Shuhuda uchaw............i upo ndugu zangunii

 


Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.


Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.


1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.


Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.


Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.


2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.


Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.


Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.




Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.


3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.


Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.


Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.


Mungu ni mwema siku zote.


Comments

Popular posts from this blog

Chombezo : Huruma Ya Dudu Sehemu Ya : Pili (2)

Leyla binti bikra -01

SEHEMU YA 06---10