Simulizi: Sitaisahau Tanga 04.



SITAISAHAU TANGA 4:

Nikakosa raha kabisa, nikarudi na kukaa kitandani nikaamua kujilaza nikitafakari, mara sms ikaingia kwenye simu yangu kuangalia ni yule binti wa kitanga "angalia mezani nimekuletea chakula"

Loh nikainuka kama nimepigwa shoti vile, kuangalia naona juisi ya Azam mango na biskuti, nikawaza kuwa ameletaje vitu vile nikaanza kupata mashaka, mara sms nyingine ikaingia

"usiogope mpenzi, kula tu"

Nilikosa amani kwakweli, nikasogelea ile juisi na kuiangalia kama ni juisi kweli ndio ilikuwa Azam mango kabisa na ndio juisi niipendayo, mmh nikaziangalia na zile biskuti zilikuwa biskuti za ukweli kabisa zile zenye mchanganyiko wa chokleti, kutokana na njaa yangu nikaanza kuvifakamia huku bado niliwaza ameletajeletaje.

Nilipomaliza tu, akapiga simu.

BINTI: Vipi mpenzi umeshiba?

MIMI: Ndio nimeshiba, kwani umeviletaje?

BINTI: Hata kushukuru hujui?

MIMI: Samahani mpenzi nilijisahau.

Akakata simu, nikakaa na mawazo pale kitandani. Mara simu ikaita kuangalia ni dada anapiga tena.

DADA: Vipi wewe yani huna hata hofu na mwenzio?

MIMI: Aaah dada samahani.

DADA: Kwahiyo unakuja au huji?

MIMI: Aaah sijui dada.

DADA: Hujui nini? Nipe jibu moja, unakuja au huji?

MIMI: Sitaweza kuja kwa leo dada, nitakuja kesho.

DADA: Nilijua tu, mxyuuuu (akanisonya na kukata simu).

Nikawa pale kitandani nimejiinamia tu huku kichwani mawazo mengi yamenitawala, mara sms ikaingia kwenye simu yangu

"si ulale mpenzi wangu jamani"

Nikaamua kujilaza huku nikijiona bonge la boya maana nipo kama vile mtu anayeongozwa na rimote.

Mara usingizi ukanipitia pale kitandani, nililala hadi nikajisahau nikaja kushtushwa na mlio wa simu.

RAFIKI: Vipi kaka mbona leo hujatokea maeneo?

MIMI: Kivipi ndugu wakati ndo kumekucha!

RAFIKI: (huku akinicheka), kumekucha wakati saa kumi na moja jioni hii?

MIMI: (nikafungua pazia na kuchungulia dirishani, kumbe kijua cha jioni ndio kipo ukingoni), acha masikhara bhana saa mbili hii (huku nikiangalia saa yangu ya ukutani).

RAFIKI: (Akinicheka tena), wee boya saa kumi na moja hii labda kama leo una kazi ya ulinzi ndio mida ya kujiandaa hii (akinicheka tena).

MIMI: (Nikiangalia vizuri ile saa ya ukutani, iliyoonyesha mshale mdogo kwenye tano na mkubwa kwenye nane), daah nilichanganya mida kaka.

Nikakata simu na kuanza kuwaza imekuwaje nimelala hadi kujisahau vile, ni usingizi wa namna gani ulinipata dah!! Mara rafiki yangu akaanza kupiga tena.

RAFIKI: Kaka, vipi ule mpango wa kwenda kwa mtaalam au umepotezea?

MIMI: Hapana sijapotezea kaka, nataka sana unipeleke itakuwaje sasa?

RAFIKI: Wewe tu, nilitaka nikupeleke leo au unaona yale majanga yako ya kawaida kaka?

Kabla sijamjibu simu ikakatika, na kuanza kuita tena kuangalia ni binti wa kitanga.

BINTI: Ulikuwa unaongea na nani?

MIMI: Rafiki tu mpenzi wangu.

BINTI: Ulikuwa unaongea nae kuhusu nini?

MIMI: Hamna kitu ni salamu tu.

BINTI: Unanificha sio?

MIMI: Hapana sijakuficha huo ndio ukweli.

BINTI: Wee ni muongo eeh!! Haya njia ya muongo fupi na mi naijua.

Akakata simu, nikabaki kwenye maswali na viulizo vya kila aina. Kwanza nikawaza juu ya usingizi niliolala hadi kusahau kuamka kwenda popote pia kusahau kula. Nikajiuliza inamaana sijala chochote tangu nilipokula juisi na biskuti usiku. Mara sms ikaingia,

"usijari mpenzi kula na kuoga na vyote vya muhimu umefanya ndotoni"

Aaah majanga haya!!

ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10