Page Bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
“ unavyoonge kama upo serious vile, any way baadae Shakti , akasema madam kisha akaondoka zake akaniacha nikiwa namuangalia….
Alipoondoka nikakimbilia chumban kwangu kisha nikaingia youtobe nikaanza kusearch “ how to approach a woman who see you a little boy, mara niangalia namna ya kuwa mtu mzima mbele ya mwanamke, mara niangalie, njia nzuri ya kumfanya mwanamke akupende sana, yaan siku hioo nilishinda yotube natafuta namna nzuri ambayo nitaweza kumuingia madam dhahara na akanielewa, kwa maana nilishachoka kukaa na langu moyoni, nilitaman ajue kuwa nampenda na anichukulie kama mwanaume, na sio kama mtoto kama namna ambavyo ananichukulia…
Ikawa nimeshika simu yangu kisha nikaanza kuandika sms ya kujielezea kwa madam dhahara kwa namna ambavyo nilikuwa nampenda, nikawa naandika kisha nafuta, naandika nafuta…
Mwisho nikaandika kuwa “ samahan madam najua utaniona kama sina adabu, lakin nadhan ambazo hazina adabu ni hisia zangu, sijui ni kwa nini zimenifanya nikupende kiasi hichi, nilianza kufall in love na wewe kuanzia nikiwa na miaka kumi na mbili, nilikuwa mdogo sana kwako najua ila nilikuwa nakupenda sana na siku zote nikawa namuomba mungu anijali nije kuwa mwanajume wako siku moja, na hata kipindi chpote ambacho hatukuwah kuonana , niliamin kuwa kuna siku nitakuona na huenda ukakubali kuwa mke wangu, nilipomaliza kuandika nikaanza kutetemeka sasa, kwa maana nilikuwa naogoppa kuisend, kuna akili ikawa inanilazimisha nijilipur, ila akili nyingine ikawa inaniamb ia kuwa jichanganye aje kukuchukia zaid…
Mwisho nikaona nifute ile sms kisha nikawa nawaza cha kufanya na hapo nilikuwa nimebakiza wik moja nirudi sudan chuon, yaan mpaka nilikuwa nataman hata kurudia mwaka, kwa maana sikutaka kuondoka nchini bila kukubaliana na mada, kwa maana nilikuwa naogopa kuja kumkuta na mwanaume mwingine, nilikuwa naogopa hata mume wake kurudi, kwa maana nilikuwa nataman hata mumewe asirudi na ikiwezekana anikubalin na abaki na mimi tu…
Nilikuwa ni mtu wa mawazo sana, yaan naogopa hata kumshirikisha mtu kuwa nampenda madam wangu, nilikuwa naona kama nitaonekana kama sina adabu vile, nitaonekana kama mtu wa hovyo mno, so sikjujua hata nafanya je ili kuponya hisia zangu….
Siku moja madam alikuja nyumban kwetu kumfundisha mdogo wangu Sandra, na kama kawaida yangu nilikuwa napita pita tu ili walau anione ila hakuwah hata mara moja kunizingatia hata kwa bahat mbaya, nadhan ile fikra yake ya kuwa mimi ni mtoto sana bado alikuwa nayo kichwan mwake, akiwa anamfundiosha mdogfo wangu mara akapigiwa simu, akaipokea ila baada ya kuipokea akaanza kulia , na kusema “ mume wangu, jaman mume wangu…
Nitaman kujua ni kwanini analia huku akisema mume wangu, nikam sogelea na kumuuliza mbona unalia, akasema “ mume wangu amefariki na mwili wa mume wangu umepatikana ukiwa na majeraha, akasimama na kuanza kuondoka,simulizi hii imeandikwa na bahari ya simulizi hakuwa sawa kabisa, ila sijui ni roho yangu mbaya au ni nini, nilijikuta natabasamu mara baada ya kusikia kuwa mumewe amefariki, nilihisi huenda ndio sababu ya mimi kuwa nae, nikaomba nimpeleke nyumban kwake, akanambia kuwa anataka kwenda kwao, akanielekeza pale nikampeleka ila wakat wote huo, alikuwa analia tu, nilikuwa namuonea huruma sana, na kuna muda sikuwa nataman hata asilie , kwa maana niliamin kuwa mimi nipo kwaajili yake siku zote, na niliamin huenda mimi ndio mume wake ambae mungu amempangia………
NAKUJA
MADAM WA TUTION 6
Page bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
Basi nilimpeleka mpaka huko kwao ambapo alikuwa anataka, na tayar walishaweka mazingira ya msiba, nikakaa pale, ila yeye alikuwa anashinda analia, siku hio nililala hapo, kwa maana niliamin kuwa madam alikuwa ananihitaji sana mimi, ingawa hakuwa anashughulika na mimi hata kidogo, ila sikuondoka kwa maana hata nikimuona tu najisikia vzr…
Mwili haukuwa umeletwa, ulikuwa bado upo nchini Kenya, asubuh ukaletwa, ambapo ndio huzun na majonzi yakazidi kutawala kwa dhahara…
Alikuwa analia mpaka anazimia, basi kama tunavyojua maiti haikai muda mreefu na harakati za mazishi zikafika na hatimae akazikwa….
