HUBA-01

ADMIN
0

 


Anaanika Laura Pettie

HUBA

Kwako kipenzi Laura najua utashangaa sana ukiona hii meseji ya kwanza coz sijui kama ulitarajia nitakuja kukuandikia kitu kama hiki but kupitia ukurasa wako nimejifunza naweza kuwa huru naweza kusema ya moyoni naweza kuongea na wewe lolote bila kuhukumiwa au kusemewa maneno mabaya, so niko hapa kukusimulia kipande kidogo au labda kirefu kuhusu huba langu ama niseme tutajua as the story goes on


Kabla ya yote niseme mimi nina usikivu hafifu kama ambavyo nimeona mara nyingi sana unazungumzia hili na ndio nimepata confidence zaidi kukuandikia nilipoipitia wall yako kimya kimya, napenda namna unavyoelimisha kwa lugha nyepesi ila yenye kueleweka na kutia moyo, nakupenda sana Laura sana sana sana kwa hiyo nipokee ukijua anayekusimulia ana hali gani na najua wewe utanielewa kila hatua, nikisema nina usikivu hafifu 


(Kwa wale ambao hawafahamu usikivu hafifu ni nini. Ni kwamba msimuliaji si kiziwi kwamba hasikii kabisa. Hapana. Ni usikivu wake umeshuka kwa kiasi fulani.) 


Mimi nilizaliwa mzima kabisa kama watu wengine wala kwetu hatuna historia na hili tatizo au kuugua masikio. Nimesoma vizuri kabisa mpaka mwaka wa kwanza chuo muhula wa pili ndipo nikapata hii hali. 


Ilianzaje? Nilikuwa nikiitwa siitiki haraka so nikawa nasemwa pembeni kuwa naringa, mara nina dharau, halafu kingine roommate wangu alikuwa analalamika nafungulia muziki kwa sauti ya juu sana while mimi nilikuwa naona mbona sauti iko kawaida tu, kihivyo kufika mwaka wa tatu hali ilikuwa si hali Laura, yaani kuzungumza na mtu ni mtihani. 


Imagine wakati wote huo sikuwahigi kwenda hospitali nilikuwa nahangaika mara mafuta ya kuku mara mafuta ya nyoka mara kwenye maombezi yaani wakati huo kila kitu kilikuwa kigumu mno.


Kutoka kusikia vizuri kabisa bila msaada wa mtu wala kuandikiwa au sijui mtu kurudiarudia hadi kuwa na usikivu hafifu my life changed drastically. Watu tuliochangamana vizuri tu walianza kuacha kunizungumzisha na kunishirikisha vitu, wanasema yule kuongea naye kazi sana, wengine wakawa wananifanyia viishara vya ajabuajabu nisiposikia vizuri, nikaanza kuitwa kiziwi kwa namna hivi kama kebehi si kebehi as if hiyo hali iliua jina langu. Nilikuwa najifungia room naliaaa namuuliza Mungu why me? Why now? Adhabu gani hii? 


Kuna baadhi ya walimu walikuwa wakifika darasani wanasoma maswali, utajijua na masikio yako, ukimfata ukimwambia unaweza ukasaidika ukapewa karatasi ya maswali au akakwambia we andika unachosikia, nilikuwa nafeli test hizo na najua why basi naumia naumia naumiaaaa. Mtu asipokupa update ya matangazo ujue imekula kwako, niishie hapo nilipita pagumu sana ila nikahitimu. 


Nimemaliza chuo nina msongo wa mawazo kupitiliza najiuliza nani ataniajiri sasa na kama najiajiri naanzia wapi Laura mpaka nilikuwa naogopa hata kuongea na watu, maana ukionyesha tu husikii vizuri mtu anaanza kukutazama kama mzigo flani, mwingine anakuona huna akili timamu, mwingine anakuona tu hujiwezi basi


Watu wa karibu nao unafiki mwingi unaomba msaada wa kukusikilizia mkifika hiyo sehemu anaona kazi tena kukusaidia kusikia. Anaongea na mhusika halafu hakwambii ameambiwa nini anakupa majibu short short, i have suffered Laura acha tu. Nilikuwa naona giza tupu na HAKUNA aliyewahi kunitia moyo Laura uwiiii hakuna, si nyumbani si marafiki kwanza ndio wanakunafikia mpaka mwisho ukija kusikia unayofanyiwa mgongoni unaumia mara mbili.


Sasa nimekuja kuongelea Huba langu, basi kipindi namaliza chuo nilikuwa na boyfriend ambaye tulisoma wote kidato cha sita, tukaenda wote  chuo kimoja. Tulikuwa na ahadi zetu nyingi na kila mtu alikuwa anajua mimi na yeye ni couple, sasa wakati mimi naanza kuhangaika na masikio mwenzangu akaona nimekuwa mzigo sasa unajua hata ile kucommunicate alianza kuona kama namchosha, akaanza kunipotezea. Tulikuwa tunapigiana sana simu ghafla mawasiliano yakawa meseji zaidi, unamtumia ujumbe saa  2 asb anakuja kuujibu saa sita usiku tena short tu, kisa huwezi  pokea tena simu, nikavumilia tu najipendekeza hivyo hivyo namshikilia asiniache, mwaka wa pili akaanzisha mahusiano na rafiki yangu tuko darasa moja grupu moja la assignment 


Huyo rafiki niliwahigi hata kumuuliza mwanaume kama anamtaka maana kuna vitu niliviona haviko sawa, akaruka yaani alikataa baadae akaanza kunijibu fikiria unavyotaka kumbe nyuma huku wanakulana, basi nikaja kujua nimezungukwa niliumiaaaaa  hilo likawa pigo la pili, imagine pamoja na kujua nilienda kwa mwanaume nikamwomba asiniache awe na sisi wawili hivyo hivyo nitavumilia, jibu alilonipa ilibaki kidogo ninywe simu ile siku, nashukuru nililia nikalia nikasema Mungu ni wetu sote.


