Simulizi: Sitaisahau Tanga 15



Nikiwa sina kumbukumbu nzuri juu ya ile boxer nikawa nimetoa macho tu hata nisijue cha kujibu. Akaniuliza tena,

BINTI: Inamaana hukumbuki uliiacha wapi?

MIMI: (Nikiwa nasua sua cha kujibu), eeh ndio sikumbuki.

BINTI: Unamkumbuka Penina?

MIMI: (Nilishtuka sana na hata sikujua huyu binti wa kitanga amemjulia wapi Penina), aah eeh ndio namkumbuka.

BINTI: Haya niambie unamkumbuka kivipi?

Hapo nikakumbuka wazi kuwa ile boxer niliisahau kwa Penina, nikamwambia yule binti wa kitanga kuwa nimemkumbuka penina sababu ya ile boxer.

BINTI: Kwanini uliacha hii boxer kwa penina?

MIMI: Penina alikuwa mke wa mtu, siku hiyo hatukujua kama mumewe anarudi katika purukushani ya kukimbia baada ya kufumaniwa ndio nikasahau boxer yangu.

BINTI: Nini kilifuata baada ya kufumaniwa?

MIMI: Penina alifukuzwa na mumewe na hivyo akaja kwangu na kudai kuwa ana mimba yangu kwa kuogopa msala na mimi nikamfukuza.

BINTI: Je unajua kilichompata Penina baada ya wewe kumfukuza?

MIMI: Hapana sijui.

BINTI: Penina alilazimika kwenda kutoa ile mimba na huko ndiko akapatwa na umauti. Je nikikupa lawama juu ya kifo cha Penina nitakuwa nimekuonea?

MIMI: (Nikiwa nimetumbua mimacho tu kama mtu nisiyejielewa), aaah mmh sijui.

BINTI: Na kwanini ulitembea na Penina wakati ulijua ni mke wa mtu? Je ulikuwa na lengo la kumuharibia ndoa yake?

MIMI: (Bado nilijiumauma wala sikuwa na jibu la moja kwa moja).

Yule binti wa kitanga aliniangalia kwa macho makali sana hadi nikaanza kuogopa, akaingiza mkono tena kwenye mkoba wake na kutoka na boxer nyingine, akaniuliza tena.

BINTI: Na hii je uliiacha wapi?

MIMI: (Nikiwa na mshangao mkubwa kuwa amezipata wapi zile boxer, ambazo hata mimi mwenyewe sina kumbukumbu ya mahali nilipoziacha. Nikabaki kutumbua mimacho tu.), mmh sijui.

BINTI: Unamkumbuka Aisha?

MIMI: Ndio nimemkumbuka, hiyo boxer niliiacha kwake wakati baba yake ametubamba kwahiyo nilivyokimbia nikaisahau.

BINTI: Baada ya wewe kukimbia nini kilifuata?

MIMI: Aisha alikuja nyumbani na kudai kuwa ana mimba yangu kwavile sikutaka makubwa ikabidi nikimbie ila hata niliporudi sikupata tena habari zake.

BINTI: Haya, Aisha naye alienda kutoa ujauzito wako ili arudi kwao akiwa mtoto safi kwa bahati mbaya umauti ukamshika. Je na yeye hujasababisha wewe kifo chake?

MIMI: (Nikiwa natetemeka kuwa vipi mimi nikawa vile hadi hao wakapatwa na umauti).

Nikiwa natafakari, akatoa tena boxer nyingine,

BINTI: Na hii uliiacha kwa Nana, naye alikuwa mke wa mtu. Kwanini uliiacha?

MIMI: Niliogopa mumewe angenifumania.

BINTI: Sasa boxer hii ndio ilimfanya Nana apigwe na mumewe hadi mauti ikampata. Je nimlaumu mume au wewe?

MIMI: Hata sijui kitu.

BINTI: Siku zote hujui kitu, inamaana wewe hutambui uyafanyayo?

MIMI: Natambua.

BINTI: Je adhabu ulizopata umeonewa?

MIMI: Hapana sijaonewa.

Akaingiza tena mkono kwenye mkoba,

BINTI: Na hii uliiacha kwa Salma kwanini?

MIMI: Salma alikuwa ni demu wa rafiki yangu ili mwenyewe asigundue katika harakati nikaiacha hiyo boxer.

BINTI: Unajua kilichofuata?

MIMI: Rafiki yangu alipoikuta, Salma akamwambia ukweli ila Salma alipokuja kwangu nikalazimika kumtimua kwani sikutaka kugombana na rafiki yangu sababu ya mwanamke.

BINTI: Na Salma alikosa mwelekeo akanywa vidonge na kujiua kwaajili yako.

MIMI: (Nikiwa nashangaa sana, kwani sikujua kama Salma alijiua kwaajili yangu).

BINTI: Mabinti wengi wametoa mimba kwaajili yako na hiyo ni sababu tosha ya mimi kwenda kuivuruga mimba ya demu wako wa dar.

MIMI: (hapo ndio nikaelewa kwanini mimba ya demu wangu wa dar ilitoka), haaa kumbe!!

Akaingiza mkono tena na kutoa boxer nyingine,

BINTI: Hii pia uliiacha kwa Tamari, niambie kuhusu Tamari.

MIMI: Tamari alikuwa ni rafiki wa demu wangu, nakumbuka ni yeye alinilazimisha niache boxer kwake.

BINTI: Vipi alipokwambia anaujauzito wako?

MIMI: Nilijua ni mbinu zake za kuniachanisha na mpenzi wangu, kwahiyo nikamkana.

BINTI: Naye akaenda kutoa mimba na kufa. Je unajua kwanini wasichana wengi wanakufa wakienda kutoa ujauzito wako?

MIMI: Hapana sijui.

BINTI: Nitakwambia sababu.

Akaniangalia na kunikazia macho sana, safari hii alitoa boxer na kuongea kwa ukari,

BINTI: Katika boxer zote na matendo yake machafu, hii ndio boxer iliyonikera na ndiyo itakayofanya upate adhabu tena.

Akainuka na kuniambia kuwa nimuandalie majibu yanayoeleweka juu ya ile boxer. Bado sikujielewa kwanini nilikuwa naacha zile boxer na kwanini ziniletee matatizo kila sehemu nilipo ziacha. Na bado nikajiuliza kwanini hao wadada walikufa wakati wanatoa ujauzito wangu, bado sikuwa na jibu ila nikangoja majibu kwa huyu binti wa kitanga ambaya hadi muda huo sikuelewa ni jini au ni mchawi au ni mzimu au ni mtu wa aina gani kwani bado alinichanganya sana.

ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10