Muda wangu wa kukaa nchini uliisha, nikawa natakiwa kurudi chuo, nilikuwa nataman hata likizo ingeongezwa maana sikuwa najua namna ambavyo naweza kutengeneza mazingira ya madam kunipenda na kuamin kuwa kumpoteza mume wake sio tatizo na wakat mimi nilikuwepo….
Mpaka naondoka bado madam dhahara alikuwa kwenye majonzi makubwa sana, hakuwa anajibu sms wala kupokea simu ya mtu yoyote, nilimtumia sms moja ya mwisho, kwa maana nikiondoka sms za kawaida hazitakuwa zinafanya kazi labda whatsapp tu, kwa maana naenda nchi za watu, na sikuwa najua kwa hali aliyo nayo sijui ataingia huko whatsapp ataingia lini, sms ilikuwa inasema “ najua unamajonzi, na unatakiwa ulie mpaka uchungu wako uishe, kwa maana unastahili kuhuzunika kwa maana nina uhakika uliishi vzr sana na mumeo, ila nakuomba sana kuwa, majonzi yako yasisababishe ukaacha kuishi na kuwaona wanaokupenda na kutaman uendelee kuwa nafuraha, naondoka madam na nitakumiss sana maana nakupenda mno….
Sms ilionesha kuwa ipo delivered, ila haikujibiwa, nilijua hata lile neno ambalo nimendika kuwa nampenda, bado ataona kama ni masihaara na atachukulia kwamba nampenda kama mwalimu wake, kumbe naaminisha nataka awe na mimi, ila sikujali, nilisema nitaendelea kueleza hisia zangu mpaka atakapouona userous wangu, mpaka atakapooona nampenda kiasi gani….
Basi nikamtuma mtu ampelekee zawad ya mwisho, hakuwa na simu nzuri, sikutaka kumkosa hewan , kwa maana niliamin njia pekee iliobaki ya mimi kuwa karibu nae ni kuwasiliana nae, na tofaut na hapo miaka miwili ni mingi, anaweza kumsahau mume wake na kuanzisha mahusiano mapya na wakat mimi nilikuwepo…….
Basi kabla sijaanza safari yangu ya kwenda sudan nilienda kwao, nikakaa sehemu nikawa namuangalia, alikuwa na majonzi makubwa sana, sikutaka hata kumsemesha nkaondoka zangu, na nikaenda mpaka uwana wa ndege wa mwalimu nyerere na kuanza safar yangu ya kwenda sudan, ila wakat wote huo nilikuwa namuomba mungu sana kuwa dhahara asipate mwanaume mwingine na asije akanisahau kamwe, hata kama mimi ni mdogo kuliko yeye, hata kama mimi ni muhindi nay eye ni mbongo, hakuna sababu ambayo inaweza kumsababisha asinipende na wakat mimi nimeshakuwa mwanaume sasa, na nina hisia kama walivyo wanaume wengine wowote wale…..
Safar yangu ilianza, na nilipofika chuoni kitu cha kwanza ni kumtafuta madam istagram, ila hakunijibu, sasa nilikuwa na line yangu ambayo nilikuwa naitumia kule, nikaona nimtafute whatsapp kwa hio namba ambayo ina code za sudan , niliamin hatunijua kiurahisi, na nikamtumia sms inasema “ hallo mrembo, kisha nikatulia nikiamin kuwa sitojibiwa..
Nikashangaa simu inajibiwa na kusem “ hallo handsome, unaendelea je au ndio umeshanimiss mara hii…
Nilipoona ile sms nilitoa macho kama fundi saa, maana sikutegemea kabisa kama naweza kujibiwa vile, kuna muda nikahisi kama sio dhahara, ila muda mwingine nikahisi huenda taarifa za msiba zimemchanganya, ingawa nilikuwa natamani aniite handsome ila sio kwa namna ile….
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
FULL SEASON 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082
