“usihofu kitu Happy muda wowote utakaokuwa na tatizo usisite kunitaarifu.I will help you.”Patrick alisema kwa kujiamini.alijisikia vizuri sana kumsaidia binti yule mwenye matatizo aliyekuwa ametengwa .
Taratibu wakaondoka mahali pale na kuanza kuelekea mnadani.
Maisha ya Patrick na Happy yaliendelea kama kawaida shuleni malangali.Kila mara walikuwa pamoja.Waliachana tu pale Happy alipokwenda hosteli kwao.Walisoma pamoja na maendeleo yakawa mazuri sana.Happy akawa ni mtu mwenye furaha kila siku .Ni kweli hakulia tena kama Patrick alivyomuahidi.Alizidi kupendeza na kuwa mrembo zaidi.Kwa muda mfupi urafiki wa Patrick na Happy ukawa gumzo pale shuleni.Wapo waliosema kuwa Patrick na Happy ni ndugu,wengine wakadai kuwa ni wapenzi ilimradi kila mtu akasema lake.Chuki dhidi ya Patrick na Happy ikaongezeka.Na kwa sasa ikawa wazi wazi.Maneno yalitamkwa bila kificho .Wengine wakadai eti Patrick anaringa ,wengine wakadai ana majivuno,wengine wakasema kuwa anaringia pesa za Happy wengine wakamwita mwanaume kama binti na majina ya kila aina.Hii ilimfanya Patrick akose rafiki wa karibu ambaye angeweza hata kumweleza matatizo yake .Rafiki yake mkuu alikuwa ni Happy .Si kwamba alipenda hali hii lakini ilijitokeza yenyewe na ikafika mahala akajikuta akiizoea.Alipenda sana kuwa na marafiki wengi lakini angewapata vipi?kila mtu hakuwa tayari kushirikiana naye.
Kwa upande wake Happy naye alikumbana na visa kama alivyokumbana navyo Patrick.Hii haikuwasumbua hata kidogo.Maneno mengi yakasemwa lakini mwisho wa siku ukweli ukabaki pale pale kuwa Patrick na Happy hawawezi kutengana.Maneno ya watu pamoja na visa walivyotendewa vilikuwa ni changamoto kubwa kwao.Siku zote walipeana moyo na ujasiri wa kutokukata tama.Waliongeza juhudi katika masomo na kila mara walionekana kufanya vizuri na kupata alama za juu.Taratibu walimu wakaanza kuwapenda kutokana na juhudi walizozionyesha darasani.Hii ikazidisha chuki miongoni mwa wanafunzi .
****************************************
Ilikuwa ni saa sita na robo siku ya jumatano.Darasani hapakuwa na mwalimu kilikuwa ni kipindi cha kujisomea.Happy akatoka na kwenda msalani.Wakati akirejea kwa bahati mbaya akaligonga daftari la mwanafinzi mmoja wa dawati la mbele kabisa na daftari lake likaanguka chini.Happy akaomba samahani na kuinama kuliokota daftari lile.
“Wewe usiguse daftari langu usije na mimi ukaniambukiza magonjwa yako”akasema kwa sauti yule binti aliyeangushiwa daftari lake na Happy .CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Happy akapandwa na hasira kali kwa kauli ile.Siku zote alivumilia kashfa za kila aina lakini hii ya leo ilimuuma mno.Wanafunzi wakaanza kucheka kwa kejeli.Kitendo hiki kikamzidishia hasira akainuka na kumzaba kofi yule binti na mara ukazuka ugomvi.
“Apigweeee huyo !!!… anaringa sanaaa…!!!!!!! acheni afundishwe adabu..”yalikuwa ni maneno ya wanafunzi wakishangilia .Wengine waliinuka na kumsaidia yule binti kumpiga Happy .Patrick ambaye alikuwa katikati ya darasa alikishuhudia kitendo kile wazi wazi naye kama ilivyokuwa kwa Happy akapandwa na hasira zisizomithilika.Akapanda juu ya meza na kuruka meza nyingine kama mbili hivi na kufika mahala pale ulipokuwa ukitokea ugomvi.Akaingilia kati na kuwaamua.Wanafunzi wawili wa kiume walipoona Patrick ameingilia kati ugomvi ule nao wakainuka na kuanza kupigana na Patrick.Kelele zikawa nyingi na zikamfikia mwalimu aliyekuwa darasa la karibu ambaye alifika haraka kuona kuna nini akakuta kuna ugomvi mkubwa.Wanafunzi walipomwona mwalimu wakakimbia kila mmoja katika kiti chake kasoro Patrick na Happy .Patrick alikuwa amevimba kwa hasira.
“haya wote mliokuwa mnagombana pita mbele”
Yule binti aliyekuwa akigombana na Happy akasimama na kupita mbele.
“Si huyu peke yake nimewaona wengi tu piteni wote mliokuwa hapa mnagombana”
Akasema mwalimu yule kwa ukali na kuwafanya wanafunzi waogope na kuanza kupita mbele .wakachukuliwa wote na kupelekwa kwa mwalimu wa darasa.
“haya nipeni sababu za kugombana”Akasema mwalimu yule mkali
Yule binti aliyekuwa akigombana na Happy akasema
“Ni huyu hapa ndiye mkorofi.ameangusha daftari langu makusudi kabisa badala ya kuliokota akaanza kunitolea maneno ya kashfa.Mimi nikamwambia kama hataki kuliokota nakuja kushtaki kwa mwalimu yeye akaninasa kibao na kusema kuwa nenda kaseme kwa huyo mwalimu wako tuone atanifanya nini.Muda huo huo huyu hapa sijui ndugu yake akainuka naye akaja wakaanza kunichangia ndio hawa wenzangu wakaja kuniokoa.”Akadanganya yule binti
Mwalimu yule akawaangalia Patrick na Happy kwa macho makali.Akawageukia wale wanafunzi wengine watano.
“Eti nyie ni kweli haya maneno aliyoyasema mwenzenu?
“kweli kabisa mwalimu” wakajibu
Haya nyie wote nendeni nitabaki na hawa watukutu wanaojifanya matajiri wa shule.”
Wanafunzi wale wengine wakaondoka na kuwaacha Patrick na Happy katika mikono ya mwalimu ambaye alikuwa ameshika fimbo kubwa .
“ leo mtanieleza nyie watoto kwa nini mnasababisha ugomvi darasani?Kwanza wewe binti hebu nyoosha mkono wako hapa”
Happy huku akilia akanyoosha mkono ili mwalimu aanze kumchapa.
“No ! Happy .Usinyooshe.”Patrick akapiga kelele na kwenda kusimama mbele ya Happy .
“ kumbe wewe ndiye unayemfundisha kiburi mwenzako.leo utanieleza . haya lala chini haraka.”akafoka mwalimu
“Hapana mwalimu silali”Patrick akajibu kwa hasira ..Happy machozi yalikuwa yakimtoka.
“Unaonekana una kiburi sana wewe."akadakia mwalimu mwingine aliyetokea ghafla..
“Wewe unajifanya tajiri na vihela vyako leo utaimba “Akasema mwingine huku akisogea akiwa na fimbo mbili mkononi
‘i walimu hali hii mpaka lini? Uonevu huu mpaka lini ? Kwa nini hamtaki kutupa na sisi nafasi ya kujieleza? Patrick akasema
“Unajifanya kujua sheria ? nakwambia leo utaona”mwalimu yule akamsogelea na kutaka kumchapa Patrick mgongoni.Patrick akadaka Fimbo.
“Unataka tupigane ? ”Mwalimu yule akatupa fimbo na kukunja ngumi.
Ofisi ikageuka kituko.Mara mkuu wa shule msaidizi akapita akasikia kelele ofisini
“wamefanya nini hawa? akauliza
“wamepigana na wenzao darasani na hawataki kuadhibiwa.”
“Siyo hivyo mwalimu.Huu ni uonevu.Huyu mwalimu kapewa maneno ya uongo naye kwa chuki zake anaamua kutuadhibu bila kosa.Chuki za wazi wazi zitakwisha lini?.Happy ananyanyaswa na shule nzima wanasema eti ana ukimwi.Hata kama angekuwa nao hivi ndivyo wanafunzi wanavyofundishwa kuishi na wenzao wagonjwa?”Patrick akaongea maneno mfululizo kwa hasira.
“Kwa hiyo mmepigana au hamjapigana" akauliza mkuu wa shule msaidizi
“Ukweli ni kwamba Happy alikuwa akitoka msalani na kwa bahati mbaya akaligonga daftari la mwenzake likaanguka chini.Akainama ili aliokote lakini wakati anataka kuliokota yule binti akasema aache daftari lake asije akamuambukiza maradhi yake.Happy akakasirika na kumnasa kibao lakini halikuwa kusudio lake.Hata kama ungekuwa ni wewe nafikiri usingevumilia.Ungejisikiaje kama huyu angekuwa mwanao na unasikia anaambiwa maneno kama yale ?
Mwalimu yule msaidizi akakaa kimya kisha akawaamuru Happy na Patrick wamfuate ofisini kwake
“Enhee vijana hebu niambieni nini kilichotokea”akasema mwalimu baada ya Patrick na Happy kufika katika ofisi yake.Happy ndiye aliyeanza kueleza
" mimi nilitoka msalani , kwa bahati mbaya nikaligonga daftari la Mwantumu likaanguka chini.Nikamuomba samahani nikainama ili niliokote.Wakati nikiliokota akasimama na kuniambia “acha daftari langu usije ukaniambukiza magonjwa yako”.Kwa kweli mwalimu kauli hii mimi iliniuma sana hasa ukizingatia kuwa hapa shuleni mimi nimekuwa nikitengwa na wanafunzi wanadai eti nimeathirika na ugonjwa wa ukimwi.Mwalimu hata kama ningekuwa na maradhi hayo wanayodai kwa nini basi wanitenge?Kwanini waninyayapae namna hii?Na kwa nini wanizushie kitu ambacho si cha kweli?Inauma sana mwalimu.Kila mwanafunzi ananichukia hapa shuleni na.Kibaya zaidi hata walimu nao wameungana na wanafunzi katika kuoyesha chuki zao za wazi kwangu.”
Mwalimu akakaa kimya na kutafakari kisha akasema.
“halafu kuna kitu nataka kuwauliza..Kuna tetesi nimezisikia kuwa nyie wawili ni wapenzi.Ni kweli?
Wote wawili wakakaa kimya .Hili lilikuwa ni swali ambalo hawakukulitegemea kabisa..Walikaa kimya kwa sekunde kadhaa bila kujibu .
“Mbona hamjibu ina maana ni kweli?”Akasema mwalimu kwa ukali.Happy alikuwa akitetemeka mwili.Ni kweli hajawahi kuwa na mpenzi mpaka hapa alipo Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kuambiwa kuwa ana mpenzi.Patrick yeye alikaa kimya akitafakari ajibu nini.
‘Mwalimu sisi si wapenzi kama ulivyosikia .Sisi ni marafiki na muda wote tuko pamoja Kitu kinacho fanya watu wahisi kuwa sisi ni wapenzi ni kwa vile tuko karibu karibu sana.Tunasaidiana karibu katika kila jambo.Tunaishi kama ndugu.Maendeleo yetu ni mazuri.Mwalimu hizo ni chuki tu za watu wasiotutakia mema.Naomba uniamini kuwa sisi si wapenzi kama watu wanavyodhani..”Patrick akasema.Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Mbele ya mwalimu mkuu msaidizi .
“haya nendeni nitakaa kikao na walimu ili kujadili suala lenu.”
Happy na Patrick wakatoka ofisini huku Happy akilia.Patrick akatoa kitambaa mfukoni na kumfuta machozi.
“Nyamaza Happy kila kitu kitakuwa sawa,Usilie.”
Moja kwa moja wakaelekea darasani.Walipoingia tu darasani minong’ono ikaanza.Happy akashindwa kuvumilia akachukua vitabu vyake na kutoka darasani macho yakiwa yamefunikwa na machozi.Patrick naye akatoka na kumkimbilia .
“Happy please hebu nyamaza.Unajua ni kwa kiasi gani unawapa ushindi wale wote wasiokupenda.tayari wanaona wamekwisha kushinda.Be strong Happy .Pambana na utashinda.I’m on your side.i’ll fight for you”Patrick akasema kwa msisitizo.
Happy akafuta machozi akatabasamu na kusema.
