SITAISAHAU TANGA 20:
Nilipogeuka nyuma nikakutana macho kwa macho na binti wa kitanga, nilianza kutetemeka kwa hofu na uoga, akawa ananiangalia huku anacheka nikazidi kutetemeka. Nilipoangalia kule nchi kavu nilimwona yule mdada akininyoshea mkono kama ishara ya kuniita, nikawa najitahidi nitoke ila yule binti wa kitanga alining'ang'ania na hadi nafika nchi kavu yeye alikuwa nyuma yangu.
Yule mdada akaniuliza tena kwa ukali,
MDADA: Umefanya vitu gani wewe?
MIMI: Sijui.
MDADA: Hujui nini? Unadhani angekufuata huyo bila sababu?
MIMI: Naomba nisaidie basi, nilienda kule nilipoitupa ile simu.
MDADA: Yani wewe umeharibu kila kitu.
Nikamwona yule dada akichukua kiwembe na kuja karibu yangu, akanichana kwenye mkono, nilipatwa na maumivu makali akanizuia kusogea popote mpaka pale aliponichana pakikauka damu.
Nikiwa naugulia yale maumivu, nikamwona yule dada akienda pembeni na kuongea kitu na mpenzi wangu, mara wote wakanisogelea pale.
Nikamwona yule dada akichukua tena kiwembe na kumchana mpenzi wangu mkononi halafu akachukua ile damu iliyokuwa inamtoka mpenzi wangu na kunipaka shingoni halafu yeye na yule mpenzi wakasogea mbali.
Kwa muda mchache nilihisi kama nataka kukata roho kwani maumivu yaliyonipata pale shingoni yalikuwa makubwa sana, hadi nikajikuta nikianguka kwenye maji na kuanza kutapatapa.
Ninachokumbuka nilipoteza fahamu.
Niliposhtuka nilijikuta nipo nyumbani, nimelala kwenye jamvi na wote ninaowafahamu wakiwa wamenizunguka, hadi yule mdada nilimwona pale kasoro mpenzi wangu tu ndiye hakuwepo pale.
Wote niliwakuta wamefurahi na nilikuwa kama mtu niliyepoteza dira.
Wakaniacha nipumzike bila kuniuliza chochote.
Baada ya siku mbili, ikabidi niongee nao kwani nilikuwa sielewi chochote.
MIMI: Mama mbona sielewi chochote, ilikuwaje kwani?
MAMA: Ni vigumu kuelezea ila umetufanya kupata majeraha yasiyosahaulika kamwe.
MIMI: Na kile chumba changu imekuwaje mama?
MAMA: Kile chumba tulikirudisha kwa mwenye nyumba kwani ungeendelea kukaa pale kungekuwa na makubwa zaidi.
MIMI: Ila mama, inaniwia vigumu kukuelewa.
Basi mama akamwita yule mdada ili nipate kuzungumza naye pia.
MDADA: Sikia, janga ulilolipata ni kubwa sana. Mimi nisingeweza kukusaidia ila babu yangu ni mtu wa huko na anajua vitu vingi.
MIMI: Kwahiyo watu walioanguka chumbani kwangu, waliamkaje?
MDADA: Kuna dawa niliwapaka wakaamka, ile dawa iliwezakufanya kazi baada ya wewe kukubali kujitoa kafara.
MIMI: (Kuna kitu nikajifikiria na kuamua kuuliza), mbona wakati nipo kwenye ulimwengu usio wa kawaida simu yangu sikuiona halafu niliposhtuka kawaida ikaanza kuita?
MDADA: Simu yako haikuwa simu ya kawaida, yule dada alikubadilishia simu muda mrefu sana ndiomana kila jambo ulilotaka kufanya ukiwa na ile simu aligundua kwa haraka.
Nikawa nawaza amebadilishaje, na mbona nilikuwa naiona kawaida.
MIMI: Ila ndugu zangu ni wazima?
MDADA: Ndio ni wazima ila...
MIMI: (Nikadakia), ila nini na yuko wapi mpenzi wangu?
MDADA: Ndio huyo ninayetaka kumuongelea.
MIMI: (Huku mapigo ya moyo yakienda mbio), kafanyaje?
MDADA: Amejitoa kwaajili yako.
MIMI: Sikuelewi, unamaanisha nini?
MDADA: (akainamisha kichwa chini na kuniambia), kwa bahati mbaya tumeshindwa kumwokoa kwahiyo amekufa.
Nilihisi utumbo ukijisokoto na tumbo likaanza kuniuma gafla.
MIMI: Hapana hapana sitaki kuamini.
MDADA: Huo ndio ukweli.
Niliona machozi yakinitoka, nilijisikia vibaya kujua yule msichana ambaye ni mpenzi wangu amekufa kwaajili yangu. Roho iliniuma sana.
Wakawepo watu pale kunifariji na kunipa moyo. Nikajiona nimepata kovu ambalo sitalisahau tena.
Rafiki yangu akaja pale na kunipa moyo.
RAFIKI: Pole sana ila yote ni mapito tu.
MIMI: Asante ila nimeumia sana.
RAFIKI: Hata sisi hatuelewi, na je sikuzote ulizopoteza fahamu ulikuwa wapi? Maana yule dada alituambia kwamba upo eneo la hatari sana.
MIMI: Ni kweli tena yalikuwa majanga sana ila ninachoweza kusema hadi sasa ni kuwa SITAISAHAU TANGA.
MWISHOoooo....!!!