Sikatai kuachwa kupo ila angalau angeenda mbali basi kwa heshima yangu maana ilikuwa gumzo la aibu kwangu nimeachwa kwa uziwi wangu nilidhalilika vibaya sana au basi angeniambia sababu ya kuniacha kuliko mateso ya kisaikolojia huku anajua mwenzake napitia mabadiliko magumu sana


Nikatoka chuo, nikaja mtaani. Nilikuwa naishi kwetu hapo kila nikitafuta kazi naitwa nikifika kikwazo ni usikivu, narudi nalia najipanga tena. Wenzangu napata tu taarifa huko kuwa wamepata kazi, wengine wamepata waume, wengine wamerudi kupata masters, mimi niko napata interviews kibao ila ukiitwa ukifika ukasema tu una usikivu wanakutaka radhi unawekwa pembeni nikawa hapo niko broke sina kazi sina hela sina masikio sina mbele wala nyuma 


Basi huku na kule nikamzoea mkaka flani hapa hapa Facebook. Niliizoea mno kampani yake tunakutana kwenye comment tunacheka, alikuwa mtu wa watu na busara nyingi na upendo mwingi, kidogo nikawa naona ni mtu ananitoa upweke, basi siku moja akaniambia nimtumie namba yangu anipigie, hilo likaniua nguvu. 


Mara kadhaa nilishazoeana na watu kirafiki tu ila kwenye kuanza kupigiana nikisema mie sisikii vizuri taratibu mtu anaanza kukupotezea, au anapiga hivyo hivyo bila kujali anakwambia we pokea tu nisikie sauti yako, hafikirii mimi najiskiaje, basi naumia najaribu kuelezea kuwa ukipiga sitakusikia ila wapi mtu anakazana mwisho unaona bora ujitenge


Sasa huyu mkaka nilimzoea halafu nilimpenda mno pia jamani, alipoomba namba ikabidi nimwambie ukweli mie niko hivi na hivi akasema poa hamna shida yeye hana tatizo na hali yangu so fresh tu, kwanza ananipenda sana so hiyo hali yangu kwake si kitu, texts kibao anatuma za kunitia moyo, akanifanya nimpende zaidi nimfungukie kweli mpaka mapito yangu, akaniaminisha yeye hawezi kuwa kama ex wangu, basi akanikaribisha kwake, alikuwa anaishi **** na sisi tunaishi ***. 


Nikapanga jumamosi moja nimtembelee, nikaenda dada bila shaka maana kwa kiasi fulani nilishamjua ilikuwa bado kuonana.


Ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa kuonana uso kwa uso. Kuna vitu vingi alikuwa anaongea simsikii vizuri so naitika kila saa kuuliza unasemaaa? au sometimes naitikia tu ili nisimchoshe kurudiarudia. Hili najua wenzangu wenye hii hali kamq yangu wanaijua. 


Kuna muda unaogopa tu kuchosha watu hasa wale ukiomba arudie zaidi ya mara mbili anaacha kuongea au anakuuliza kwani bado husikii? Au anakukunjia uso so unaitikia hata kama hujaelewa mambo yasiwe mengi


Sasa yeye ilikuwa hadi anaelekea jikoni anaongea alafu ananifata anauliza nimekuita hujanisikia? Nikaanza kuona kama  yale maongezi ni adhabu, ilikuwa kama ananifosi nisikie sometimes anashauti kwa sauti sana anashangaa kwani na hapo sijamsikia? nikajikaza hivyo hivyo ila nahisi na yeye alikuwa bored kimtindo na hali yangu na hakujifunza aongee vipi na mimi. Nikajipa moyo ni mwanzo tu tutakaa sawa as long as amesema anaielewa hali yangu na ananipenda.


Basi hapa na pale nikajikuta tu nimekubali mambo mengine. Ikawa tumeonana mara ya kwanza na tumekutana kimwili pia japo tulijali afya. Sikuwa na wasiwasi maana tulianza uhusiano wa mbali kwa muda hadi kufikia hapo, basi akanidrive mpaka home. Tukaagana fresh.


Sasa nimeingia ndani  ukapita muda akanitumia ujumbe, mbona hujanitumia kama tulivyoongea? Nikajiuliza kutuma nini? Nikajua kuna maongezi nitakuwa sikuyasikia basi nikamtext, kutuma nini babe? Hakujibu hapo alikaa mpaka saa tano usiku akanijibu au basi acha sometimes naona kama unafanya vitu makusudi coz ulinisikia ukaitikia.


Nikahisi moyo unapasuka. Makusudi? Yapi sasa? kuitikia labda kweli niliitikia kwa kuogopa kumchosha. Nikajiskia vibaya sana


Nikamtumia meseji sijakuelewa labda uliongea kitu muhimu sikukusikia, akajibu tuyaache hayo. Nikaomba aniambie hicho alichosema nimtumie ili nitume. Na namna hiyo hakujibu meseji zangu tenaaaa. Imagine Laura nilikuwa najisikiaje? 


Weeee acha kabisa nilikuwa nahisi moyo unawaka moto kama ninywe maji labda utapoa ila wapi, nikaanza kuomba msamaha kwa kutokumsikia, meseji after meseji akanichoka akanipa block, nikaingia messenger mikono inatetemeka, namuomba anisamehe hata mimi sikupenda kutosikia, akanipa block na huko. nikahisi moyo unachanika kwa maumivu


ATAENDELEA...

Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top