“Ahsante sana Patrick .Nafahamu kuwa uko pamoja na mimi.Naomba kwa sasa nikapumzike tutaonana baadae.Nasikia kichwa kinaniuma .”
Patrick akamtazama Happy usoni kisha akasema.
“Ok Happy nenda kapumzike tutaonana baadae.”
Wakaacha na Patrick akarejea darasani.Ilikuwa ni siku ndefu na ngumu kwa Patrick.Kila mara alikuwa akitafakari juu ya tukio la leo.Ni tukio ambalo lilimuuma sana na kumfanya afikie hatua ya kupigana.Toka amezaliwa hajawahi kupigana na mtu yeyote.Hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza kupigana .Ilimuuma sana.
“lakini sikuwa na jinsi.Ni lazima nimtetee Happy .Kwa gharama yoyote ile.Kwa nini binti yule anyanyasike bila kosa?Nitahakikisha katika uwepo wangu hapa shuleni ninamsaidia kwa kila hali.Lazima siku moja heshima itapatikana..” akawaza Patrick huku ameinama chini .Mawazo yalikuwa yakija na kupita kwa kasi.Mara akakumbuka kitu.Akakumbuka swali waliloulizwa na mkuu wa shule msaidizi.
“halafu kuna kitu nataka kuwauliza..Kuna tetsi nimezisikia kuwa nyie wawili ni wapenzi.Ni kweli? Patrick akatabasamu alipoyakumbuaka maneno haya ya mwalimu mkuu
“Kumbe siku zote watu wanahisi kuwa sisi ni wapenzi .Nadhani hii ni mojawapo ya sababu inayopelekea watu kuwa na chuki zaidi kwetu kwani Happy ni binti mrembo kupita maelezo.Na kadiri siku zinavyozidi kusonga anazidi kupendeza na kuwa kama malaika.Sasa kama wao hawaupendi ukaribu huu wangu na Happy basi wameumia .Tutaendelea kuwa karibu zaidi ya hapa.Lakini kuna dalili zozote za mapenzi kati yetu?.Hapana. Nadhani tunapenda kama marafiki wa kawaida .Sijui ya huko mbele kwa sababu naona urafiki wetu umekuwa mkubwa sana na unazidi kukomaa kadiri siku zinavyosonga mbele.”.
Kwa upande wake Happy baada ya kutoka darasani mchana ule akaenda mpaka katika hosteli yao akajitupa kitandani na kuanza kutafakari.juu ya tukio zima la leo.
“sikuwahi hata siku moja kuwaza kuwa nitakuja kugombana na mtu .Nimevumilia mambo mengi lakini hii ya leo ilivuka mipaka..Kwa nini wananichukia namna hii?Mbona mimi sina tabia ya maringo kama wanavyodai?Mbona sijivuni japokuwa wazazi wangu wana uwezo?Nafikiri ni kwa sababu wengi hawaupendi ukaribu wangu na Patrick.Wasichana wenzangu wana chuki hawapendi sana jambo hili.Nadhani hii ni sababu kubwa ya kuwa na visa vya wazi wazi.Kumbe tayari wamepeleka maneno hadi kwa walimu kuwa mimi na Patrick ni wapenzi.Mhh jamani!!.Maskini Patrick anaonewa bure kaka wa watu.Wangejua jinsi alivyo wala wasingezusha tuhuma hizo.Lakini hata kama ingekuwa ni kweli kwani wao inawahusu nini?Wivu wao unawasumbua tu..Nasema Patrick simuachi na nitazidi kuwa rafiki yake wa karibu.Patrick ni mtu pekee ambaye amenifikisha hapa nilipo sasa.Nilikwisha kata tamaa kabisa hata ya kuendelea kusoma hapa lakini ni yeye aliyenipa moyo na kunisaidia katika kila kitu .Amenipa msaada mkubwa kimasomo.Ni yeye tu ambaye amekuwa nami siku zote pale ambapo jamii nzima imenikataa.Potelea mbali watakavyosema na waseme.Mimi sijali .Mbona wao wana wanaume kila kona mimi siwafuatiliii mambo yao .Kwa nini basi wao wafuatilie ya kwangu.?.Lakini hata kama ingekuwa ni kweli ,kuna ubaya wowote mimi na Patrick kuwa wapenzi?Nadhani hata kama nikiamua kuwa na mpenzi basi ni wazi ni lazima atakuwa ni Patrick .Kwani ni yeye pekee mpaka sasa hivi ambaye amekuwa ni mtu wangu wa muhimu sana.Ni yeye pekee ambaye anaweza kunikosesha usingizi kwa kutomuona.Je ni kweli kuwa hii ni dalili ya kuchipua kwa penzi kati yetu? Inaweza kuwa kweli kwa sababu sijawahi kuwa karibu na mvulana yeyote zaidi ya Patrick.Ni yeye ambaye amenifundisha nini maana ya kuwa rafiki wa dhati.nadhani hizi ni dalli njema.lakini hata kama nikiamua kumchagua Patrick kuwa mpenzi wangu nitamwambiaje?Mhh ! ngoja niachane na haya mambo huu si wakati wake." akawaza happy.
CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kengele ya dharura ikagongwa ikiashiria kuwa na jambo ambalo si la kawaida.Wanafunzi wote wakatoka darasani kwa haraka kama inavyotakiwa mara tu inaposikika kengele hii.Kwa haraka haraka mistari ikapangwa na huku kila mwanafunzi akiwa kimya akisubiri kusikia ni nini kitakachojiri.Walimu wote walikuwa wamejipanga na mara akatokea mkuu wa shule.Wanafunzi mioyo ikawaenda mbio kwani ni nadra sana kwa mkuu wa shule kuonekana katika eneo hilo la mkusanyiko.Mara zote anapoonekana eneo hilo huwa ni kwa sababu maalum tu.
“Habari za asubuhi wanafunzi” Akasalimu wanafunzi.
“Nzuri shikamoo mwalimu”
“Wanafunzi nimesimama mbele yenu asubuhi hii ili kuzungumzia mustakabali mzima wa maendeleo ya shule yetu.kwa siku za karibuni shule yetu imekuwa na mambo ambayo katu hayafurahishi na ambayo yanaenda kinyume na maadili mazima ya mwanafunzi.
Kwanza kabisa kumekuwa na vitendo vya ubaguzi.Wanafunzi mmeanza kubaguana.Mnawanyanyasa na kuwabagua wenzenu ambao ni wagonjwa.Hivi ndivyo mnavyofundishwa na wazazi wenu majumbani? Kuna binti mmoja nimepata malalamiko yake kuwa yeye ametengwa na wanafunzi wenzake eti kisa ni mgonjwa.Hii ni aibu kubwa kwa shule yetu..Sasa ninasema hivi kuanzia sasa wewe ukibainika kuwa unafanya kitendo chochote cha kibaguzi adhabu yake ni kufukuzwa shule.Sintataka kukuona tena katika shule yangu.Kuweni makini sana na hilo.Jambo la pili ninalotaka kulizungumza leo ni nidhamu .Kumekuwa na uvunjaji mkubwa sana wa sheria za shule.Imefikia mahali sasa ambapo mwanafunzi anaweza akamgomea hata mwalimu .Mwanafunzi anaweza akafanya kitu chochote anachotaka bila kuogopa.Hivi kweli wewe mwanafunzi unaweza ukabishana na kutaka kupigana na malimu wako?mwalimu wako ni sawa na mzazi wako hapa shuleni.Nasema kuwa kuanzia sasa sheria na taratibu za shule zitafuatwa kwa ukaribu sana.Endapo utakwenda nje ya taratibu basi tutakushughulikia kikamilifu.Kwa sasa naomba nitakaowataja wapiti mbele haraka: Patrick Charles,Happy kibaho.Mwantumu ramadhani.Pius augustinie,Pili Juma,Maria asey,Steven amanuli na Benson Chiteu.”
Wanafunzi wale walioitwa ,wakajipanga mbele ya alipokuwa amesimama mkuu wa shule,halafu akaendelea.
“Hawa mnaowaona mbele yenu mnajua wamefanya nini? Akauliza mkuu wa shule.wanafunzi wote wakawa kimya .Hakuna mtu aliyethubutu kusema kitu ingaa walkuwa wakifahamu juu ya ugomvi uliotokea.
“Wanafunzi hawa walioko mbele yenu walivunja sheria za shule kwa kugombana darasani.Baada ya kukutwa wkipigana mwalimu aliyewakamata akawapeleka kwa mwalimu wa darasa Patrick na mwenzake Happy ambao ndio kiini cha ugomvi wakagoma kuadhibiwa.Kibaya zaidi ni kwamba Patrick alikuwa tayari kupigana hata na mwalimu wake wa darasa.Sijui jeuri hii mnaitoa wapi ninyi watoto..Mwanafunzi unataka kupigana na mwalimu wako kweli? Hii tabia mbaya ambayo katu haitavumiliwa katika shule yetu.Kingine ni kwamba Patrick na Happy ambao wote ni wanafunzi wa darasa moja wamekuwa wakijihusisha na masuala ya kimapenzi wakiwa shuleni kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za shule.Bodi ya shule imekaa na imeamua yafuatayo.Moja wanafunzi Mwantumu Ramadhani,Pius Augustine,Pili Juma,Maria asey ,steve amanuli,na Benson chiteu watapata adhabu ya kung’oa kila mmoja visiki vitatu kwa muda wa siku sita kuanzia leo.Wanapata adhabu hii kwa kosa la kupigana darasani.Hili ni fundisho kwa wengine .Wanafunzi Patrick charles na Happy Kibaho wao wanasimamishwa masomo kwa muda wa mwezi mmoja.Hii ni kwa sababu wamesababisha ugomvi ,wamapigana darsani,wakagomea adhabu ya mwalimu na zaidi ya yote wanajihusisha na mahusiano ya kimapenzi wakiwa shuleni.Adhabu hii ni fundisho kwa wanafunzi wengine.Ninasema kuwa kuanzia sasa tutakuwa wakali mno kwa yeyote yule ambaye atajaribu kwa namna yoyote kuvunja sheria za shule.Nasema ole wenu ,ole wenu.” Mkuu wa shule akamaliza na kuondoka zake.mwalimu wa zamu akawatawanyisha wanafunzi warudi madarasani.Sehemu kubwa ya wanafunzi walkikuwa wakifurahia adhabu ile waliyoipata Patrick na Happy .Kwao uilikuwa ni alama ya ushindi mkubwa.Katika darasa la akina Patrick ilikuwa ni kama sherehe.Wanafuzi walikuwa wakipongezana.
Happy macho yalijaa machozi.Alikuwa akilia.Hakuamini kuwa kosa lille lingepelekea yeye na Patrick wasimamishwe masomo.Hakuwahi kuota kama iko siku atakuja kusimamishwa masomo.Mbaya zaidi aliumia moyo kwa uongo wa wazi kabisa .Ni wazi ulikuwa ni ukandamizaji mkubwa.Zilikuwa ni chuki za wazi .Patrick alikuwa katika hali ya mstuko kutokana na adhabu ile ambayo kwa kiasi kikubwa haikuwa ya haki.Ulikuwa ni uonevu mkubwa.Walikuwa wamesingiziwa uongo mkubwa .Ilimuuma Patrick kwa kiasi kikubwa lakini hakuwa na la kufanya .tayari maamuzi yamekwisha fanywa na kilichobakia ni utekelezaji.Kwa muda huu mfupi shule hii ilikuwa imeanza kumchosha.Taratibu akamsogelea Happy na kumshika mkono.Akatoa kitambaa mfukoni na kumfuta machozi .
“Happy be strong.Najua inauma sana lakini hatuna jinsi.Tusiwape faida maadui zetu.Wanapotuona tuko na huzuni ni furaha kwao.Let us act kama vile hakuna chochote kilichotokea.
* * * *
“Patrick ninasikia uchungu sana ..Kusingiziwa kitu ambacho sijakifanya inauma mno .Inaniuma sana Patrick”Happy akashindwa kuvumilia akaanza kulia .Ilikuwa ni majira ya saa kumi na moja za jioni walipokutana katika hoteli moja kijijini baada ya kuachana mchana na kila mmoja akaenda kupumzika na kutuliza akili.Happy macho yalikuwa yamemvimba na mekundu kwa kulia..
