After block mbili hayo maumivu yake yaani huli ukashiba wala hulali ukaota, yaani unatamani umsimulie kila mtu namna moyo unavyouma. Chukua hayo maumivu changanya na maumivu ya kwamba nimepoteza usikivu, sina mbele sina nyuma na hapo nilishaumizwa ile mara ya kwanza.
Mtu akisema amejikubali kwa hali yake hasa ulemavu ujue mpaka anajikubali kuna mwendo kaupitia sema huwaga ngumu kuelezea umepitia nini na nini mpaka kuufikia ushujaa, that is what i believe kwa experience yangu binafsi
Basi bwana hilo block lilifanya nikonde haswaa maana nilimpenda jamaa na alinipa matumaini hewa na akanipitia akijua wazi moyo wa kunihandle na shida yangu hana.
Nimekaa nauguza moyo kimya kimya unajua tena hizi familia zetu za kiafrika, heartbreak unakufa nayo mwenyewe. Niko najimezea zangu piriton japo nilale usiku, mama akaja na habari, kuna kijana wa rafiki yake anataka mke.
Nikamwambia mama, mmemwambia hali yanguuu? Akasema ndio we olewa tu mengine mtaelewana ndoani, sikukataa wala kukubali lakini sikuwa tayari maana kwanza nafsi ilikuwa imekufa ganzi kabisa.
Nikatambulishwa kwake na siku ya kumjua uso kwa uso nafsi ilimkataa pale pale ila kukataa mdomoni sikuweza, wiki hivi ndio nikamwambia mama mimi hii ndoa hapana, Eeh mama akaniuliza kwanini mie tena jibu sina
Wiki hiyo nikaja kuona meseji wanatumiana na dadangu wa kwanza, dada anasema mtu mwenyewe hajiwezi kusikia na kazi hana alafu anataka kuchagua chagua akimpoteza huyo kaka atachunda home. Maneno yale yaliniuma sana kwa hasira nkasema bora nitoke nikajue mbele kwa mbele maana kumbe mimi ni kama mzigo hapa ndan. Tulikaa miezi minne nikaolewa yaani huyo bwana hata kuchekeana nae nilikuwa siwezi,
Kiukweli na mimi niligeuka kuwa toxic kidogo, mkali sana, majibu ya karaha ndio usiseme, yaani nilikuwa najihami vibaya mno, mshari hatari, ukijichanganya sina subra hata moja utakula mineno mpaka ushangae, at that time ungeniambia niko toxic ningekataa ningekwambia ndio kujiamini kwangu, nilikuwa nimejaa uchungu flani hivi.
Niko hivyo alafu nina mume ndani nae hajui anitendeeje sijui alinikubali wa kazi gani, mwenyewe ananiona kama sijui hamnazo yaani nimsikie nisimsikie nitajua mwenyewe, stori na mimi hana, kuna muda anapiga simu usipopokea ananuna, au anakuachia maagizo ya mdomo anaongea anaangalia ukooo humwelewi, nami kichwa kikichemka namuwakia na mineno usipime.
Bado ukweni, mawifi hawakunikubali yaani nikienda wananipita kama kuni tu hapo alafu ukiuliza kitu usiposikia wanacheka, ukisikia vibaya wanacheka, ila ma mkwe kidogo alikuwa na utu.
Ndoa ilikuwa ngumu mno Laura ngumu mno nikaanza kuumwa miguu inakufa ganzi, hapo ndio kabisa nikahisi maisha yangu yanaenda ukingoni. Kila kitu mwanaume anakupuuza mradi ameacha hela ya kula basi mengine ni geuka pa pa pa pa geuka usingizi imeisha hiyo
Mwaka wa tatu sina tumbo mawifi midomo mikali balaa, mume maugomvi hayaishi akaanza kunipiga hapo ndoa ikavunjika, siku nami aliponipiga bao la uso nikamrudishia akanipiga nusu aniue. Nikarudi nyumbani.
