Simulizi: Sitaisahau Tanga 19

 


SITAISAHAU TANGA 19:

Sikutegemea nilichokiona, niliposhtuka nikajikuta nipo kitandani, nikamwona mpenzi wangu akiwa pembeni yangu pale kitandani, nikawa nashangaa shangaa tu.

Nikamwona yule mpenzi wangu akifurahi sana kuwa nimeamka na akaharakisha kwenda nje, kurudi ndani akawa ameongozana na yule mdada aliyekuja na mke wa rafiki yangu, yule mdada mwenye maruhani.

Nikawa bado nashangaa shangaa tu. Bado sikuelewa kitu, nikazidi kushangaa shangaa tu. Kitu cha kwanza kabisa nikawaambia,

MIMI: Naombeni maji ya kunywa.

Kabla sijajibiwa, mara simu yangu ikaanza kuita muda ule ule niliposhtuka, nikawa napapasa ili niipokee, mara yule mdada wa mwanzo akaniamuru nimpatie ile simu, nilipompatia akaniambia,

MDADA: Hii ndio imekusababishia mambo yote.

Nikashangaa kivipi simu imenisababishia mambo yote yale. Na alipoichukua yule dada ile simu ikaacha kuita.

Kwanza nikawa sielewi wala siamini kama nipo kwenye ulimwengu wa kawaida. Nikaanza kuwashangaa tu yule mdada na mpenzi wangu, huku nikijiuliza maswali mengi mengi imekuwaje wakawa pamoja na wengine wako wapi. Pia nikashangaa kile chumba kwani kilikuwa ni chumba tofauti kabisa na chumba changu.

MIMI: Mbona humu sio chumbani kwangu? (huku nikizidi kushangaa).

MDADA: Ipo sababu kubwa ya kukuondoa mule kwenye chumba chako.

MIMI: Mbona sielewi?

MDADA: Ndio huwezi kuelewa mpaka utakapoeleweshwa.

MIMI: Niambieni kwanza, nipo dunia ya kawaida au dunia ya kinyumenyume?

MDADA: (Akacheka), upo kawaida, na upo salama sasa. Ila usalama wako utaongezeka pale utakapoamua kuinuka hapo ili twende baharini ukaoge maji ya bahari, na hii simu(akionyesha ile simu yangu aliyoshika), tunaenda kuitupa baharini.

Sikuweza kubisha wala kupinga, nikainuka pale nikiwa mimi yule mdada na mpenzi wangu. Tukakodi kibajaji kikatupeleka hadi baharini.

Kufika pale baharini, nikajishangaa nimekuwa mzito sana kuitupa ile simu, nikajikuta nikisita kufanya hivyo. Yule mdada akaniambia,

MDADA: Unapenda kuishi maisha ya kawaida?

MIMI: Ndio napenda.

MDADA: Basi tupa hiyo simu.

MIMI: Ila simu yangu ni ya gharama sana jamani.

MDADA: We itupe tena uirushe mbali kama unayapenda maisha yako, nitakupa sababu ya kufanya hivyo.

Roho iliniuma sana kila nikiangalia ile simu, nilizidi kuumia moyoni. Yule mdada akaniangalia tena kwa macho makali na kusema,

MDADA: Tupa hiyo simu.

MIMI: Ujue nilinunua laki tano hii simu!

MDADA: Haya, laki tano na maisha yako kipi bora?

MIMI: Bora maisha yangu.

MDADA: Basi itupe hiyo simu.

Bado nikawa nasitasita, nilimtazama mpenzi wangu naye aliniangalia kwa jicho la huruma sana, nikapatwa na mfadhaiko wa moyo nikakumbuka yote niliyowatenda wadada kwa tamaa zangu. Nikakumbuka mateso niliyopata kwenye dunia ya kinyumenyume.

Hapo nikaamua kuchukua maamuzi magumu na kuirusha ile simu katikati ya maji, mara gafla nikashtuka,

MIMI: Aaah laini yangu!!

MDADA: Imefanyaje?

MIMI: Nimeitupa nayo.

Kabla hajaniambia kitu tena mara gafla tukaona moshi mwingi ukitokea pale nilipoirusha ile simu, nikaanza kutetemeka kwa uoga. Yule dada akaniambia kuwa niingie kwenye maji ili niweze kujisafisha zile nuksi na mabalaa. Ila bado sikujua wale ndugu niliowaacha ndani ni nini kimewapata, je ni wazima au wamekufa, nikaamua kumuuliza yule dada,

MIMI: Na ndugu zangu je ni wazima au wamekufa?

MDADA: Hilo swali niulize baada ya kujisafisha ndio nitakupa jibu. Nikamwangalia tena yule mpenzi wangu bado alionyesha huruma sana na hata sikumwelewa kuwa ananihurumia mimi au anaonyesha huruma ya nini.

Nikaangalia tena pale nilipoirusha simu yangu bado palikuwa panafuka moshi.

Yule mdada akaniamuru tena kuwa niende kwenye maji nikaoge, ila nikawa nasita kufanya hivyo na yule mpenzi wangu alizidi kunyong'onyea na pia alizidi kuonyesha huruma.

Nikaamua kwenda kuoga hayo maji ya bahari, yule dada akanielekeza sehemu ya kwenda kuoga ilikuwa ni mbali kidogo na pale nilipoitupa ile simu yangu na pia akanionya kuwa nisifike pale nilipoitupa simu yangu.

Nikiwa ndani ya maji ya bahari, wazo likanijia kuwa nisogee karibu zaidi na nilipoitupa ile simu labda nitaiona tena.

Nikawa nimesogea karibu huku nikiwa kama naogelea kumbe najaribu kupapasapapasa, ili kama nikiipata basi niitoe ile laini yangu tu. Mara gafla maji yakawa ya moto sana mule baharini hadi yakawa yananiunguza, wakati nataka nikimbilie nchi kavu, nikakuta kuna mtu amenishika bega kwa nyuma ile kugeuka ni macho kwa macho na binti wa kitanga, amefikaje na anataka nini sijui.

ITAENDELEA

Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10