‘Kinachoniuma zaidi ni wewe kusimamishwa masomo.wewe hukustahili kwa namna yoyote ile kuipata adhabu hii.Mimi ndio chanzo cha haya yote.Mimi ndiye niliyekusababishia matatizo haya .Ni bora ningesimamishwa masomo peke yangu.Nasikitika sana Patrick .Naomba unisamehe kwa hilo.Haikuwa adhma yangu na wewe uingie katika matatizo haya .Najua hustahili adhabu hii………………….” Akasema Happy huku machozi yakimtoka lakiniPatrick akamzuia na kusema
“Shhhhhhhhhhhhhhhhhhhh………….”Patrick akamfumba Happy mdomo kwa kidole.
“Happy usiseme hivyo.Ninafurahi kupata adhabu hii .Ninastahili.Ulikuwa ni wajibu wangu mimi kukutetea.Nimetimiza wajibu wangu.Kumbuka niliahidi kuwa nawe katika kila jambo.Niliahidi kupambana na yeyote yule ambaye angekufanya ulie.Nimefanya nilivyopaswa kufanya..Usijilaumu Happy ninastahili adhabu hii .”Parick akasema kwa kujiamini.Akamuangalia happy kwa makini na kusema
“Happy si hapa duniani tu hata nikiwa Mbinguni sintavumilia kuona mtu yeyote akikusumbua.Nitapambana naye.”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kwa mara ya kwanza Happy akacheka kwa kauli ile ya Patrick..Patrick akatabasamu kwa kuifanya sura ya Happy ikajaa tabasamu tena.
“ Umeanza vituko vyako.Mbinguni hakuna uonevu wa namna hii” akasema Happy huku akicheka
“nimesema hivyo kukuthibitishia kwamba sintakuwa tayari kuona mtu yeyote yule akikunyanyasa Happy..” akasema patrick na kumfanya Happy atabasamu tena
“Happy hii ni vita na sisi ni wapiganaji. kuna msemo wa kiingereza unaosema winners never quit.Na sisi ndio washindi hivyo tusikate tamaa.Kukata tamaa ni kuwapa ushindi wale wote wasiotupenda,wasiotutakia mema.Wao wanapamba na sisi lakini sisi tupambane na muda.tumeelewana?”
“sawa Patrick nimekuelwa.nashukuru sana Patrick sijui hata nipate neno gani la kukushukuru kwa jinsi ulvyojitoa mhanga juu yangu.Sidhani kama kuna mwanaume ambaye anaweza kufanya haya uliyoyafanya kwangu.Kama wapo basi ni wachache mno.”
Patrick akatabasamu na kusema...
“Happy utaanzaje kuwaeleza wazazi wako juu ya tukio hili mpaka wakakuelewa.? Manake kwa mujibu wa barua zilivyoandikwa za kuwapelekea wazazi mhh ni hatari tupu.”
Happy akakaa kimya kwa muda kisha akasema.
“Patrick hilo suala linaniumiza kichwa kupita kiasi..unajua baba yangu ananiamini sana na hajawahi kusikia sifa yangu mbaya hata siku moja .Siku zote nimekuwa mfano hata kwa wenzangu , leo akisikia nimesimamishwa masomo mhhh !! sidhani kama kutakuwa na amani nyumbani.Kuna hatari akakataa hata kunipokea kwa jinsi baba yangu alivyo mkali.Nilikuwa nafikiria niende kujificha kwa shangazi yangu Morogoro mpaka adhabu itakapokwisha.Shangazi yangu ni mwelewa na nina imani nikimwelezea atanielewa.Sitaki baba yangu afahamu kuhusu suala hili.Akijua tu nimekwisha.Wewe je umepanga nini? Patrick akafikiri kidogo na kusema
“mimi sina tofauti na wewe hata kidogo.Mzee wangu hatavumilia akisikia nimesimamishwa masomo.Hata mimi nilikuwa ninafikiria niende mahala nikatulie mpaka adhabu hii itakapoisha.Mwezi mmoja si mrefu.”
Kimya kikapita Patrick ambaye alikuwa ameinama akiwaza akainua kichwa na kusema.
“Happy kuna jambo nimelifikiria.Kwa kuwa sisi sote tuna wazo moja la kutotaka kuzifahamisha familia zetu juu ya adhabu hii tuliyopata ,kwani hata kama ukienda kwa shangazi yako anaweza akamweleza tu mzee wako na hapo ndipo itakuwa mbaya zaidi. kama ni hivyo kwa nini basi tusitafute mahala tukaenda kukaa kwa muda wa huo mwezi mzima mahala ambako hakuna mtu anayetujua,na tutakaa kwa raha mstarehe huku tukipata nafasi ya kutosha ya kusoma hadi muda wa adhabu utakapoisha?
Happy akatabasamu lile tabasamu lake adimu sana.
“That’s a good idea Patrick.Wewe una akili sana.Ni wazo zuri Patrick .Sasa ni wapi ambako unafikiri tunaweza kwenda kukaa kwa muda huu wote bila ya kufahamika? Akauliza Happy na Patrick akakaa kimya kidogo akafikiri kisha akasema
“Umewahi kwenda Bagamoyo?”Patrick akauliza.
“hapana sijafika huko”
“Basi ninafikiria twende huko.Kule tutapumzika vya kutosha.Hakuna mtu yeyote anayetufahamu.Tutakaa kwa raha mustarehe.Tutapata nafasi nzuri ya kujisomea.Tutatembelea sehemu mbali mbali za kihistoria.Tutajifunza mambo mengi sana tukiwa kule.Usijali kuhusu gharama bado nina akiba ya kutosha ya pesa na wala hatutapata shida kwa muda kwa huo wote wa mwezi mmoja.Nafikiri hii itatusaidia sana kutoka nje ya ulimwengu huu wa watu wasiokuwa na upendo hata chembe”
Furaha ya wazi ikajidhihirisha usoni mwa Happy .Hakuwa amewaza jambo kama lile hapo kabla.Huzuni yote aliyokuwa nayo ikayeyuka ghafla.
“ Patrick nashindwa hata nisemeje.You are my Hero.Toka nimefahamiana na wewe maisha yangu ytamekuwa na furaha sana.Najihisi niko slama muda wote ukiwa pembeni yangu.Nafurahi kwa kuwa najua niko na rafiki anayeyenijali na kunithamini.Sina kitu cha kukulipa Patrick kwa wema wako huu ”akasema Happy.Patrick akatabasamu.
“ Sifanyi hivi kwa kuhitaji malipo Happy.Ninafanya hivi kwa sababu moyo wangu umenituma” akasema Patrick.Walijhadiliana mambo mengi hadi ilipotimu saa moja za jioni wakaondoka kwa ajili ya kwenda kujiandaa na safari ya kesho yake ya kuelekea Bagamoyo
Ulikuwa ni usiku mrefu sana ambao Happy hakuwahi kuupata hapo kabla.Alitamani asubuhi ifike haraka ili aweze kuondoka hapa shuleni.Tayari alikwisha maliza kufunga baadhi ya vitu vyake muhimu ambavyo angevihitaji katika safari yake ya kuelekea Bagamoyo.Vingine vilivyobaki akavikabidhi kwa mkuu wa hosteli.Wanafunzi wenzake walikuwa wakimshangaa sana kwa hali aliyokuwa nayo.Badala ya kuwa na huzuni kwa kusimamishwa masomo yeye alikuwa na tabasamu muda wote.
“Me and Patrick together in bagamoyo” Neno hili lilijirudia rudia kichwani mwake mara nyingi.
“Nashukuru nimepata nafasi ya kuwa na Patrick peke yangu kwa mwezi mzima..Walau nitajitenga na karaha za shule hii kwa muda.Nafikiri baada ya kurudi nitakuwa na mabadiliko makubwa.Safari hii ya Bagamoyo nina imani itanisaidia sana kisaikolojia.Nitakuwa mtu mpya tena.”Aliwaza.
kwa upande wake Patrick alikuwa akifikiria jinsi atakavyomaliza mwezi mzima akiwa na Happy . “Ni vipi ikija kugundulika kuwa kwa mwezi mzima tulikuwa tumejificha Bagamoyo?Hii itadhihirisha wazi kuwa kuna kitu kinaendelea baina yetu.Lakini potelea mbali hata kama ikigundulika siogopi tena .na hata kama tukiwa wapenzi hakuna mtu anayehusika katika kuamua masuala ya maisha yetu .”Akawaza Patrick.
* * * *
Kengele ya mlangoni ikalia na kumwamsha Patrick toka katika usingizi mzito.Taratibu akainuka na kwenda kuufungua mlango.Alikuwa ni Happy akiwa ndani ya tabasamu pana.Ni siku yao ya kwanza katika mji wa Bagamoyo.Walifika jioni ya siku iilyotangulia na kupanga vyumba viwili katika nyumba ya kulala wageni yenye hadhi ya kawaida lakini yenye ulinzi wa kutosha na huduma nzuri.
“Mhh ! Patrick amka basi uoge tunywe chai .Nimeenda kununua chai katika mgahawa wa mama mmoja hapo jirani.Kwa kuwa tutakuwepo hapa Bagamoyo kwa muda mrefu amenipa chupa ya chai na baadhi ya vyombo ambavyo tutakuwa tukitumia katika muda wote tutakaokuwepo hapa ”akasema Happy .
“ Happy kumbe umeshaamka !Ahsante kwa kuniamsha nilikuwa nimeshajisahau kabisa.” Patrick akasema huku akijiinuataratibu pale kitandani.
“Nimekwisha amka kitambo Patrick..Jiandae ninakusubiri tunywe chai ” akasema Happy.Patrick akaelekea bafuni akaoga na kisha wakapata kifungua kinywa.
Baada ya kupata chai wakatoka na kuanza kuzunguka katika mji wa kihistoria wakifurahia mandhari yake .Walizunguka sana na mchana wakaenda kupata chakula katika mgahawa uliomilikiwa na mama mmoja wa makamo.Walimuomba mama yule awe akiwatengenezea chakula kwa muda wote watakaokuwa pale Bagamoyo.Mama yule akakubali kuwahudumia bila matatizo.Kisha pata chakula wakarudi hotelini kupumzika hadi saa kumi jioni halafu wakaanza kusoma.
“Happy tunatakiwa tuutumie muda wetu mwingi hapa Bagamoyo kwa ajili ya kusoma ili kuwa sawa na wenzetu waliobaki shuleni .Tutakaporudi shuleni tutakuwa tunakaribia kipindi cha mitihani na lengo langu mimi ni sisi kufanya vizuri zaidi ili wale wote ambao wanatuonea wivu waone aibu.”
“Usijali Patrick nina imani tutasoma na tutafanya vizuri.”akajibu Happy .
Saa mbili usiku wakaenda kupata chakula cha usiku kisha wakarejea tena kusoma hadi saa tano za usiku halafu kila mmoja akaenda kulala.Hii ilikuwa ndiyo ratiba yao kubwa kila siku.Jumamosi na jumapili walizitumia kutembelea sehemu mbali mbali za kihistoria hapo Bagamoyo.
Ilikuwa ni jumamosi angavu .Kijua kilikuwa kikali .Ni siku ya ishirini tangu wamewasili Bagamoyo. Saa sita mchana iliwakuta Patrick na Happy katika sehemu moja maarufu sana hapa Bagamoyo.Ni Patrick ndiye aliyeweka msisitizo mkubwa kuwa ni lazima wafike mahali hapa kabla hawajarudi shuleni.Hapa ni sehemu inayojulikana kama kaburi la wapendanao.Sehemu hii ni sehemu maarufu sana na watu wengi hupenda kwenda mahali hapa wakiwa na wapenzi wao na kuwekeana ahadi mbali mbali mbali katika safari nzima ya mapenzi hasa kutokana na historia ya watu hao waliozikwa hapo.
“Happy hii sehemu ndiyo inaitwa kaburi la wapendanao.Waliozikwa hapa inasemekana ni watu waliokuwa wamependana kwa dhati .”CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Happy akatabasamu ,na huku akiogopa ogopa.
