MADAM WA TUTION - Sehemu ya 17

Simulizi master
0


Page Bahari ya simulizi

WhatsApp 0755090082



Siku hio ndio siku ambayo nilikuwa na wasiwasi sana, nilikuwa nahisi kama nimesalitiwa, nilikuwa nahisi kama ndio dhahara wangu ameshaibiwa hivyo, nilishindwa kabisa kulala, kwa maana nilikuwa na wasiwasi sana…

Kwenye majira ya saa kumi na mbili nikasikia sms imeingia, kwa maana sikuzima data, haraka sana nikaenda kuangalia ni nani…
Alikuwa ni dhahara, yaan mapenzi sijui yana nini, kwa maana nilikuwa na kisiran ila nilipoona sms yake nikajikuta natabasamu sasa mwenyewe, bila kutaka ……..

“ samahan sana boyfriend wangu, jana nilipotoka kwenye graduation simu yangu ilikuwa imezima chaji, na nimefika nyumban nikapitiwa na usingizi ,. Ndio nimeshtuka nikasema nikujulie hali, kwa maana nimeogopa kuendelea kukuacha na wasiwasi, sms ilisema hivyo, nikajikuta nimeshusha pumzi, kwa maana nilikuwa na wasiwasi kupita maelezo…..

“ dhahara mama unajua umenilaza macho, siku nzima nilikuwa nimekaa na simu nataka kuangalia ni muda gani utanitafuta, umejua kunitesa sana leo, naomba usije ukarudia kufanya tena kitu ulichokifanya leo, kwa maana watu wengine tuna mioyo midogo mno, hatuwezi heka heka za moyo, hatuwez kuvumilia maumivu na wasiwasi, hatuwez kuushikilia wivu wetu, yaan unaweza usiamin ila leo ndio nimegundua kama nikishiriki mashindano ya wanaume wenye wivu zaidi duniani, basi ni lazima nitashinda tu, nikawa nasema na dhahara kaanza kucheka na kusema, “ sina mwanaume mwingine zaidi yako kwa maana nakupenda sana na nakupenda wewe tu…..

“ haya niambie kwenye ile graduation wa Yule mwanafunzi wako wa kihindi ulienda mwenyewe eee? Nikauliza, na hapo nilikuwa nataka kujua kuwa Yule aliepiga nae picha ni nani, maana bado akili yangu haikuwa imetulia…
“ nilienda na mdogo wangu yupo form six sasa hivi, sasa ndio karudi likizo nikaona niende nae akasafishe macho kidogo, akasema dhahara, na hapoo ndio nikasikia afueni maana nilikuwa nakaribia kupasuka kwa wivu….
“ sawa mamaa naomba usirudie tena kuwa kimya muda mrefu, hata kama simu yako imezima naomba uombe hata ya mtu kwa maana nimeteseka sana mwenzio, nikasema na dhahara akacheka kisha akasema ‘ punguza wivu chibaba wangu nakupenda …..

Basi amani ikarudi, dhahara akawa analalamika sana kuhusu kuchelewa kazin, nikawa namkazania aende akajifunze driving, kweli nikawa namlipia na anajifunza kuendesha gari, sikuwa na pesa za kumnuniuli gari, nikaanza kujiwekeza kwa maana niliamin kuwa dhahara wangu anatakiwa kupata kila anachokitaka…

Basi akajifunza driving, nikamuahidi kuwa nikirudi Tanzania nitamnunulia gari….
Basi mapenzi yakawa moto moto, nikawa nimebakiza mwezi mmoja nirudi Tanzania, dhahara akanambia kuwa anataka kuja kunipokea, nikakataa na kumuambia kuwa kutakuwa nan dg wengi, na anaomba anitambulishe rasmi kwenye familia yao na sio airport kwa maana inakuwa haina maana sana, nikasema na dhahara akaonekana kunielewa kabisa ….

Basi siku zilienda na hatimae nikamaliza mafunzo yangu na siku niliokuwa nataka kurudi nchini ikafika, nilikuwa nawasiliana na dhahara kwenye safar nzima, ila pia nilikuwa na wasiwasi sana siku akija kujua huyo bilal anaempenda na kutaman kumuona kwa hamu kubwa ndio Shakti kijana anaemchukulia kama mdogo wake, itakuwa je…….

Basi wazaz wangu walikuja kunipkokea, na nikiwa kwenye gari dhahara akanitumia sms na kuniambia kuwa anaenda kwa akina Sandra kwani kaka yake anarudi leo, so Sandra amemuomba aende nyumban kwao kwani kutakuwa na party ya kumkaribisha, nikajikuta natabasamu kwa maana nilikuwa nataman sana kumuona, so nikamtaka apendezeb sana, na ikiwezekana akapige picha anitumie, akakubali, ila akanambia na huo wivu wako, tangu lini ukataka nipige picha na mwanafunzi wangu, tena wakiume, bila kujua huyo mwanafunzi mwenyewe ni mimi…

JE NINI KITAENDELEAAA!! "
OFAA LEO NA MWAGA OFAA SEASON ZOTE MBILI MPK MWISHO KABISA KWA 1000 TU

WAHI WHATSAPP 0755090082 UKIFIKA WHSTAPP SEMA NAOMBA OFAAA YA SEASON ZOTE MBILI KWA 1000 NITAKUTUMIA

Tags

Post a Comment

0 Comments
Post a Comment (0)

Made with Love by

Pixy Newspaper 11 Template is Designed Theme for Giving Enhanced look Various Features are availabl…
To Top