Simulizi: Sitaisahau Tanga 09
Nikajihisi kama kupagawa hivi na wala sikujua cha kufanya kwa muda ule. Mara mlango ukagongwa,
MIMI: Nani wewe?
KAKA: Mimi hapa kaka yako.
MIMI: Kaka si nimekwambia usije tena jamani!
KAKA: Acha masikhara wewe, hebu nifungulie mlango.
MIMI: Hapana kaka, wee nenda tu.
KAKA: Kwani una nini wewe? Hebu fungua huko.
Kaka akawa anasukuma sukuma mlango, ikabidi niinuke na kwenda kufungua mlango, kaka akaingia ndani moja kwa moja nami nikaurudishia mlango.
KAKA: Hiki ndicho ulichokuwa unanikataza nisiingie ndani, umemfanyaje mwenzio?
MIMI: Sijamfanya kitu kaka.
KAKA: Sema ukweli mdogo wangu, umemfanyaje huyu?
MIMI: Sijui kaka ameanguka mwenyewe.
KAKA: Aaah acha masikhara bhana, ataangukaje mwenyewe? Fanya fasta tumpeleke hospitali.
MIMI: Haitawezekana kaka.
KAKA: Haitawezekana kivipi bhana? Hebu njoo tuite msaada hapo nje tumbebe tumpeleke hospitali.
MIMI: Unajua nini kaka....(kabla sijajibu vizuri, simu yangu ikaanza kuita)
Nikaipokea ile simu,
BINTI: Kaka yako anataka kujua kilichompata rafiki yako?
MIMI: Ndio.
BINTI: Mpe simu nimweleze mwenyewe.
Nikampa simu kaka ili aongee nae ila kabla ya kuongea akaniuliza,
KAKA: Kwani ni nani?
MIMI: Wee ongea naye tu.
KAKA: Nitaongea vipi na mtu nisiyemfahamu?
MIMI: Ongea naye tu kaka.
Kaka akachukua ile simu, ikawa ni kitendo cha sekunde tu kwani kaka alianguka chini kama gunia huku jasho jingi likimtoka na macho akiwa ameyatoa tu, nikaanza kupatwa na uoga kwani kaka hakuongea chochote. Nikajiuliza yule binti kawafanya nini wale hadi hawajitambui tena. Roho ikawa inaniuma sana hata sikujua cha kufanya kwa muda ule kwakweli nilihisi kuchanganyikiwa kabisa nikatamani nichimbe shimo nijifukie.
Nikiwa bado natafakari yale yaliyopo, mlango wangu ukagongwa tena kwa nguvu.
MIMI: Nani wewe unagonga kwa nguvu hivyo?
DADA: Mimi hapa
MIMI: Wewe nani ndio? (kana kwamba nimeisahau sauti yake)
DADA: Dada yako ina maana huijui sauti yangu?
MIMI: Nenda tu dada.
DADA: Vipi tena jamani?
MIMI: Weee nenda tu bhana.
DADA: Niende wapi jamani mdogo wangu wakati nimekuja kwako?
MIMI: Nenda bhana, sitaki mgeni.
DADA: Kwani kaka yuko wapi?
MIMI: Sijui bhana, wee nenda.
DADA: Unajua unanichanganya wewe, unachogoma kunikaribisa humo ndani ni nini?
MIMI: Nenda bhana mbona huelewi wewe?
DADA: Ok, ngoja nikamchukue mama nije nae ili tujue unachoficha humo.
MIMI: Usifanye hivyo dada, dada dada (kimya alikuwa ameshaondoka).
Nikazidi kupagawa sasa dada ameenda kumchukua mama si balaa hili litanipata jamani mimi dah.
Yule binti akanipigia tena simu,
BINTI: Ndugu zako wanajua kufatilia mambo eeh?
MIMI: Sikuelewi jamani sikuelewi.
BINTI: Hunielewi eeh!! Ngoja utanielewa wakifika hao ndugu zako.
MIMI: Tafadhari usiwatende vibaya.
BINTI: Wameyataka wenyewe, na watanijua vizuri mtoto wa kitanga.
MIMI: Jamani jamani nakuomba tafadhari usinifanyie hivyo.
BINTI: Si nilikwambia uwakataze umeshindwa? Sasa ndio utajua vizuri leo.
Akakata simu nikabaki kupagawa tu na wala nisijue la kufanya. Nilijihisi kama vile mtu aliyechanganyikiwa.
Nikiwa bado na mawazo, nikasikia sauti ya mama na dada nje ina maana nao wamefika kwangu. Nikajihisi baridi ikipenya mwilini mwangu, nilikuwa nikitetemeka balaa. Sikuwa na raha wala furaha.
Mara sms ikaingia kwenye simu yangu,
"yote yale yalikuwa ni majaribio sasa picha kamili itaanza."
ITAENDELEA
Comments
Post a Comment