Patrick akamsogelea Happy akamsika mikono yote miwili kisha akamwangalia machoni
“Happy toka tumekuja Bagamoyo tumetembelea sehemu mbali mbali za kihistoria.Tumejifunza mambo mengi.Hii nilitaka iwe ni sehemu ya mwisho kwa sisi kutembelea tukiwa hapa Bagamoyo.” Akanyamaza kidogo kisha akaendelea
“Nina sababu kubwa ya kuamua kuja eneo hili.Happy waliolala hapa chini ni watu ambao inasemekana upendo wao ulikuwa wa kweli.Hii ndio sababu kubwa ambayo watu wengi na hasa wapenzi hupenda kuja mahali hapa na kuwekeana ahadi mbali mbali katika safari yao nzima ya kimapenzi.Nadhani utajiuliza kwamba na sisi je nini kilichotuleta hapa? Happy nimeamua kukuleta hapa leo hii ili niweze kudhihirisha jinsi gani ninavyokupenda.Nakupenda sana Happy .Toka tulipokutana na kuwa marafiki niliona ishara na kuamini kuwa wewe ndiwe pekee uliyeumbwa kwa ajili yangu.Tafadhali Happy naomba unikubalie ombi langu .Naomba uwe mpenzi wangu.Nakuahidi mbele ya watu waliolala hapa chini kwamba siku zote nitakupenda ,nitakujali na kukuthamini hadi kifo kitakapotutenganisha.Hata siku moja sintakutoa machozi” akasema Patrick akimtazama Happy usoni huku ameishika mikono yake
Taratibu Happy akaiachia mikono ya Patrick,akiwa kama vile mtu aliyepigwa na bumbuwazi.Akamtumbulia macho Patrick kana kwamba ni kwa mara ya kwanza kumuona.Moyo ukamwenda mbio kijasho kikamtiririka.Akafumbua mdomo kutaka kusema kitu lakini akajikuta anashindwa.Patrick ambaye leo hii alikuwa na ujasiri wa aina yake akamsogelea ,akamshika mkono.,akamwangalia usoni.
“Happy I’m sorry.Sikutegemea kama ningekuudhi.naomba vile vile ufahamu kuwa sina lengo baya na wewe,sina lengo la kukuharibia masomo au maisha yako.Naheshimu ndoto zako ,naheshimu maisha yako na ninakuheshimu wewe pia.Natambua kuwa una ndoto zako nyingi siku za usoni na hata mimi nina ndoto zangu pia na ambazo ni lazima nizitimize na moja kati ya ndoto zangu kubwa ni kuwa na wewe.You are my dream Happy .Lakini naona kama vile nimekukwaza na kauli yangu hivyo naomba usahau.Just pretend I didn’t say anything.Naomba kauli yangu hii ya leo isije ikavuruga urafiki wetu .I’m sorry.Happy” Patrick akasema .
Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Mashavu yake yote yalikuwa yamelowa machozi.Alitamani kusema neno lakini midomo ilikuwa ikicheza cheza na kushindwa kuongea.Akajikaza na kusema
“Patrick ! siyo hivyo unavyofikiri.Patrick huwezi jua jinsi gani ulivyoustua moyo wangu.Sikutegemea kama ungeweza kunitamkia maneno haya leo…
“Shhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!.I’m sorry Happy .Nilishindwa kuvumilia .Nimeshindwa kupigana na hisia zangu kwako .Sahamani sana” Patrick akasema
“No Patrick usinifikirie vibaya.Simaanishi hivyo unavyofikiria wewe.Ni kwamba sikuwa nimetegemea kama utakuja kuniambia kitu kama hiki leo.Naomba niwe wazi kuwa nimekuwa nikiumia sana moyoni kwa muda mrefu nikisubiri siku kama hii ya leo ambayo ungeniambia maneno haya.I love you Patrick.I love you so much.Th…….”Akashindwa kuendelea akaanza kulia kwa kwikwi.Patrick akatoa kitambaa na kumfuta machozi .Happy akamtazama Patrick usoni kwa sekunde kadhaa kisha wakakumbatiana kwa nguvu..
“Thank you so much Happy kwa kunipenda.I promise you that I’will never hurt you.Nakuahidi hapa mbele ya kaburi la wapendanao kuwa sintakubali kitu chochote kitutenganishe .Naomba kifo tu ndicho kiwe kitu pekee cha kuweka kutufanya tutengane.Naomba hata kama tukitenganishwa na kifo basi kama kuna uwezekano tufe sote na kuzikwa pamoja kama watu hawa hapa chini.” Patrick alitamka maneno haya kwa umakini mkubwa na ni wazi yalitoka ndani kabisa mwa moyo wake.Happy macho yalikuwa yamemjaa machozi wakati akisikiliza maneno ya Patrick.
“Patrick hata mimi nashukuru sana kama hisia zako kwangu ni za kweli .Ninaichukua ahadi yako kama ilivyo na kuihifadhi moyoni mwangu.Na mimi kama ulivyofanya wewe nakuahidi kuwa sintakuwa radhi kutengana nawe.Naahidi kuwa hakuna chochote kitakachoweza kututenganisha zaidi ya kifo..Ila naomba hapa tuwekeane ahadi kuwa pamoja na kwamba tumekubaliana kuwa wapenzi lakini hatutafanya mapenzi mpaka hapo tutakapokuwa tumemaliza masomo yetu.Niahidi hivyo Patrick”akasema Happy
Patrick akamwangalia Happy kwa tabasamu kubwa kisha akasema.
“Nalifahamu hilo Happy .Ndio maana nikasema kuwa nitakuheshimu na kuziheshimu ndoto zako.Nafahamu hatari za mapenzi shuleni hivyo niko makini sana na suala hilo.Usitie shaka natumai tutakuwa na muda mzuri baada ya kumaliza masomo yetu.”
Happy akatabasamu na kumkumbatia Patrick.Walibaki wamekumbatiana kwa takribani dakika kama tano hivi huu ulikuwa ni mwanzo wa ukurasa wao mpya
Siku mbili kabla ya adhabu yao kumalizika Patrick na Happy wakarejea shuleni.Mara tu baada ya kuwasili kwao shuleni tayari maneno ya chini chini na vijembe vikaanza.Muda huu walioutumia wakiwa Bagamoyo uliwajenga na kuwafanya wawe majasiri hivyo hali hii haikuwatia hofu.Uhusiano wao ukaendelea kama kawaida na safari hii wakawa karibu zaidi.Muda mwingi waliutumia kusoma pamoja hivyo kuwafanya wanafunzi wenzao kuongeza udadisi zaidi.
Ilikuwa ni wiki ya tatu siku ya jumamosi tangu Patrick na Happy warejee toka katika adhabu.Siku hii kulikuwa na tamasha la michezo lililojumuisha shule ya Malangali na shule ya sekondari Ifunda.Lilikuwa ni tamasha kubwa na lililopendeza sana.Uongozi wa shule uliamua kufanya tamasha hili ili kuwaburudisha wanafunzi kabla ya kipindi cha mitihani ya kumaliza muhula wa pili kuanza.
Tamasha lilianza saa nne asubuhi kwa michezo mbali mbali kama vile kukimbia ,kucheza ngoma ,sarakasi nk.Kisha maliza awamu ya kwanza ,wanafunzi wakaenda kupata chakula cha mchana kabla ya kuanza kwa awamu ya pili mchana huo.
Saa nane mchana ikaanza awamu ya pili.wanafunzi wote wakakusanyika katika viwanja vya michezo.Michezo iliyokuwa ikifanyika mchana huu ni mpira wa kikapu,wavu,pete na mwisho kabisa mpira wa miguu.
Karibu katika kila mchezo shule ya sekondari Ifunda ikachukua ushindi.Na sasa ushindani ukahamia katika mpira wa miguu.Wanafunzi wote wakahamia katika uwanja wa mpira wa miguu.
Patrick na Happy walikuwa wakishuka taratibu sana wakielekea katika uwanja wa mpira ili kushuhudia mtanange huo wa kukata na shoka.Hawakuwa wamehudhuria mchezo wowote toka tamasha lilipoanza.Walikuwa wamejificha mahala akijisomea.Wote wawili hawakuwa wapenzi sana wa michezo.
Kiujumla walikuwa wamependeza mno siku hii ya leo na kila aliyepisha nao hakukosa kugeuka kuwatazama.Hawakujali macho ya watu ,wakafika uwanjani na kutafuta sehemu moja iliyokuwa na msingi wa nyumba wakakaa.Waliamua kujitenga kabisa na wenzao.
Mpira ukaanza kwa kasi sana.Dakika ya kumi na moja ya mchezo Ifunda wakapata bao la kuongoza.Mpira ukaendelea na dakika ya arobaini wakapata tena bao la pili.Mpaka mapumziko Ifunda walikuwa wakiongoza kwa mabao mawili.Ilikuwa ni simanzi kubwa kwa upande wa malangali kupoteza kila mchezo.
Kipindi cha pili kikaanza kwa kasi.Dakika ya tisa ya kipindi cha pili Malangali wakapata bao lakini refa akakataa kwa madai kuwa mfungaji wa bao lile likuwaameotea.Wanafunzi wa Malangali wakavamia uwanja na ikazuka vurugu kubwa.Wachezaji wa Ifunda wakatoka uwanjani na kuanza kukimbia wakijaribu kujiokoa na ile vurugu.Mawe,fimbo ,chupa vikawa vikirushwa uwanjani.
“Happy tuondoke mahali hapa si salama tena”Akasema Patrick huku akimshika mkono Happy lakini kabla Happy hajamaliza kuvaa viatu vyake vya kuchomeka alivyokuwa ameviweka kando ya miguu yake jiwe kubwa lililorushwa upande wao likampiga kichwani akaanguka chini huku damu nyingi ikimmwagika.
“Nooo..!!!!!!!.........” Patrick akapiga ukelele mkubwa baada ya kumuona Happy akiwa amelala chini huku damu nyingi ikimvuja kichwani.
Akamwinamia Happy kwa haraka huku machozi yaliyoambatana na hasira yakimtoka.Mwalimu Vicent ambaye alikuwa karibu na mahali pale aliliona tukio lile naye akakimbia haraka kuja kuangalia hali ya Happy .alistuka kwa hali aliyoikuta.haraka haraka akakimbia na kwenda kumwita dereva wa shule akaja na gari na kwa haraka wakampakia Happy wakamwahisha katika kituo cha afya cha karibu.Patrick hakuongea kitu machozi yalikuwa yakimchuruzika.
Kituo cha afya Malangali hakikuwa mbali sana na shule.Kwa bahati mbaya wakati walipofika pale hakukuwa na daktari.Alikuwepo muuguzi mmoja tu.Kwa dakika kama mbili hivi hawakujua wafanye nini kwani hata muuguzi yule alionekana kuwa na hofu kutokana na hali aliyokuwa nayo Happy.
“I have to do something” Patrick akawaza.ghafla akatoka mbio kuelekea kijijini.Hakuna mtu yeyote aliyejua Patrick anakwenda wapi.Dakika kama kumi baadaye gari moja aina ya Toyota pick up ikaja kwa kasi kubwa maeneo hayo ya hospitali huku ikiwa imewasha taa.Watu waliokuwepo hapo nje wakaanza kuingiwa na wasi wasi labda kuna maafa mengine yametokea.Gari ikafunga breki kali na mara bila kutegemea Patrick akashuka.
Mpaka muda huo bado Happy alikuwa ndani ya gari akiwa hana fahamu huku mwalimu na yule muuguzi wakizuai damu kuendela kuvuja huku wakijadiliana jinsi ya kumpata daktari ambaye kwa wakati huo hawakujua alikuwa wapi.
“Haraka haraka,nisaidieni kumbeba.”Akasema Patrick akiwaambia watu wawili aliokuja nao katika ile gari.Huku mwalimu na muuguzi wakishangaa Happy akashushwa toka katika gari ya shule na kupakiwa katika ile gari ndogo aliyokuja nayo Patrick.
‘Patrick unafanya nini??.................Alipaaza sauti mwalimu akiwa haelewi nini Patrick alikusudia kufanya.
“Dereva ondoa gari achana na huyo mwalimu”Patrick alisema huku akifunga mlango .
gari ikaondolewa kwa kasi ya ajabu kila mtu akibaki ameduwaa.
* * * *CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“ahsanteni sana ndugu zanguni nashukuru mmenisaidia”Patrick akawaambia dereva na yule msaidizi wake baada ya kufika katika hospitali ya Makambako na Happy kuanza kupatiwa matibabu.
“Usjali dogo siku yoyote ukiwa na tatizo unasema.sisi sote binadamu lazima tusaidiane.”akasema dereva.
