Riwaya:penzi la mfungwa 15
ni nini hasa kinamfanya apotee katika mazingira yoyote? Pia ili ujanja wake huo utoweke njia gani itumike? Na je, hatomstukia pindi atakapo muuliza hayo maswali?
Maswali hayo yalimuumiza sana kichwa Veronica ila swali ambalo aliliona ni pasua kichwa ni kuhusu pindi pale Zabroni atakapo mstukia na kumuona kuwa hayupo naye kimapenzi zaidi ya kumpeleleza.
Siku moja asubuhi mapema Veronica alimpigia simu kamanda mkuu ili amsaidie japo ushauri kuhusiana na hilo swali. Kamamda akamjibu "Mpe mapenzi ya dhati,mfamye awe na furaha wakati wote. Naamini atanogewa na kukuona mtu wa muhimu kwake. Wanaume tukipenda tunakuwa kama mazezeta Kwahiyo nafasi hiyo itumie kumuuliza historia ya maisha yake japo kwa ufupi akisita kukwambia basi mtoe muende kupata kinywaji sehemu nzuri ya utulivu,hapo mmbembeleza kumnywesha pombe. Akilewa yote atasema ", aliongea kamanda mkuu. Veronica aliposikia maelezo ya kamanda wake alishusha pumzi ndefu kisha akajibu "Ahsante sana tutaendelea kuwasiliana"
"Sawa kuwa makini"
Baada ya maongezi aliirudisha simu juu meza halafu akajitupa kitandani. Siku hiyo hakwenda kokote, aliamua kupumzika.
Siku zilisonga..Mapenzi ya Vero na Zabroni nayo yakiendelea kushika kasi. Wiki mbili baadaye zilikatika bila ya wapenzi hao kuonana,hakika kila mmoja alimkumbuka mwenzie hasa hasa Zabroni aliyezama kwenye penzi la Veronica,alitamani sana amtie machoni kwani siku nyingi hawajaonana. Hivyo wakati analitamani hilo suala litokee,mara ghafla Veronica alifika kwenye ghetto lao ambalo aliwakuta vijana Zabroni na Bukulu wakicheza drafti.
Walimkaribisha lakini Veronica hakuweza kukaa bali baada ya salamu alimuita faragha Zabroni kisha akamwambia "Mpenzi unajua siku nyingi hatuja onana? Yote ni kwa sababu ya haraka za masomo chuo ndiyo ilinifanya nikawa kimya. Kwahiyo rasmi nimekuja nina hamu na wewe sana sijui hata nisemeje.
Chazaidi naomba ujiandae twende mjini ukakae japo siku sita tu tufurahi pamoja istoshe sijawahi kulala na wewe au hujui kama mimi na wewe ni wapenzi?.." alisema Veronica kwa sauti nyororo huku akimfuta futa Zabroni nyuzi za buibui kichwani,kwani alikuwa ameegemea ukuta. Kuta nyingi za nyumba za vijijini zinakuwa na utandu wa buibui.
"Najua kama unanipenda, basi kaa kidogo nijiandae ili twende lakini siku sita tu sizidishi sawa?.."
"Sawa mpenzi wangu",alijibu Veronica huku moyoni akiamini kuwa hizo ndio siku pekee za maangamizi. Siku ambayo Zabroni atakamatwa baada kusumbua sana. Siku za hatari.
Zabroni alijiandaa haraka haraka,alipokuwa tayari kwa safari alimuaga rafiki yake ambaye ni Bukulu. Bukulu alimtakia kila raheri huku akimtania kwamba ahakikishe anamfyonza mpaka yaliyofichwa. Zabroni alicheka sana akifurahishwa na maneno ya Bukulu, lakini yote kwa yote Zabroni aliondoka zake sambamba na Veronica.
Zabroni alijikuta akisahau masharti ya yule babu kutoka Nigeria, ikumbukwe kipindi Zabroni anajiwekea nia ya kulipa kisasi cha wazazi wake tayari alikuwa nyumbani kwa huyo babu. Kwani hakuwa na sehemu nyingine ya kuishi,nyumba yao iliteketea kwa moto huku wazazi wake wakifia ndani ingawa baba yake alikuwa ameshajinyonga.
