Simulizi: Miss Tanzania Sehemu ya 06

ADMIN
0

 


“Nakusukuru sana Margreth nimekuelewa vizuri”Mike akasema huku akitabasamu.


“Happy amekwambia anakwenda wapi? Mike akauliza


“hapana hajanieleza ni wapi anaelekea.Karibu ndani upumzike wakati ukimsubiri”


“Nashukuru sana margreth lakini kwa kuwa sina uhakika kwamba atarudi saa ngapi mimi naona itakuwa vyema kama nikiondoka nitaonana naye kesho” Mike akasema na kuingia katika gari lake akaondoka.


“Nilimuonya Happy kuhusiana na mpango wake wa kuachana na Mike.Inavyoonekana hajamweleza kitu chochote Mike na hivyo kuzidi kumfanya awe na mawazo mengi sana.Happy Anasema Patrick amepatwa na matatizo,ni matatizo gani hayo? Nahisi yanaweza yakawa yanahusiana na huu mpango wao wa kuachana na wapenzi wao wa sasa ili waweze kurudiana.Namuonea huruma sana dada yangu ,yuko katika wakati mgumu.” Akawaza Margreth akitembea taratibu kuingia ndani.


* * * *


“Nimeamua kuachana na Vero na kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa yetu”


Ni maneno ambayo yalikuwa yakijirudia kichwani kwa Veronika ambaye alikuwa akiendesha gari la mama yake hukua akilia.Baada tu ya mama yake kuanguka na kuzirai kutokana na maneno aliyoyatamka Patrick kwamba hakutakuwa na harusi tena,Veronika akainuka kwa kasi kitini akamwendea mama yake pale alipokuwa ameanguka na kwa haraka akaunyakua ufunguo ambao ulikuwa umeanguka pembeni baada ya mama yake kuanguka akaingia katika gari la mama yake na kuondoka kwa kasi kurudi nyumbani kwao.


Machozi yalikuwa yakimtiririka na kulilowanisha shati lake kama vile amemwagiwa maji.Kuna wakati ilimbidi asimamishe gari pembeni ya bara bara akainamia usukani akalia na kisha akaendelea na safari.


“Siamini kama jambo hili ni kweli au niko ndotoni.Patrick huyu huyu ninayempenda kupita kitu chochote katika dunia hii ndiye huyu leo amenifanyia jambo kama hili !! Hapana si kweli.Hii si kweli” Happy akaupiga usukani kwa mikono yake miwili


“That’s not Patrick.Kile ni kivuli chake tu.Patrick ninayemfahamu hawezi kamwe kutamka maneno kama yale.Patrick ananipenda na katu hawezi kufanya vile alivyofanya” Vero akauma meno kwa hasira.Bado machozi yaliendelea kumchuruzika


“My God ! show me that this isn’t true,Im just dreaming, because if its true I don’t know whats going to happen….” Vero akaomba kimya kimya huku akifuta machozi


Alipofika nyumbani kwao akashuka garini na kukimbia kwa kasi kuelekea chumbani kwake akajitupa kitandani na kuanza kulia kwa nguvu huku akitupa mashka na mito chni kwa hasira


“Ouh Patrick! Patrcik!! Kwa nini lakini umenifanya hivi? Kwa nini ?? Sikutegemea katu kama siku moja ungeweza kunifanyia kitendo cha kikatili kama hiki.Sioni tena thamani ya maisha yangu bila wewe.Patrick umeniua…Umeniua Patrick…” Vero akalia kwa uchungu mkubwa.


Sura ya Patrick amesimama akiongea ikamjia tena na kumfanya ainuke na kuzidi kulia.


“Its true…Its not a dream….”


“Kwa sasa nimepata picha kamili .Kumbe siku zote hizi Patrick amekuwa akiteseka kumbe amemuona Happy !! Why this time Happy? Kwa nini umetokea wakati huu na kuja kuyaharibu maisha yangu? Patrick ndiye maisha yangu,ndiye pumzi yangu,ndiye kila kitu kwangu.Kwa nini umekuja wakati huu ? Bastard ! “ Vero akaendelea kulia


“Ninamfahamu Patrick lazima atakuwa amerogwa na mchawi hapa ni huyu huyu Happy ambaye amesababisha Patrick ashindwe kumsahau hata bada ya miaka hii yote kupita.He still loves her…he loves her….” Vero akaendelea kulia


“Nimeumia sana.Umeniumiza sana Patrick na huyo Malaya wako Happy.Kwa sasa kuna kitu kimoja tu ninachotakiwa kukifanya.Only one thing” Vero akasema kwa hasira huku akiigonga meza kwa mkono wake wa kulia.Kwa kasi akatoka mle chumbani na kuelekea katika chumba cha mama yake.Akalifungua kabati kubwa la nguo na kuvuta droo ndogo akachomoa kiboksi kidogo na kukiweka kitandani.Akakiangalia na kukifungua.Ndani yake kulikuwa na bastora nyeusi.


CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


Akiwa na mpira wa maji mkononi Andrew alikuwa nyumbani kwake akiosha gari lake ,mara simu yake ikaita.Akauweka chini mpira ule wa maji na kuifuta mikono yake halafu akaichukua simu .Mpigaji alikuwa ni Patrick


“Hello Patrick” akasema Andrew


“Andrew uko wapi ? Akauliza Patrick kwa sauti ambayo kidogo ikamfanya Andrew astuke.


“Niko nyumbani ninaosha gari .Patrick.you sound so strange.” akasema Andrew.


Patrick akavuta pumzi ndefu na kusema


“Andrew kuna matatizo yametokea”


“Matatizo ? Andrew akauliza


“Ndiyo Andrew.Niko hapa hospitali kuu ya moyo.Mzee amepatwa na shinikizo la damu kwa hiyo tumemleta hapa hospitali”


“Ok nakuja hapo sasa hivi”


Andrew akasema na kukata simu akabaki amesimama mahala pale kwa muda wa kama dakika mbili akiwaza


“kazi imeanza.Nilijua toka mwanzo lazima mambo kama haya yatajitokeza tu pindi Patrick atakapotangaza kusitisha ndoa yake na Vero.Nina amini kabisa kwamba shinikizo la damu alilolipata mzee wake linatokana na jambo hili.Pamoja na kwamba Patrick ni rafiki yangu mkubwa lakini jambo alilokuwa amekusudia kulifanya mimi siliafiki kabisa na nilimweleza ukweli kwamba anavyofikiria kufanya si sawa lakini akakataa kunielewa.Nilikwisha ona mbali kuhusu mambo yatakayokwenda kutokea Ngoja niende huko hospitali nikajue kinachoendelea lakini tayari Patrick amekwisha tuingiza katika matatizo makubwa”


Andrew akaingia ndani kwa haraka ili avae nguo na kuelekea hospiotali kuu ya magonjwa ya moyo ambako ndiko baba yake Patrick alikuwa amepelekwa.Wakati akiwa chumbani kwake akijiandaa simu yake ikaita.Akaichukua na kutazama mpigaji.Alikuwa ni Vero.Akasita kuipokea


“Ninayo kazi kubwa siku ya leo.Sijui Vero anataka kunieleza kitu gani” akawaza Andrew na kisha akabonyeza kitufe cha kupokelea simu


“Hallo Vero habari yako? Akasema Andrew


“habari mbaya Andrew” akasema Vero


“habari mbaya ? unaumwa?


“Ina maana hujui kilichotokea? Vero akauliza kwa ukali


“kwani kumetokea nini Vero? Mimi sielewi chochote” akasema Andrew.


“Andrew usinifanye mimi mtoto mdogo ambaye mnaweza mkanichezea akili wewe na rafikiyo.Wewe na Patrick lenu moja na unafahamu kabisa nini ambacho kimekuwa kikiendelea kwa sababu wewe ndiye mshenga wake.Nimekupigia simu kukueleza kwamba ninashukuru kwa mambo mliyonifanyia.Sikutegemea kama iko siku mngeamua kunifanyia mambo kama haya”


“Vero unaposema hivyo unakuwa unanichanganya.Mimi sielewi jambo lolote lile.Naomba tafadhali unieleze nini kimetokea kwa sababu Patrick naye amenipigia simu muda si mrefu na akaniambia kwamba yuko hospitali kuu ya moyo lakini hajanieleza kimetokea nini.” Akasema Andrew


“ Andrew kama unaelekea hospitali,basi tutakutana huko huko.hata mimi naelekea huko sasa hivi” akasema Vero na kukata simu


Andrew akabaki ameishikilia simu ile akiwa na mawazo mengi .


“Kumekucha.Mambo yameanza kupamba moto.Patrick ameniingiza katika matatizo makubwa.Kwa sauti aliyokuwa akiongea Vero inaonekana huko hospitali anakoenda anakwenda kwa shari.Itanilazimu kuwahi ili kuepusha shari inayoweza kutokea.Nilimuonya Patrick toka mapema kwamba suala lile lingeweza kusababisha matatizo makubwa lakini hakutaka kunisikia na haya ndiyo matokeo yake.Mambo yameshaharibika na sijui nini kitatokea huko mbele.Ngoja niwahi hospitali” akawaza Andrew huku jasho likimtoka kwa wingi.Haraka haraka akatoka na kuingia katika gari lake na kueleka hospitali.


****************************


“Huyu shetani Happy ni kwa nini ameibuka katika wakati huu ? Laiti ningelijua mapema kama yangekuja kunitokea mambo kama haya ningelihakikisha ninammaliza Happy angali bado mapema.Nilifanya kosa kubwa sana kumuacha hai wakati ule.Sikutegemea kama baada ya miaka mingi kupita mpaka leo Patrick bado moyo wake uko kwa Happy.This devil must have done something to him because I know Patrick loves me with his life so why he changed all over sudden?? Lakini ni kwa nini Patrick anitende hivi? Alitakiwa anieleze na tulijadili suala hili kabla ya kufikia maamuzi aliyoyafikia .Kama bado anampenda Happy mimi nisingemzuia na kwa namna ninavyompenda ningekubali hata kuwa mke mwenza ili mradi niwe katika ndoa na mtu ninayempenda kuliko watu wote hapa duniani.You’ve killed me Patrick..you’ve killed me…” Akawaza Vero akiwa katika gari kuelekea katika hospitali ya moyo ambako baba yake Patrick alikuwa amelazwa.Michirizi ya machozi ilionekana mashavuni mwake.


“Patrick nimetoka naye mbali sana.Ni mimi ndiye niliyemtoa ukiwa aliokuwa nao gerezani na kumrejeshea tena furaha aliyokuwa ameipoteza.Nimefanya kila nililoweza kumfanya asahau maisha yake ya nyuma na kumrejesha tena katika maisha yenye furaha tele.Toka siku ya kwanza niliyomuona Patrick pale gerezani nilimpenda na kuamini kwamba ndiye furaha ya moyo wangu na hii ndiyo sababu iliyonifanya nitunge uongo ule ili niweze kuwa naye.Ninampenda Patrick toka moyoni na yeye analifahamu hilo.Haikuwa kazi rahisi kuweza kuufanya moyo wa Patrick ukubali kupenda tena.Ilikuwa ni kazi ngumu lakini nilifanikiwa na Patrick akazama katika mapenzi na mimi.Baada ya kazi hii ngumu niliyoifanya kwa miaka mingi ambayo bado muda kidogo tu matunda yake yaonekane kwa mimi kufunga ndoa na yeye,lakini anatokea huyu shetani Happy… a stupid girl from nowhere and try to undo all that I’ve done for Patrick.I cant let that happen…I swear I cant let that happen..!! Vero akasema kwa hasira huku akipiga ukukani kwa nguvu kwa mikono yake na ghafla gari ikaserereka na mara sauti za matairi yaliyojiburuza katika barabara kutokana na breki za ghafla zikasikika .Vero akawahi kukanyaga breki.Huku moyo ukimuenda mbio akauninamia usukani wa gari na kuanza kulia kwa kwikwi.


“Binti una matatizo gani? Akauliza mzee mmoja aliyekuwa amesimama dirishani.


“Siku nyingine kama una matatizo yanayokusumbua tafadhali naomba usiendeshe gari.Umetaka kusababisha ajali mbaya sana “ akasema kwa ukali mzee yule huku akirejea katika gari lake.Vero aliendelea kuuinamia usukani wa gari lake akiendelea kulia.


“ Ni bora hata kama ningekufa katika ajali kuliko kuishi bila ya Patrick.Mateso haya sintaweza kuyavumilia kamwe..” akawaza na mara mlango wa gari lake ukagongwa kwa nguvu.Akainua kichwa kwa hasira na kutazama ni nani aliyekuwa akigonga mlango


“mwanangu una matatizo gani? Eneo hili si zuri kwa kuegesha gari.Eneo hili lina vibaka wengi sana na wamekwisha anza kukuzungukia.tafadhali ondoka eneo hili na ukaegeshe sehemu nyingine yenye usalama mkubwa.” Alisema mama mmoja mnene .


“Nashukuru mama” akajibu kwa ufupi Vero na kuliwasha gari na kisha akaingia barabarani na kuondoka eneo lile.


***********************


“Lolote litakalotokea na litokee tu lakini sintabadili msimamo wangu.Nimekwisha fanya maamuzi na hakuna mtu yeyote ambaye atanifanya nibadili maamuzi yangu.Niko tayari kwa lolote lile ili mradi niweze kuwa na Happy.Nilifungwa gerezani kwa ajili yake na kwa maana hiyo siogopi lolote lile litakalotokea.Ninajua ni mambo mengi sana yanakwenda kutokea ikiwamo kutengwa na familia lakini sintajali .Happy ni mwanamke pekee ambaye nimempenda na ambaye ninataka kuwa naye katika siku zote za maisha yangu yaliyobaki hapa duniani.Ni Mungu pekee ambaye ana uwezo wa kunizuia nisiweze kuwa na Happy katika maisha yangu.” Patrick alikuwa akiwaza huku akitembea tembea nje ya chumba cha wagonjwa mahututi ambamo baba yake alikuwa amelazwa akipatiwa huduma..


