MWISHO WA UBAYA NI AIBU

Simulizi master
0






Watsap 0742443214
SEHEMU YA 3

Naumwa nimepewa ruhusa...

Hivi Cay unataka mpaka shetani aje na mapembe ndio ukubali uambiwacho..

Nikakaa kimya basi akasema sawa utakaa nje mpaka nitakavyorudi basi nikaelekea nyumbani nikiwa karibu na kile kibanda cha chips nikaitwa na mpika chips tunamwita Malolo akasema Cay njoo nikaenda na kusema mambo niambie akasema bwana mdogo wangu Dan kasema nikuambie ukitaka chips uwe unakula tu kulipa bili juu yake..

Nikacheka na kusema unachelewa nini sasa embu nipe na mishikaki akasema vipi mbona umewahi nikasema sijisikii vizuri..

Basi nikala chips na kusema akija mwambie aongeze na juisi basi tukacheka na kuendelea kula nilipomaliza nikatoka pale mpaka nyumbani nikaruka ukuta na kukaa kwa ndani maana nilikuwa nimechoka na ule ugomvi, nilikaa kama masaa mawili mamdogo alirudi na kusema umepitia wapi kijizi wewe..

Nikasema mama nisingeweza kukaa nje kwani nimekwambia sijisikii vizuri akasema kwani hapa ni rufaa nenda hospital kama unaumwa nikainuka kumfuata wakati anafungua mlango wa kuingia ndani akasema iwe mwanzo na mwisho kuruka ukuta utakuja wafundisha wezi basi nikavua uniform na kuzifua maana nilikuwa nimeshiba..

Akasema vipi ulimwambia T anywe dawa nikaitikia kwa kichwa kukubali ila kiukweli wala sikumwambia basi tuliishi ivyo mpaka tukafunga shule kwaajili ya pasaka siku moja nikiwa chumbani simu niliyopewa ikaita nikaangalia na kukuta anaepiga kajisevu Amour nikapokea akasema mmmh cay unaroho mbaya hata kunipigia nikasema wewe nani akasema niliekupa simu nikasema kumbe ndio unaitwa Amour akajibu yaah

"unasemaje.. Nilimuuliza

"Nimekukumbuka nikaona nikusalimie nimerudi jioni ya leo nilikuwa south nikasema asante kisha nikasema usiku mwema..

Noooo kesho vipi tunaweza kuonana nikasema ili tuvumbue nini akasema Cay be serious..

Nikamjiibu sina muda basi akasema poa zawadi zako nitakupaje nikasema wape yatima kisha nikakata simu na kuizima unajua mi sipendi usiku mikelele nakumbuka toka T atoe mimba ilipita kama wiki tatu, basi nikiwa chumbani nilalako nikagongewa na kuinuka kufungua mlango mama akasema Cay embu njoo uku yani chumbani yaani kwao maana analala na mwanae..

Nikaingia akasema Cay nisamehe nikasema nini kwani mama akasema yani leo kati yangu na T kuna mmoja anaenda mochwari na mwingine central nikasema kivipi mama akatoa kipimo cha mkojo na kusema kanasa tena huyu mtoto nifanyaje mimi...

"Eeeh tena!?.. Niliuliza kwa mshtuko huku nikimuangalia T.

"bahati mbaya mama..

"kelele kenge wewe miaka 17 tu ivyo je ukifika umri wangu itakuwaje........

T alikuwa akiomba msamaha tu mimi nikakaa kitandani na kusema mama unafanyaje sasa ndio ishatokea..

Akaanza kunilaumu mimi wewe ndio chanzo uwa nasema kuwa makini na T..

Nikasema mama jamani akanikatisha na kusema kelele kwanini unamruhusu kuwa mbali na wewe nikasema hanipendi na pia hataki ukaribu na mimi...

Hapo alitulia na kumuuliza mwanae "wewe kunguru ina muda gani T akajibu sijui moyoni nilijisemea duh makubwa..

Mama T akasema sijui nifanyaje nikasema muache azae we nilitukanwa mwanga mkubwa unajifanya mtakatifu zaa wewe kisha akaendelea kumuuliza mwanae Tayana mimba ni ya nani hii?..

T alikuwa anaogopa baada ya kubanwa sana akasema "Ya kaka ake Tayha anaitwa tariki..

Mama akasema aya chukua simu mpigie atume pesa sasa hivi ukatoe hiyo mimba, kweli T akachukua simu na kupiga akaweka sauti ili mama asikie "halo Tariki mimi Tayana..