Hivyo mzee yule kutoka Nigeria alimkabidhi dawa Zabroni ya kumfanya apotee mazingira yoyote,kitu kilicho mplekea Zabroni kulipa kisasi kwa uhuru huku akijivunia hiyo dawa. Na kila aliyejaribu kumfuatilia alipotezwa kama mzee Baluguza mganga nguli,lakini pia Madebe bila kumsahau Bruno.
Wote hao walipotezwa kiani yake. Lakini sharti moja ya hiyo dawa aliyopewa Zabroni ni kufanya mapenzi,endapo kama atafanya mapenzi basi dawa hiyo itapotea.
Walifika mjini,hapo sasa ndipo mkakati wa Veronica ulipoanza. Siku ya kwanza Veronica aliitumia kuzurula mjini hapo na Zabroni huku akimpitisha kwenye kumbi mbali mbali za starehe, kumbi za hadhi huku wakila na kunywa kwani bajeti aliyopewa Veronica ilidhihirisha kabisa. Hapo Zabroni akaamini kwamba mke kapata, kiasi kwamba ilimpelekea pole pole kumsahau Tina.
Siku ya pili,siku hiyo Veronica aliitumia kuzungumza na Zabroni kuhusu mahusiano yao ambayo yalionekana kunawili kila kukicha. Kiukweli mtukutu Zabroni alionekana kumpenda sana Veronica ikiwa upande wa Veronica,yeye hakumpenda abadani ingawa usoni alionyesha hisia kwa kwake ila ukweli ukiwa ni kwamba alikuwa kikazi. Ukitaka cha uvunguni sharti uiname ndio msemo aliodumu nao moyoni Veronica, afande aliyekabidhiwa jukumu la kumkamata Zabroni.
Katika ya mgawahawa mmoja ndani ya huo mji mdogo. Mgahawa ulionekana kuwa wa kifahari ,walionekana Veronica na Zabroni wakiwa wameketi huku wakinywa vinywaji. Tabasamu lao lilionyesha kuwa bashasha,vile vile kila muda walikuwa wakigongeana mikono kudhihilisha kwamba zogo walililokuwa wakipiga lilikuwa limenoga.
"Zabroni unajua kwamba wewe ni mwanaume mzuri sana?..na pia namuomba Mungu atujalie tuje tuzae watoto!", alisema Veronica akimwambia Zabfoni. Zabro aliachia tabasamu pana kisha akanywa kinywaji chake kilichokuwa ndani ya grasi halafu akamjibu "Asante sana,vile vile hata mimi naona ni bahati kuwa na mrembo kama wewe. Veronica we mzuri bwana"
"Kweli?.." alihoji Veronica.
"Ndio kwani huamini? "
"Sawa naomba tupendane mpenzi wangu",aliongeza Veronica ambapo waligongeana grasi ishara ya furaha halafu wakanyeshwana. Zabroni akimnywesha Veronica kinywaji chake,ilhali Veronica nae akijibu mapigo. Hakika furaha ilionyesha kutawala eneo hilo,na mwisho wa yote walishikana mikono wakarejea nyumbani kupumzika.
Usiku wa siku hiyo wala wa jana Veronica hakutaka kufanya naue mapenzi Zabtoni ingawa alimuweka katika matamanio,kitendo hicho kilimuumiza sana Zabroni kwani usiku wa jana aliamini kwamba huwenda akapewa kitumbua siku ya kesho ambayo ndio siku hiyo ambayo nayo ilionekana hakuna dalili yoyote ya kupewa ili ajilie vyake.
Sio kwamba Veronica alikuwa hajui jinsi Zabroni anavyoumia,lahasha alifahamu fika ila alifanya hivyo makusudi ili kesho yake amuulize mambo kadhaa wa kadha huku akimuahidi kumpa $$## chake endapo kama atamjibu inavyotakiwa.
INAENDELEA
Comments
Post a Comment