“Nafahamu kwamba hakuna mtu yeyote atakayenielewa ni kwa nini nimefanya hivi kwa sababu hakuna anayefahamu nini maana ya penzi la kweli japokuwa nilijaribu kuwapa historia ya maisha yangu na bni kwa nini Happy ni mtu muhimu sana katioka maisha yangu .Wote wananihukumu mimi na kuniona ni mtu mkatili sana kwa kitendo nilichokifanya.hakuna hata mtu mmoja wa kukaa upande wangu.Hakuna hata mtu mmoja ambaye anaonekana kunielewa ni kwa nini nimeamua kufanya maamuzi haya…Pamoja na hayo …….” Ghafla akiwa katikati ya mawazo mengi mara akasikia sauti ikimuita nyuma yake .kwa haraka akageuka kumtazama mtu aliyemuita.Alikuwa ni Happy.


“ Happy !! akasema Patrick na mara Happy akamkumbatia kwa nguvu.


“Ouh Patrick…”akasema Happy huku amemkubatia Patrick .


Watu wote waliokuwepo pale wakageuza vichwa vyao na kuwaangalia na kuanza kusemezana wao kwa wao.Patrick aliliona hilo akamshika mkono Happy na kisha wakapanda katika ghorofa ya juu


“nini kimetokea? Akauliza Happy wakiwa katika ghorofa ya juu.


“Tell me my love what happened” akauliza tena Happy kwa wasi wasi


“baba amepatwa na shinikizo la damu ghafla ikatulazimu kumkikmbiza hapa hospitali.” Akasema Patrick


“Hali yake inaendelea vipi?


“Mpaka sasa bado hali yake si nzuri .Yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi madkatari wanajaribu kumpatia huduma .”


“Ouh my love…Pole sana Patrick” akasema Happy akiwa na sura yenye huzuni.


“Ahsante Happy.” Akajibu Patrick na kutazama chini


“ Tell me Patick…nini kimesababisha hali hii kutokea? Akauliza Happy kwa wasi wasi.Patrick akageuka na kutazama chini katika mlango wa kuingilia chumba alimokuwa amelazwa baba yake idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka.


“Tulikuwa katika kikao kile nilichokwambia kwamba kinafanyika leo.Nimewaeleza ukweli bila kuficha hata neno moja na mwisho nikatangaza kwamba mimi na Vero basi na nimesitisha kila kitu kuhusu mipangilio ya harusi.Hapo ndipo kizaa zaa kilipoibuka.Watu wamezimia na wengine kuangua vilio kama vile kuna msiba umetokea.Kitu cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja ambaye amejaribu kuwa upande wangu.Kila mmoja ananiona kama shetani kwa kitendo nilichoifanya…” akasema Patrick na kuinama chini.Happy akatoa kitambaa katika mkoba wake akavua miwani yake na kuyapangusa macho yake yaliyojaa machozi.


“Patrick..nasikitika sana kwa mambo haya yote kutokea.Sikutegemea kama mambo yangekuwa namna hii….” Akasema happy na kabla hajamaliza Patrick akasema


“Happy naomba tafadhali usijilaumu hata kidogo kwa yote yaliyotokea.kwa sasa tunapigna vita na katika vita lolote linaweza kutokea kwa maana hiyo hatuna budi kujiandaa kwa kila litakalotokea.Katika vita tunawapoteza makamanda hodari na shupavu lakini bado vita inaendelea kupiganwa hadi mwisho.Huu ni mwanzo tu na hatupaswi kukata tamaa.Mimi sikati tamaa na sijutii hata kidogo maneno niliyoyasema leo kwani nimeeleza ukweli na kuuanika ubaya na ukatili wa Vero lakini hakuna hata mmoja ambaye anaonekana kunielewa.Hakuna hata moja anayeonekana kujali furaha ya maisha yangu.Kitu muhimu kwao ni kula na kunywa katika harusi na kisha baada ya hapo hakuna mwenye muda wa kufahamu kama maisha unayoishi yana furaha na amani.Mimi nayajali maisha yangu na ninafahamu ni kitu gani ninakitaka maishani.Ninahitaji furaha na furaha hiyo nitaipata ikiwa nitakuwa na wewe pekee katika maisha yangu.Kwa maana hiyo niko tayari kwa lolote lile litakalotokea” Patrick akamwambia Happy ambaye alikuwa ameinama machozi yakimchuruzika.


“Patrick nakupenda sana na nitakupenda mpaka siku naingia kaburini.hata baada ya kupata taaria kwamba umekufa sikuacha kukupenda.Nakubaliana nawe kwamba tunatakiwa tuwe jasiri na kusimama imara katika maamuzi yetu..Lakini mpenzi wangu nina wasi wasi kwamba maamuzi haya yatawaumiza watu wengi sana.So many people will get hurt ..kwa nini tusia……………….” Happy akataka kusema kitu lakini akakatishwa na sauti ya Andrew aliyetokeza ghafla


“Patrick….” Akasema Andrew


“Andrew !! karibu sana ..kutana na Happy..Happy kutana na Andrew my best friend” akafanya utambulisho mfupi Patrick.Andrew na Happy wakashikana mikono


“Nafurahi kukufahamu” akasema Andrew


“Vipi hali ya mzee inaendeleaje? Akauliza Andrew


“anaendelea kupatiwa huduma na madaktari ili kuhakikisha shinikizo linashuka na kuwa la kawaida.Tumuombee Mungu.Mbona unaonekana umeloa maji namna hiyo?


“Nilikuwa naosha gari uliponipigia simu.Niliogopa sana ikanibidi kuondoka kwa kasi ili kuwahi hapa hospitali.Vipi hali ya nyumbani ikoje na mbona mmejitenga huku peke yenu?


“Nimeamua kukaa huku kwa sababu kila mtu ananiona mimi kama shetani .Ninaonekana kama mtu mbaya sana ,binadamu nisiye na roho.Kuhusu nyumbani sifahamu hali ikoje kwa muda huu kwa sababu wakati ninaondoka kuja hapa hospitali hali ilikuwa ni ya vilio na watu walikuwa wameanguka wamezirai.Sijapata taarifa nini kinaendelea hko nyumbani na sina haja ya kufahamu.” Akasema Patrick.


“Ok Patrick ngoja nijaribu kufuatilia hali ya nyumbani ikoje.Kuna watu nimewaona wamekuja muda huu ngoja nikajaribu kuwauliza hali ikoje huko nyumbani ili tujue nini cha kufanya.I’ll be back” akasema Andrew na kushuka ngazi kwa haraka.CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


“Happy wakati huu ni mgumu sana kwetu na tunatakiwa tushikamane more than ever.Tafadhali naomba uwe jasiri na tusimamie maamuzi yetu.Mengi yatasemwa na hata kutokea lakini mwisho wa siku tutashinda na tutakuwa pamoja katika maisha.Tutaishi raha mustarehe” akasema Patrick akiwa amemshika happy mikono.


“Patrick mimi niko tayari kwa lolote lile na sintaweza kurudi nyuma katika maamuzi yetu.Pamoja na hayo Patrick ndugu ,jamaa na rafiki zako watanichukuliaje mimi? Wataniona kama Malaya ,muhuni niliyeuvunja uchumba wa watu,Sidhani kama nitakubalika katika familia yako” Happy akasema kwa wasi wasi.Patrick akamvuta kwake na kumkumbatia.


“Nisikilize Happy.Wewe ndiye mboni ya jicho langu.wewe ndiye pumzi yangu.Yeyote atakayekupenda nitampenda kwa sababu atakuwa ameipenda mboni yangu ya jicho amayo ni kitu muhimu sana .yeyote atakayekuchukia nitamchukia pia.Niko tayari kutengwa na familia,ndugu jamaa na marafiki kwa sababu yako.You are my family,you are my friend,you are my every thing.Siku moja dunia nzima itaufahamu ukweli na wale wanaofahamu nini maana ya penzi la kweli watauona ubaya na ukatili aliotufanyia Vero na watasimama upande wetu wakituunga mkono lakini wale waliokuwa wamejiandaa kwa kula na kunywa katika sherehe watabaki wakisema na kutoa kila aina ya laana hadi siku wanaingia kaburini.Nakuomba tafadhali usiwaze lolote kuhusiana na suala hili..one more thing that you have to know is hata kama dunia nzima itakutenga I’ll be the only person standing by your side.I’ll always be there for you my angel till my last breath…..” Patrick akamwambia Happy maneno yale ambayo yalimuongezea faraja na matumaini.


“Patrick !! “ Ilikuwa ni sauti kali ya Andrew iliyowastua Patrick na Happy waliokuwa wamekumbatiana wakipeana faraja.Patrick akainua kichwa na ghafla akakutananna kitu ambacho hakukitarajia.


“Vero !! Patrick akasema kwa mshangao…


Vero alikuwa amesimama mita kadhaa toka mahala alipokuwa amesimama Patrick na Happy na mkononi alikuwa ameshika bastora.Nyuma yake alikuwepo Andrew ambaye alionekana kama vile alikuwa akitetemeka kwa woga.


“Vero tafadhali punguza hasira na tukae chini tuongee mambo haya ili tuyaweke vizuri.Kila kitu kinawezekana iwapo tutakaa a kuzungumza” akasema Andrew aliyekuwa amesimama mita kadhaa nyuma ya Vero


“Shut up Andrew…usinieleze upumbavu wako wowote la sivyo nitaanza na wewe” akasema Vero kwa ukali


“Vero please acha utani na silaha za moto” akasema taratibu Patrick akimsihi Vero


“Nakufahamu vizuri Vero ,wewe si muuaji and you are not going to shoot me.tafadhali weka bastora chini” akaendelea kusisitiza Patrick


“You know me ? You don’t know the second side of me..and today I’m going to show you my second side..How I look like …” akasema Vero kwa hasira huku midomo ikimtetemeka


“vero tafadhali acha utani na silaha za moto”akasema Patrick


“Utani ! Patrick uaniona kama ninafanya utani ? Unaniona kama ninakutania Patrick ? Akasema Vero kwa ukali na mara akaielekeza bastora kwa Happy na mlipuko mkubwa ukasikika.Happy akaanguka chini.




Eneo lote la hospitali likawa kimya baada ya kusikika mlio ule wa risasi iliyotoka katika bastora aliyokuwa ameishika Veronika.Baada ya dakika kama mbili hivi za ukimya na taharuki iliyowapata watu kutokana na mstuko wa mlio wa risasi ,watu wakaanza kuulizana juu ya kilichotokea.Taratibu Patick akainua kichwa na kumtazama Veronika ambaye alikuwa amesimama machozi yakimtoka akiwa anatetemeka kwa hasira na bastora yake ikiwa inafuka moshi.Akageuza shingo yake na kumuona Happy akiwa amelala chini na kwa kasi akainuka na kumuendea


“Happy….Happy my dear ….amka…amka Happy my love..” Patrick akasema huku akimgeuza Happy.Happy akafumbua macho.Hakuwa amepigwa risasi kama wote walivyokuwa wamedhani.Veronika alipiga risasi nguzo ambayo Happy alikuwa amesimama .


“Ouh Happy my love..you are ok…thanx God..I love you” akasema Patrick huku akimkumbatia na kumbusu Happy baada ya kuhakikisha kwamba yuko salama.Happy machozi yalikuwa yakimtoka..Hakuamini kama alinusurika kifo .


Andrew ambaye alikuwa amesimama mita kadhaa nyuma ya Veronika akapiga hatua na kutaka kumuendea Patrick na Happy pale chini walipokuwa wamekaa wamekumbatiana.


“Stay where you are Andrew..or I will shoot you..” Akasema kwa ukali Veronika na Andrew akapiga hatua kurudi nyuma.


Eneo lote la hospitali likawa katika taharuki baada ya kusikika kwamba kuna mtu ana bastora na anataka kufanya mauaji. Watu waliokuwa maeneo yale ya hospitali wakaanza kukimbia kuelekea juu ya ghorofa ambako Veronika na akina Patrick walikuwepo.


Taratibu Patrick akainuka mahala pale alipokuwa na kumtazama Vero kwa macho makali sana.


“ Vero tafadhali naomba uweke silaha chini…tafadhali naomba uache mchezo na silaha za moto” akasema Patrick kwa ukali.


“Patrick umenifanyia kitu kibaya sana na sintaweza kuvumilia.After all these years..leo unakuja kuniacha namna hii? Sintaweza kuvumilia unitende namna hii Patrick..so today its me ,you na huyo Malaya wako..” akasema Veronika kwa ukali mdomo ukiwa unamtetemeka kwa hasira.


“Vero tafadhali naomba upunguze hasira..Hasira zako zinakupelekea ufanye kitendo ambacho utakijutia maishani mwako..tafadhali Vero punguza hasira na uiweke chini bastora yako then tutaongea..” akasema Patrick.


“Hakuna kitu cha kuongea mimi na wewe tena Patrick.Umekwisha weka wazi kwamba mimi na wewe tumefikia mwisho kwa hiyo hakuna kitu tunachoweza tukaongea tena.Its over Patrick..its over…Una roho ya kikatili Patrick..you are so cruel..sikutegemea kama mtu niliyempenda kwa moyo wote ,nikajitoa mwili na roho kwa ajili yako leo hii umenigeuka na kunitupa kama taka taka…I loved you Patrick ..I loved you sooo much..and I still do…lakini kitendo ulichokifanya leo kimenifanya nigeuke mnyama.Nimeumia sana.Umeniumiza kiasi ambacho sikutegemea..Maisha yangu yote niliyakabidhi kwako na sioni kama kuna sababu ya kuendelea kuishi hapa duniani bila ya kuwa na wewe.Wewe ulikuwa ni kila kitu kwangu lakini sasa nakuona kama ni kiumbe usiye na roho..so today its our end..me and you..” akasema Vero huku machozi yakimtoka.Ni wazi alikuwa ameumia sana moyoni.Machozi yalikuwa yakimtiririka.Patrick alikuwa akipiga hatua za taratibu kumkaribia Vero.