Baada ya kuwalipa pesa zao wakaondoka kurudi malangali na kumwacha Patrick hapo hospitali.Giza tayari lilikwisha ingia.Happy alikuwa katika chumba cha upasuaji akishonwa jeraha lake la kichwa.Lilikuwa ni jereha kubwa lililompelekea apoteze damu nyingi .Bado alikuwa hajarejewa na fahamu.Patrick bado alikuwa nje ya chumba hicho akisubiri kujua hali ya Happy itakuwaje .Moyoni bado alikuwa na fundo kubwa lililomkaa juu ya kilichokuwa kimetokea.Alianza kuvuta picha ya jinsi tukio lile lilivyotokea .Alikumbuka wakati vurugu imeanza na mawe kuanza kurushwa.hadi jiwe lile kumpata Happy kichwani, ni wazi tukio lile lilikuwa limedhamiriwa.
“Naanza kupata picha kuwa mrushaji wa jiwe lile alikuwa amedhamiria kabisa kumjeruhi Happy au mimi.”akawaza Patrick.akiwa katika lindi la mawazo mara mlango wa chumba cha upasuaji ukafunguliwa na machela ikatoka.
“Kijana hali ya mwenzio inaendelea vizuri .Tumeshona jeraha lake na sasa tunampeleka wodini .Tutamuongezea damu kwa sababu amepoteza damu nyingi sana.wewe unaweza kwenda kupumzika .Uje asubuhi”Alisema daktari mama wa makamo ambaye alionekana kuwa na roho ya huruma.
“Ahsante daktari kwa kazi kubwa mliyoifanya.Lakini nitabaki hapa hapa mpaka asubuhi kwa sababu tayari imeshakuwa usiku na mimi hapa Makambako ni mgeni”
“Nyie mmetokea wapi” Akauliza yule daktari
“sisi ni wanafunzi wa shule ya sekondari malangali” patrick akajibu.Baada ya mahojoano mafupi na yule mama akamwangalia Patrick kwa sekunde kadhaa kisha akasema.
“Umefanya kitendo cha kijasiri sana ..kama ungeendelea kukaa pale shuleni hali ya mwenzio ingekuwa mbaya zaidi na hata kupoteza maisha.Nitamwambia dereva wetu akupeleke nyumbani kwangu ukapumzike hadi kesho.Umeonyesha moyo wa ujasiri sana wa kumsaidia mwenzako..Nisubiri hapo hapo” Alisema yule mama na kuingia ndani.
Patrick aliendelea kumwomba Mungu kimoyo moyo hali ya Happy iwe nzuri.
“Twende” akasema yule daktari wakaondoka na kisha Patrick akapanda gari la hospitalina kupelekwa nyumbani kwa yule daktari
.
* * * *
Saa kumi na mbili asubihi ilimkuta Patrick tayari amekwisha fika hospitali.Hakuweza kupata usingizi usiku huo licha ya kuhakikishiwa kuwa hali ya Happy ilikuwa nzuri.Moyo ulikuwa ukimwenda mbio.Aliingia katika wodi aliyolazwa Happy kwa wasi wasi mwingi.Lakini ghafla akakutana na sura angavu yenye matumaini ya Happy .tayari alikwisha pata fahamu toka usiku.Patrick akafumba mdomo kwa kiganja cha mkono wake akionyesha mshangao.kwa haraka akakimbia na kumkumbatia Happy pale kitandani.
”Pole sana Happy ”
‘ahsante Patrick.nashukuru sana kwa msaada wako”
“Usijali Happy ulikuwa ni wajibu wangu kufanya hivyo”akajibu Patrick.
“ nilikuwa na wasi wasi mwingi wakati fahamu zimenirudia nikiwaza nilifikaje fikaje hapa..Muuguzi mmoja aliyekuwapo zamu ya usiku akaniambia kuwa kuna rafiki yangu mmoja anaitwa Patrick pamoja na watu wengine wawili ndio waliokuleta hapa.Nilifurahi sana kusikia hivyo.nashukuru sana Patrick.Kwa sasa naamini kuwa upendo wako kwangu ni wa kweli.”
Patrick hakujibu kitu akatabasamu.
“sasa Patrick nina imani nitazidi kuwepo hapa hospitali kwa siku kadhaa hivyo nitakupa namba hizi za simu umpigie mama yangu na umweleze mkasa mzima jinsi ulivyokuwa ili aje anihudumie kwa kipindi hiki chote nitakachokuwa hapa hospitali. Kwa sababu wewe unatakiwa kwa sasa uanze kujiandaa na mitihani ambayo haiko mbali sana.”
Patrick akakubaliana na ushauri ule na kuzichukua zile namba.
‘ Happy ungependa kula ni ni asubuhi hii”Patrick akauliza
“Mimi nimeshashiba kwa kukuona wewe tu.Patrick wewe ni chakula tosha kabisa.Usisumbuke Patrick sintakula kitu .Jitahidi ukawasiliane na mama najua atanihamisha hapa na kwenda kutibiwa Mbeya.”
Waliongea mambo mengi asubuhi hiyo hadi muda wa kuwaona wagonjwa ulipoisha kisha Patrick akamuaga Happy kuwa anaenda kupiga simu.
Saa tano na dakika ishirini na saba gari moja ndogo yenye vioo vyeusi lilifunga breki katika hospitali ya Makambako .Mama mmoja akiongozana na binti mmoja ambaye ni wazi alionekana kuwa ni mwanae walishuka ndani ya gari lile na kuelekea mapokezi.Waliongea na wauguzi waliokuwapo pale mapokezi kisha wakapelekwa kwa mganga mkuu.Baada ya muda wakatoka wakiwa wameongozana na mganga mkuu na kuelekea maeneo ya wodi za wagonjwa.
Patrick alikuwa nje ya wodi aliyokuwa amelazwa Happy .Hali ya hewa ilikuwa ya kiubaridi baridi kama ilivyo ada ya hali ya hewa ya Makambako.Kijua kilichomoza na kuzima.Hii haikumsumbua sana kwa sababu alikuwa bado amevaa suti aliyokuwa ameivaa jana yake.Mara akawaona mama mmoja na mwanae wakiwa wameongozana na daktari mkuu.
“Mhhhh!!” Patrick akaguna.Akazidi kuwaangalia kwa makini watu wale wakija .
“Yule msichana mbona kafanana sana na Happy ? anaweza akawa ndiye yule ndugu yake ? hata yule mama amefanana sana na Happy” Patrick akaendelea kuwaza huku akiwatazama yule mama na yule binti wakielekea katika wodi aliyokuwa amelazwa Happy..
Mama yule ,binti yake pamoja na daktari mkuu wakampita Patrick pale nje na kuelekea moja kwa moja katika wodi ile aliyokuwa amelazwa Happy wakaingia ndani.
“Nahisi ni wenyewe hawa.nahisi huyu ndiye mama yake Happy .”Akawaza Patrick huku akijiweka sawa kwani alitegemea ni lazima wangeonana..Dakika kama tano hivi toka yule mama aingie mle wodini alikuja muuguzi na kumwita Patrick ndani.
“mama huyu ndiye Patrick ni rafiki yangu na ndiye aliyeyaokoa maisha yangu kwa kunileta hapa hospitali haraka.”
Akasema Happy baada ya Patrick kuingia
“ooh ! Ndiye huyu ! Ndiye huyu aliyenipigia simu asubuhi?”
“Ndiye mimi mama.Shikamoo” Patrick akasema kwa adabu
“Marahaba mwanangu.nashukuru sana kwa msaada wako.”
“Ahsante mama”Patick akajibu.
Mama yake Happy alikuwa ni mtu mchangamfu na mcheshi sana.
“Patrick huyu ni mdogo wangu anaitwa Margareth.” Happy akasema
“Nafurahi sana kukufahamu margareth.”Akasema Patrick huku akishikana mikono na Margareth.Mama yao alikuwa akitabasamu akasema
“Patrick tunashukuru sana kwa msaada wako lakini itabidi Happy tumuhamishe hospitali.Tutaenda naye Mbeya akatibiwe kule.Kwa hiyo wewe unaweza ukarejea shuleni.Utapewa barua na mganga mkuu wa hapa ili uipeleke shuleni ya kuthibitisha ugonjwa wa mwenzio.”
“sawa mama” akajibu Patrick
Saa saba na nusu za mchana Patrick akawasili shuleni na moja kwa moja akaelekea katika ofisi ya mkuu wa shule msaidizi.
“Patrick !!.. akasema mkuu wa shule msaidizi baada ya Patrick kuingia ofisini kwake.
“Naam mwalimu”
“Umefanya nini tena? Hata wiki mbili hazijaisha toka utoke kwenye adhabu leo tena unarudia mambo yale yale? Akasema mwalimu kwa ukali
“Sikiliza mwalim…………………..”
“noo !! sitaki kusikiliza upuuzi wako.kwa nini ukamchukua mgonjwa na kukimbia naye mahala kusikojulikana?Sisi kama walimu ndio walezi wenu ninyi mkiwa hapa shuleni . tutajibu nini kwa wazazi wake pindi tatizo kubwa likimpata? Akaendelea kufoka mwalimu mkuu msaidizi
‘.Mwalimu,siku ile ya mashindano baada ya kutokea vurugu Happy alijeruhiwa na jiwe kichwani akapoteza fahamu.damu nyingi ikawa ikimvuja.Mimi na mwalimu Steve pamoja na dereva wa shule tukampakia garini na kumpeleka zahanati .pale hakukuwa na daktari na muuguzi tuliyemkuta pale alikuwa akisita hata kumuhudumia Happy .Mimi sikuridhika na hali ile ikanibidi nikodi gari kwa pesa zangu na kumuwahisha Happy hospitali ya Makambako ambako alipatiwa matibabu,akashonwa jeraha lake ,akaongezewa damu pia.na hii hapa ni barua toka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Makambako.”
Mkuu wa shule msaidizi akaichukua barua ile na kuisoma kisha akamwangalia Patrick kwa sekunde kadhaa.
“Ulifanya jambo jema Patrick .Uliokoa maisha ya mwenzio lakini siku nyingine unatakiwa ushauriane kwanza na sisi na siyo kuchukua maamuzi yako binafsi .Mashitaka yaliyoletwa hapa kwangu ni kwamba ulifanya vurugu na kumchukua Happy .Hivi sasa tulikuwa katika maandalizi ya kuripoti suala hili katika vyombo vya usalama vitusaidie kukutafuta na kukuchukulia hatua.Haya nenda ukapumzike ila kuwa mwangalifu sana kwa sasa unafuatiliwa kwa kila unachokifanya” akasema mwalimu
“Ahsante sana mwalimu nitakuwa mwangalifu”
Patrick akatoka ofisini kwa mkuu wa shule msaidizi na kuelekea bwenini.Akaoga na kujilaza kitandani.
Mwezi wa kwanza mwaka uliofuata shule zikafunguliwa na ikawa ni awamu mpya kwa Patrick na Happy .Kwa sasa walikuwa kidato cha nne na walifahamu nini walichokuwa wakihitajika kukifanya hivyo hawakuwa na mzaha katika kusoma.Walisoma kwa bidii kubwa kwa lengo moja tu la kutimiza ndoto zao.Wawili hawa kwa ghafla waka ni mfano wa kuigwa na wengine.Tofauti na mwaka uliotangulia kwa sasa wakaanza kuwa na marafiki wengi wa madarasa ya chini yao ambao mara nyingi walipewa msaada mkubwa katika masomo.Kitendo cha kuheshimiwa na wanafunzi wa vidato vya chini kilizidi kuwapa wakati mgumu wale wanafunzi adui zao ambao walikuwa hawawatakii mema.
Ilikuwa ni tarehe 14/03 siku ya jumamosi ambapo wanafunzi walikuwa wametangaziwa kuwa siku hiyo kungekuwa na burudani ya muziki.Burudani kama hizi huja mara chache sana hapa shuleni,hivyo wanafunzi walikuwa wamejiandaa vilivyo.Patrick na Happy nao walishauriana na kukubaliana kuwa wangeingia ukumbini japo kwa muda mchache tu halafu waendelee na ratiba yao za kujisomea.
Baada ya mlo wa jioni milango ya ukumbi ikafunguliwa na wanafunzi wakaanza kujitoma ndani.Disko likafunguliwa rasmi na wanafunzi wakaanza kuserebuka.Patrick na Happy wakaingia ndani ya ukumbi lakini hawakukaa sana kutokana na joto ,wakatoka na kwenda kupunga upepo nje.Wakiwa nyuma ya bwalo la chakula wakipunga upepo huku mbalamwezi ikumulika mara ghafla likatokea kundi la vijana waliokuwa wamefunika nyuso zao wakiwa na mapanga matatu wakawazingira.Happy akaogopa na kumkumbatia PatrickCHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mama yangu !!!!,”Happy akasema kwa mstuko
“ kaa kimya na usijaribu kupiga kelele kwani tutawaua sasa hivi.”Akasema jamaa mmoja aliyekuwa na sauti nzito .Happy alikuwa akitetemeka.Patrick naye mikono ilikuwa ikimtetemeka.
