⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪
Laula akashtuka kumuona mtu huyo akimtazama kwa macho ya msisitizo! akaamua
baada ya Laula kuondoka,,ghafla ule mzimu ukajitokeza katika mkusanyiko wa watu hao,,ni baada ya kugundua kuwa mrithi wa jina lake yuko katika eneo hilo ,,kumbe Laula aliondoka dakika chache zilizopita!!! watu wote waliokuwepo katika eneo hilo wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,kila mtu alitimua mbio na kupita njia yake,,huku wengi wao wakipiga kelele za uwoga!
Laula hakuwa mbali sana,,,akazisikia kelele hizo,,akageuza shingo yake kutazama kule kwenye mkusanyiko wa watu wengi...akaona wanatimua mbio,hakujua kinachoendelea akaona hiyo ndio nafasi pekee arudi kuichukua ile pochi pale chini!
bila kuchelewa akatimua mbio kuelekea huko!
⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪
Laula aliendelea kukimbia kwa kasi,lakini alistaajabu kuona watu wakisamabaa kutoka eneo lile kuelekea upande mwingine......Laula akasita kuendelea kukimbia ,,akasimama aakageuza shingo yake huku na kule kutazama ,,huenda akaona chanzo na sababu ya watu kukimbia,,hakuweza kuona kitu chochote.........akaangaza macho yake kutazama ile sehemu aliyoona ile pochi ndogo...akafanikiwa kuiona pochi hiyo akazipiga hatua za haraka haraka,,kuifuata.
alipokaribia eneo hilo...akasita akahisi kama kaona kitu lakini kitu hicho ni kama kimepita kwa kasi mbele yake! akainama kuokota ile pochi ndogo,,,ghafla ukajitokeza ule mzimu! Laula alilishuhudia hilo,mzimu huo ukatoweka kimiujiza,,ghafla Laula akahisi kunakitu kimeingia ndani ya mwili wake! punde si punde Laula akasimama wima! akatoweka kimiujiza.
upande mwingine kule kijijini,,alianeka mwanaume mmoja akizipiga hatua kutokea porini! mwanaume huyo alikuwa kavalia ngozi ya fisi ,huku upande wajuu akiwa kifua wazi! shingo yake ilionekana kujawa na kamba nyingi zilizoshikilia irizi! mkononi alikuwa kashikilia mkia wa mnyama NYATI, kwa kumtaza kwa haraka bila shaka ni mganga wa kienyeji.
aliendelea kuzipiga hatua kuelekea katika kile kijiji kilichokumbwa na janga ambalo mpaka sasa halijafahamika chanzo chake.
baada ya masaa kadhaa kupita akawa amefika katika kijiji hicho,,,wanakijiji walimshangaa sana mtu huyo,,wengi wao walimkumbuka,,kwa sababu mtu huyo anasadikika kuishi porini miaka mingi iliyopita! alikuwa na nguvu za ajabu zilizojaa mambo ya kimiujiza...kwa wazee au watu wazima waliozaliwa miaka ya 60. walimtambua mtu huyo alikuwa anauwezo wa kukutazama machioni na ukafa papo hapo! mtu huyo aliogopeka kama aogopwavyo mnyama mkali.
Wazee na watu wazima waliozaliwa miaka ya 60 ,,wakaanza kutimua mbio kwa kuhofia usalama wa uhai wao..
kitendo hicho kikazua gumzo kwa wanakijiji ambao ni vijana,,wakaingiwa na hofu....pia na wao wakatimua mbio!
gjafla ikasikika sauti ikisema,,"msikimbie,,nimekuja kwa nia njema,,kuwasaidia kwa sababu nami ni mzawa wa kijiji hiki...sauti hiyo ilisikika ndani ya masikio ya kila mwanakijiji hata ambaye hakuwepo katika eneo hilo! kwa muda huo!
baadhi ya wanakijiji wakaanza kuingiwa na imani,,wakaamua kurudi kumsikiliza mtu huyo!
baada ya dakika kadhaa wanakijiji wakawa wamekusanyika kwa wingi!
bila kuchelewa mtu huyo akasema,,"nadhani baadhi yenu unanikumbuka,,lakini napenda kuwatoa hofu kuwa nimekuja kuondoa tatizo ndani ya kijiji hiki! kuna jambo ambalo hakuna anayefahamu ukweli wowote kuhusu hilo,,tatizo ni JINA.
mtu huyo aliongea hivyo kwa msisitizo kisha akasita kuongea neno lingine,,
mwana kijiji mmoja akauliza kwa mshangao,,"JINA!!?? limefanyaje?
yule mtu akatabasamu kisha akageuza shingo yake kutazama upande wa pili,,akasema" ndio,,tatizo ni jina,,na jina hilo ni la urithi ndilo linalozua mabalaa katika kijiji hiki!
wanakijiji hawakuelewa anachokizungumza,,japokuwa wamesikia maneno aliyoyaongea! ikazuka minong'ono wanakijiji hao wakiongea chini chini!
yule mtu akasema,,"mimi ninanguvu za kimiujiza,,na haya niliyaona kabla hayajatokea! nani kati yenu anamkumbuka mwanamke NJILE?
wanakijiji wakashtuka! ghafla ikasikika sauti kutoka katikati ya mkusanyiko wa wanakijiji hao ikisema,,"mwanamke yule alizaa mtoto wa ajabu! bila shaka alikuwa ni mchawi,,na tulimfukuza katika kijiji hiki!
kabla hajamaliza kuongea sentensi yake...ukasikika mvumo wa upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu...upepo huo ulitoa mlio wa kutisha ukitamka maneno haya,,"MIMI NDIYE.........
ITAENDELEA.....