“Patrick..usijaribu kunikaribia..nitakupiga risasi kabla ya wakati niliopanga kukuua kufika ” akasema Vero kwa ukali na kumfanya Patrick asimame.




* * * *


Katika mlango wa kuingilia sehemu ile ya ghorofa waliyokuwapo akina Patrick Andrew alikuwa na kazi ngumu ya kuwazuia watu waliokuwa wakijaribu kutaka kushuhudia kilichokuwa kikiendelea na wengine walitaka kumkamata Vero ili asiweze kufanya jambo baya.


“Jamani hali iliyoko huku juu si nzuri hata kidogo..tafadhali msijaribu kutaka kuingia kwa kasi huku juu kwa sababu mtaifanya hali kuzidi kuwa mbaya.Kinachotakiwa kutumika hapa ni busara ya hali ya juu sana ili kumshawishi huyu mwanadadda aweke silaha chini.Lakini iwapo mtajaribu kutaka kutumia nguvu ya aina yoyote ile mtaifanya hali kuwa mbaya.Huyu dada mwenye silaha ana hasira sana na kutokana na jinsi alivyoumizwa moyo,yuko tayari kufanya jambo lolote lile kwa hiyo nawaomba ndugu zanguni msijaribu kutaka kuingia kwa kasi huku juu..tujaribu kuwa watulivu ili tuone nini tufanye kuepusha maafa yanayoweza kujitokeza.Ninamfahamu Patrick vizuri atamtuliza na kila kitu kitakuwa shwari..Naomba tuvute subira kidogo ndugu zangu .” akasisitiza Andrew akiwazuia baadhi ya ndugu na jamaa ambao walitaka kwenda kumzuia Vero asiweze kufanya jambo lolote baya.


“Unashauri tufanye nini? Kwa sababu tunavyozidi kuchelewa huyu mwanamke anaweza akasababisha maafa.” Akauliza mzee mmoja ambaye ni mmoja wa ndugu za Patrick na alikuwepo katika kikao kilichosababisha mambo haya yote kutokea.


“Ninachoweza kushauri kwa sasa hebu tusijaribu kuingilia mambo haya kwa sababu haya ni masuala ya kihisia zaidi na wanaogombana ni watu walioishi kama wapenzi kwa muda mrefu kwa hiyo kuna kila dalili kwamba wanaweza wakafikia muafaka na wakamaliza haya matatizo.Tusubiri tuone mwisho wake utakuwaje..” akasema Andrew na kuwafanya watu wale watulie


“Lakini kwa nini tusiwataarifu polisi kwamba kuna mtu mwenye silaha na anatishia usalama wa raia? Tutakuwa tunafanya jambo la kijinga kuendelea kukaa hapa na kumuangalia msichana huyu ana silaha na anatishia kuwaua wenzake.Tayari amekwisha piga risasi moja na hatujui ni kitu gani amedhamiria kukifanya.Tuwataarifuni polisi haraka kuhusiana na tukio hili ili waweze kufika haraka na kumdhibiti huyu msichana” akasema mmoja wa madaktari ambaye naye alikuwa amesimama pale mlangoni.


“Hapana daktari..naomba msifanye hivyo kwanza kwa sababu kuwaleta polisi mapema kunaweza kukampandisha hasira Vero ambaye anaweza akafanya jambo lolote baya.Tafadhali naomba msifanye hivyo kwanza hadi tutakapohakikisha kwamba hali inazidi kuwa mbaya .” akasisitiza Andrew.


* * * *


“Simama hapo hapo Patrick na usitembee hata hatua moja…ama la nitakupiga risasi Patrick..” akasema kwa ukali Vero baada ya Patrick kutaka kupuuza onyo alilompa awali la kutaka kumkaribia.


“Vero nakufahamu vizuri..huwezi kunipiga risasi…mambo yote haya umeyataka wewe mwenyewe.Ulifanya jambo baya sana ulipofanya ule udanganyifu mkubwa na kusema kwamba eti nimekufa.na eti Happy ameolewa na mzungu na kuniacha peke yangu gerezani.Huwezi kujua ni kwa kiasi gani niliumia kwa udanganyifu ule..Niliumia sana ..hakuna mtu anayeweza kufahamu kiwango gani niliumizwa..Vero wewe ni mkatili na mnyama mkubwa tofauti na muonekano wako.Hauna mapenzi na mimi hata kidogo na kama ungekuwa na mapenzi ya kweli na mimi usingethubutu kutunga uongo ule mkubwa na kusababisha mimi kupata uchungu mkubwa sana moyoni.You are selfish..you only care for yourself.Hukujali kama mimi na Happy tulikuwa na mapenzi mazito,ulitunga uongo mkubwa kututengenisha mimi na Happy wakati ukifahamu fika kwamba nilikuwa pale gerezani nikitumikia kifungo kwa sababu ya kumlinda Happy asidhalilishwe kwa sababu ni mwanamke pekee ninayeweza kufanya jambo lolote kwa ajili yake.Kwa roho yako mbaya ya kikatili na kinyma hukulijali hilo na ukawa tayari kusababisha maumivu makubwa kati yetu sisi ili kutimiza lengo lako.Ndiyo, ulitimiza lengo lako kwa kuwa na mimi kama ulivyokuwa ukihitaji lakini napenda kukueleza wazi kwamba pamoja na kuwa nawe lakini moyo wangu siku zote ulikuwa kwa Happy.Sikuacha hata mara moja kumpenda Happy..not for one second.kwa sababu ni yeye pekee niliyepangiwa niwe naye hapa duniani.Namshukuru Mungu kwa sababu amekuumbua ,uongo wako umejulikana na leo hii unayasikia machungu kama niliyoyasikia mimi siku ile uliponidanganya kwamba Happy amenikimbia na kuolewa na mzungu..Machungu kama aliyoyasikia Happy siku alipopata taarifa kwamba mwanaume aliyempenda kupita kitu chochote kile amefariki dunia..Kama kweli unafahamu kama ulitenda kosa kubwa kutunga uongo na kunitenganisha na Happy ,weka silaha chini na mambo haya yaishe kwa amani.Hata ufanye ufanyavyo mimi sitishiki Vero..hata ukitaka kuniua..niko tayari kwa hilo lakini utambue kwamba nitakufa nikilitamka jina la Happy mwanamke pekee ninayempenda katika dunia hii.Now if you want to shoot me..go ahead..shoot me now…” akasema Patrick huku akitembea taratibu kumuendea Vero pale alipokuwa amesimama.Bado mkono wa Vero uliokuwa na Bastora uliendelea kumuelekea Patrick


“Patrick tafadhali usinisogelee..don’t come near me !! akasema kwa ukali Vero.Patrick akampuuza na kuendelea kutembea taratibu kumuendea Vero.


“Patrick usimkaribie Vero tafadhali…!! Alipaaza sauti Andrew ambaye alikuwa ameiweka mikono yake kifuani kwake kwa uoga mkubwa baada ya kumshuhudia Patrick akitembea taratibu kumuendea Vero bila kuijali silaha aliyokuwa ameishika mkononi.


“My God Patrick !! Unataka kufanya nini? Akasema Andrew kwa sauti ndogo akiwa ni mwingi wa wasi wasi.


“Shoot me now..” akasema Patrick akiwa karibu kabisa na Vero..Vero alikuwa akitetemeka kwa hasira akamsogelea Patrick na kumuwekea bastora kichwani.


“I did all that because I love you…Nilifanya kila nililoweza kukusahaulisha huyu Malaya wako Happy lakini hukuweza kumsahau…You are good for nothing Patrick..you are idiot…you are stupid….you don’t deserve to live in this world….Kwa mambo uliyonifanyia nasema hivi leo nakuua wewe na Malaya wako..ni bora wote tukakosa.” Akasema Vero kwa hasira


“Vero tafadhali usifanye hivyo..tafadhali Vero naomba tukae tuyaongee masula haya ili yaishe bila madhara yoyote.” Akapaaza sauti Andrew lakini kabla hajamaliza kauli yake akakatishwa na sauti kali ya Vero aliyegeuka ghafla na kumuelekezea bastora .


“shut up you fool..!! ..kuwadi mkubwa wewe.. you’ll have to pay for th…….” Kabla hajamalizia sentensi yake Vero akastukia mkono wake uliokuwa na bastora umeshikwa kwa nguvu na Patrick.


“Patrick nakwambia niachie !! …” akapiga kelele Vero.Happy ambaye alikuwa amekaa ameinama akilia akastushwa na ukelele ule alioupiga Vero.Akageuza shingo na kuangalia kilichokuwa kinaendelea.Akastuka baada ya kuona Patrick na Vero wakigombania bastora iliyokuwa katika mkono wa Vero.


“Ouh My God !! akasema Happy kwa mstukoCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


“Mwanamke huyu anaweza akasababisha mauaji.Dhamira yake si nzuri hata kidogo..amekwisha nikosa kwa risasi..si wa kumuachia aendelee kuimiliki ile silaha.” Akawaza Happy huku akijiinua toka pale sakafuni.


Kukurukakara ikaendela kati ya Patrick na Vero na bila kutazamia Patrick ajikuta akizidiwa nguvu na Vero na kugandamizwa ukutani na kumuwekea bastora kichwani


“Nimesema leo lazima nikuue mwanaharamu wewe..” akasema Vero kwa hasira.


“You want to kill me? ..kill me now…!! Akasema kwa ukali Patrick


“Ouh No ! .Happy akasema kwa mstuko huku akiushika mdomo wake kwa uoga .


“Andrew do something !! …..” akapiga ukelele Happy akimuamuru Andrew ambaye alikuwa amesimama asijue la kufanya.


“Waiteni polisi haraka..hali ya hapa si nzuri hata kidogo” akapiga kelele Andrew baada ya kuona hali imebadilika na sura ya Vero ilionyesha kila dalili za mauaji.


Ghafla bila kutazamia Happy akavua viatu vyake virefu alivyokuwa amevaa na kukimbia kwa kasi na kwa nguvu zake zote akamsukuma Vero ambaye alijibamiza ukutani kwa kishindo kikubwa na kuanguka chini.Damu zikaanza kumtoka mdomoni na hakufurukuta tena.


“Are you ok Patrick “ akauliza Happy na kumkumbatia Patrick


“Thank you my angel..umeyaokoa maisha yangu.” Akasema Patrick na kukumbatiana na Happy.Mara Patrick akastuliwa na sauti ya Andrew aliyekuwa ameinama pale chini mahala alipolala Vero .


“Patrick !!…..”


Patrick akageuka na kukutanisha macho yake na macho yaliyojaa hasira na machozi ya rafikiye mkubwa Andrew aliyekuwa pembeni ya daktari aliyekuwa akimpima Vero.


“Patrick umefanya nini sasa ? kwa nini umemuua Vero ? Andrew akauliza na akashindwa kujizuia kuangusha machozi


“Unasemaje?? ..Vero amekufa ? akauliza Patrick kwa mstuko.. na wakati huo huo watumishi wa hospitali ile wakiwa na machela wakafika na kumchukua Vero na kuondoka naye kwa kasi .Happy akaishiwa nguvu akakaa chini akainama.


“Patrick nimeua…nimeua Patrick !! Happy akalia kwa sauti ndogo….


Patrick ambaye naye miguu ilikuwa ikimtetemeka akamuinamia Happy pale chini


“Shhhhhhh…Happy nyamaza kulia.Hujaua mtu yeyote.Vero bado hajafa..amezirai tu. Tusubiri taarifa ya daktari inasemaje.” Akasema Patrick na kumkumbatia Happy.Mara polisi waliokuwa wamejiandaa kwa ajili ya kumdhibiti mtu waliyetaarifiwa kwamba ana silaha silaha wakaingia kwa kasi .Happy alipowaona akazidi kulia.


" Patrick please dont leave me.I'm so scared" akasema Happy.Patrick ambaye naye alijawa na hofu kubwa akawatazama maaskari wale ambao walianza kuwatawanya watu wote waliokuwa kule ghorofani.


" Patrick nimeua...Nimeua Patrick.." akazidi kulia Happy.Patrick akamkumbatia na kukilaza kichwa cha Happy kifuani pake.




" Happy tafadhali usilie my love...tafadhali usilie mpenzi wangu" Patrick akambembeleza happy lakini bado aliendelea kulia.


" Patrick please dont leave me..dont leave me Patrick" Happy akasisitiza


" Happy my love I'm here..I'll never leave your side." akasema Patrick akimpiga piga Happy mgongoni.


Askari mmoja ambaye alikuwa na cheo cha mkaguzi aliyeonekana kama mkuu wa kikosi kile kilichofika pale kwa dhumuni la kutuliza fujo akawasogelea Patrick na Happy pale chini walipokuwa wamekaa.


" Ndugu zangu kuna usalama hapa? akauliza yule askari.


" Tuko salama afande" akajibu Patrick


" Hakuna mtu yeyote aliyedhurika? akauliza tena


" hakuna afande wote tuko salama." akajibu Patrick.


" Ndugu unaweza ukatueleza ni kitu gani kimetokea hapa ? akauliza yule askari


Patrick akajaribu kufungua mdomo wake ili aweze kuongea lakini akashindwa .Midomo ilikuwa ikimtetemeka.


" Jitahidi ndugu yangu utueleze ni nini chanzo cha vurugu hii iliyotokea hapa muda mfupi uliopita mpaka ikafikia hatua ya kutishiana silaha? akauliza tena yule mkaguzi wa polisi.


Patrick akajitahidi na kusema


" Afande nashindwa nikueleze vipi................." akasema Patrick kisha akamkumbatia Happy zaidi.


"Ni nani aliyewatishia wenzake kwa silaha? akauliza askari.


" Afande kilichotokea hapa kinahitaji maelezo marefu lakini nitajaribu kukueleza kwa ufupi.Ugomvi uliotokea hapa unanihusisha mimi na mpenzi wangu wa zamani aitwaye Veronika ambaye tumeachana muda si mrefu .Mpenzi wangu yule hakuridhika na kitendo cha kuachana naye hivyo akanitafuta mahala nilipo akagundua kwamba nimekuja hapa hospitali na yeye akaja na kwa bahati mbaya akanikuta niko na huyu hapa mpenzi wangu wa sasa " akasema Parick na kutulia baada ya kumuona askari yule akimtazama sana Happy.