Kundi lile lilikuwa na vijana zaidi ya kumi na wote walikuwa wamefunika nyuso zao.
Mmoja ambaye ndiye aliyeonekana kuwa kiongozi wao aliwasogelea na kumshika mkono Happy .
“Tuna shida na huyu binti” Akasema yule jamaa huku akimvuta Happy kwake.
Patrick akainua mkono lakini kabla hajafanya lolote akapigwa na chuma kizito shingoni akaanguka chini na kuona giza, yule jamaa akamshika Happy kisha kwa haraka wakamjaza vitambaa mdomoni ili asiweze kupiga kelele.
“Haya jamani haraka haraka tumalize kazi.Leo ni leo.Keo nenda kaangalie kama kuna mtu yoyote anakuja maeneo haya .Ukiona kuna mtu anakuja tufahamishe haraka.”
Akaamrisha yule jamaa ambaye alionekana kuwa ndiye kiongozi wa genge lile
Happy alikuwa ameshikwa bara bara kiasi cha kutoweza kufurukuta akabebwa juu juu na kupelekwa katika kichaka cha karibu.Kwa kasi ya aina yaka yule jamaa kiongozi akaichana blauzi nyepesi aliyokuwa ameivaa Happy na kuyashuhudia matiti machanga ya kimwana huyu.Udenda ukamtoka.Happy alikuwa akilia lakini sauti yake ilikuwa haisikiki kutokana na vitambaa walivyomuweka mdomoni.
Fedhuli yule akaishusha suruali yake hadi magotini na kuanza kumsogelea Happy huku uume wake ukiwa umesimama wima.Akaivuta suruali ya Happy na kuishusha chini kisha akaivuta nguo ndogo ya ndani aliyokuwa ameivaa na kuichana Akaitupa pembeni akawaamuru wale watu waliokuwa wamemshika Happy wampanue miguu.
“Hii niyo dawa yake mshenzi huyu.Halafu anaonekana bado bikira.Hii ndiyo dawa ya wasichana kama wewe wenye maringo”
Akasema yule jamaa huku akiuchezea uume wake tayari kumwingilia Happy kwa nguvu
Taratibu Patrick akapata fahamu na kuhisi maumivu makali sana maeneo ya shingoni na mara kumbu kumbu zote zikarudi.Akakumbuka kuwa walikuwa wamevamiwa na yeye akapigwa na kitu kizito shingoni.
“Happy yuko wapi?” Akajiuliza na mara akakumbuka kwamba wale wahuni waliowavamia walimchukua kwa lengo la kumtenda vibaya.Akajikaza na kuamka pale alipokuwa amelala huku akihisi maumivu makali mno.Happy hakuwapo na wala wale jamaa waliowavamia hawakuwapo.Hasira ikampanda .
“ I must do something immediately kabla hawa jamaa hawajatekeleza mpango wao” AkawazaPatrick.Pale chini akakiona kile chuma alichopigwa nacho akainama na kukiokota kisha akaanza kunyata kuelekea mahala aliposikia minong’ono ya watu.Alinyata taratibu akiwa amefura kwa hasira.
Ndani ya kichaka Happy alikuwa ameshikwa barabara kiasi kwamba hakuweza kufurukuta wala kupiga kelele kutokana na matambara yaliyojazwa mdomoni.Kiongozi wa genge lile alikuwa akijiandaa tayari kabisa kutekeleza kitendo cha kumbaka Happy .Ni machozi pekee ndiyo yaliyokuwa yakimtoka binti huyu mrembo .Roho ilimuuma sana kwa kushuhudia kitendo kile alichotaka kufanyiwa.Vile vile aliumia sana roho baada ya kumfikiria Patrick.Hakuwa na uhakika kama atakuwa salama kwani alishuhudia yeye mwenyewe kwa macho yake Patrick akipigwa na chuma kizito akaanguka chini.Ni uchungu ambao hauwezi kuelezeka aliokuwa nao binti huyu.Hakuwa na tumaini la kupata msaada wa aina yoyote kwa wakati ule.Msaada pekee alikuwa ni Patrick na ambaye aliamini kuwa kwa pigo lile lazima atakuwa katika hali mbaya ya kutokujitambua kama sio kufa kabisa
Wakati jamaa yule akiuchezea uume wake mkubwa ,Happy huku machozi yakimtoka akafumba macho na kuomba
“Ee Mungu najua sina ubaya wowote na mtu yeyote yule hadi kufanyiwa kitendo hiki.Ee baba kama sistahili kufanyiwa hivi basi na isiwe lakini kama …….
Hakumaliza maombi yake mara ghafla yule jamaa aliyekuwa tayari kumwingilia akapiga ukelele mkubwa na kuanguka chini.Kilichofuata hapo ni kusikia vishindo vya watu wakikimbia.Ulikuwa ni muujiza ambao Happy hakuutegemea katu.Kijana mmoja ambaye hakuweza kumtambua kwa haraka kutokana na giza alikuwa amesimama mbele yake na kisha akamwinamia.
“Happy are you ok?” Ilikuwa ni sauti ya Patrick ambaye aliongea akiwa katika maumivu makali sana.
Happy hakusema kitu ni machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakimtoka .Hakuamini kabisa kwa alichokuwa akikiona.
Patrick akamtoa yale matambara aliyokuwa amewekewa mdomoni kisha akambusu.
“:Patrick you are my Hero.” Ni neno hilo tu ambalo Happy aliweza kulisema kwa wakati huu.Mwili wote ulikuwa ukimtetemeka.
“Hawajakufanya kitu chochote washenzi hawa? Akauliza Patrick
“Hwakuwahi, ulifika kwa wakati muafaka kabisa bado walikuwa hawajatimiza azma yao.Ahsante Patrick”Akasema Happy huku machozi yakimtoka
Pale chini alikuwa amelala yule kiongozi wa genge lile la wahuni akivuja damu kichwani mahala alipopigwa na chuma .Patrick akamwangalia kwa hasira sana.
“Patrick huyu jamaa ni mzima kweli? Happy akauliza
“I don t know Happy .Sijui kama atakuwa mzima.Nilimpiga kwa nguvu zangu zote nilizokuwa nazo..Hiyo ni adhabu yake” akajibu Patrick
Ghafla wakasikia makelele ya watu wakija kwa kasi kule mahala walikokuwa.
“Happy lets get out of here.wasije wakatukuta hapa hawa watu.tayari wamekwisha ambizana.” Akasema Patrick na kumshika Happy mkono wakaanza kukimbia kushuka katika korongo.Hawakufika mbali wakamulikwa na tochi usoni.
“Hey ! simameni hapo hapo,mkikimbia ninaachia mshale huu”Ilikuwa ni sauti nzito ya mwanaume.Patrick na Happy wakasimama.Walikuwa ni watu wanne waliokuwa na mbwa .Watu hawa walikuwa ni wawindaji waliokuwa wakifuatilia mitego yao porini.
“Tafadhali jamani naomba mtuache tuondoke tuna matatizo makubwa” Akasema Patrick
“Hapana kwanza ninyi mnaonekana ni wanafunzi.Usiku huu mnafanya nini porini?Haya anzeni kuongoza tunawarudisha mpaka shuleni” Akaamuru jamaa mmoja ambaye alionekana kuwa ndiye kiongozi wa wale wawindaji.
Jitihada za Patrick an Happy kuomba waachiwe hazikuweza kuzaa matunda,jamaa wakaanza kuwaongoza kuwarudisha shuleni.
Hawakuwa na ujanja tena zaidi ya kufanya vile walivyoamriwa.
* * * *
“wameuaaaaaa !!!....wauajiiiiiiiiii!!!!!!......wauaweeeee!!!!!!!!!!” Hizo ni kelele zilizoufunika mji wa Malangali kwa muda huu wa usiku.Patrick na Happy walikuwa katika mikono ya polisi kwa ajili ya usalama wao.Yule jamaa aliyepigwa na chuma kichwani na Patrick alikuwa amekufa.
Karibu kijiji chote kilikuwa kimeamka kutokana na makelele ya wanafunzi na kukusanyika shuleni.Wote walitaka washuhudie ni wanafunzi gani waliofanya mauaji.Baada ya kuingizwa katika kituo kidogo cha polisi kilicho pembezoni mwa shule ikawabidi polisi kupiga risasi za moto juu ili kuwatawanya wanafuzi ambao walikuwa wameanza kurusha mawe wakitaka watuhumiwa waachiwe ili wauawe pia.Ilikuwa ni kazi kubwa kuwatawanya lakini hatimaye walifanikiwa baada ya kupiga risasi kadhaa hewani.
Happy machozi yalikuwa yakimtoka.Hakutegemea kama siku moja angeweza kuingia katika dhahama ile.Hakuwahi kuota kama siku moja angeitwa muuaji.
“Nyamaza Happy ,usilie mambo yameshatokea..Jipe moyo Mungu yupo na yeye ndiye anayeufahamu ukweli.” Patrick akambembeleza Happy
“Patrick nina uchungu mwingi sana .Ni bora ningekuwa mwenyewe lakini sasa nimekuingiza na wewe katika matatizo makubwa namna hii.tayari nimekwisha kuharibia mwelekeo mzima wa maisha yako……….”
“Shhhhhhhh..!!!....Usiseme hivyo Happy .I did the right thing.Hata nikinyongwa nitakuwa na amani kwamba niliua kwa ajili ya kukulindia heshima yako.Hakuna mwanaume yeyote anayeweza kukubali kuona mpenzi wake akifanyiwa kitendo cha kinyama kama walichotaka kukufanyia hawa jamaa.nadhani nilifanya kitu sahihi.Sijutii kosa langu kwa sababu nimefanya kwa ajili ya mtu nimpendaye”
Happy akamkumbatia Patrick kwa nguvu huku akilia .
Kwa ajili ya usalama wao usiku huo huo wakapakiwa katika gari la polisi na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Iringa mjini .
*******************************
Uchunguzi wa kesi ya mauaji inayowakabili wanafunzi wawili wa kidato cha nne Patrick na Happy ulianza kwa kasi .Wazazi wa happy wakishirikiana na wale wa Patrick waliweka mawakili sita wa kuwatetea watoto wao.Pamoja na jitihada hizo zote za kuhakikisha kuwa watoto wao wanaachiwa huru na mahakama bado kesi ikaonekana kuwa ngumu kutokana na ushahidi mkubwa wa wanafunzi kuwakandamiza Patrick na happy.Wanafunzi zaidi ya kumi walikubali kusimama mbele ya mahakama na kutoa ushahidi kuwa Patrick na Happy kwa pamoja walishirikiana katika mauaji ya Angatile mmoja kati ya wanafunzi watukutu hapo shuleni.
Baada ya miezi miwili Happy akaachiwa huru na mahakama alipoonekana hakuwa na kesi ya kujibu.Patrick ambaye alionekana kuwa ana shataka la kujibu akabaki gerezani huku kesi yake ikiendelea kusikilizwa.Huo ukawa ni ukurasa mpya wa maisha yake gerezani.
Miezi ilizidi kukatika Patrick akiwa bado gerezani akiendelea kushikiliwa kwa shitaka la mauaji.Happy ambaye alikubaliwa na uongozi wa shule yao kuwa ataruhusiwa kurudi kufanya mtihani wake wa kidato cha nne aliendelea na masomo jijini Mbeya..Alidhoofu kwa mawazo na ukiwa aliokuwa nao.Furaha yote aliyoipata kwa muda mfupi ilikuwa imetoweka.Hakuwa tena na rafiki Rafiki yake mkuu alikuwa ni Patrick ambaye kwa sasa alikuwa gerezani.Kila siku alikuwa akilia na kumuomba Mungu amsaidie Patrick aweze kutoka gerezani .Moyoni alijua ni yeye ndiye aliyesababisha Patrick kuwapo gerezani .Patrick aliua wakati akijaribu kumtetea yeye asibakwe.Aliumia sana kila alipolifikiria suala hili.