"Eeh nambie T unasemaje?..

"Mama kagundua nina mimba..

"Hivi T form three kweli unapata mimba unatakaje sasa..

"naomba ela nitoe akaulizwa shilingi ngapi T akamalizia kwa kusema laki kweli kwenye simu ilitumwa laki na elfu tatu mia sita hili akitoa apate laki mama akampa vidonge viwili sikujua ni vyanini kisha akasema Cay kalale nilirudi kulala huku nikisema mungu nijalie mimi nipite njia njema..

Tuliamka asubuhi mama alikuwa kakasilika kwani hakukuwa na dalili yeyeto ya mimba kutoka akasema jiandae tumsindikize Kunguni hii sehemu kwakuwa tulikuwa likizo tukajiandaa tulienda kwenye kidispensary fulani wakaingia na mama ake mi nikiwa nje walikaa kama dk 40 wakatoka tukaondoka na kurudi nyumbani njiani hakuna aliesema chochote basi tukafika nyumbani mama akasema Cay kuanzia leo uyu mjinga atajua kwa kwenda sitaki kumuona humu ndani kwangu aliongea huku akilia nitaiweka wapi sura yangu mimi nilimuonea huruma kwa jinsi alivyokuwa analia basi alimkamata alimpiga mpaka nikasema mama msamehe ishatokea..

Weee alimuacha T na kunifata nilikimbilia nje akafunga mlango nikabaki nje alipoona hasira zimepungua akaja kufungua mlango na kusema nimeumbuka..

Mwanae akasema mama niache nizae ukinizuia najiua.

"Jiue mbwa mzee wewe kisha akasema huku akinitazama wewe usienenepa funga mdomo huyu nampeleka sehemu..

Basi nikakubali kweli walitoka sikujua wanaenda wapi ilipofika usiku mama alirudi peke ake kisha akasema we Cay njoo nikaenda akasema kuna mtu yupo nje sasa nitakuacheni muongee..

Nikasema mtu gani mama akasema sasa ole wako uzingue sikuelewa chochote basi nikatoka na kumkuta mkaka akiwa ndani ya gari akasema mambo nikasema poa nakusikiliza akasema ingia nikasema niingie wapi akasema we vipi mama yako ajakuambia nikasema kaniambia nije nikusikilize..

"Nishalipa twende zetu..
Mmmh mbona makubwa nikamwambia sijakuelewa ujue..

Akachukua simu na kusema oya mbona umezingua mtu wako anasema haelewi kisha akakata simu na kuniangalia nikasema sijui chochote kwahiyo mimi narudi ndani ile narudi nikakutana na mama mdogo mlangoni akasema unaenda wapi nikasema ndani akanivuta mpaka kwenye gari na kumwambia yule kaka acha uboya mchukue nilianza kufurukuta nikasema mama nimekukosea nini kwahiyo unaniuza ili na mimi nipate mimba siamini wakanisukumia ndani ya gari na kurock milango kisha gari likaondoka nilikuwa nalia uku nikimwambia yule kaka anionee huruma alinipeleka mpaka nyumba moja hivi na kusema nishatoa laki kwahiyo nataka huduma nzuri nililia na kusema nisamehe mi sijawahi fanya hivyo hapo nikamuona kama huruma ishamuingia..

Akaniuliza unaitwa nani nikasema Cay
"Unasoma? nikasema ndio kidato cha tatu akasema yule ni mama ako kabisa nikasema hapana akasema dah pole wewe wazazi wako wapo wapi nikasema yupo mama ila yupo nje ya nchi akasema dah pole nisamehe mimisasa kwanini unafanya biashara hii..

"Sifanyi biashara mimi kwanza sijawahi kufanya mambo ya ufuska..
akacheka na kusema ok sasa wewe lala kesho ukirudi utamwambia umefanya nilikuwa naogopa sana sikuweza kulala nikiogopa atanibaka nilikesha mpaka asubuhi basi akasema njoo nikurudishe kwenu ile natoka nikakutana ana kwa ana na Amour nikashtuka kisha akasema bro vipi ikabidi amuadithie yaliyotokea alisikitika na kusema sasa utafanyaje nikasema nitajua nikifika asanteni.....

JE UNAJUA NINI KITAENDELEA??
FULL SEASON ZOTE MBILI NI 1000 UJANJA NI UWAHI WHATSAPP 0742443214😂😂 



Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top