" Huyu si yule msichana aliyeshinda taji la Miss Tanzania juzi juzi? akauliza yule askari


"Ndiye huyu "akajibu Patrick


" Huyu ni mpenzi wako? akauliza tena askari.


" Ndiyo ni mpenzi wangu." akajibu Patrick.


" Ouh My God sijui ni kwa nini wasichana wengi wanaposhinda taji hili hujikuta wakiingia katika migogoro hasa ya kimapenzi.Huyu amechaguliwa juzi tu lakini tayari amekwisha anza kutengeneza vichwa vya habari." akawaza askari yule.


" Kwa hiyo nini kilisababisha ugomvi kutokea?


" Kilichotokea ni kwamba mimi na huyu mpenzi wangu tukiwa huku juu ghrofani akatokea Vero akiwa na bastora mkononi na akaanza kututisha kwamba leo ama zetu ama zake.Baada ya majibizano ya maneo ya muda mfupi nikajaribu kumsihi apunguze hasira na tuweze kukaa tukayaongea masuala haya yakaisha.Badala ya kutuliza hasira vero akapandisha zadi na kuachia risasi iliyomkosa Happy.baada ya kitendo kile ikanilazimu kumsogelea karibu ili niweze kumzuia asiweze kuleta madhara." Patrick akanyamaza na kumtazama Happy ambaye bado aliendelea kufuta machozi.


" Nini kilifuata baada ya hapo? akauliza mkaguzi wa polisi


Happy akauinua uso wake na kumtazama Patrick.


"Nini kilitokea ? akauliza tena


" I must save her..This is the time I have to show her how important she is to me.I must prove my love now.I cant let anything happen to a woman I love..I cant let her suffer" akawaza Patrick kisha akasema


" Veronika alishindwa kunipiga risasi mkono wake ulikuwa ukitetemeka.Nikamsogelea karibu zaidi nikataka kumnyang'aya silaha na hapo ndipo vurugu ilipoibuka .Tukaanza kusukumana na ......." Kabla Patrick hajaendelea kumueleza mkaguzi wa polisi nini kilitokea mara akatokea daktari akamuita yule askari mkaguzi pembeni na kuanza kuongea naye.Katika maongezi yao alikuwa akimuelekezea kidole Happy ambaye alipoona daktari akimuelekezea yeye kidole akapatwa wasi wasi mwingi akaanza kulia.


" Patrick ninaogopa sana.Please dont leave me" akasema Happy huku akilia kwa uoga


Patrick akauweka mkono wake wa kulia kichwani kwa Happy na kumgeuza kichwa ili aseweze kuwaona daktari na yule askari.


" Usiogope Happy,hakuna jambo lolote baya lililotokea"


" Nina wasi wasi mwingi Patrick..itakuwaje kama ni kweli nitakuwa nimemua Vero? Akasema Happy kwa uoga.Patrick akamuwekea kidole mdomoni


" Shhhhhhhhhhhhhh.!!!!!!......


" Usiwaze kitu kama hicho Happy.Hujaua mtu and you'll never kill anyone.Whatever happened here my love you havent done anything..you understand me ? Patrick akamwambia Happy ambaye bado alikuwa akifuta machozi


" Umenielewa Mpenzi? akauliza Patrick baada ya kuona Happy hamjibu


"Do you understand me ? akauliza kwa mara nyingine kisha akaigeuza shingo ya Happy na kumuangalia usoni.


" What? akauliza Happy


" we have to do something ...first swear to me that you'll do as I tell you to do."


Huku akifuta machozi Happy akasema


" I swear ..."


" Good.." akasema Patrick kisha akayashika mabega ya Happy.


" What happened here you are not involved in anything..I am the one who did everything here"


" Patrick No ! Please dont do that...." akasema Happy


" Happy naomba unisikilize kwa makini sana.Nimeanza kuhisi kitu kibaya kinaweza kutokea kwa maana hiyo lazima nichukue hatua za kukulinda na kila kitu kwa sababu wewe ni mwanamke pekee ambaye niko tayari hata kuyatoa maisha yangu kwa ajili yake.Kwa maana hiyo mimi ndiye nitakayekuwa muongeaji mkubwa na hata kama ukiulizwa kana kila kitu na useme mimi ndiye niliyehusika na vurugu yote.Please do that for me Happy." Patrick akasema.Kabla Happy hajajibu kitu daktari na askari mkaguzi wakawasogelea Happy na Patrick.


" Kijana na mchumba wako kuanzia sasa inatulazimu kuwashikilia kwa mahojiano zaidi .Kwa mujibu wa maelezo ya daktari ambaye amekuwa shuhuda wa vurugu hizi toka mwanzo na hadi kilipotokea kifo cha Veronika." akasema askari mkaguzi na kuwafanyia ishara askari watatu waliokuwa wamesimama pembeni wafike pale haraka .Baada ya kauli ile ya askari happy nguvu zikamuisha akataka kuanguka chini Patrick akamdaka.


" be strong Happy..be strong my love" Akasema Patrick halafu akamgeukia daktari


" Daktari ni kweli vero amefariki dunia?


" Ndiyo..Baada ya kwenda kumpima tuligundua kwamba alikwisha fariki kitambo"akasema daktari.


Patrick akakishika kichwa kwa mikono yake miwili.


" Ouh My God,..why this is happening to me ?


" Daktari hebu nieleze nielewe mazingira ya kifo chake.." akasema tena Patrick


"Alisukumwa na kujigonga ukutani kwa nguvu na tunahisi ubongo wake ulitikisika na kusababisha kifo chake.Lakini tutapata majibu yenye uhakika baada ya mwili wa vero kufanyiwa uchunguzi wa kina katika hosptali ya Muhimbili"


Patrick akainama akifikiri.Alihisi kuchanganyikiwa.Mwili ulikuwa ukimtetemeka.Hakutegemea kama tukio lile lingeweza kujitokeza.


" Mungu wangu sikutegema kama mambo yangekuwa hivi..Kila kitu sasa kimeharibika.Nimepoteza kila kitu.Ouh My God Please help me.." akawaza Patrick halafu akainua uso wake akamuangalia yule askari mkaguzi.


"Afande naomba tafadhali mumuache huyu mchumba wangu aende zake.Yeye hahusiki na kitu chochote kilichotokea hapa.Mimi ndiye niliyemsukuma Vero akajigonga ukutani na hivyo kusababisha kifo chake.Nichukueni mimi na mumuache Happy aende zake" Patrick akamwambia yule askari mkaguzi.


" Kijana kwa taratibu za kipolisi ninyi nyote mtachukuliwa na kupelekwa kituoni na mtachukuliwa maelezo yenu na baadae kama ikionekana huyu mchumba wako hahusiki na suala hili basi ataachiwa huru.Kwa sasa nyote mtashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi"


" Afande ninafahamu hivyo lakini nakuomba tafadhali mumuache huru Happy.Nichukueni mimi ambaye ndiye muhusika wa tukio hili .Happy hajajihusisha na jambo lolote lile..." akasema Patrick na mara daktari aliyekuwa amesimama pembeni ya askari akasema kwa hasira


" Afande huyu kijana anakudanganya kwa sababu mimi nilikuwapo hapa wakati mambo yote yanatokea na nimemshuhudia kwa macho yangu huyu msichana akimsukuma mwenzake ambaye alijigonga ukutani na kufariki dunia." Patrick akapandwa na hasira akataka kumvamia daktari yule askari wakamzuia.


" Kijana tafadhali usijaribu kuleta vurugu .mfungeni pingu mpelekeni katika gari." akaamuru mkaguzi


" No ! Hamuwezi kumfunga pingu mpenzi wangu.Leave her alone" akasema kwa ukali Patrick.Happy aliyekuwa amekaa chini akitoa machozi akasimama akamuendea Patrick na kumshika usoni kwa mikono yake akamwambia


" Patrick usibishane nao.Please let me go with them."


" No ! Happy you cant go with them." akasema Patrick huku akiruka ruka .Tayari mikono yake ilikwisha fungwa pingu.Mkaguzi wa polisi akamfuata Happy.


" Samahani Binti..nafahamu mchumba wako hataki uongozane na sisi k wenda kituoni lakini kwa taratibu za kipolisi ni lazima tuwashikilie ninyi nyote ili tuweze kufanya uchunguzi na baada ya uchunguzi kukamilika basi tutamuachia huru ambaye ataonekana hahusiki na tukio hili.Nafahamu wewe ni mrembo wa Tanzania na ninakupa heshima yako.Sitaku ufungwe pingu ila nakuomba ukubali kuongozana nasi kuelekea kituoni.Uko tayari kuongozana nasi kwa amani? akauliza mkaguzi


" Niko tayari afande.Nitaongozana nanyi kwenda kituoni.." akasema Happy.


Sauti za vilio toka kwa akina mama waliokuwa wamekuja kufuatilia maendeleo ya baba yake Patrick zikaanza kusikika mara tu iliposikika taarifa kwamba Vero amefariki dunia.Ilikuwa vigumu kuamini kama ni kweli vero amefariki dunia. Patrick na Happy wakapakiwa katika gari la polisi .


" Dont worry my love..everything will be ok..we'll be ok" akasema Patrick akimpa moyo Happy aliyeonekana kukata tamaa.


" No matter what happens you have to say as I told you to say " akasema Patrick.Happy hakujibu kitu aliendelea kumwaga machozi.




Japokuwa alijitahidi kuonyesha ujasiri mkubwa kwa nje lakini kwa ndani Patrick alikuwa akitetemeka ..aliogopa sana kwa tukio lililotokea.Kwake aliona tukio lile ni kama ndoto.Hakuamini moja kwa moja kama ni kweli Vero amefariki dunia.


" Its hard to believe..vero amekufa ? ...No this cant happen..." akawaza


Picha ya vero akiwa ndani ya tabasamu pana sana ikamjia akilini.Akajikuta akiuma meno kwa uchungu.


" Ouh Vero.....!! " akawaza Patrick na kushindwa kuyazuia machozi kumtoka.


" She loved me... Alikuwa ni msichana mzuri sana ,mwenye kila sifa ya uzuri.Masikini Vero..why I did this for you?`..Patrick akasikia uchungu mkubwa moyoni.Kifo cha Vero kilimuumiza sana.


Picha ya yeye na vero wakiwa bafuni asubuhi ikamjia kichwani akazidi kuumia moyo.Akainama chini akafikiri kwa muda halafu akageuza shingo na kumuangalia Happy aliyekuwa ameinama akilia.


" masikini Happy..hakufanya vile kwa kupenda..hakukusudia kufanya vile.hakuna aliyetegemea lingetokea jambo kama hili.hakuna aliyetegemea Vero angefariki dunia.Happy ana wakati mgumu sana.Siwezi kukubali Happy akaingia gerezani.She's the woman I love and I'll do everything to protect her..." akawaza Patrick.


Kitanda cha magurudumu kikatolewa ndani ya chumba kikisukumwa na wauguzi wawili na nyuma yao walifuata wauguzi wengine wanne na madaktari wawili pamoja na askari polisi wanne.Wote walionekana na nyuso zilizojaa simanzi.Juu ya kitanda kile kilichokuwa kikisukumwa,kulikuwa na mwili wa mtu uliokuwa umefunikwa shuka jeupe.gari la kubebea wagonjwa la hospitali likasogea taratibu karibu na mlango ,wauguzi wakafungua milango yake ya nyuma halafu shuka lililokuwa limeufunika ule mwili likaondolewa na sura ya mtu aliyekuwa juu ya kile kitanda ikaonekana wazi.Ilikuwa ni sura ya msichana mrembo aliyekuwa amefumba macho kana kwamba amesinzia.Ulikuwa ni mwili wa Veronika.Alikuwa amelala usingizi wa milele na hatoweza kuamka tena.Alikuwa amefariki dunia.Taratibu wauguzi wakauingiza mwili ule katika gari tayari kwa kuupeleka katika hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi wa sababu ya kifo chake.


Wakiwa chini ya ulinzi mkali ,ndani ya gari la polisi ambalo halikuwa mbali sana na lile gari la wagonjwa ,Happy na Patrick waliushuhudia mwili wa Veronika ukipakiwa garini.Happy akashindwa kuvumilia akaanza kulia


" Ouh ! Patrick why I did that ?.....


Patrick akamvuta kwake akamkumbatia na kumziba mdomo wake kwa kiganja cha mkono.


" Shhhhhhhhhh......!!!!!!!!!." Patrick akamwambia Happy kwa sauti ndogo


" Stop crying Happy..you are going to be fine..trust me"


" It hurt me Patrick..It hurt so much ..I didnt mean to k.................." Kabla hajamaliza sentensi yake akastuka ghafla na kumtazama Patrick usoni kwa sekunde kadhaa kisha akamkumbatia Patrick kwa nguvu.


" Don't leave me Patrick..dont let me die" akasema Happy kwa sauti ndogo.Patrick akainama kidogo akambusu katika paji la uso na kumwambiaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


" Sintakuacha Happy..I will always be here for you" akasema Patrick na kumkumbatia zaidi Happy halafu akaigeuka shingo yake na kuwatazama wauguzi wakiifunga milango ya ile gari iliyoubeba mwili wa Veronika na taratibu gari lile likaanza kuondoka huku likisindikizwa na gari moja la polisi.Patrick akasikia uchungu mkubwa.Machozi yakamdondoka lakini akawahi kuyafuta ili Happy asigundue kama alikuwa akilia.


" Ouh Vero....masikini Vero..sikutegema kama yangetokea haya.Sikufikiria kabisa kama suala hili lingetufikisha hapa lilipofika na kupeleka mauti yako..Bado siamini kama umekufa Vero..Its so hard to believe.Ni asubuhi ya leo tulipokuwa tukiongea na kucheka kwa furaha lakini jioni hii eti umefariki.!! .Ouh Jamani Vero it hurt so much" akawaza Patrick.Michirizi ya machozi ikaonekana katika mashavu yake.


