Simulizi; Jina la Urithi 03
SEHEMU YA TATU(03)
⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
mwanzo nilihisi ni utani,,lakini kadri sekunde zilivyozidi kusonga akadondoka chini na kutulia tuli..
ghafla wakajitokeza wazee wawili,,ambao ni baba na mama yake..lakini wazee hao walishakufa miaka mingi iliyopita! wakati Njile anaendelea kusimulia,,ghafla yule mzee akajitokeza ndani ya nyumba ya msamalia huyo! Nje aliweza kumuona mzee huyo,,akasita kuendea kusimulia,,macho yakamtoka na hofu ikazidi kuongezeka,,
Ye msamalia akastaajabu,,kumuona Njile amebaki kimya huku macho yake yakitazama uoande mwingine kwa muda mrefu...akaamua kugeuza shingo yake naye aone Njile anatazama kitu gani kilichomfanya akodoe macho. alipogeuza shingo yake,ghafla mlango ukafunguliwa kwa pupa!!!
KIZAA ZAA!!!!!
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
akashtuka,,,akashika kifua chake upande wa moyo,,huku akipumua kwa haraka,,,kumbe Njile alikuwa katika dimbwi zito la mawazo,,,akikumbuka matukio yaliyotokea miaka sita iliyopita,
na aliyefungua mlango si mwingine,,ni yule mtoto wake,,kwa sasa anamiaka sita...hizo ni kumbukumbu zilizomjia katika mawazo,
Njile akauliza kwa mashangao! ,,"kulikoni mbona umefungua mlango kwa pupa?
mtoto Laula akajibu,,"nimeona limtu linaniita, linatisha!
Njile akashtuka akaanza kudadisi kwa kumuuliza maswali mtoto wake,,"anafananaje?
Laula akajibu,,"ni mzee nilishawahi kumuona,,
Njile akamtazama mwanae kwa macho ya umakini huku akisikiliza kile anachokiongea Laula.
Njile akahisi kuchanganyikiwa,,akasema,,"mwanzo ulimuona wapi?
kama ilivyokawaida ya watoto,,huwa wanaeleza jambo kama jinsi alivyoliona,,hapunguzi neno wala haongezi neno,,Laula akasema,,"kunasiku alikuja nyumbani usiku,,nikakuamsha lakini haukuamka,,akqsema eti ni babu yangu..akanichukua na kunipeleka hukooo!!!!
Njile akashtuka! akajisemea moyoni,,"bila shaka yale mambo yameanza upya! lakini kwanini mimi tu?
alijisemea maneno hayo kwa uchungu...kisha akamkumbatia mwanae,,ghafla Laula akauliza,,"baba atakuja lini? mbona harudi?
Njile akajikuta anaangua kilio!
kwa sababu alimdanganya mwanae kuwa baba yake amesafiri...alishindwa kumwambia ukweli wa mambo yaliyotokea miaka sita iliyopita hivyo miaka hiyo yote Laula anajua kuwa baba yake kasafiri,,huwa anamuuliza mama yake mara kwa mara kuhusu baba yake! lakini Njile aling'ang'ania msimamo wake kuwa baba yake Laula kasafiri.
****BAADA YA MIAKA MINNE KUPITA*****
Laula alitimiza umri wa miaka kumi(10)
siku zilisonga na maisha yakaendelea,,lakini katika kijiji hicho kukawa na uvumi kuwa Laula ananguvu za kimiujiza,,watoto wa lika lake walishuhudia maajabu mbalimbali wakati wakiwa wanacheza na Laula....lakini hakuna aliyeamini maneno ya watoto hao! kadri miezi ilivyozidi kusonga Laula akawa tishio kwa watoto wenzake! hata shuleni walimu walimuogopa kwa sababu,,kila mwalimu aliyethubutu kunyanyua mkono wake kumpiga Laula,,basi mwalimu huyo,,anapoteza uhai usiku wa siku hiyo hiyo...
pamoja na hayo yote,,Laula huyafanya hayo pasipo kujitambua,,na wakati anafanya matukio hayo,, huwa anapoteza kumbukumbu juu ya alichokifanya!
failia ya Laula ikawa ni tishio la kijiji hicho,,,
siku moja nyakati za usiku wa manane,, Laula alidamka kutoka usingizini,,lakini macho yake hakuyafumbua! akazioiga hatua kuufuata mlango,,ghafla akatoweka kimiujiza! akajitokeza kwenye eneo la makaburi,,akaendelea kuzipiga hatua na kulifuata kaburi moja lililokuwa katikati ya makaburi mengine! kaburi hilo linasadikika kuwa ni kaburi la Muanzilishi wa ukoo wao,,alizikwa miaka zaidi ya miamoja iliyopita,,na jina lake aliitwa LAULA,,na mrithi wa jina lake ni Laula huyu ambaye ni mtoto pekee wa mwanamke Njile!
kumbe kuna siri nzito ambayo alikuwa anaijua Baba yake Laula...mbaya zaidi alikufa pasipokusema maana chimbuko la Jina hilo alilomrithisha mwanae wa pekee.
ilikuwa hivi,,enzi za ujana wa baba Laula,,alikuwa anaugua ugonjwa ambao haikujulikana ni ugonjwa gani,,kumbe baba baba mzazi aliwahi kumtukana marehemu baba yake ambaye ni babu yake baba Laula,,na siku ambayo anakufa mzee huyo alisema,,daima kizazi chako hakitafanikiwa kuishi katika dunia hii,,aliongea maneno hayo na kukata roho papohapo...
miaka ilizidi kusonga,,hatimae baba Laula akazaliwa,,,lakini aliishi na kufanikiwa kuoa Lakini akaanza kuota magome ya miti katika mwili wake akapelekwa hospitali lakini haikufahamika anaumwa ugonjwa gani,,,ndugu zake wakaamua kumpeleka kwenye tiba mbadala wakampeleka kwa mganga wa kienyeji....mganga akasema,,mkitaka mtu huyu apone,,ni lazima akafukue kaburi la muanzilishi wa ukoo wake,,achukue jino la mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake...ikalazimika afanye hivyo! siku hiyo akadamka usiku wa saa sita akaelekea makaburini! alipolikaribia kaburi hilo mara ghafla!!!!!
↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔
Comments
Post a Comment