Page Bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
Kuna muda nikawa nahisi kama kuna mtu anamjibia, kwa maana kwanza namba ilikuwa ngeni, alafu kwa namna ninavyojua namna ambavyo anajiheshimu asingeweza hata kidogo kunijibu vile, ila nikasema liwalo na liwe, hata kama sio yeye ambae anajibu ila angalau Napata faraja, basi nikawa nachart nae sana, na alikuwa anaonekana kama anapenda kuchart sana, kwa maana kila dakika yuko online, nilikuwa najisikia vzr sana, na mara kadhaa akawa ananiomba hela, nikawa natafuta namna ya kumtumia hela, nikaona anafuraha sana , kwa namna alivyokuwa anachart nikahisi kabisa sio dhahara, kwa maana namjua kabisa dhahara wangu………
Akawa anaomba sana pesa, mpaka nikawa namshangaa, sasa wakat wote ambao nachart nae sijawah kumuomba picha, kwa maana niliogopa asije akaomba picha yangu, ila siku hio nikaona nimuombe picha, kwa maana zile hisia zangu nyingi kwa dhahara sikuwa nazo nikiwa nacghart nae, nikaamin kabisa kuwa siyo yeye..
Kweli akanitumia picha, alikuwa anaonekana kama mwanafunzi kabisa, na alikuwa anaonekana kama ni mdogo hata kuliko mimi, alikuwa anaonekana kabisa kama mwanafunzi, nikaona ndio maana sikuwa na hisia, ikabidi nimuulize vzr kuwa ile simu ni yake, kwa maana alikuwa amefanana sana na dhahara…..
“ sio yangu bana, mimi nyumban hawaruhusu kabisa niwe na simu, sasa dada yangu kafiwa na mumewe, yaan anatelekeza hovyo simu yake na hana muda nayo kabisa, ndio nikaona nitumie tumie, walau kidogo, ndio mungu akaleta bahat nikakutana na wewe my wangu, nakupenda sana, akatuma sms Yule mtoto….
Nikajikuta nacheka kwa maana inakuwaje anampenda mtu ambae hata hajawah kumuona sura, yaan hata jina langu halisi halijui, ndio nikasema ehee, hawa ndio wale wanawake wanaopenda wanaume kwa sababu anakitu, na anajishaua kunipenda kwa maana nilikuwa namtumia tumia vihela, akajua tayar ameshapata bonge la bwana, na kwaakili ya hivi vitoto nikawa na uhakika ameshawasimulia mpaka marafiki zake kuwa amepata bonge la bwana, tena linajua kuhonga hilo, kumbe mimi nina shida na dada yake na sio yeye…
“ unaitwa nani kwani? Ikabidi nimuulize…
“ dalha , naitwa dalha kakanijibu….
“ samahan kwa nitakachokuambia, ila mimi nilikuwa natakab kumfarijib dada yako kwa maana najua amefiwa na mume, ila nikawa nashangaa ananiambia maswala ya mapenzi, nikahisi labda ni upweke ndio maana nikawa najibu vzr, ila ukweli ni kwamba, mm sijakosea namba na nakuomba umrudishie mwenye simu simu yake, kwa maana ni rafiki yangu, na usijal sitamuambia chpchote kile ulichokifanya, nikatuma sms kumtumia dalha….
“ wewe ulinambia unanipenda sana, na mimi nakupenda pia, kwann lakin, nimekubali uwe rafiki wa dada yangu, ila naomba uwe mwanaume wangu jaman, akasema dalha …
‘ una miaka mingapi? Ikabidi nikaulize …
‘ naingiza miaka kumi na saba mwaka huu, kaka jibu, nikaona ehee haka katoto kanataka kuniletea kesi ya kuembea na mwanafunzi na hakana lolote lile, na hakuna namna yoyote ile zaidi ya kumkwepa tu……
“ nakuomba sana, siku nyingine usirudie kutumia simu ya dada yako hata mara moja, kwa maana usitehgemee kama utakutana na mwanaume mstaarabu kama mimi, naweza nikakutumia maana nakuona kabisa unatamaa kisha nikakuacha, nikasema na kale katoto kaka sonya kisha kakaniblock kakijua kamenikomoa, sijui kalijua kuwa nina kapenda kumbe mm nimekufa nimeoza kwa dada yake, na yeye nilikuwa namuona kama kakahaba flani kasicho jielewa tu….
NAKUJA
MADAM WA TUTION 8
Page bahari ya simulizi
WhatsApp 0755090082
Nilitaka kwanza muda upite, hata walau miezi mitatu, kwa maana nilikuwa na uhakika kuwa dhahara alikuwa na upweke na majonzi makubwa, so angalau hata akishaanza kusahau maumivu ndio nitafute namna nzuri ya kumuingia…….