" Nasikia uchungu mkubwa mno kwa tukio hili.Nimemuweka Happy katika wakati mgumu sana ..Hakuwahi kutegemea kama angeua mtu katika maisha yake.Mimi ndiye niliyemsababishia dhambi hii kubwa.Najua moyoni mwake ameumia mno .I must save her..Yes I must save Happy.." akawaza Patrick.


Picha ya Veronika akiwa katika tabasamu ikaendelea kumjia kichwani na kumuumiza sana.


" Forgive me Vero...Nisamehe Veronika." akawaza Patrick akiwa amefumba macho yake na kuuma meno kwa uchungu.Picha ya Vero akiwa amesima ameshika bastora ikamjia tena kichwani.Akakumbuka uoga aliokuwa nao pale Vero alipoachia risasi moja iliyomkosa Happy. Akaukunja uso wake.


"Haya yote umeyataka wewe mwenyewe Vero..Nilikupenda sana lakini sikuwa nimefahamu ukatili uliotufanyia mimi na Happy.Ulitunga uongo na kututenganisha hali ukijua fika kwamba Happy ndiye mwanamke pekee ambaye moyo wangu unampenda kuliko wanawake wote.Ninaumia ninapokumbuka nyakati zile za furaha tulizokuwa nazo,tulipendana sana hadi kufikia mamuzi ya kufunga ndoa .Lakini Inaniuma zaidi kila nikifikiria mateso na maumivu uliyotusababishia mimi na Happy kwa uongo ulioutunga .Niliumia mno nikijua ni kweli Happy amenisaliti .Ni Mungu wangu pekee ndiye anayefahamu maumivu niliyoyapata wakati ule.Maumivu yale niliyoyapata yameendelea kwa miaka hata miaka hadi nilipokutana na Happy na tukaufahamu ukweli.Sifurahii kifo chako lakini ukweli utasimama pale pale kwamba wewe ndiye chanzo cha haya yote na hili ni fundisho kwa wengine kwamba alichokipanga Mungu siku zote binadamu hawezi kukipangua. Najua bado nina safari ndefu na ngumu katika mapenzi yangu na Happy lakini niko tayari kwa lolote lile litakalotokea kwa sababu Happy ndiye mwanamke pekee ambaye ninaamini amezaliwa kwa ajili yangu " Patrick akastuliwa kutoka katika mawazo baada ya watu wengine wanne kupandishwa ndani ya ile gari.Mmoja wa watu wale alikuwa ni Andrew.Patrick akaonyesha mshangao lakini Andrew akamsogelea karibu na kumnong'oneza sikioni.


" Tumechukuliwa kama mashuhuda wa tukio .Tunakwenda kutoa maelezo yetu jinsi tukio lilivyokuwa" akasema Andrew.Patrick akamfanyia ishara kwamba asogeze sikio lake karibu ili aweze kumweleza jambo.


" Andrew ulikuwepo eneo la tukio na kuona kila kilichotokea ,katika maelezo yako andika kwamba Happy hakuhusika na kitu chochote kilichotokea hapa na kusababisha kifo cha Vero.Tuhuma zote zielekeze kwangu kwamba mimi ndiye niliyesababisha kila kitu.Eleza kwamba mimi ndiye niliyemsukuma Vero akagongesha kichwa chake ukutani na kufariki dunia.Umenielewa? akauliza Patrick.Andrew hakumjibu kitu akabaki akimtazama kwa mshangao


" Patrick.............." Andrew akataka kusema jambo lakini Patrick akamzuia.


" Do as I say Andrew" Akasema Patrick kwa ukali na kuwafanya wale askari waliokuwa wakiwalinda kugeuka ghafla.Andrew akainamsha kichwa


" Sasa nimeamini Kweli Patrick anampenda Happy.Hata baada ya kitendo alichokifanya cha kusababisha kifo cha Vero bado Patrick anathubutu kusimama na kumtetea? Its hard to believe this is happening.....yaani Patrick anataka kujitwisha yeye mzigo huu wa mauaji?...This is insane.." akawaza Andrew huku akimuangalia Happy kwa macho makali .


" Msichana huyu ndiye chanzo cha haya matatizo yote yaliyotokea.Toka ameonana tena na Patrick nimekuwa nikihisi lazima kuna jambo baya linaweza likatokea na nikamuonya Patrick kwamba aachane na huyu mwanamke lakini hakutaka kunisikia.Tayari yeye na Vero walikwisha kuwa na maisha mazuri yenye furaha.Walikuwa wanapendana sana na tayari maandalizi yote ya ndoa yalikwisha fanyika.Zilibaki siku chache sana wafunge ndoa .Masikini Patrick namuonea huruma sana rafiki yangu ana wakati mgumu mno.Amemkosa Vero na sasa anataka kwenda gerezani kwa kosa ambalo hajalifanya.Hili ni kosa la mauaji na linaweza kupelekea akapata adhabu ya kunyongwa au hata kifungo cha maisha gerezani.No ! I cant let that happen..I cant let my friend go to jail just because of this good for nothing woman..Haiwezekani hata kidogo Patrick afungwe au anyongwe kwa sababu ya mwanamke huyu..This woman must pay for what she has done.."Andrew akazidi kuwaza na kumuangalia Happy aliyekuwa amekilaza kichwa chake kifuani kwa Patrick kwa jicho la chuki.Akamtazama tena rafiki yake na kumkuta ameinama akiwaza.


" Sijui mwanamke huyu amempa nini Patrick hadi akampenda kiasi hiki.Upendo huu umepitiliza.Pamoja na kupita miaka mingi hawajaonana na kila mmoja kuendelea na maisha yake lakini baada tu ya kuonana kila kitu kimebadilika.Penzi lao limerudi kwa kasi ya ajabu sana na kusababisha madhara makubwa si kwao tu bali hata kwetu sisi tunaowazunguka.Nashindwa nifanye nini..Je nisimame katika ukweli halisi kwamba Happy ndiye aliyemuua Vero? au nifuate maelekezo ya Patrick kwamba yeye ndiye aliyesababisha kifo cha Vero?..Patrick ni rafiki yangu mkubwa na ni zaidi ya rafiki itakuwaje kama nikienda kinyume na matakwa yake na kusimama katika ukweli? Mhhh Hapana ! ..Ninamfahamu vizuri Patrick ,kama nikienda tofauti na anavyotaka yeye basi kuna hatari hata urafiki wetu unaweza ukafikia mwisho.Ouh God help me to decide whats best for my friend" akawaza Andrew.Akainua kichwa akawatazama tena Patrick na Happy.Mikono ya Patrick ikiwa imefungwa pingu mikononi.


" Masikini Patrick anatia huruma sana .Mara ya kwanza kukutana naye ilikuwa ni gerezani ambako alikuwa amefungwa kwa kosa la mauaji na aliua kwa ajili ya kumtetea huyu huyu Happy.Kuna hatari kubwa akarejea tena gerezani kwa mara ya pili kwa kosa lile lile la mauaji.Kama kungekuwa na mashindano ya mapenzi ya kweli basi Patrick na Happy wangechukua ushindi kwa sababu inaonekana wanapendana kweli.Nimeamini katika penzi la kweli chochote kinawezekana.Sipati picha huyo mchumba wa Happy akisikia juu ya tukio hili ataamua nini.." Andrew akastuliwa toka mawazoni na gari moja lililoingia kwa kasi eneo lile.Alilifahamu gari lile.


Gari lile aina ya rav 4 likasimama na kwa haraka akashuka mwanadada mmoja mrefu ,mwembamba mwenye nywele ndefu alizozifunga kwa nyuma.Kwa mtazamo wa haraka haraka ungedhani kwamba mwanadada yule alikuwa akjishughulisha na masuala ya urembo kutokana na umbo lake . Alikuwa amevaa suti nyeupe iliyo mkaa vyema na kuzidi kumfanya apendeze zaidi.Sauti ya mlango wa gari ukifungwa ikamfanya Patrick ainue kichwa chake na mara akamuona mwanadada yule aliyeshuka katika ile gari, akatabasamu.


" Savana ! " Patrick akatamka kimoyo moyo.


Savana alikuwa ni wakili wa kujitegema na alikuwa na kampuni yake ya uwakili iitwayo Savana & Company Advocates moja ya kampuni za uwakili zinazosifika kwa kuwa na wanasheria mahiri sana.Savana anasifika kwa umahiri wake katika kusimamia kesi na amekuwa akisimamia kesi mbali mbali kubwa na kati ya hizo nyingi amekuwa akishinda na kumfanya aingie katika orodha ya mawakili maarufu nchini.


" Nilimpigia simu Savana nikamwambia aje mara moja" Andrew akamwambia Patrick ambaye hakujibu kitu.


Toka ameshuka garini Savana amekuwa akiongea na simu.


" Ok nashukuru,nitakupigia tena simu baadae,kuna jambo ninalifuatilia " akasema Savana akikatisha maongezi na mtu aliyekuwa akiongea naye simuni kisha akaiweka simu mfukoni na kumuendea askari polisi mmoja aliyekuwa amesimama karibu kabisa na gari lile walilokuwa wamepakiwa akina Patrick.Akasalimiana na yule askari polisi akamuuliza jambo na askari yule akamuelekeza katika jengo la utawala la hospitali ile.Kwa haraka Savana akapiga hatua kuingia ndani ya lile jengo aliloelekezwa. Ndani ya jengo lile akawakuta askari polisi watatu na madakatari wawili akawasalimu kwa ujumla na kuomba kuonana na Meja Simoni Mkerege .Meja mkerege akamuomba amsuburi nje kwa kama dakika tano hivi ili weze kumaliza maongezi muhimu na madaktari.


Dakika kumi baadae Meja Simon akatoka nje ya lile jengo na kumkuta Savana akimsubiri.Akamsogelea na kumuuliza


" Nkusaidie nini?


" Ninaitwa Savana Pius Nkere.Ni wakili wa kujitegemea toka katika kampuni ya Savana & company Advocates.Nimetaarifiwa kwamba mteja wangu aitwaye Patrick anashikiliwa kwa kosa la kusababisha mauaji.Nimekuja hapa kama mwanasheria wake ili kufuatilia na kuhakikisha kwamba mteja wangu anapata haki zote anazostahili kama mtuhumiwa kwa mujibu wa sheria." akasema Savana.


" Ouh kumbe wewe ndiye Savana ! Nimekuwa nikikusikia sana .Wakili maarufu sana hapa mjini.Nashukuru kukufahamu.Mteja wako ni kweli tunamshikilia kwa tuhuma za kusababisa kifo cha msichana aitwaye Veronica.Tunamshikilia yeye na msichana mwingine aitwaye Happy ambaye inasemekana ni mpenzi wake.Taarifa za awali zinaonyesha kwamba kulitokea ugomvi kati ya Patrick na Veronika ambao ulisababishwa na wivu wa kimapenzi.Inasemekana kwamba Veronika alikuwa ni mpenzi wa Patrick na kukatokea matatizo katika mahusiano yao na hivyo Patrick akaamua kumuacha na kuwa na huyu mpenzi wake mpya Happy.KItendo hicho hakikumpendeza Vero ambaye aliwafuata akiwa na silaha na kuanza kutishia kuwatoa uhai na ndipo vurugu kubwa ikaibuka na hatimaye kusababisha kifo chake.hayo ndiyo machache tunayoyafahamu kwa sasa ." akasema Meja Simon.


" Ahsante kwa taarifa Afande..je naweza kuruhusiwa kuonana na mteja wangu japo kwa muda mfupi? " akasema Savana.


" Kwa sasa yuko ndani ya gari,tunawapeleka kituoni yeye na mwenzake Happy pamoja na watu kadhaa ambao ni mashuhuda wa tukio hili watakaotoa maelezo yao.Nakushauri uvute subira tufike kwanza kituoni na pale nitakusaidia ili uweze kuongea na mteja wako kwa uhuru zaidi." akashauri Meja Simon.


" Sawa afande." akasema Savana.




Hatimaye Patrick na Happy wakafikishwa kituo cha polisi chini ya ulinzi mkali.Andrew na wale watu wengine wanne wakachukuliwa maelezo yao kama mashuhuda wa tukio lile wakaruhusiwa kurejea majumbani kwao.Patrick na Happy wakawekwa katika mahabusu za hapo kituoni kwa ajili ya kuchukuliwa maelezo yao siku itakayofuata.


Jitihada za Savana za kutaka kuonana na mteja wake zikazaa matunda na hatimaye ikaruhusiwa kuonana na Patrick ambaye alitolewa mahabusu na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na mafaili mengi ambamo ndimo Savana alikuwamo.


" Pole sana Patrick" akasema Savana baada ya kubaki wao wawili peke mle chumbani.Savana alikuwa ameomba apewe uhuru wa kuweza kuongea na mteja wake na hivyo askari wakatoka nje na kuwaacha wao peke yao chumbani.


" Ahsante Savana." akasema Patrick kwa unyonge


" usijali Patrick,jipe moyo mambo haya yatakwisha.Hebu nieleze tukio hili lilitokeaje? Nilistuka sana nilipopigiwa simu na rafiki yako Andrew akanifahamisha kwamba unashikiliwa kwa mauaji ikanilazimu kuacha kila nilichokuwa nakifanya nikaja mara moja" akasema Savana.Patrick akavuta pumzi ndefu kisha akaanza kumsimulia Savana kila kitu kilichotokea.


" Pole sana Patrick...Ni mkasa mzito sana lakini usijali mambo haya yatakwisha...Pamoja na hayo kuna jambo moja ambalo nataka unihakikishie Patrick " akasema Savana


" Jambo gani hilo Savana?


"Patrick una uhakika kwamba ni Happy ndiye aliyemsukuma Vero na kusababisha kifo chake? akauliza Savana huku akimuangalia Patrick kwa umakini mkubwa.


