Simulizi: Jina la urithi 10.

ADMIN
0



                ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪


Laula akashtuka kumuona mtu huyo akimtazama kwa macho ya msisitizo! akaamua kumuuliza,,"mbona wanitazama? kuna jambo ambalo haliko sawa?

yele mtu akaamua kudanganya akasema,,"nilikuwa najaribu kukumbuka jambo fulani,,

aliongea hivyo huku akizioiga hatua kurudi upande wa jikoni....alipofika katika korido,,ghafla akasikia tena vitu vikidondoka kule chumbani...sasahivi hata vyombo vilivyokuwa katika kabati la vyombo jikoni,, viligongana na vingine kupasuka...jambo hilo lilimfanya mtu huyo aingiwe na hofu...punde si punde likatokea tetemeko la ardhi na nyumba ikaanza kutikisika....mara ghafla!!!!!!!!!


                 ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪


yule mwanamke akahisi kama kamuona mtu akitokea chumbani kwake na kuingia katika chumba kingine!! mtu huyo alikuwa kavalia mavazi yaliyochakaa na yenye kuchanika chanika!

hofu ikazidi kuongezeka akapaza sauti, akauliza kwa mshangao!

wewe ni nani? umeingiaje humu ndani?

aliongea maneno hayo huku mwili wake ukitetemeka,na mapigo yake ya moyo yalipiga kwa kasi ya ajabu!

punde si punde tetemeko la ardhi likatoweka kimiujiza,,vile vitu vilivyodondoka chini,,na vyombo vilivyopasuka,,vilirudi katika hali ya kawaida kama vilivyokuwa mwanzo!

macho yakamtoka,,tangu azaliwe hajawahi kuona maajabu ya namna hiyo! akaamua kutimua mbio kuelekea sebuleni,,akaparamia mlango akaufungua kwa pupa na kutoka nje ya Nyumba!

kitendo hicho kilimfanya Laula naye aingiwe na hofu,,akatimua mbio na kutoka nje kwa sababu mlango ulikuwa wazi! alikimbia pasipokujua kinachoendelea,,ni kama alifuata mkumbo.


wakati huo huo kule chumbani,,ulionekana ule mzimu! ukiendelea kumtafuta Laula,,lakini haukufanikiwa kumpata Laula.

Laula aliendelea kukimbia,sasahivi hata njaa ilibaki stori!

upande mwingini yule mwanamke akiwa njiani ghafla ule mzimu ukajitokeza mbele yake! ili amuangamize ,,kwa sababu yeye ndiye aliyesababisha Laula kukimbia ndani ya nyumba ile! mwanamke yule akapatwa na mshtuko akadondoka chini na kupoteza fahamu..ghafla ule mzimu ukasita kumfuata mwanamke huyo pale chini alipodondoka! mzimu ukageuza shingo yake upande wa kushoto,,kwa kuhisi Laula yupo upande huo! punde si punde ukatoweka kimiujiza kumtafuta Laula amabaye ni mrithi wa jina lake!


Upande mwingine,,kule kijijini,,ukimya ulitawala,,hakuonekana hata mwanakijiji mmoja akirandaranda,,wote walijifungia ndani ya nyumba zao,,sauti ya ndege warukao angani....hakuna aliyethubutu kutoka nje! baada ya masaa kadhaa kupita,baadha ya wanakijiji wakatoka nje ya Nyumba zao,,ni baada ya ukimya wa masaa kadhaa...sasahivi hapakuwepo na hali ya kutisha...ikapigwa mbiu,,wanakiji watoke ndani ya nyumba zao na kuendelea na shughuli zao kama kawaida...baada ya lisaa limoja kupita! wale walioshiriki kuchoma nyumba ya Njile,,wakaanza kufa moja baada ya mwingine! walikufa vifo vya kutatanisha katika nyakati tofauti tofauti..jambo hilo liliwashtua wanakijiji,haijawahi kutokea vifo vya watu zaidi ya kumi kufa kwa siku moja tena ni vijana shupavu na wachapakazi ndani ya kijiji hicho!hofu ikazidi kuongezeka kwa wanakijiji.


masaa yalizidi kusonga,,hatimae giza likaanza kutanda,,Laula akonekana akiwa kwenye mkusanyiko wa watu wakitazama mpira wa miguu kwenye Runinga! akaona si haba naye ajumuike nao huenda akapata angalau msaada aweze kupata mlo...alisimama hapo kwa dakika kadhaa,,aliposogeza mguu wake akahisi kama kakanyaga kitu chini ya unyayo wake!! akainamisha uso wake kutazama ni kitu gani hicho! akaona ni pochi ndogo ya mfukoni..lakini akashindwa kuokota pochi hiyo kutokana na mkusanyiko wa watu wengi hivyo hapakuwa na nafasi ya kuinama.

wakati Laula anafanya jitihada za kuinama,,akaonekana ni msumbufu..hivyo mtu aliyekuwa amesimama nyuma yake akahisi kama Laula anataka kumuibia,,

kutokana na umri mdogo wa Laula akafukuzwa eneo hilo,,aende akalale,,huo sio muda wa watoto kuwepo maeneo hayo.

Laula akaondoka zake kishingo upande huku akisononeka rohoni,,kwa sababu aliamini ile pochi inapesa ndani yake......

baada ya Laula kuondoka,,ghafla ule mzimu ukajitokeza katika mkusanyiko wa watu hao,,ni baada ya kugundua kuwa mrithi wa jina lake yuko katika eneo hilo ,,kumbe Laula aliondoka dakika chache zilizopita!!! watu wote waliokuwepo katika eneo hilo wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,kila mtu alitimua mbio na kupita njia yake,,huku wengi wao wakipiga kelele za uwoga! 

Laula hakuwa mbali sana,,,akazisikia kelele hizo,,akageuza shingo yake kutazama kule kwenye mkusanyiko wa watu wengi...akaona wanatimua mbio,hakujua kinachoendelea akaona hiyo ndio nafasi pekee arudi kuichukua ile pochi pale chini!

bila kuchelewa akatimua mbio kuelekea huko!


ITAENDELEA.....

Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top