyaga breki kwa nguvu kiasi kwamba matairi ya gari yalitoa harufu. 


Papo hapo aligeuza gari kurudi kule alipotoka huku moyoni akijisemea "Huyu ndio niliyekuwa namsaka kwa muda mrefu,ngoja nikamalizane naye mapema kabla hajatoweka ndani ya hili jiji",alijisemea hivyo Mr Rasi ilihari muda huo Tina alikuwa ameshanyamanza amebaki sasa kushangaa namna Mr Rasi anavyo endesha gari kwa fujo kumfuata Zabroni. 


Kwani naye alitoka rumande ili amuue Zabroni kama njia ya kulipiza kisasi,ilihali Zabroni naye vile vile alitoroka jela ili amuue Mr Rasi ikiwa kama njia ya kulipiza kisasi.


INAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10