" Savana wewe ni rafiki yangu na ni mwanasheria wangu vile vile kwa hiyo siwezi kukudanganya.Ni kweli Happy ndiye aliyemsukuma Vero na kusababisha ajigonge ukutani na kupoteza maisha.Lakini hakukusudia kufanya vile bali alikuwa katika harakati za kuniokoa mimi kwa sababu wakati ule mimi na Vero tulikuwa tuking'ang'ania silaha aliyokuwa ameishika Vero mkononi.Kwa maana hiyo Savana nakuomba ufanye kitu kimoja"


" Kitu gani Patrick" akauliza Savana


" Nataka Happy asihusishwe kabisa katika kesi hii.Kila kilichotokea katika tukio lile na kusababisha kifo cha Vero nataka nikibebe mimi.Happy is innocent..Umenielewa Savana? akauliza Patrick.Savana akamuangalia kwa makini kisha akamuuliza


" Patrick are you out of your mind? How could you do such a thing? Happy ndiye anayetakiwa kubeba mzigo wote wa kesi hii na si wewe.." akasema Savana


" Naomba unisikilize vizuri Savana..Sitaki Happy ahusishwe katika jambo lolote lile kuhusiana na kesi hii.Nataka aachiwe huru.Nina sababu zangu za msingi kutaka iwe hivyo na niko tayari kubeba adhabu zote kuhusiana na kesi hii kwa hiyo nakuomba Savana ufanye hivyo ninavyokutaka ufanye.Nitakulipa kiasi chochote kile cha pesa unachokitaka kwa ajili ya kufanikisha suala hili." akasema Patrick.Savana akainama akafikiri kisha akasema


" Patrick niko hapa si kwa ajili ya kutafuta fedha.Niko hapa kwa ajili yako kama mtu wangu wa karibu ,kama rafiki yangu.Niko hapa kwa ajili ya kutaka kukutoa katika kesi hii ya muaji lakini mambo unayoniambia niyafanye yamenistua sana .Kwa nini ubebe mzigo wa mtu mwingine? Na vipi kama utakutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa?Uko tayari kunyongwa kwa kosa ambalo hukulitenda? Akauliza Savana.


" Savana naomba ufanye ninavyokuomba ufanye.If you cant do that for money then do it as my friend." akasema Patrick.


" Savana nafahamu kwamba nimekushangaza sana kwa maamuzi haya lakini naomba ufahamu kwamba haya ni maamuzi magumu niliyoyachukua kwa ajili ya kumuepusha Happy na kifungo.She didnt kill on purpose.She was trying to help me..She was helping me..you understand? Kama nikifungwa basi nitafungwa badala yake..Niliweza kufungwa mara ya kwanza kwa ajili yake na safari hii niko tayari tena kufungwa kwa ajili yake pekee kwa sababau ninampenda na sitaki aingie gerezani.Tafadhali Savana fanya kila uwezalo ili uweze kunisaidia katika suala hili." akasema Patrick.


" Patrick nadhani unahitaji muda wa kufikiri zaidi kuhusu maamuzi haya unayoyafanya .Nakuomba tuzungumze tena ukisha tulia ." akasema Savana


" No Savana..Akili yangu iko sawa.Nakuomba tafadhali ufanye hivyo.Ninafahamu uwezo wa kufanya hivyo unao kwa hiyo nakuomba usiniangushe Savana.Najua hupendi kufanya hivyo lakini nakuomba usinihofie mimi.I'll be fine." akasema Patrick.Savana akainama akafikiri kisha akasema.


" Ok Patrick I'm going to do it.I'll do what you want but in record I dont like this.I real dont like doing this to my friend lakini kwa kuwa umeniomba na kunisisitiza sana sina budi kufanya kadiri ya matakwa yako.Nitahakikisha Happy anatoka lakini nakuomba baada ya kesi hii kufika mwisho na matokeo yoyote yatakavyokuwa itakubidi utafute mwanasheria mwingine kwa sababau sintaendelea tena kuwa mwanasheria wako.Moyo wangu utakuwa unaumia sana." akasema Savana kwa masikitiko.


" Nashukuru sana Savana kwa kukubali kunisaidia katika suala hili.Umenifanyia jambo kubwa mno na nitakushukuru katika uhai wangu wote uliobaki" akasema Patrick.


" Happy umekwisha muelekeza namna atakavyotoa maelezo yake? Akauliza Savana.


" Nilijaribu kumweleza na akaonyesha kukubali"CHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


" Good.Sasa hivi ndivyo utakavyoandika katika maelezo yako na huo ndio utabaki msimamo wako.Nitaonana na Happy pia naye nitamuelekeza namna ya kuandika maelezo yake."


Savana akampa Patrick maelekezo ya namna atakavyo andika maelezo yake halafu wakaagana.


Baada ya kumaliza kuongea na Patrick Savana akafanya juhudi za kuonana na Happy akafanikiwa.


Happy hakuwahi kuonana wala kufahamiana na Savana .Akapelekwa katika kile kile chumba alichotoka Patrick .Savana alipomuona Happy akastuka.Akamuangalia tena kwa makini kisha akasema


" Pole sana Happy"


" Ahsante sana dada" akajibu Happy


" Mimi naitwa Savana ni mwanasheria wa Patrick .Nina kampuni yangu ya uwakili inaitwa Savana & Company advocates.Mimi nikishirikiana na mawakili wenzangu ndiyo tutakaowatetea katika kesi hii inayowakabili.Patrick ni rafiki yangu mkubwa na ndiyo maana baada ya kupata taarifa za tukio hili nilifika haraka sana eneo la tukio.Pole sana Happy matatizo ni sehemu ya maisha na huja bila ya kutazamia."


" Ahsante sana Savana.." akasema Happy na kutoa machozi


" Usilie Happy..Naomba kuanzia sasa uwe jasiri.Ni ujasiri pekee ambao utakuwezesha kusimama imara na hatimaye kushinda kesi hii.Kuanguka ni jambo la kawaida na ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.Sote tunaanguka lakini tuangukapo hatupaswi kukaa chini na kulia.Tunatakiwa kuinuka na kusonga mbele.Kwa hiyo hata wewe hutakiwi kuangusha chozi hata kidogo. Halafu wewe ni mrembo wa Taifa.Kama msichana ambaye ulifanikiwa kutwaa taji kubwa kama lile ni lazima ulikuwa ukijiamini kwa hiyo ujasiri ule uliokuwa nao wakati ukishindania taji lile ulete hapa na usimame imara katika suala hili.Tumeelewana Happy?


" Tumeelewana" akasema Happy huku akifuta machozi


" Ok vizuri..Sasa Happy nimekuita hapa usiku huu kuna mambo mawili matatu ambayo kama wakili ninayekwenda kuwatetea ningependa kuyafahamu.Ninakuomba uwe muwazi katika kila nitakachokuuliza .Kwanza kabisa naomba unieleze japo kwa ufupi tukio hili la leo lilitokeaje? akasema Savana.Happy akainama akafikiri kidogo halafu akaanza kumsimulia Savana kila kitu anachokifahamu kuhusiana na tukio lile.


" Ok nashukuru sana Happy kwa kuwa muwazi.Lakini kuna jambo ambalo ningependa unihakikishie.Naomba unihakikishuie kwamba wewe ndiye uliyemsukuma vero akajigonga ukutani na kupoteza maisha"


" Ni kweli mimi ndiye niliyemsukuma Vero akajigonga ukutani" akasema Happy


" Lakini sikufanya vile kwa kukusudia.Nilikuwa nikijaribu kumzuia Vero asiweze kufanya madhara kwa sababu wakati huo alikuwa ameshika bastora mkononi na tayari alikwisha nikosa na risasi ."


" Sawa Happy nimekuelewa pole sana kwa mkasa huu. Patrick amenieleza jambo moja ambao lilinistua kidogo lakini akasisitiza kwamba ni lazima nilifanye.Ameniambia kwamba wewe usihusiswe na jambo lolote kuhusiana na kesi hii.Anataka tukutoe kabisa na mzigo wote aubebe yeye.Je alikudokeza jambo kama hili?


" Ndiyo alinidokeza jambo hilo"


" wewe ukaamua nini?


" Alinisisitiza sana ikanibidi nimkubalie anavyotaka iwe." akajibu Happy.


" Je unafahamu kwamba Patrick anakupenda sana kiasi cha kuamua kujitwisha yeye mzigo wote wa mauaji?


Huku akitoa machozi Happy akajibu


" Ninafahamu ..Ninafahamu jinsi gani Patrick ananipenda ..Hata mimi ninampenda sana .."


Savana akamuangalia Happy kwa makini kisha akasema


" Happy naomba ufahamu kwamba Patrick ni rafiki yangu mkubwa sana na sikuwa tayari kufanya hivyo anavyotaka lakini baada ya kunisisitiza sana na kuonyesha wazi ni kwa namna gani anavyokupenda na hataki uguswe kabisa na mkondo wa sheria nikakubaliana naye.Nitakutoa katika kesi hii ila nakuomba Happy sadaka hii kubwa aliyoitoa Patrick isiende bure.Siku zote nakuomba uwe karibu naye na kumpa moyo na faraja.Endapo nitasikia kwamba unaponda raha na wanaume wengine wakati Patrick yuko gerezani kwa sababu yako naapa mbele za Mungu kwamba nitayafaya maisha yako yawe magumu sana na utatamani hata kufa.Umenielewa Happy"


Happy akafuta machozi kisha akasema


" Nimekuelewa Savana..Patrick ndiye maisha yangu na siku zote nitakuwa upande wake" akasema Happy


" Vizuri..sasa maelezo yako utakayoyatoa yatakuwa namna hii." akasema Savana na kumwelekeza Happy maelezo ya kutoa kisha wakaagana na Happy akarudishwa mahabusu




Mrembo wa Tanzania Happy Kibaho kuhusishwa katika tukio la mauaji ndiyo habari kuu iliyokuwa ikiongelewa kila mahali nchini. Tukio hili liliwastua sana watu.Vyombo vya habari hususan magazeti yalipamba kurasa zao kwa habari hii ya kustusha.Nje ya kituo cha polisi ambacho Happy na Patrick walikuwa wakishikiliwa kwa siku ya tatu sasa kulijaa waandishi wa habari wakijaribu kupata habari ya kuandika kuhusiana na tukio lile lililogusa hisia za watu wengi..Eneo la kituo liligeuka kuwa eneo lenye pilika pilika nyingi tofauti na ilivyozoeleka.


Saa nane na dakika ishirini za mchana ,katika mlango mkubwa wa kuingilia kituoni kilitokea kitu ambacho hakuna aliyekuwa amekitazamia. Miss Tanzania Happy kibaho akiwa ameongozana na familia yake yaani baba na mama yake mzazi na mdogo wake Isabella wakajitokeza.Pamoja nao walikuwepo wakili Savana,mkurugenzi wa Miss Tanzania,msemaji wa Miss Tanzania pamoja na watu wengine wanne.Kitendo cha sura ya Happy kuonekana akitoka mlangoni kundi kubwa la wapiga picha na waandishi waliokuwa wamepiga kambi pale kituoni wakisubiri taarifa ya kamanda wa polisi kuhusiana na tukio lile likasogea karibu na kuanza kumpiga picha.Happy hakuwajali akaendelea kupiga hatua japo miguu ilikuwa mizito kutembea.Baadhi ya waandishi wa habari wakajaribu kumuhoji maswali lakini Happy hakuwa tayari kuongea lolote.


" samahani ndugu waandishi ,Happy kwa sasa hayuko tayari kwa kujibu maswali yenu.Nawaomba ndugu zangu mumuache akapumzike kwa sasa na akili yake ikishatulia atawajibu maswali yenu yote." Msemaji wa Miss Tanzania Abdool azizi Sharrif akawaambia waandishi wa bahari huku akijaribu kuwazuia kutomsonga zaidi Happy.


" Tunaomba basi utueleze nini kimetokea? Mbona miss Tanzania ameachiwa huru wakati anahusishwa na tuhuma za mauaji? mmoja wa waandishi wa habari akamuuliza Abdoolaziz.


" Kwa ufupi ni kwamba Happy ameachiwa huru baada ya kuonekana hahusiki na jambo lolote lililosabisha kifo." Akasema Abdoolazizi kwa ufupi .


Happy akaongozwa kuelekea katika gari moja aina ya Noah yenye rangi nyeupe.Ndugu jamaa na marafiki ambao walikuwepo pale kituoni,walimpa pole na kumfanya ashindwe kuzuia hisia zake na kudondokwa na machozi.Hatua chache kabla ya kulifikia lile gari,kijana mmoja mtanashati aliyevalia nadhifu akajitokeza toka katika gari moja dogo lenye namba za kibalozi.Kijana yule mwenye umbo lililojengeka vyema akatabasamu huku akimuendea Happy.Happy ambaye alikuwa akitembea huku ameinamisha kichwa akaguswa bega na mdogo wake akageuka.


" Mike huyu hapa" akasema Margreth na kumfanya Happy astuke ghafla kana kwamba ameona kitu cha kutisha.Happy akasimama halikadhalika Mike naye akasimama wakaangaliana kwa sekunde kadhaa kisha bila kujali kamera za waandishi wa habari na wapiga picha Mike akamwendea na kumkumbatia Happy kwa furaha akambusu lakini Happy hakuonyesha furaha wala kuongea kitu chochote.Mike akaishika mikono ya Happy na kutaka kusema neno lakini Happy akajitoa katika mikono ile na kutembea kwa kasi kuliendea lile gari ambalo tayari mlango wake ulikwisha funguliwa.Mike akabaki ameduwaa.Hakuelewa sababu ya happy kumfanyia vile.


" Usikasirike Mike ..give her sometime." Margreth akamnong'oneza Mike aliyekuwa amesimama akimshangaa Happy.


Waandishi wa habari ambao waliokuwa makini kufuatilia kila hatua anayopiga happy wakaliona tukio lile na kumzunguka na kuanza kumuhoji ili wafahamu nini kilitokea.Mike hakujibu swali lolote la waandishi wa habari.Taratibu akaelekea liliko gari lake lenye namba za kibalozi akafunguliwa mlango akaingia garini kisha gari ikaondoka pale kituoni.