Kweli muda ukaenda, nikasajili line nyingine ya huko huko sudan, kwa maana nilikuwa nikimaliza masomo yangu, nakaa naangaklia picha za madam dhahara, natafuta nlikuwa na gauni moja ambalo nilishawah kumnunulia ila nikawa naogopan kumpelekea, so napulizia ile pafyumu yake kisha ndio Napata usingizi…
Mimi ni mwanaume tena gentraman kabisa, na nilishwah kuanzisha mahusiano mchwara na muhindi mwenzangu, ila sikuwa nayafikiria kabisa, kwa maana hata nitakapopata hisia, nilikuwa navuta picha tu niko a madam dshahara, na vile nimeshawah kuona upaja wake, ndio kabisa nikawa najimaliza zangu, na baada ya hapo nalala…..
Kiukweli nilishachoka kuishi kwa hisia, nilitaman hata mara moja nimmiliki, kwa maana sikujua nitaishi vle mpaka lini…..
Basi siku moja nikamtafuta, nikasema hi..
Sms wakatv huo huo ikajibiwa…
“ wewe ni dalha au dhahara, nikatuma sms nyingine inasema hivyo…
“ nisamehe kaka yangu, najua sikujui, ila dalha alikuwa anatumia simu yangu kucharty na wajinga wenzake, so kama unamuhitaji dalha, nasikitika kusema kuwa sasa hivi hana simu, ikaingia sms nyingine inasema hivyo…
Yaan nikajikuta mpaka natabasamu, yalikuwa ni maneno ya kawaida, ila yalipenya mpaka kwenye uvungu wa moyo wangu….
“ sikuwa namtafuta dalha, bali nilikuwa nashida na dhahara, hope ndio wee, nikatuma sms nyingine…
‘ ndio ni mimi, ila sidhan kama tunafahamiana, akasema dhahara…
Nikaanza kuwaza nitajitambulisha vipi, kwa maana niliamin kuwa akijua ni mimi anaweza kunichukulia kama mtoto na wakat nilikuwa nataman anione gentral man, tena niwe ndio mwanaume wa ndoto zake…..
Nikakumbuka kuwa alinambia kuwa alishawah kusoma udom, kwenye college ya education na alikuwa ni amirati pale, nikaona niingilie hapo hapo, kwa maana niliamin kwakuwa alikuwa amirat basi watu wengi watakuwa wanamfahau ila yeye hatakuwa anamjua yoyote Yule…..
“naitwa bilal, na mimi nilikuwa nachukua BAED hapo hapo Udom madam amirat, nikatuma sms inasema hivyo..
“ sidhan kama nakukumbuka, akajibu..
“ ni ngumu kiongozi kujua kila anaemuongoza, ila anaowaongoza ni lazima wawe wanamfahamu, so ni kweli huenda haunijui kabisa, ila mimi nakufahamu vzr sana dhahara, nikatuma sms nyingine inasema hivyo…
“ owww sawa nambie, akajibu…
‘ sijui kama ni sawa nitakachokuambia ila nilikuwa nakuona kama una maadili sana, so nilitaman kujifunza vingi kutoka kwako, nikatuma sms nyingine inasema hivyo…
Dhahara akatuma biimoji vya kucheka na baada ya hapo akatuma sms inasema “ najua unataka kunipamba tu, ila sina ninachokijua, ila kama unaifahamu vzr dunia na una elimu ya akhera walau kidogo basi tutakuwa tunajuzana mawili matatu, ambayo huenda yakatukumbusha kuhusu mola wetu, akajibu dhahara hivyo….
Nikajua kabisa huyu ni mtu wa dini, na mimi kwenye dini sina chochote kile ninachokijua hata kimoja, nikaona hapa ili twende sawa, niwe na mimi ni shekhe, na hapa ndipo nilipoamin kuwa mwanaume yoyote Yule anaweza kubadilika kwa mwanamke anaempenda….
Basi akaniuliza swali, akasema “ una mpango gani na akhera yako…
Nikaona eheee kazi imeanza, nikaingia google na kuandika unampango gani na akhera yako, yakawa yanakuja majibu hata siyaelewi, nikaanza kutafuta mashekhe wa mtandaoni hata wanijibie hili swali, kuwa mtu akikuuliza unampango gani na akhera yako unatakiwa kumjibu vipi, ili nisije nikaharibu kila kitu…
Ila sikupata jibu la moja kwa moja, nikasema “ nina mpango nikienda akhera niende na kupata ma hur lain wazuri na wenye maadili kama wewe, nilipo send ile sms nikaanza kuogopa na kuanza kujiambia, leo ndio naachwa kabisa, kwa maana dhahara ataona kama nawaza mapenzi tu, alafu nikawa najifariji kuwa, hata kama ataona kama nawaza mapenzi si ninampenda atajua mwenyewe …..…..
JE NINI KITAENDELEAAA!! "
FULL SEASON 1000 TU
WAHI WHATSAPP 0755090082
