Nina hamu mwenzio.
( PATRICK akaona acha ale kisela anafika mlangoni afunge mlango anaona unagongwa anayegonga joji white)
" PATRICK Samahani.
( PATRICK akafungua mlango akatoa kichwa tu)
" Niambie joji.
" Naomba unisindikize hospital anjel anaumwa sana.
" Dah poa Shemeji anaumwa sana.
" Yah hapa nishaita uba inakuja twende ndugu mimi sijawai kuuguza naona mtihani kweli.
" Poa.
( PATRICK akaingia ndani akamwambia amina)
" Angel ugonjwa umemzidia namsindikiza hospital ukitoka funguo niweke chini ya zulia.
" Poa ila angel na yeye kwanini asiumwe Kesho.
( PATRICK akutaka kusikiliza sana akatoka wakamchukua anjel wakampeleka hospital sasa anjel analia ila joji kubembeleza mgonjwa ajui anamfokea)
" Jikaze anjel watu wote wanatuangalia sisi mpaka aibu jikaze kidogo.
" Siwezi tumbo linauma sana mume wangu uuuwii linauma.
( PATRICK ndio anabembeleza)
" Pole Shemeji litakaa Sawa tu ngoja tumuone dokta.
" Sawa shemeji.
( Walipofika hospital anjel anazidi kulia sasa watu wote wanamwangalia yeye hapo joji anamwambia anjel)
" Nitakuacha na Shemeji yako mimi mambo aya siyawezi unalia kama mtoto mdogo.
" Mume wangu naumwa sifanyi makusudi.
" Ndio ulie si ujikaze hapo tumbo je ukienda kujifungua itakuwaje.
( PATRICK anamwambia joji)
" Uyu alii kwa kupenda maumivu yanasababisha kulia mpe maneno ya falaja sio kumfokea.
" Mimi izo pigo sina PATRICK wewe pambana na Shemeji yako mimi nitakuja baadae yani watu wote wanatuangalia sisi.
( Joji aliondoka...PATRICK akaingia nae chumba cha Dokta...dokta akampima akasema)
" ngoja tumpe kitanda kwanza kuna dawa izi ameze.
" Sawa dokta.
" Wewe ni mumewe au kaka yake.
" Ni Shemeji yake.
" Basi toka nje anatakiwa apunguze nguo ya juu hili apate hewa nzuri.
( Anjel akasema)
" Dokta muache tu Shemeji yangu asitoke nje.
" Sawa.
( PATRICK alikaa na anjel...na anjel alifunuliwa brauzi kidogo tu na Dokta sasa anjel akishika tumbo anaisi maumivu yanapungua ila sasa mwili unamuwasha akamuomba PATRICK)
" Naomba unishike tumbo mimi nijikune naona mwili unawasha.
" Sawa Shemeji.
( PATRICK ameshika tumbo la Shemeji yake uku anjel anajikuna kuna anasikia raha PATRICK anajali....dk 30 akakaa Sawa kidogo...PATRICK akatoa mkono na Dokta akasema)
" Kuna sindano atachoma mbili saizi atapumzika alafu Kesho utamleta amalizie mbili.
" Sawa.
( PATRICK akamwambia Shemeji yake)
" Angel mimi natoka nje unatakiwa uchomwe sindano mbili.
" Shemeji naomba unishike mimi muoga wa sindano.
" Vumilia ndio uzima wako.
" Najua nitavumilia ila naomba unishike usitoke nje.
" Sawa.
( Dokta kweli alimchoma sindano mbili za makalio uku PATRICK ndio kamshika Shemeji kaona robo ya makalio....baada Muda kwenda akawapa ruxsa...PATRICK anampigia joji)
" Oya tayari upo wapi?
" Nipo home.
" Kwaiyo?
" Chukua usafili uje nae mimi utanikuta home.
" Poa.
( Anjel aliumia kimoyoni yeye yupo hospital mumewe karudi home ila PATRICK anamliwaza kwa maneno matamu ya falaja...mpaka anjel anatamani angekuwa mke wa PATRICK...kweli walifika walimkuta joji ametulia anaangalia tv anjel akasema kimoyoni....ungekuwa na TV kama ya PATRICK ata hospital usingenisindikiza wewe.......ila anaongea kimoyoni...PATRICK akawaaga)
" Jamani mimi naenda kulala.
" Poa PATRICK nashukuru sana mwamba mimi siwezi kuuguza kama atalia tena nitakuita.
( Anjel anatamani ajibu....basi nikalale kwa PATRICK....ila kanyamaza ammalizi mumewe...PATRICK akasema)
" Joji unatakiwa ujue kuuguza mgonjwa afokewi anatakiwa falaja.
" Kipaji icho sina Poa wewe nenda kalale.
" Poa.
( PATRICK anarudi chumbani kwake mlango umefungwa na funguo ajaacha pale chini amina...anawaza akamgonge mke wa mtu je kama mumewe karudi itakuwaje?...alikaa chini anawaza amina au yupo ndani...akazunguka dirishani kuchungulia ndani amna mtu...sasa na wingu la mvua limetanda akaona liwalo na liwe akaenda kugonga chumbani kwa amina)
" NGO NGO NGO.
( Kumbe kweli mume wa amina alikuwa karudi..amina kuchanganyikiwa simu ya mumewe alifunga mlango wa PATRICK na akaondoka na funguo...sasa PATRICK anagonga aliyetoka ni mume wa amina)
" Karibu PATRICK niambie mbona usiku unagonga kwangu kulikoni?.
ITAENDELEA
PATRICK ATAJIBU NINI?