Mama angu hakuwa na neno ila dada na baadhi ya ndugu walikuwa kama mkaa wa moto mguuni. Ni kusemwa kutwa kudhihakiwa na kuchekwa, mwezi after kurudi nyumbani nikagundua nina mimba. Ikabidi nimjuze bwana akaniambia ataamini vipi mimba ni yake? Hilo jibu likanifanya nifute namba nifute kila kitu, mpaka najifungua yule bwana hakukanyaga nyumbani wala ndugu zake.
Kuja kwa mtoto kukanifanya nijue natakiwa kuishi yaani piga ua lazima nipambane mtoto apate mahitaji, nyumbani mama alikuwa ananisaidia kidogo ila masimango mengi sana na kunitaka nirudi kwa mwanaume hakuna wa kunioa kwa hali hio yaani kwetu kutoka kwenye ile ndoa ilikuwa kama nimepoteza kitu cha thamani sana coz waliona nani angenioa sasa na hii misikio mibovu ongeza na mtoto juu
Kuna kipindi maisha yalikuwa magumu nikatamani hadi kumpigia mwanaume niombe msamaha japo atuhudumie ila nikiwaza hata mtoto hakumtaka nikaona nichukulie amekufa tu. Nilifanya vibarua vingi na huko vibaruani jamani mitihani mitupu na katikati hapo mtoto akiwa na mwaka nilipata mahusiano yakaishia pabaya nikapumzika kabisa. Nimekaa miaka minne sina mtu wala mahusiano ni mimi na mwanangu na shida zangu.
Jumamosi hiyo nimetoka kupeleka visheti na maandazi dukani kwa Mangi ndio biashara nilijaribu kufanya, akaja mkaka pale dukani akanisemesha mie sikumwelewa nikamjibu za saa hizi nikaenda zangu. Tukaanza kugongana dukani mara kwa mara sina maneno mengi wala simsikilizi, siku moja wakati nampita akanishika mkono kama kunivuta hivi nikageuka kumtazama akaniambia mambo yaani na macho kayatoa kusisitiza salamu, nikamsikia nikamjibu poa halafu akacheka akaniachia.
Kufika nyumbani sasa kulikuwa na binamu yangu hapo home akaniambia nimekuona na mkaka dukani kakushika mkono, nikamwambia hata simjui akanambia ni mgeni kahamia nyumba fulani. Mie haya. Siku zimekatika Binamu yangu akaniambia anampenda huyo kaka yaani sana, alikuwa anafuma sweta akasema atamzawadia. Mie haya. Huyu kama Tumwite Abed.
Siku hiyo nimefuata hela yangu kwa Mangi nikamkuta ananunua mahitaji yake. Mie simzingatii hata. Amemaliza kununua akanishika mkono. Ikabidi nimtazame akaandika meseji kwenye simu yake, naomba namba yako. Nikamwambia hapana hapo nina simu yangu mkononi, akaichukua kinguvu akaandika namba zake akapiga, akaniandikia save hii namba andika My Husband Abed... Nilicheka kwanza halafu nikamsonya nikaachana nae. Kufika nikatamani kumwambia mfuma sweta kilichotokea ila nikaona ngoja tu nipuuze kwanza sitamtafuta
Sasa usiku kama saa tatu tuko mezani, akaja mtu kunambia nje kuna mtu wangu yaani nje ya geti, nikainuka kufika nje namkuta kasimama, kuna kigiza akaniandikia kwenye simu mbona hujanicheki, nikamwambia we mwehu nini kwani lazima? Akasema au amuite mama yangu amuombe ruhusa ya kuseviwa kwenye simu. Nikamwambia acha ujinga hapo mama nae ananiita. Nikamwambia ondoka nitatumia ujumbe, akaniambia usipotuma narudi hapa kugonga
Nikaingia ndani nahisi akili inakwenda mbio. Mama anauliza ni nani? Nikamjibu Mangi ameniletea hela iliyobaki. Maswali yakaishia hapo na meseji sikutuma wala nini.
Kesho yake asubuhi saa 12 hivi mama akaniamsha we mwana we amka kuna mgeni wako getini. Namuuliza nani? akanijibu sijui ni mkaka mie simjui. we jicho likanitoka.
ATAENDELEA...
