Riwaya:penzi la mfungwa 21

 


Ramso anamtafuta kwa udi na uvumba Veronica ambaye ni huyo rafiki yake kipenzi aliyekuja kumtembelea siku hiyo.


"Usijali tutaenda, pamoja", Zabroni alijibu pasipo kujua ni nani huyo anayekwenda kumuona.


Wawili hao walijiandaa haraka haraka kisha wakaanza safari;wakati huo jioni ishatoweka,giza totoro tayari lilikuwa limeshatanda ndani ya jiji la Dar es aSalaam. Walipokuwa ndani ya gari,Zabroni na mpenzi wake wakuitwa Lina walikuwa wakiongea mambo mbali mbali hasa hasa kuhusu mahusiano yao.


Lina alisema "Kiukweli Ramso sijatokea kumpenda mwanaume kama ninavyokupenda wewe,ndio maana baba alipotaka kukurudisha jela nikatishia kujiuwa "

"Ahsante sana kwa maneno yako matamu, je kwa mfano angenirudisha huko ungejiuwa kweli ama ulikuwa unamtisha tu?.."


"Kha Ramso,hakyaMungu ningejiuwa sitanii. Ujue mimi sipendi kukosa furaha katika maisha yangu. Lakini pia istoshe wazazi wangu wananipenda sana na ndio maana baba aliponiona nimeshika kisu haraka sana akakufungua pingu " alisema Lina huku akiwa amemgeukia Zabroni ambaye naye alionekana kuwa makini barabarani.


Inaendelea

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10