Simulizi: Jina la urithi 02

 


SEHEMU YA PILI (02) 


                    ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪


ni sauti ya mwanaume mzee kati ya watu hao wawili waliojitokeza kimiujiza,,kisha akaisogelea maiti hiyo akachomoa kisu na kukata kipande cha nyama katika mwili wa maiti hiyo.

Njile akatamani kutimua mbio,,lakini alishindwa kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu hata za kumuwezesha kutembea,,akastaajabu kumuona mzee huyo,,akimfuata,,na kumnyang'anya mtoto kwa nguvu! punde si punde yule bibi akazioiga hatua kumsogelea mzee huyo aliyekuwa kamshikilia mtoto mchanga,,Njile alipowatazama kwa makini wazee hao akashtuka kuona ni baba na mama wa mumewe,,kilichomshangaza zaidi wazee hao walikufa na wakazikwa miaka mingi iliyopita....wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla!!!!

TAHARUKI!!!!!!


                       ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪


Mzee huyo akachukua kile kipande cha nyama ya maiti ya baba wa mtoto huyo mchanga,,pamoja akamlambisha mtoto huyo,,kisha akamsogelea Njile kwa hatua za taratibu,,lakini hakuonekana kama anatembea,,miguu yake ilikuwa haikanyagi kwenye ardhi! mzee huyo naye akasema,,"mtoto huyu aitwe LAULA.

Njile akaingiwa na hofu lakini akajikuta anakuwa jasiri,,na kumpokea mtoto wake mchanga! alipomgusa mtoto huyo,,akahisi anaishiwa nguvu,,mwili wake ukawa regevu maradufu! akaona giza totoro limetanda mbele ya macho yake akapoteza fahamu,,,hakujua kilichoendelea....


Baada ya masaa kadhaa kupita,,akajikuta yumo ndani ya nyumba ya mwanamke ambaye alikuwa anaishi jirani na nyumba ya Njile,,mwanamke huyo alimpa msaada baada ya kumkuta Njile akiwa kalala kando ya barabara ndogo,huku mtoto mchanga akiwa juu ya kifuachake,,alimuonea huruma,,akamshawishi mumewe wampe msaada mwanamke huyo,,ndipo wakashirikiana kumbeba na kumpakiza kwenye kiti cha baiskeli,,wakaondoka nae mpaka nyumbani kwao,


Njile akauliza kwa mshangao! ,,"hapa ni wapi,,na nimefikaje hapa?

mwanamke aliyempa msaada akasema,,"mimi na mume wangu tulikukuta ukiwa umelala kando ya barabara, na ulikuwa umemkumbatia mtoto wako kifuani..mwanamke huyo aliongea maneno hayo huku akimuonyesha mtoto...Njile akachukua mwanae na kuanza kumtazama kwa macho ya huruma,,akajikuta anatokwa na machozi! akainua uso wake kumtazama mwanamke huyo,,kisha kafuta machozi na kusema,,"asante kwa kuokoa uhai wa mimi na mwanangu,,Mungu akubariki!

pumde si punde Njile akahisi maumivu makali sehemu zake za siri...kumbe wakati anamsukuma mtoto atoke tumboni alichanika sehemu zake za siri,,sasahivi kapata ufahamu na maumivu anayasikia! 

ye msamalia akauliza ,,"ilikuwaje mpaka ukajifungua katika mazingira hayo!? Njile akasita kuongea kwa sekekunde kadhaa kisha akasema,,"ndugu we acha tu, ni stori ndefu,,ambayo hata mimi sielewi imekuaje! kifupi ni kwamba uchungu uliponishika nilihangaika sana,,,nilijitahidi kutoka nje ya nyumba,,angalau nipate msaada lakini,,Mungu si Athumani,wala Mabula,,wakati natoka nje ya nyumba,,ndio wakati ambao mume wangu alikuwa anarudi nyumbani...baada ya kuongea maneno hayo,,Njile akasita kuendea kusimulia...akajikuta anatokwa na machozi...

ye msamalia akaingiwa na wasiwasi,,akihisi huenda mume wa Nje alimoiga mkewe n akumtelekeza huko....hivyo msamalia huyo akawa na shauku ya kutaka kujua mume wa Njile yuko wapi? na ni sababu zipi zilizomfanya amtelekeze mkewe katika hali ile!

Njile akafuta machozi kisha akasema,,"mume wangu amekufa..

msamalia akashtuka! akauliza kwa mshangao,,kafa?? 

Njile akaitikia ,,"ndio kauwawa!

Msamalia huyo akazidi kustaajabu! akajisemea moyoni ,,"mara kafa mara kauwawa! bila shaka mwanamke huyu atakuwa kaathiriwa na mazingira yale aliyojifungulia,,lakini naimani akili zake zitakaa sawa,, na ufahamu wake utarejea...lakini cha kushangaza Njile alionekana kuendelea kulia mfululizo tena kwa uchungu wa hali ya juu! kitendo hicho kilimfanya msamalia huyo,,ahisi kunajambo ambalo halipo sawa! na linamtatiza Njile.

akauliza kwa sauti ya unyenyekevu,,"niambie umeoatwa na nini? naomba usinifiche jambo hata moja,,ili nijue namna ya kukusaidia.

aliongea maneno hayo huku akimfuta Njile machozi yaliyokuwa yametapakaa kwenye mashavu.

Njile akaendelea kusimulia,,"wakati tupo njiani kuelekea hospitali...uchungu ulinizidia,,na chupa ya uzazi ilikuwa tayari imeshapasuka,nikamwambia mumewangu anilaze chini nijifungue,,kwa sababu niliamini hatutofika mbali,,kutokana na hali yangu ilivyokuwa,,wakati na najifungua,,,nikashangaa mume wangu anahangaika,,kuvuta pumzi,,huku akiwa kashikilia sehemu ya shingo yake,,mwanzo nilihisi ni utani,,lakini kadri sekunde zilivyozidi kusonga akadondoka chini na kutulia tuli..

ghafla wakajitokeza wazee wawili,,ambao ni baba na mama yake..lakini wazee hao walishakufa miaka mingi iliyopita! wakati Njile anaendelea kusimulia,,ghafla yule mzee akajitokeza ndani ya nyumba ya msamalia huyo! Nje aliweza kumuona mzee huyo,,akasita kuendea kusimulia,,macho yakamtoka na hofu ikazidi kuongezeka,,

Ye msamalia akastaajabu,,kumuona Njile amebaki kimya huku macho yake yakitazama uoande mwingine kwa muda mrefu...akaamua kugeuza shingo yake naye aone Nje anatazama kitu gani kilichomfanya akodoe macho. alipogeuza shingo yake,ghafla mlango ukafunguliwa kwa pupa!!!

KIZAA ZAA!!!!!


↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔


Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

Chombezo: mwajamu utamu sehemu ya 15 (mwishoo)