Familia yote ya Happy ikaingia garini tayari kwa kuondoka .


" Happy jitahidi upate mapumziko marefu ili uweze kutuliza akili.Pamoja na hayo usisahau tuliyoongea juzi" akasema Savana .Happy bado machozi yaliendelea kumtiririka.


" Ahsante sana Savana kwa msaada wako.Siwezi kusahau" akasema Happy.


" Stop crying Happy..usilie tena.you have to be strong..be strong for you and Patrick..." akasema Savana huku akimfuta Happy machozi kwa kitambaa..Mama yake Happy ambaye alikuwa ameketi mbele akiongea na simu aliposikia jina patrick linatajwa akastuka na kugeuka ghafla akamuangalia Savana kwa macho makali.Savana akaufunga mlango na taratibu gari ile ikaondoka maeneo ya kituoni ikiongozana na gari nyingine nne.


Baada ya kuhakikisha Happy ameondoka kituoni,waandishi wa habari hawakuondoka waliendelea kusubiri taarifa toka kwa kamanda wa polisi ambaye alikuwa ameahidi kulitolea ufafanuzi suala lile ambalo lilikuwa limeteka hisia za watu wengi na kugubikwa na upotoshwaji mkubwa hususan toka katika vyombo vya habari.


Saa tisa za alasiri waandishi wa habari wakaitwa ofisini kwa kamanda wa polisi .Bila kupoteza muda kamanda wa polisi akawaambia.


" Ndugu zangu wanahabari nimewaiteni hapa ili kuweza kuwapeni taarifa kadhaa za kipolisi na vile vile kutolea ufafanuzi kuhusu suala linalomuhusu Miss Tanzania ambaye alikuwa akishikiliwa kwa tuhuma za kusababisha mauaji"


Kamanda James fungakata akatoa taarifa mbalimbali kuhusiana na matukio mbali mbali ya kiuhalifu yaliyotokea halafu akasema


" Katika wiki hii pia kumetokea tukio ambalo limezua gumzo kubwa katika kila kona ya nchi.Kumekuwa na upotoshwaji mkubwa sana kuhusiana na tukio hili.Tukio hili linamuhusu mrembo wetu wa Tanzania Happy Kibaho.Taarifa sahihi ni kwamba kulitokea ugomvi uliosababisha kifo cha mwanamke aitwaye Veronika.Sababu kuu ya ugomvi huo inasemekana ni wivu wa kimapenzi.Kijana mmoja aitwaye Patrick alikuwa na mahusino ya muda mrefu na marehemu Veronika na tayari walikuwa katika maandalizi ya kufunga ndoa.Wakiwa katika maandalizi hayo ya harusi,ukaibuka mgogoro mzito kati yao uliomsababisha Patrick kuamua kusitisha kila kitu kuhusiana na ndoa na kuvunja kabisa mahusiano yao ya kimapenzi.Kitendo kile kilimchukiza sana Veronika na hasa baada ya kugundua kwamba Patrick alikuwa tayari na mahusiano ya kimapenzi na msichana mwingine aitwaye Happy kibaho .Veronika alipata taarifa kwamba Patrick na Happy walikuwa pamoja katika hospitali kuu ya moyo.Akawafuata pale akiwa na silaha mkononi na kuanza kutoa vitisho vya kuwaua wote .Silaha aliyokuwa nayo Veronika ni hii hapa" Kamanda akaiinua bastora ile juu akawaonyesha waandishi wa habari.


" Msichana huyo Veronika " akaendelea kamanda James


" Alikuwa na lengo la kulipa kisasi kwa Patrick kwa kitendo chake cha kuamua kumuacha na hasa katika hatua za mwisho za maandalizi ya ndoa yao.Ili kuthibitisha kwamba alikuwa amedhamiria kuwadhuru Patrick na mpenzi wake akaachia risasi ambayo ilimkosa Happy.Kitendo kile cha kumkosa Happy kwa risasi kilimkasirisha Patrick ,akamfuata na kutaka kumny'ang'anya ile silaha na hapo ndipo ikaibuka purukushani ya kugombea silaha ile.Katika purukushani hiyo Veronika akajigonga ukutani na kufariki papo hapo. Jeshi la polisi lilikuwa likiwashikilia Patrick na Happy lakini baada ya mahojiano tumeamua kumuachia huru Happy baada ya kuthibitika kwamba hakuhusika na ugomvi ule uliosababisha kifo cha Veronika.Kwa sasa bado tunaendelea kumshikila kijana Patrick ambaye amekiri kugombana na Veronika na kusababisha kifo chake.Kwa sasa tunaandaa mashitaka na muda wowote atapelekea mahakamani kusomewa shitaka la mauaji. Kwa ufupi huo ndio ukweli halisi kuhusiana na tukio hili" akamaliza kamanda James .Kwa kuwa muda ulikuwa umekwenda sana hakukuwa na nafasi ya kuuliza maswali.




Safari ya kuelekea nyumbani ilikuwa ya kimya kimya.Happy hakutaka kuongea na mtu yeyote.Macho yake hayakukauka machozi. Baada ya kufika nyumbani Happy akashuka garini na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake akifuatana na mdogo wake Margreth.Kabla hajafunga mlango wake akamgeukia mdogo wake na kumwambia


" Margreth sihitaji kuona na mtu yeyote leo..I need to be alone...." akasema Happy.Margreth akamwangalia akamwambia


" kweli happy suala hili ni zito sana...you need more time to rest...nitahakikisha hakuna mtu atakayekusumbua.." akasema Margreth..


" Ahsante sana Margreth..." akasema Happy kisha akaufunga mlango wake akalala.Margreth akabaki amesimma pale mlangoni kwa Happy akiwa na mawazo mengi mara akatokea mama yake..


" Mbona umesimama hapa nje peke yako? Happy amekuzuia kuingia ndani? akauliza mama yake


" Happy anahitaji kuwa mwenyewe kwa sasa..Hataki kuonana na mtu yeyote" akajibu Margreth


" Kwa hiyo amekuweka wewe askari wake? akauliza mama yake kwa ukali huku akikishika kitasa cha mlango wa Happy.


" Mama please !!!..Happy anahitaji kuwa mwenyewe kwa sasa...naomba tafadhali usimsumbue hadi kichwa chake kitakapotulia.." akaomba Margreth . Mama yake akamuangalia kisha akasema.


" Nahitaji kuongea na happy...Jambo lililotokea ni zito sana .Sikutegemea kama siku moja Happy angeweza kuwa na tuhuma kama hizi..Halafu nataka kufahamu huyu Patrick ni yule yule aliyekuwa amefariki au ni Patrick yupi? Mambo haya yametuchanganya akili zetu mno...." akasema mama yake akiwa amesimama pale mlangoni akimuangalia Margreth..


" Mama nakuomba tafadhali mpe Happy nafasi ya kuweza kutuliza kichwa chake kwa sababu jambo hili ni zito sana..Baada ya kutulia atatupa majibu ..." akajibu Margreth..


" Ulikuwa unafahamu kwamba Happy ana mahusiano na huyo Patrick? Mama yake Happy akamuuliza Margerth huku amemkazia macho.Margreth akashindwa kujibu akabaki ameinama chini.


" Naomba unijibu Margreth..Ulikuwa ukifahamu kwamba Happy ana mahusiano na Patrick? Umewahi kuonana na huyo Patrick? Naomba unijibu tafadhali"


"Mama suala hili ni gumu sana .Ni Happy pekee ambaye anaweza akakueleza na si mimi" akajibu Margreth kisha akaondoka kwa kasi akaelekea chumbani kwake akajifungia.


" Masikini Happy..kwa nini lakini yamemtokea haya? Namuonea huruma dada yangu.Anateseka sana kwa sasa..Hakujua kama mambo yangekuwa hivi.." akawaza Margreth..."


" hata mimi sikutegemea kabisa kama mambo yangekuwa namna hii japokuwa nilikwisha hisi toka mwanzo kwamba suala lile halitakuwa na mwisho mzuri.Maamuzi haya waliyoyachukua Patrick na Happy ya kutaka kurejesha mahusiano yao ya kimapenzi lazima yangekuwa na madhara.Tayari wote wana wapenzi na mahusiano yao yamekwisha piga hatua kubwa .Patrick alikuwa katika maandalizi ya kufunga ndoa na Vero.Happy nae tayari amekwisha vishwa pete ya uchumba na Mike.Du ! nashindwa kupata jibu ..Jambo hili limekuwa gumu tofauti na tulivyotazamia." akawaza Margreth akiwa ameka kitandani .


"masikini Patrick harakati zake zote za kutaka kurudiana na Happy zimemfanya aishie gerezani.Itamchukua muda mrefu sana kutoka gerezani na kuna uwezekano asiweze kutoka kabisa kama atahukumiwa kunyongwa.MasikiniPatrick kwa nini kila mara akiwa na Happy yanamkuta haya? Why always you Patrick? namuonea huruma sana kwa sababu mara ya kwanza alifungwa kwa kosa kama hili la mauaji na alifanya mauaji yale akiwa katika harakati za kumuokoa Happy. Safari hii anarejea gerezani kwa kosa kama .lile la mwanzo la mauaji .Ouh Patrick ! nashindwa kuelewa ni kwa nini mambo haya yanakutokea......" Margreth akafuta machozi yaliyokuwa yakimtoka.


"Ni ukweli ulio wazi kwamba Patrick na Happy wanapendana sana Sina shaka kabisa na hilo kwa sababu hata baada ya kutengana kwa miaka mingi na kila mmoja akalazimika kuendelea na maisha yake ikiwa ni pamoja na kuanzisha mahusiano mapya lakini mara tu walipokutana tena ile mbegu ya mapenzi yao ya dhati ambayo bado iko mioyoni mwao imechipua kwa kasi kubwa na kuwafanya watake kurudisha tena mahusiano yao na kuamua kuachana na wapenzi wao wa sasa" akawaza margreth na mara simu yake ikaita.Akaichukua na kuangalia mpigaji.Alikuwa ni Mike.Margreth akavuta pumzi ndefu na kuangalia simu ile ikiita na kukatika.Ikaita kwa mara ya pili na kukatika.Ikaanza kuita tena kwa mara ya tatu ,akapiga moyo konde na kuipokea.


" hallow Mike" akasema Margreth.Mike akasikika akivuta pumzi ndefu na kusema


" Margreth sifahamu nianzie wapi kwa mambo haya yaliyojitokeza. Nahisi kichwa changu kinaweza kupasuka kwa mawazo mazito niliyonayo.Margreth naomba tafadhali unifafanulie juu ya mambo haya yaliyotokea ili niweze kufahamu tukio lile limetokeaje tokeaje." akauliza Mike.Margreth akanyamaza akafikiri kidogo kisha akasemaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


"Mike nasikitika kwamba sina lolote la kuweza kukwambia kwa sasa.Mambo haya hata mimi yamenistua sana .Tafadhali Mike naomba uniache kwanza ili niweze kulifahamu suala hili kwa undani wake " akasema Margreth.


" Margreth tafadhali naomba unieleze hata kile kidogo unachokifahamu kuhusiana na tukio hili.Najua lazima kuna jambo unalifahamu.Niambie kuhusu huyu kijana Patrick ambaye anasemekana alikuwa na Happy usiku wa tukio.Niambie Margreth huyu Patrick na Happy wana mahusiano yoyote? Walikuwa wanafanya nini usiku huo walipokutwa na msichana aliyefariki?" akauliza Mike.Margreth akaanza kuhisi kijasho kwa mbali.


" Mike kama nilivyokwambia awali kwamba suala hili limetustua sana hata sisi na mpaka sasa hivi hakuna yeyote mwenye kufahamu undani wa jambo hili.Ni Happy pekee ndiye mwenye kufahamu.Ni yeye pekee ndiye mwenye kuweza kukueleza ukweli halisi." akasema Margreth.


" Unaweza ukanisaidia ili niweze kuongea naye? akasema Mike.


" hapana Mike..Kwa sasa Happy amepumzika .Jambo hili lililomtokea ni jambo kubwa na zito kwa maana hiyo anahitaji kupewa muda wa kutosha ili aweze kutuliza kichwa chake...." akasema Margreth.


" Margreth naelewa kuna kitu unakifahamu lakini hutaki kuniambia.Kuna jambo gani linaendelea kimya kimya ?Na kwa nini hutaki kunieleza? Nimeyaona macho ya Happy pale kituo cha polisi na nimehisi kuna jambo amb........." Mike akakatishwa ghafla na Margreth.


" Mike tafadhali naomba uniache nipumzike.Nipigie baadae" Margreth akakakata simu.


" Jamani mbona happy ameleta mambo ! Mike anateseka sana kijana wa watu.Amekuja toka Marekani kwa lengo la kukaa na kufurahi na Happy lakini badala ya furaha imekuwa ni majonzi .Happy kwa nini umewatesa watu wengi namna hii? Kwa mara ya kwanza ninaona ingekuwa vyema kama wewe na Patrick msingekutana kabisa katika maisha yenu yaliyobakia" akawaza Margreth


* * * *


Ni saa mbili za usiku bado Happy amejifungia chumbani kwake.Toka amerejea nyumbani hajatoka chumbani kwake na hajataka kuonana na mtu yeyote yule.usiku huu familia yake yote ilikuwa imekaa mezani ikijiandaa kwa ajili ya chakula cha usiku.


" Happy amekwisha taarifiwa kuja hapa mezani? akauliza mzee Kibaho baba yake Happy


" Nimejaribu kugonga mlango wake lakini amekataa kunifungulia.Nilipomgusia kuhusu suala la chakula amesema kwamba hasikii njaa.Nina wasi wasi sana na happy kwa sababu toka amerejea hapa nyumbani hajatia kitu chochote tumboni." akasema margreth.


" Ngoja nikamtoe huko chumbani.Asituumize vichwa huyu mtoto." akasema mama yake Happy akionekana kukasirika.


