Simulizi: Sitaisahau Tanga 16



Nikiwa sijielewi elewi kabisa na huku nikijiuliza maswali mengi mengi.

Yule binti wa kitanga akarudi na kunishtua,

BINTI: Haya niambie ni wapi uliacha hii boxer?

MIMI: Samahani, niliacha kwako kwa bahati mbaya.

BINTI: (Akacheka sana), bahati mbaya! Ulikuwa na maana gani?

MIMI: Sikuwa na maana yeyote ile nilijisahau tu.

BINTI: Ulijisahau tu au ulitaka kuonyesha jinsi gani wanipenda?

MIMI: Aaah mmh sijui.

BINTI: (Akacheka tena), kwahiyo hukunipenda?

MIMI: Naam!

BINTI: Kwani nimekuita au nimekuuliza, kwahiyo hukunipenda?

MIMI: Mmmh Sijui.

BINTI: Wewe una matatizo sana, yani hujui kama ulinipenda au la?

MIMI: Mmmh ndio sijui.

Akaniangalia kwa macho makali sana kama vile anasoma kitu kwenye ubongo wangu. Nikawa na mawazo ya uoga kichwani mwangu, akanigeukia na kuniuliza tena.

BINTI: Unamjua Leila?

MIMI: Ndio namjua.

BINTI: Eeh kwanini ulimdanganya yeye na familia yake kuwa unaenda kutoa mahari?

Nikabaki natoa mimacho tu na kushangaa huyu binti ameyajuaje yote hayo, maana nilipokuwa na Leila nikapenda niwe nae karibu zaidi kwahiyo nikaenda kupeleka barua kwao ili nitambulike ila ilipofika kipindi cha mahari hapo ndio utata ulianza maana sikuwa na jinsi zaidi ya kuwadanganya kuwa nitaenda ila nikawapotezea. Nikashangaa sana huyu binti amejuaje.

Akaniuliza tena,

BINTI: Kwanini hukumfatilia tena Leila?

MIMI: Ujana tu ndio ulinisumbua dada.

BINTI: Heeee, nishakuwa dada yako tena?

MIMI: Mmmh aaah sijui.

Akacheka sana na kuniangalia kwa dharau,

BINTI: Haya unajua kwanini wanakufa wakitoa mimba zako?

MIMI: Sijui chochote.

BINTI: Wanakufa kutokana na zindiko ulilofanyiwa ukiwa mdogo, mama yako ukimuuliza atakwambia.

MIMI: Mmmmh

BINTI: Je unajua hatma ya Leila ilikuwaje?

MIMI: Sijui.

BINTI: Leila alichanganyikiwa sana kwa aibu uliyompa kwao, akaamua kujiua. Tatizo umetembea na wanawake wengi ndiomana ukimwacha mmoja humfatilii tena.

Bado nikawa sijielewi na mawazo lukuki juu ya huyu binti wa kitanga.

Akaniambia nimuulize swali nitakalo.

MIMI: Vipi mchumba angu wa dar, je ni mzima?

Akacheka sana, kisha akaniambia nimfuate. Nikainuka na kuanza kumfuata, mara gafla nikamuona Leila amesimama mbele yangu, nikaanza kutetemeka na kuogopa sana, nikiwa sijielewi nilistukia nikichapwa viboko kila sehemu. Mbele yangu alikuwepo Leila na yule binti wa kitanga, nilichapwa sana hadi nikapoteza fahamu.

Niliposhtuka nilikutana na giza nene yani sioni chochote cha mbele yangu. Nilipoinuka mahali pale, nikaanza kutembea kwa kupapasa ila kila nilipokanyaga nilikanyaga mwiba kumbe pale chini palijaa miba mitupu.

Kwahiyo ikanipasa kutembea kwa tahadhari, nilipofika mbele nikakutana na yule binti wa kitanga, akaniambia "njoo huku" nikawa namfata, kufika mbele gafla akatokea binti mmoja niliyemjua kwa jina la Salma, huyu alikuwa ameshika gongo kubwa sana akanibamiza nalo kichwani, nikaanguka na kupoteza fahamu.

Kuja kushtuka nilikuwa kwenye mto mkubwa tena katikati, nilitetemeka sana mwili ulipatwa na baridi ya ajabu, nikaogopa sana pale katikati ya mto.

Nikaanza kujikongoja taratibu ili niweze kutoka kwenye ule mto, wakati nafika juu yani nimeshatoka mtoni akatokea mtu na kunisukuma tena gafla mtoni nikawa natapatapa na kuhangaika, kumwangalia vizuri yule mtu ni yule binti wa kitanga, nikabaki natahamaki na nikaamua kumuuliza.

MIMI: Je hizi ndio adhabu zangu?

BINTI: (Akacheka sana), hapana hapa tunacheza tu kama kombolela, adhabu yenyewe ni moja tu utaipata.

Nikanyong'onyea gafla kwani mwili wote ulikuwa una niuma yani kila sehemu ni maumivu tupu.

ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10