Kila mwishoni mwa wiki alikwenda kumtazama Patrick na kumpelekea vitu mbali mbali.Wazazi wa Happy halikadhalika walikwenda mara kwa mara kufuatilia maendeleo ya kesi ya Patrick na kumjulia hali.Happy alikwisha waeleza kwa kina juu ya kilichosababisha Patrick kuwepo gerezani.Wazazi wa Patrick walijitahidi kwa kila walivyoweza ikiwa ni pamoja na kuongeza mawakili maarufu wa kujitegemea katika jopo la mawakili wanaomtetea Patrick.Kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa familia zote mbili .
Hatimaye kikafika kipindi cha kufanya mitihani ya Taifa ya kumaliza kidato cha nne Patrick akiwa bado gerezani.Siku tatu kabla ya mtihani huo kuanza Happy akamtembelea gerezani ambako waliongea mambo mengi.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Patrick mpenzi nasikia uchungu sana kwa hali hii.Tulikuwa na malengo mengi sana ya maisha yetu kwa siku za usoni lakini yote yameyeyuka.Sijui lini utatoka gerezani mpenzi wangu…………” Happy akashindwa kujizuia akaanza kulia ,Patrick akamkumbatia na kumbembeleza.
“ Nyamaza Happy .Hutakiwi kulia.Be strong.Haya ni mambo ya kawaida.Kila kitu hutokea kwa sababu maalum Huwezi kujua kwa nini sisi yametutokea haya.Maandiko matakatifu yanatuasa tushukuru katika kila jambo linalotufika.Sijutii kuwapo hapa kwa sababu niko hapa kwa ajili ya mwanamke nimpendaye.Kitu kimoja tu ninachokuomba jiandae vyema na mitihani yako na Mungu akujalie ufanye vizuri.Mimi nipo na Mungu atanisaidia siku moja nitatoka.Nitakuwa nimepoteza muda mwingi na mwelekeo mzima wa maisha yangu lakini nitakuwa na furaha kuwa nilipigana kiume kulinda heshima ya mtu nimpendaye duniani.Ila nakuomba kitu kimoja Happy ………”Patrick akanyamaza akavuta pumzi ndefu ,akamwangalia Happy kwa sekunde kadhaa ,akamfuta machozi .
“Happy naomba kabla muda wetu wa maongezi haujakwisha unihakikishie kitu kimoja kwamba pamoja na kuwa sijui lini nitatoka gerezani,pengine nitanyongwa lakini naomba kusikia kutoka kwako leo hii kuwa hautakuwa na mwanaume mwingine zaidi yangu pamoja na hali yangu hii kwa sasa.Naomba haya yote yaliyotokea yasipotee bure,naomba uendelee kuheshimu ahadi zetu tulizowekeana,naomba ue……………..”Patrick akashindwa kujizuia kutokwa na machozi.
“Patrick mpenzi wangu ,nyamaza kulia.Najua inauma sana na ni ngumu kuibeba adhabu hii kubwa lakini naomba nikuhakikishie kuwa kwa namna yoyote ile sintadiriki kuwa na mwanaume yeyote zaidi yako.Nitakusubiri kwa muda wote mpaka utakapotoka ili tuweze kutimiza ndoto zetu pamoja.I promise.”
Akasema Happy kisha wakakumbatiana kwa hisia kubwa huku kila mmoja machozi yakimdondoka.Muda ukaisha Happy akaombwa aondoke.
Muda ulikwenda kwa kasi .Na hatimaye matokeo ya kidato cha nne yakatoka na Happy akachaguliwa kuendelea na kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Iringa.Alifurahi sana kwa kuchaguliwa kwenda pale kwani atakuwa bado karibu na Patrick ambaye kwa sasa alikuwa ni sehemu ya maisha yake .Ingawa bado hakukuwa na matumaini yoyote ya Patrick kutoka gerezani kutokana na mwenendo wa kesi kuwa mgumu,lakini bado Happy alizidi kumpenda na kumpa moyo.Kila wiki alikuwa akienda kumtazama gerezani na kumpa faraja..
“Patrick matokeo yametoka “Alisema Happy alipokwenda kumtembelea Patrick gerezani mara baada ya matokeo kutoka.
“Hizo ni habari njema sana.Unakwenda shule gani ? Patrick akauliza
“nimechaguliwa kuendelea na masomo hapa hapa Iringa.Nitasoma Iringa girls.Nilikuwa nikiomba Mungu nisipangwe shule yoyote ya mbali ili isiwe vigumu kuja kukutembelea.Patrick wewe ni sehemu ya maisha yangu na kamwe siwezi kuvumilia kuwa mbali nawe.Nashukuru Mungu amesikia kilio changu .” Happy alisema huku amemkumbatia Patrick .
“Happy nimefurahi sana kusikia hivyo.Mungu bado anatupenda.Pamoja na misuko suko yote iliyotukumba lakini bado umeweza kufanya vizuri na kufaulu mtihani wako.Hongera sana Happy.Kumbuka kama imeandikwa kuwa mimi na wewe tutakuwa pamoja maishani hakuna ambaye anaweza kututenganisha.” Patrick akasema
Ilikuwa ni siku ya furaha sana kwao.
Mpaka Happy anamaliza kidato cha sita bado Patrick alikuwa akisota katika mahabusu ya gereza kuu la Iringa.Kesi yake ilikuwa ikisomwa na kuahirishwa mara kwa mara.Tayari Patrick alikwishazoea maisha ya kukaa mahabusu.Afya yake ilikuwa imedhoofu kutokana na maisha magumu ya gerezani.Faraja pekee aliyokuwa nayo ni Happy aliyekuwa akienda kumtazama kila jumamosi pamoja na wazazi wake.Upendo wa Happy haukupungua hata kidogo.Kila siku upendo wake kwa Patrick ulikuwa ukiongezeka.
Jumamosi moja Happy alienda kumtembelea Patrick kama ilivyo kawaida yake.Kwa sasa tayari alikwisha maliza shule na alikuwa akisubiri matokeo ya kidato cha sita.Wakati wakiongea Patrick akamtazama Happy usoni kwa makini na kusema.
“Happy mpenzi naomba nikufahamishe kuwa Jumatatu ndo ile siku yangu ya Hukumu .Nashukuru Mungu kwani baada ya kusota gerezani kwa muda mrefu hatimaye nitaenda kusomewa hukumu yangu.Sijui nini kitatokea.Mwenendo mzima wa kesi yangu unaonesha kuwa nina hatia japokuwa kesi ilibadilishwa na ikawa ni kuua bila kukusudia...Siyo siri ninaogopa.Sijui kama nitafungwa maisha au nitahukumiwa miaka mingapi gerezani.Mungu anajua kuwa sikukusudia kufanya vile lakini nilifanya kwa sababu ya kumlinda mtu nimpendaye asidharirishwe na wahuni wale.Happy naomba usiwepo mahakamani siku hiyo ya hukumu.Sitaki uumie.Ni wewe tu ndiye unayeufahamu ukweli hivyo kusikia hukumu nitakayoipata najua itakuumiza mno.Ila kumbuka vyovyote vile itakavyokuwa naomba ujue kuwa nakupenda sana.I love you so much Happy .Wewe ni mtu pekee ambaye ninayatoa maisha yangu kwake.Sintapenda mtu mwingine kama ninavyokupenda wewe…………….”Patrick akasema kwa hisia kali
Huku akitokwa na machozi Happy akasema
“Patrick nashindwa hata niseme nini.Siku zote tumekuwa tukiomba siku hii ifike haraka ili tujue hatma yako lakini kwa sasa naona kama vile siku hii isije.lakini siwezi kuizuia isifike.I’ll be strong.Nitajitahidi kuwa jasiri na kuwepo siku hiyo ya hukumu.I must be there Patrick.I mus………………” Happy akaangua kilio.
Ilichukua muda kumbembeleza Happy .Huzuni kuu ilitanda kwa vijana hawa.Hawakuongea sana walikuwa wamekumbatiana huku kila mmoja akiwa kimya.Kila mmoja akiwaza lake.
* * * *
Ni siku ya Jumatatu mahakama ilifurika watu.Wote walikuja kushuhudia hukumu ya Patrick,kijana mwanafunzi aliyemuua mwanafunzi mwenzake.
Ndugu za Patrick wote walikuwa wamewasili mapema sana hapa mahakamani.Si wao tu hata familia nzima ya akina Happy ilikuwa imewasili kusikiliza hukumu hii.Familia ya Happy na ile ya Patrick kwa sasa zilikuwa zimekwisha fahamiana na wote walikuwa kitu kimoja katika kumsaidia Patrick.
Saa mbili kamili juu ya alama gari lililowabeba washtakiwa wa kesi za mauaji ambao walikuwa wakisomewa hukumu zao liliwasili eneo la mahakama.Simanzi kuu ikatanda eneo hilo baada ya watuhumiwa wale kuwasili.Happy alishindwa kujizuia kudondokwa na machozi pale aliposhuhudia Patrick akishushwa toka katika gari maalum la kubebea mahabusu maarufu kwa jina la karandinga..Margreth na mama yake walijitahidi kumbembeleza na kumtaka ajikaze.Happy akanyamaza.
Hatimaye ule muda uliokuwa mgumu sana katika historia ya Patrick ukawadia.Muda wa hukumu.Patrick akapandishwa kizimbani akiwa ni mwenye majonzi makubwa .Macho yake yalikuwa hayaoni vizuri kutokana na machozi yaliyokuwa yanamtoka.Baadhi ya watu ambao hawakumuona kwa muda mrefu walikuwa wakimsikitikia kijana huyu kwa jinsi alivyodhoofu.Akiwa kizimbani mara akagonganisha macho yake na mama yake akajikaza na kutabasamu.Si mbali sana na alipokaa mama yake akakutanisha macho na Happy .Happy akatoa tabasamu la kulazimisha lenye kuonyesha kukata tamaa.Macho yake yalikuwa yamevimba kwa kulia.
Akapata faraja kubwa baada ya kugundua kuwa ndugu zake wote walikuwa wamekuja kusikiliza hukumu yake.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jaji kutoka mahakama kuu akaanza kusoma historia ya kesi na baada ya masaa matatu ukafika ule wakati mgumu kupita wote ,wakati wa jaji kuisoma hukumu..Happy moyo ulikuwa ukimwenda mbio.Mwili wote ulikuwa ukimtetemeka.Jasho lilikuwa likimtiririka.mama yake Patrik midomo ilikuwa ikimcheza kwa uoga .Kila mtu alikuwa akiuogopa sana wakati huu.Patrick yeye alikuwa ameinama akisali kimoyo moyo akimwomba Mungu ampe ujasiri wa kuweza kuipokea adhabu yoyote atakayopewa.
Mahakama iliridhika na ushahidi wa pande zote yaani upande wa mashtaka na upande wa utetezi.Kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili mahakama ikaridhia kuwa Patrick alikutwa na hatia ya kuua bila kukusudia hivyo akahukumiwa kwenda jela miaka mitano.
Mara tu baada ya hukumu kusomwa Happy akazimia na kutolewa nje kwa ajili ya huduma ya kwanza.Mama yake naye alishindwa kujizuia na kuangua kilio baada ya kumwona mwanae akipakiwa katika gari tayari kwenda kuanza kukitumikia kifungo chake cha miaka mitano.Patrick akajikaza kiume asilie ingawa alikuwa amepatwa na mstuko mkubwa .
Gari lililowabeba mahabusu likaondoka mahakamani hapo na kuacha vilio vikiendelea.mama yake Patrick naye alikuwa amezirai.Ni tukio ambalo lilivuta hisia za watu wengi. Hatimaye Patrick akayaanza maisha mapya ya gerezani katika gereza kuu Iringa.
MWAKA MMOJA GEREZANI
Tayari Patrick alikwisha kuyazoea mazingira ya gerezani humo.Hayakuwa mageni sana kwani amekwisha sota mahabusu kwa miaka kadhaa kabla ya kuanza rasmi kutumikia kifungo kwa hiyo maisha haya alikwisha yafahamu.na kuyazoea.Tayari alikwisha zoeana na wafungwa wengi ambao walimpenda kutokana na busara zake.Alikuwa ni kijana mdogo lakini mwenye busara za hali ya juu.Aliheshimika na kila mtu gerezani.
Kila mwishoni mwa wiki alikuwa akitembelewa na ndugu na jamaa zake.Happy ni mtu pekee ambaye hajawahi kukosa kila mwisho mwa wiki kuja kumtembelea mpenzi wake.Kufungwa kwa patrick bado hakukuwafanya watengane.Bado waliendelea kupendana kwa kiwango cha juu .Alijitahidi kwa kila alivyoweza kumwonyesha upendo wa pekee Patrick kwani aliamini yeye ndiye sababu kubwa kwa Patrick kuwapo pale gerezani.