" hapana usiende..Ntakwenda mimi" akasema mzee Kibaho akainuka na kuelekea katika mlango wa chumba cha Happy akagonga mlango na kusema taratibu


" Happy mwanangu naomba unifungulie mlango nataka kuongea nawe." akasema mzee Kibaho.Happy hakujibu kitu.Mzee Kibaho akagonga tena mlango.


" Happy !! fungua mwanangu.."


Toka ndani ya chumba ikasikika sauti dhaifu ya Happy


" Daddy I want to be alone...I'm sorry"


" Happy nafahamu kwamba unahitaji nafasi ya kuwa peke yako lakini naomba niongee nawe dakika tatu tu"


Kikapita kimya kifupi mlango ukafunguliwa.Sura ya Happy ilikuwa imesawajika.Macho yake mazuri yalivimba na kuwa mekundu kwa kulia.Baba yake akashikwa na uchungu mwingi kwa hali ile aliyomkuta nayo mwanae akamkumbatia na kumfariji.


" Be strong my dear,you are going to be fine...you'll be ok" akasema mzee Kibaho huku akimpiga piga mwanae mgongoni .Kitendo kile kikaamsha tena kilio kwa Happy.Baba yake akamketisha katika sofa lililokuwamo mle chumbani na kumfuta machozi.


" Daddy why always me? akauliza Happy huku akilia.


" Happy mwanangu usilie ,usisikitike na wala kuhuzunika na kujiuliza kwa nini wewe? Nafahamu moyo unauma sana lakini naomba ufahamu kwamba matatizo tumeumbiwa sisi wanadamu na matatizo huja pasi na taarifa.Matatizo yanatukomaza na kutufanya tuwe majasiri hivyo kaza moyo mwanangu na yote yatakwisha.Sisi sote tuko pamoja nawe katika kipindi hiki kigumu kwako..we love you and we support you..."


Maneno yale ya mzee Kibaho yakamfariji sana Happy akafuta machozi .Mara akaingia mama yake akiwa na sahani iliyojaa chakula akaiweka mezani halafu akaenda kukaa pembeni ya Happy.


" Pole sana mwanangu.Huyu baradhuli anataka kukuharibia maisha yako..Kila nikikuona ninapatwa na hasira kali.Kwa nini atake kukusababishia matatizo makubwa namna hii? Ouh Happy mwanangu naomba umuogope kabisa kijana huyo..achana naye kabisa huyo shetani......."


Happy akayafikicha macho yake , akamtazama mama yake na kusema


" Mama tafadhali naomba usirudie tena kumtukana Patrick na kumuita shetani " akasema happy akionyesha kukerwa na kauli ile ya mama yake.


" Mwanangu ninaumia sana kukuona ukiwa katika hali hii.Nina hasira sana na huyo kijana ambaye ninamfananisha na shetani kwa sababu ametaka kukuingiza katika matatizo makubwa.Amesababisha ukalala polisi.Ameliharibu jina lako zuri.Happy mwanangu nakuomba uvunje kabisa urafiki na huyo kijana ..."


" Mom thats enough !!!..tafadhali naomba usiongee kitu ambacho hukifahamu..Naomba niwafahamishe wazazi wangu kwamba Patrick huyu ambaye mnasikia nilikuwa naye wakati tukio hilo linatokea ni yule yule ambaye alifungwa jela kwa ajili yangu.Patrick hakufa kama ilivyokuwa imezushwa."


Wazazi wake wakastuka sana kwa taarifa ile .Wakatazamana usoni. Happy akaendelea


"Katika tukio hilo naomba mfahamu kwamba ni mimi ndiye niliyemsukuma Veronika akajigonga ukutani na kupoteza maisha na wala si Patrick kama watu wanavyofahamu.Kwa kuniepusha mimi na adhabu ya kufungwa,kunyongwa au kifungo cha maisha jela,Patrick ameamua kuubeba yeye mzigo wote wa kesi hii na yeye kuonekana ndiye muuaji.Amefanya yote haya ili kuniweka mimi huru.I'm free now because of him..so this man doesnt deserve to be called a devil. Akasema Happy machozi yakaanza kumtiririka upya.


Hakuna aliyeongea tena wote wakaa kimya.Mzee Kibaho akambembeleza Happy ale chakula japo kidogo Happy akakubali akala chakula.Mama yake alikuwa ameshika tama akimtazama mwanae.




Ni saa tatu kasoro za usiku Savana alikuwa ndani ya chumba kimoja katika kituo cha polisi akizungumza na Patrick.


" Patrick kesho utapandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kusomewa shitaka halafu utapelekwa mahabusu katika gereza la Uwangwa. Hautaweza kupatiwa dhamana kutokana na uzito wa kosa lenyewe. Nasikitika sana Patrick kwa kupandishwa kizimbani lakini yote haya ni matakwa yako ...Lakini usijali nitatumia kila uwezo nilionao kuhakikisha kwamba unashinda kesi hii.." akasema Savana .Patrick akainama akafikiri kisha akasema


"Nashukuru sana Savana kwa msaada wako mkubwa.Jambo ulilonifanyia ni kubwa sana .Kuhakikisha kwamba Happy anaachiwa huru ni jambo kubwa sana kwangu." akasema Patrick huku akitabasamu


" Patrick mimi siwezi kupingana nawe katika maamuzi yako lakini bado nina mashaka sana na maamuzi uliyoyafanya ya kuamua kuubeba mzigo wa Happy..unafikiri yeye anakupenda kiasi cha kuweza kufanya kama ulivyofanya wewe?..anaweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yako? akauliza Savana


" Ninamuamini Happy ananipenda na kwa hilo sina shaka naye.." akasema Patrick..


" Ndiyo unamuamini lakini una hakika kwamba anakupenda kiasi cha kuweza kuyatoa maisha yake kwa ajili yako? akauliza Savana.Patrick akanyamaza kimya.


" Patrick nimekuuliza makusudi swali hili kwa sababu wewe ni rafiki yangu,ninakujali na kukuthamini na ndiyo maana sitaki sadaka hii ya maisha yako uliyoitoa kwa ajili ya Happy iende bure..Nina wasi wasi sana lakini sitaki kuingilia masuala ya ndani ya moyo wako.Wewe ndiye mwamuzi wa maisha yako. Ninachotaka kukuhakikishia kwamba mimi na timu yangu tutasimama kidete na kwa uwezo wetu wote tulionao tutajitahidi kwa kila tuwezavyo kukutetea katika kesi hii..." akasema Savana na kuagana na Patrick akaondoka.Kichwa chake bado kilikuwa kizito mno kuhusiana na kesi hii ya Patrick.


" Patrick ananisikitisha sana .kila nikimuona ninaumia mno..kwa nini ayaweke maisha yake katika hatari kwa kosa la mtu mwingine? ..Patrick ni mtu wangu muhimu sana na nitafanya kila niwezalo ili kumsaidia ." akawaza Savana.


Saa tano za usiku Savana akawasili nyumbani kwake.Akashuka garini na kuelekea ndani.Msichana wake wa kazi alikuwepo sebuleni akimsubiri.Savana akasalimiana naye na kuelekea moja kwa moja chumbani kwake.Mumewe george tayari alikuwa amejilaza kitandani .Mara tu Savana alipoingia akamuendea George akamtikisa na George ambaye alikuwa ameanza kupitiwa na usingizi akaamka.Savana akambusu mumewe halafu akaelekea bafuni kaoga na kurejea kitandani.Akambusu mumewe na kugeukia upande wa pili tayari kwa kulala.


" Savana kuna jambo gani limekutokea katika siku hizi tatu? Nakuona umebadilika sana..Unachelewa kurudi na ukirudi unakuwa umechoka na hutaki hata kuongea na mimi tena.Una matatizo gani? George mume wa Savana akauliza


" George naomba uniache kwa sasa kichwa changu kina mambo mengi mazito" akasema Savana


" Savana naomba unisikilize.Mimi ni mumeo na nina haki ya kukuuliza .Siwezi kukuona ukichelewa kurudi nyumbani na hunielezi chochote .Huna tena muda na mimi mumeo.Unanipa wasi wasi sana Savana.Hebu angaliani hii ni saa ngapi unarejea nyumbani kama mke wa mtu? akauliza George ambaye alionekana kuanza kukasirika.


" George nina kesi ngumu ninayoisimamia kwa sasa .Patrick anashikiliwa kwa kosa la mauaji.." akasema Savana.


" Patrick !! akauliza George kwa mshangao.


" Ndiyo..Patrick..Ina maana hujasikia tukio lililotokea siku tatu zilizopita likimuhusisha Patrick na mauaji? akauliza Savana


" Patrick huyu ambaye aliwahi kuwa mpenzi wako? akauliza George


" Ndiye huyo...." akasema Savana.George akainuka na kumuangalia Savana usoni.


" Sasa nimepata picha halisi.Kumbe kuchelewa kote huku ni kwa ajili ya kesi ya aliyowahi kuwa mpenzi wako..Kwa maana hiyo yeye ni muhimu sana kuliko mimi mumeo ? akauliza George


" George tafadhali usiseme maneno hayo.Patrick ni rafiki yangu na mteja wangu vile vile kwa hiyo sina budi kuishughulikia kesi yake..Kuna tatizo gani kuisimamia kesi yake ? akasema Savana.


" Tatizo lipo..tena tatizo kubwa..Unasimamia kesi nyingi lakini hakuna hata siku moja umewahi kurejea nyumbani usiku kama huu..Yaani unamthamini Patrick ambaye ni muuaji kuliko hata mumeo? Lakini sioni kama ni jambo la ajabu kwa sababu nilihisi lazima jambo hili litatokea siku moja.Bado hujaweza kumtoa Patrick moyoni mwako.Pamoja na miaka hii yote kupita lakini bado hujafanikiwa kumtoa Patrick moyoni mwako..You still love him ...I'm so stupid" akasema George.Savana akainuka na kumtazama George kwa hasira


" George tafadhali naomba usiseme hivyo..Ndiyo niliwahi kuwa mpenzi wa Patrick lakini baada ya kukupata wewe nikaachana naye kwa sababu tayari yeye alikuwa na mpenzi wake Veronika.I'm with you now and not Patrick." akasema SavanaCHANZO:  https://deusdeditmahunda.blogspot.com/


" Yes you are with me ..but am I in your heart? akauliza George


" george mambo gani hayo unayaongea leo? akauliza Savana.


" Savana nafahamu kabisa kwamba hujawahi kumsahau Patrick. Nimekununulia vito vingi vya thamani lakini mbona huvivai na unaendela kuvaa vile alivyokununulia Patrick? You still love him isnt it? akauliza George ambaye tayari alipandwa na hasira


" George ...!! akasema Savana.George akamkaribia Savana na kumuangalia usoni.


" Savana naomba uniangalie machoni na uniambie kwamba unanipenda na unanipenda mimi peke yangu.." akasema George.


" George mambo gani haya unayafanya? ...akauliza Savana


" Savana nimekuuliza swali mbona hunijibu? Huna jibu la kunipa?


Savana akabaki kimya akimtazama George huku akihema kwa nguvu.


" Nilijua tu.You never loved me.All this long you still love Patrick..." akasema George


" George hebu achana na hayo mawazo yako ya kijinga..You know I've always loved you..." akasema Savana.


" Do you love me Savana? Una hakika kwamba unanipenda? akauliza George


"yes I love you and you kow that" akajibu Savana


" Vizuri..sasa kama kweli unanipenda naomba ufanye yafuatayo..Nataka uachane kabisa na kusimamia kesi ya Patrick..Kama kweli mimi ni mumeo na unanipenda nataka uachane na ukae mbali kabisa na kesi hii" akasema George.Savana akainama akafikiri kisha akainua uso wake.macho yake yalijaa machozi.Akamuangalia George usoni kisha akatikisa kichwa.


"I'm sorry George I cant do that..siwezi kufanya hivyo unavyotaka nifanye...Patrick is my friend and he needs me now more than ever..siwezi kuacha kumtetea hata iweje.akasema Savana.George akamuangalia kwa makini usoni kisha akasema.


" Vizuri..huwezi kuacha kumtetea kwa sababu unampenda .Kama hivyo ndivyo naona ni bora nikuache huru uendelee kumtetea Patrick ashinde kesi na uje uishi naye hapa.Mimi nimechoshwa na vituko vyako Savana.Toka tumeanza kuishi pamoja mpaka leo hii ni vituko kila siku..Ni miaka mingapi mpaka leo na hutaki hata kusikia suala la mtoto? Nimechoka Savana.Nakuacha uendelee na huyo Patrick." akasema George huku akivaa nguo zake.Savana akasimama na kumuangalia George kwa macho makali.


" Mimi naondoka Savana..nitakuja kuchukua vitu vyangu kesho..Siwezi kuendelea kuishi nawe wakati moyo wako unampenda mtu mwingine..Siwezi kuendelea kugombania nafasi katika moyo wako..nafasi ambayo tayari amekwisha pewa mtu mwingine.Nimevumilia mengi na ninashukuru kwa kupata jibu leo kwamba chanzo cha haya yote ni Patrick..Nakutakia maisha mema na huyo mhalifu wako...." akasema George


" Dont you dare insult Patrick again infront of me...kwa taarifa yako ninampenda Patrick na nitafanya kila niwezalo niwe naye tena..You are nothing compared to him." akasema Savana kwa hasira..George akakasirika na kutaka kumnasa Savana kibao


" ukijaribu kunigusa nitahakikisha unaozea gerezani...." Savana akamtisha George ambaye alimuangalia kwa hasira kisha akaanza kuondoka.Savana machozi yakamtoka akajitupa kitandani kwa hasira


" Patrick siwezi kukuacha hasa kwa kipindi hiki..Niko tayari kwa lolote lile lakini si kuacha kukutetea..Hakuna mtu yeyote ambaye atanizuia nisikutetee ..Nitasimama nawe hadi dakika ya mwisho .That bastard George is right.sijaweza kukutoa katika moyo wangu hadi leo hii..I still love you so much Patrick.I'll make you love me Patrick and when this is over you'll be mine" akawaza Savana




ITAENDELEA

Email This

BlogThis!

Share to X

Share to Facebook

Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top