Simulizi; Sitaisahau Tanga 14
Nikiwa nimechoka kukimbia, nikaanguka chini na lile joka likanisogelea karibu kabisa nilikuwa natetemeka sana.
Lilipofika karibu yangu likabadilika tena na kuwa mwanamke mzuri sana tena mwenye kuzidi mvuto na urembo kushinda yule wa kwanza, nikawa naogopa sana, yule mwanamke akanishika mkono na kunisimamisha, akaniangalia sana kisha nae akaniuliza tena kwa sauti ya kubembeleza,
"vipi mimi unanihitaji?"
Nikawa nimetoa mimacho na kutikisa kichwa, gafla niliona yule mwanamke amegeuka na kuwa simba nikaanza kukimbia tena yani nilikimbia sana, ila nikigeuka nyuma naona ni bonge la simba likinikimbiza.
Nilizidi kukimbia ila mbele nikakutana na mto ile wakati nauvuka nikiwa nimejawa na uoga tela nikajikwaa na kuanguka chini ila niliangukia jiwe kubwa kwahiyo nikapoteza fahamu.
Kwa matumaini yangu nilijua nikishtuka pale basi nitakuwa duniani yani kwenye ardhi yenye watu wa kawaida kama mimi.
Ila niliposhtuka nilijikuta nimewekwa kitandani tena nimevuliwa nguo zote na kubaki mtupu kabisa, pembeni yangu alikuwepo mwanamke mrembo sana nae akiwa mtupu kabisa alikuwa ananipaka vitu kama mafuta ya maji ila ni malaini sana, akawa ananisiliba na kufanya kama vile ananikandakanda mwili mwangu. Mmh nikawa natetemeka sana, nikamwomba Mungu anipe ujasiri mkubwa kwa wakati huo tena ikiwezekana basi niwe kama mwanaume asiye na nguvu za kiume tena.
Yule mwanamke alizidi kunikandakanda kwa mtindo wa kupapasa mwili wangu, alishuka hadi sehemu zangu za siri, nilizidi kutetemeka tena niliogopa sana ni kweli sikupatwa na hisia zozote kwa wakati ule najua Mungu alinisaidia.
Yule mwanamke kuona kuwa hata sionyeshi dalili yoyote ya mshtuko wa hisia akachukia sana, akaanza kunifanyia mambo ya ajabu ajabu hata hayafai kuelezea, nilikuwa kama kifaranga cha kuku kilichoachwa na mamaye, kwakweli nilikuwa mpweke na mwenye huzuni kubwa.
Yule mwanamke akaniamuru niinuke pale, nami nikainuka, akiwa vile vile mtupu akatangulia mbele ili nimfate nyuma, nilijitahidi kukwepesha macho yangu maana haya macho haya ndio yanayotutia majaribuni vijana wengi sana.
Nikaongozana nae hadi kwenye kisima, kile kisima kilikuwa cha maajabu kwani maji yake yalikuwa yakitokota sana.
Nikiwa nae pale kisimani, akaniuliza,
"unanihitaji?"
Nikazidi kutetemeka mahali pale, nikawa nimemkodolea macho tu, akasema tena,
"nijibu, unanihitaji?"
Niliogopa kujibu kwani nilijua wazi ni jambo gani lingefatia, nilizidi kutetemeka, yule mwanamke akanikazia macho kuashiria kuwa anahitaji jibu, nami nikatikisa kichwa kuashiria kuwa simuhitaji, akachukia sana na pale pale akanitumbukiza kwenye kile kisima kwakweli niliiva tena sana nilitokota kama vile napikwa ili niliwe, nililia mule kisimani hadi nikapoteza tena fahamu.
Kuja kushtuka nilijikuta nipo Tanga tena eneo lile lile ambalo nilikutana na yule binti, na tena mbele yangu alikuwepo yule yule binti wa kitanga.
Akanishika mkono na kunipeleka eneo lile lile ambalo mimi na yeye tulikuwa tukikutana na kupiga story nyinginyingi, nikawa natetemeka kwani sikujua ni nini anachotaka kunifanyia.
Alikuwa na mkoba, mara akatoa boxer kwenye ule mkoba wake, akaniuliza
BINTI: Unaikumbuka hii? (akinionyeshea ile boxer).
MIMI: (Nikashangaa gafla nimepata uwezo wa kuongea), ndio naikumbuka.
BINTI: Uliiacha wapi?
MIMI: (Nikijaribu kuvuta kumbukumbu ya sehemu nilipoiacha ile boxer).
BINTI: Hakikisha uwe sawa na majibu utakayo toa kwani jibu lako linaweza kukuokoa au kukuangamiza, na pia usinipe jibu la kubuni nataka jibu la ukweli na uhakika. Ninazo hapa kama hizi tano na zote ni za kwako kwahiyo uwe na majibu ya uhakika.
Nikawa nimemtumbulia mimacho tu huku nikifikiria cha kumjibu.
ITAENDELEA
Comments
Post a Comment