MWISHO WA UBAYA AIBU

Simulizi master
0





SEHEMU YA 1

Umesema unaitwa nani nikacheka na kusema "naitwa Cay kwani vipi..

akatabasamu na kusema mmmh chineke mtoto upo vizuri🤣..

Nikacheka na kusema wewe unaitwa nani akasema naitwa Dan nikasema sawa niende tutaonana kesho..

*****
Kwajina naitwa Cay naishi na mama mdogo mdogo wake na mama angu naishi kwake kwakuwa Mama angu yupo nje ya nchi kimaisha basi mama mdogo ana mtoto wa kike umri kama wangu anaitwa Tayana,

kiukweli ma mdogo hanipendi kwakuwa mimi napendwa sana na majirani.
Basi aliyekuwa ananiuliza naitwa nani ni mkaka tuliekutana dukani ndipo nilipomuaga na kurudi nyumbani nikamkuta mamdogo mama tayana akiwa amesimama ananisubiri akasema we punda ulienda kununua Tunduma Kengemaji wewe leta hapa nilichokutuma akanisonya na kusema mwenzio anataka samaki mpikie nikasema sawa mama..

Usiku ulishaingia nikajiuliza usiku huu napata wapi samaki Cay mimi jamani nikatoka mpaka mgahawani nashukuru mungu nilimkuta samaki mmoja nikamnunua na kuanza kurudi nyumbani nikiwa nakimbia nikaingia ndani mpaka jikoni kisha nikampikia ilipoiva nikamwekea kwenye sahani na kumpelekea nilikuta kakaa na Ma mdogo..
Tayana akasema we pungasese nani kakwambia mimi nataka samaki..

nikamwangalia mama mdogo kisha ma mdogo akajibu "Nawe T si umesema samaki kula bwana.

Nikatoka na kuanza usafi maana kesho kuna mitihani nilikuwa nasoma kidato cha tatu nikafanya usafi nikiwa nimechoka nikaingia kulala kwenye kachumba kangu tunakoweka mikaa na mizigo mbalimbali nikajilaza mpaka asubuhi ile naamka nikakuta unifomu zangu zimelowekwa kwenye maji nikasema nitavaa za nyumbani kweli nikavaa nguo za nyumbani mpaka kwa dispilini masta nikamueleza tatizo alinielewa na kuniruhusu niingie darasani na kufanya mitihani...

Pale shuleni T ana kikundi chake wanajiita BORN TO SHINE wenyewe hawasomi ni starehe tu wapo wanne Tayha, Tahma Tayana na Tekra nilipomaliza mitihani T wetu akaniita na kusema mama kakuona ulivyova?

"Nikasema kuvaa mpaka mama anione🙄..

Akasema ok tutaonana nyumbani basi mda wakutoka shule ukafika tukaruhusiwa nikamuaga besti angu Anna na kuanza kurudi nyumbani sikuwa na nauli hivyo nilikanyaga kuna kaaumbali nilifika nyumbani na kukuta T kashafika ile naingia mama T akasema "waooh ulikuwa wapi..

Nikamuamkia shikamoo akasema kuwa nawe upewe yako ulikuwa wapi nikasema shuleni akashika pua na kusema shuleni unanifanya mtoto mdogo hivi Cay unajua sikupendi!?..

Nikasema najua akanimwagia juisi aliyokuwa anakunywa na kusema kafiri mkubwa plz usinifundishie mwanangu umalay@ tu..

Nikatabasamu haimaniishi kwamba niliifurahia kauli yake ilikuwa ni tabasamu la uchungu basi nikasema nisamehe mama..
Akacheka na kusema niondokee uko nikaingia kubadilisha nguo maana nililowa juisi kisha nikatoka kuangalia chochote nikakuta hakuna hata chakula..

Nikatoka na kusema mama naomba ela ninunue mboga akakaa kimya nikatoka nje karibu na kwetu kuna kibanda cha kaka mmoja nikaenda na kuchukua chips nikasema nitakulipa ijumaa akasema Cay ujue nakudai nikasema nife njaa kisa deni nikiwa nakula akaingia Dan yule tulieonana jana akasema ninabahati na wewe..

Basi me nikala na kuinuka niondoke Dan akaniomba namba nikasema sina simu akasema acha roho mbaya Cay nikasema kweli tena basi mkaka muuza chips akasema Cay nenda akija Mama ako hapa italeta shida nikaaga kwaherini..

Kisha nikaondoka sikujua nyuma waliongea nini nilirudi ndani mama akasema ulikuwa wapi nikasema jogging akasema mwenzio ajisikii vizuri mfulie nguo nikasema Mamdogo mimi sijala siwezi kufua najisikia njaa akanifuata na kusema mbwa wewe unalipa kodi hapa na je ushawahi nunua hata sukari umekua mama ushajua kunijibu....

Nilikaa kimya kisha nikasema mama kabla sijamaliza simu yake iliita ilikuwa video call akasema sasa mama ako anapiga funga bakuli lako hilo kama kopo la chooni nikaichukua simu na kuipokea nikasema Hii Mummy mama akasema vipi unaumwa mbona macho mekundu nilishindwa kujizuia nikalia😭😭 mama alistuka na kusema Cay shida nini mamdogo akachukua simu na kusema kakumiss mwanao fanya uje nawe khaaaa...

Sikujua mama alisema nini ila ma mdogo akasema sawa dada usijali na wakaagana alipokata simu akasema wewe nyoko mfyuuuuu unadhani namuogopa mama ako chefuuuuuu nenda uko kujiliza uko vipi ingia jikoni washa mkaa bandika maharage..

Nikasema T hatumii maharage akasema mwanangu hali mbegu bandika uende ukamnunulie soseji leo hayupo vizuri

Nikasema sawa nikaingia jikoni na kuwasha mkaa nikapima kikombe cha maharage nikabandika, nikiwa kule jikoni mamdogo aliniita cay njoo nikaenda mbio nakukuta kampakata T anatapika akasema kalete tax nimpeleke mkoani (hosp) nikatoka nakimbia mpaka wanapopaki tax nikachukua mpaka nyumbani wakamchukua t mpaka mkoani, nilibaki nyumbani ila kama lisaa walirudi t na mama ake, mama T alikuwa kakasirika sana akaniita na kusema cay niambie ukweli usinifiche nikasema ndio akauliza unamfahamu mpenzi wa T nikasema hapana simfahamu..

Akasema Cay je ulijua kuwa T ni mjamzito!?..

Nikashtuka na kusema hapana akasema sasa nyani huyu mjamzito ole wako ufungue korongo lako kumwambia mtu nitakuua niliogopa sana na kusema hapana sitasema kisha nikamuuliza T unaendeleaje mama yake alinipiga bonge la kofi mgongoni nakusema acha unafki hapo umefurahi kisha akaanza kulia.....
UNAJUA NINI kiliendelea
Full season zote mbili ni 1000 wahi watsap 0742443214 


Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top