Riwaya:penzi la mfungwa 19
waliambizana kwamba waache waone nani mbabe. Hivyo walijifanya wako bize kupiga zogo ilihari huku wafungwa tayari wameshaweka uzio kwa duara ili kuangalia mpambano. Mtu wa kwanza kurusha ngumi alikuwa Bluyner, alirusha kumi na mateke harakaraka yaliyomfanya Zabroni kurudi nyuma akiyakwepa mateke hayo.
Lakini licha ya kurudi nyuma ila teke moja lilimpata,Zabroni akawa ameanguka chini. Nafasi hiyo Bluyner akaitumia kujirusha juu mfano wa sama soti kisha akatua moja kwa moja kwenye kifua cha Zabroni. Zabro alitema mate ya damu,wafuasi wake wakashika vichwa vyao ilihari upande wa wafuasi wa Bluyner wao walilipuka shangwe huku wakimtaja Bluyner kwa kumshangilia.
Upande mwingine yule Askari aliyempatia Zabroni hirizi alionekana kusikitika pia kuingia na hofu,alihofia uwezo wa Zabroni kupigana Bluyner kijana ambaye alionyesha uwezo wa juu kupigana.
"Amka sasa nikunyooshe! Amka sasa kama unayaweza",alisema Bluyner huku akipiga kifua chake. Zabroni aliweka mikono yake kifuani kudhihirisha kwamba kaumia eneo la kifua. Baada ya hapo alinyanyuka kisha akasimama ila kabla hajakaa sawa,Bluyner aliruka juu kwa mara nyingine akiwa angani alirusha mguu wa kulia juu ya kichwa cha Zabroni, na mguu wa kushoto ukawa umempata ambapo Zabroni alianguka chini kama mzigo kisha akaanza kupumua kwa shida. Pigo mbaya sana hilo alilopigwa kichwani kiasi kwamba alihisi Malaika mtoa roho anamnyemelea. Wakati huo huo Bluyner alimsogelea akachuchumaa chini akamtazama usoni,akacheka kisha akasema "Zabroni, wewe huna uwezo wa kupigana na mimi.
Amini kwamba walionichangua kuwaongoza nyinyi abadai hawakukosea,sasa iweje uthubutu kuangusha mwamba ulio shindikanika?", akacheka Bluyner kwa mara nyingine tena halafu akaendelea kusema "Umepima maji kwa kijiti pasipo kujua kuwa mahali hapa kuna kina kirefu,kwanini usizame? ", kwisha kusema hivyo alirudia tena kucheka kisha akakunja ngumi kwa niaba ya kumpiga Zabro lakini kabla hajaishusha ngumi,Steve alifika haraka sana akamshika mkono ule uliokuwa umekunja ngumi.
Wakati huo upande wa pili Askari waliokuwa na jukumu la kuwarinda na kuwasimamia hao wafungwa,wao walikuwa kando wakishuhudia huo mpambano. Askari mmoja kati yao alipotataka kuingilia kati alizuiwa na yule Askari aliyemrudishia Zabroni hirizi. Hivyo ikabidi watulie waangalie nani bingwa ingawa Askari huyo aliyempa hirizi Zabroni, moyoni hakuwa na amani kama Zabroni ataweza kuibuka kidedea.
"Bluyner, tafadhali naomba umuache. Tayari umejizihirusha kuwa wewe ni nwamba. Naomba usiendelee kumpiga utamuuwa kaka nielewe tafadhali", alisikika akisema hivyo Steve huku akiwa ameung'ang'ania mkono wa Bluyner uliokunja ngumi.
Bluyner alifura hasira mara dufu ambapo alinyanyuka kisha akamtazama Steve usoni,Steve aliogopa lakini hakusita kumuombea msamaha rafiki yake kipenzi. Bado aliendelea kumuombea msamaha Zabroni,kitendo ambacho kilipelekea kipigo kuhamia kwake.
Alipigwa sana Steve wakati huo Zabroni pale alipokuwa amelala ghafla kumbukumbu ilimjia, ambapo alikumbuka maisha ya nyuma kidogo kabla ile dawa iliyomfanya asumbue kila mahali haijapotea mwilini. "Mimi ni Zabroni! Mimi ni Zabroni",nisauti ambayo ilikuwa ikijirudia kichwani mwake wakati huo akikumbuka baadhi ya matukio aliyowahi kufanya.
Alikumbuka jinsi alivyomtumbua mama mjamzito, alikumbuka ugomvi mkubwa aliowahi kupigana na Madebe pia Bruno ambaye kwa sasa Mr Rasi. Yote hayo ikiwa ni ndani ya kulipa kisasi cha wazazi wake ingawa marehemu Madebe na Mr Rasi waliingilia ugomvi huo ukiwa hauwahusu.
Basi kumbukumbu za Zabroni hazikuishia kwenye matukio hayo tu lahasha alikumbuka zaidi mpaka alivyozama kwenye penzi la Afande Veronica pasipo kutambua kwamba Veronica ni Afande na yupo kwa niaba ya kumtia katika mikono ya sheria,jambo ambalo lilikwenda sawai.
Hapo sasa ndipo Zabroni alipotikisa mkono,mara ghafla akahisi kumuona mtu aliyevaa nguo nyeupe akimsogelea mahala pale alipoangukia baada kupokea kichapo kikali kutoka kwa Bluyner. Mtu huyo aliyevaa nguo nyeupe alikuwa akimfuata Zabroni huku akisema "Amka Zabroni, wewe ni mwanaume hupaswi kushindwa kizembe. Aaamka Zabroni amka babaaa ",sauti hiyo baada kulindima ipasavyo kichwani mwa Zabrini, hatimaye alijihisi kupata nguvu.
Alifumbua macho yake kisha akasimama,ilihari upande mwingine kijana Steve alikuwa akichezea kichapo huku baadhi ya wafungwa wakiingilia kati kumtetea ambapo baada kuonekana bado Bluyner anakuwa mgumu kumuachia,Askari nao waliingilia kati lakini Bluyner alizidi kumganda Steve akigoma kumuachia. Hivyo hapo pakawa hapatoshi,vurumai la kutisha lilizuka sehemu hiyo ila lilikuja kutulia baada kusikika sauti ya Zabroni ikisema "Mimi ni Zabroni! ",wafungwa wote akiwemo na Bluyner waligeuka kutazama kule ilipotokea sauti hiyo.
Walimuona Zabroni akiwa amesimama kidete huku mkono wake wa kulia wenye hirizi akiwa amekunja ngumi moja nzito ikiwa uso wake nao ukisweta jasho mchanganyiko na damu. Wafungwa baadhi walio mkubali Zabroni walishangilia baada kuona kidume kanyanyuka. Bluyner alizungusha shingo kuilaza kulia na kushoto,mishipa ililia mfano wa kijiti kilicho vunjika kisha akamsogelea Zabroni huku akiwa ametunisha mbavu zake.
INAENDELEA
Comments
Post a Comment