Mwaka wa kwanza ulikatika ukaanza wa pili na hatimaye Happy akamaliza masomo yake ya kidato cha sita.Pamoja na kumaliza masomo yake lakini bado alikuwa akiendelea kumtembelea na kumjulia hali Patrick kila mwisho wa wiki..Matokeo ya kidato cha sita yalitoka na Happy akafaulu vizuri sana kwa daraja la kwanza. Ilikuwa ni furaha kwao wote baada ya matokeo haya kutoka.
Jumapili moja ,Happy alikwenda gerezani kama ilivyo kawaida yake akiwa katika sura iliyoonyesha kuwa na simanzi kubwa.Patrick akamshika mkono na kutaka kujua kitu kilichopelekea yeye Happy akawa katika hali ile.Huku akilia Happy akasema
“Patrick nashindwa kuelewa ni kwa nini kila wakati mimi ninakuwa katika majaribu makubwa.Niko katika majaribu makali sana Patrick” Happy akainama na kuanza kulia.
“Kwani kuna nini ? Hebu nieleze Happy ” Patrick akahoji
Happy akasita kidogo kisha akasema
“Baba amenitafutia Chuo nchini Marekani .natakiwa niende kuanza masomo katika chuo cha Howard university . Matokeo bado“
Kilipita kimya cha ghafla humo ndani.Wote wawili walizama katika lindi zito la mawazo.
“Patrick nisikilize.Najua ni kwa kiasi gani habari hii imekuumiza.Ulivyoumia wewe na ndivyo hivyo hivyo nilivyoumia mimi.Nimeumia sana Patrick.Na mpaka sasa kuna ugomvi mkubwa kati yangu na baba.Nimekataa kwenda Marekani.Siwezi kwenda na kukuacha hapa peke yako.I cant leave you alone Patrick.”
Patrick akageuza sura yake na kumwangalia Happy ambaye naye macho yake yalikuwa yamejaa machozi.Akatumia vidole vyake kumpangusa machozi kisha kwa sauti ya taratibu na upole akasema.
“Happy mpenzi wangu najua kuwa unanipenda sana .nafahamu pia kuwa unaelewa ni jinsi gani ninavyokupenda.Nafahamu haya yote yanayotokea hivi sasa ni majaribu tu ambayo iko siku yatapita na kutuacha sisi bado tunapendana.Nakuamini sana Happy na sina shaka yoyote juu yako kuhusu upendo wako kwangu.Sitaki Happpy ugombane au kushindwa kuelewana na wazazi wako kwa ajili yangu.Alichoamua mzazi ni kwa faida yako kwa siku za usoni. Nakushauri usigombane na wazazi wako kwa ajili yangu.Kubali kwenda kusoma Marekani.Mimi nipo na nitaendelea kuitumikia adhabu yangu hadi hapo nitakapomaliza.Natumai pindi ntakapomaliza adhabu yangu ,nawe utakuwa umemaliza au unakaribia kumaliza masomo yako na hivyo tutaungana tena na kuwa pamoja”
Patrick alitamka maneno haya ingawa moyoni alikuwa na uchungu mwingi.
Happy ambaye alikuwa amemshikilia Patrick akamwachia na kumtazama kwa mshangao
“Patrick are you out of your mind? Hivi kweli na wewe unakubali mimi niondoke na kukuacha hapa peke yako wakati uko hapa gerezani kwa sababu yangu???
Patrick akatabasamu na kumshika Happy mkono.
“Happy kama nilivyokwisha kueleza kuwa nakuamaini sana na wala sina wasi wasi wowote juu ya penzi lako kwangu.Uamuzi huo wa kwenda kusoma ni wa wazazi wako hivyo ni lazima tuuheshimu.Happy mimi ninafurahi kwa sababu unaenda kutengeneza msingi bora wa maisha yako kwa siku za usoni.Mimi nipo na siku zote nitakuombea na kukutakia mafanikio mema katika masomo yako.Ila naomba tu uniahidi kitu kimoja kuwa hutakuwa na mwanaume mwingine yeyote huko Marekani au kwingineko kokote zaidi yangu mimi.Niahidi kuwa utanisubiri mpaka nimalize adhabu yangu ili tuweze kutimiza ndoto zetu pamoja.”
Happy akatabasamu kisha akasema.
“Patrick nimekwisha kuahidi mara nyingi tu kuwa , chini ya jua sintakuwa na mwanaume mwingine yeyote ambaye si wewe.Wewe ni wa kwanza na wa pekee.Na kuahidi hivyo .Nashukuru sana kwa kuridhia mimi nikasome Marekani .Naenda huko ingawa moyo wangu hautaki kabisa.Najua utabaki mkiwa kwa kunikosa.Pamoja na kwamba nitakuwa mbali nawe kimwili lakini moyo wangu naucha hapa kwako ubaki nao.”
* * * *
Pamoja na umbali kati yao mawasiliano kati ya Happy na Patrick yaliendelea kuwa mazuri.Happy alikuwa akiandika barua kwa Patrick kupitia kwa mkuu wa gereza na Patrick hujibu na kumkabidhi mkuu wa gereza ambaye ndiye aliyejitolea kuhakikisha mawasiliano kati ya vijana hawa yanakuwa mazuri.Mkuu huyu wa gereza alisikia historia ya wawili hawa ikamgusa na kumfanya aahidi kuwasaidia kwa kila alivyoweza..
Chuoni Howard university Happy alikuwa ni miongoni mwa wanafunzi wachache kutoka bara la Afrika .Alikuwa ni binti mpole kupita wote chuoni hapo na kwa muda mfupi aliweza kujulikana sana kwa upole wake.Muda mwingi alipenda kuwa peke yake katika sehemu tulivu.Hakupenda kujiunga na makundi ya wenzake na wala hakushiriki katika burudani yoyote ile.Mawazo yote yalikuwa Tanzania gerezani alikomwacha Patrick akitumikia kifungo chake.
Hali hii ilivuta udadisi mkubwa miongoni mwa wanafunzi wenzake.Wapo waliodhani labda ni hali ya ugeni,wengine wakadhanii labda ni uoga na wengine wakadiriki kumwita mshamba.
Siku moja profesa Adelin shawlight ambaye ndiye anayehusika na maendeleo na mienendo ya wanafunzi akamwita Michelle ,msichana anayeishi na Happy chumba kimoja na kumuhoji juu ya tabia za Happy
“Hata mimi nimekuwa nikijiuliza sana juu ya hali ya mwenzangu huyu.Toka tumefahamiana hatujawahi kuzungumza mambo yoyote zaidi ya salamu.Tunaishi chumba kimoja lakini mpaka leo hii sijui ametokea nchi gani.Akiwa chumbani huwa mkimya sana na kama mara tatu hivi nimemkuta akiangalia picha Fulani huku akilia.Mi naona kuna jambo ambalo linamsumbua akili yake na pengine anahitaji msaada wa kisaikolojia zaidi “ akasema Michelle
Profesa Adellin akakubaliana na Michele kuwa ni lazima kuna tatizo linalomsibu Happy na wakaweka nia ya kumsaidia ili aweze kuwa ni mtu mwenye furaha kama wenzake.
Siku moja jumapili Michelle akatembelewa na kaka yake aitwaye Mike cambell anayefanya kazi katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani.Mike na Michelle ni watoto pekee kwa wazazi wao waishio katika jimbo la California.Michelle alimchukua Mike na kwenda naye hadi chumbani kwao wanakoishi yeye na Happy .Baada tu ya kuingia chumbani humo Mike akapigwa na butwaa baada ya kukutanisha macho na Happy ambaye alikuwa amekaa kitandani akiwa na kompyuta yake ndogo.
“Wow ! how beautiful the gal is.Looks like a black angel…….”Mike akawaza.
“Hi “ Mike akamsalimu Happy .
“Hi “ Happy akajibu na kuendelea na shughuli zake.
Michele akafungua vinywaji toka katika friji lililokuwapo humo chumbani akampatia Mike Happy lakini akakataa.
Mike alikuwa akisumbuliwa na kitu moyoni mwake.Uzuri wa Happy ulikuwa umemstua sana.
Baada ya kuongea na dada yake akaomba aondoke .
“Bye baby” Mike Akamuaga Happy
“Bye” Happy akajibu bila hata kugeuza shingo yake
“Michelle hebu niambie yule mwenzio ametokea nchi gani?Akauliza Mike wakati wakishuka ngazi
“Mimi sijui .tangu tumekutana hatujawahi ongea lolote zaidi ya salamu.Ulivyomuona ndivyo alivyo vile vile.Haongei na mtu na wala hataki urafiki na mtu yeyote.Ni mkimya mno.Lakini nahisi kuna kitu kinachomsumbua”
“Michelle unakosea.” Akasema Mike
“Ki vipi Mike.”
“Wewe ndiye unayetakiwa kuwa karibu naye zaidi kwa sababu mnalala pamoja na hata kama tatizo likimtokea wewe ndiye utakayeweza kumsaidia.Wewe unatakiwa uwe mwenyeji wake hapa marekani.Pengine ni ugeni unaweza kuwa unamsumbua” akasema Mike
“Si ugeni Mike,nahisi kuna kitu anakificha.Kuna jambo linamsumbua” akasema Michelle
“sasa sikiliza Michelle,Jitahidi kwa jinsi yoyote ile kuwa naye karibu sana.Jitahidi uweze kumzoea na hapo ndipo utakapoweza kumsaidia.Nasikitika sana kumuona binti mrembo kama yule akiwa katika ukiwa wa namna ile”
“Mbona unaongea kwa msisistizo Mike ?
“Anavutia yule binti ,ningependa kumfahamu zaidi “ akajibu Mike.Michelle akatabasamuna kusema
“kama ndio hivyo basi hakuna shida nitajitahidi sana niwe naye karibu.ili hata kama unamuhitaji basi iwe rahisi.Hata hivyo ni binti mrembo hata mimi ananivutia sana kwa urembo wake.”
“Nitafurahi sana Michelle kama utafanikiwa kuwa karibu na binti yule.Utakuwa umenifanyia kitu kikubwa sana katika maisha yangu.”Mike akasisitiza.
“Usihofu Mike nitajitahidi kwa kila namna niwezavyo ili kuwa karibu naye “
Waliagana kisha Michelle akarudi chumbani kwao akiwa ni mwingi wa mawazo jinsi gani atakavyoanza kumzoea Happy msichana ambaye hakutaka mazoea na mtu yeyote yule.
Michelle akaingia chumbani akajimiminia kinywaji katika glasi na kuanza kunywa huku akimtazama Happy kwa makini sana.CHANZO: https://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Excuse me my dear sister” Michelle akajikaza na kumsemesha Happy ambaye bado alikuwa anafanya kazi na kumpyuta yake ndogo
“Yes ,what’s up “ Akasema Happy bila kumuangalia Michelle.
“Sister unajua tangu tumepangwa kuishi wote katika chumba hiki hatujawahi kuongea hata siku moja,hatujawahi hata kufahamiana.Binafsi sipendezwi na staili hii ya maisha tunayoishi.Tuko katka chumba kimoja yatupasa tuishi kama ndugu,tupendane na kusaidiana.Mimi naitwa Michelle camble natokea California.” Akaanzisha mazungumzo Michelle.Happy akaacha kufanya kazi katika kompyuta yake akamuangalia Michelle kwa muda kisha akasema
“Naitwa Happy ..Happy Kibaho ,natokea Tanzania”
“Uuugh ! nafurahi sana kusikia unatoka Tanzania.I love Tanzanians.Nasikia ni watu wapole na wakarimu sana.Mama yangu amewahi kwenda Tanzania kupanda mlima Kilimanjaro na aliporudi akatuhadithia kuwa hajawahi kukutana na watu wakarimu kama watanzania.”
Happy akatabasamu .Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Michelle kumuona happy akitabasamu.
“Happy you are so pretty.Unajua sikuwahi kukuangalia vizuri.You are amazing” Michelle akajibu na kumfanya Happy afurahi.
“Jina lako zuri sawa kabisa na sura yako..ukitabasamu unakuwa mzuri zaidi ya malaika..” akasema Michelle na kumfanya Happy acheke kwa nguvu.
Huo ukawa ni mwanzo wa urafiki mkubwa kati ya Happy na Michelle.
ITAENDELEA
.jpeg)