wangu",alisema Zabroni akimwambia Veronica, ndani ya moyo wake Vero aliamini tayari Zabroni hana ujanja kwake. Hivyo kupitia nafasi hiyo alimuuliza "Mmh nitakuaminije? Usije ukaniuwa na mimi humu ndani"
"Kukuuwa? Hapana siwezi bwana hebu acha utani",alijibu Zabroni huku akiyastaajabu maneno aliyoyasema Veronica.
"Kwahiyo unataka kusema kwamba dawa imeshaisha mwilini? ", akijifanya mtu mwenye hofu alimuuliza swali hilo Zabroni.
"Kabisa,hata hivyo yule babu alinambia kwamba ili dawa aliyonipa ili ipoteze nguvu ni pale nitakapo fanya mapenzi, na tangu niachane na yale matukio sijawahi kufanya mapenzi ingawa naaamini kwamba dawa imeshapoteza ubora kwani kitambo sana sijaitumia"
"Mmmh",aliguna Veronica wakati huo moyo wake ukiwa umefura furaha isiyo kifani.
"Ndio hivyo"
"Kwahiyo unataka kusema hujalala na mwanamke?.."
"Niamini Veronica kama mimi nilivyokuamini mpaka nikaweza kukwambia hii siri nzito. Sijawahi kumwambia mtu yoyote ila wewe,ingawa nakusihi usimwambie mtu yoyote. Ingawa wanasema hakuna siri ya watu wawili lakini naomba hii iwe siri ya watu wawili tu. ", Zabroni alisisitiza.
"Zabroni mpenzi ", kwa sauti ya upole Veronica akamuita Zabroni.
"Naam! Mpenzi Veronica "
"Unanipenda kweli?.."
"Ndio nakupenda sana"
"Sawa nikuulize swali?.."
"Uliza tu upo huru"
"Hivi ikitokea labda nimevujisha hii siri utanifanya nini?..", akastuka Zabroni baada kuulizwa swali hilo,alikaa kimya kidogo kisha akajibu "Sitikufanya chochote ila nitafurahi kama utaniomba msamaha". Veronica alicheka kidogo halafu akasema "Hapana siwezi kufanya hivyo kwani hata mimi nakupenda sana"
Siku ya tatu ikawa imeishia hivyo,hapo Veronica alibaki kumaliza kazi aliyopewa kwani tayari kile alichokuwa alikitaka amekipata. Ndani ya nafsi yake akajikuta akijisemea "Ama kweli dunia ina mambo. Kwa mwendo huu kamwe wasingemuweza huyu mtu". Upesi akatoa taarifa kwa uongozi "Safi sana Veronica, wewe ni jembe unafaa sana.
Sasa nafikiri ng'ombe mzima umeshamaliza bado mkia tu", alijibu kamanda wake mkuu akifurahishwa na hatua nzuri aliyofikia kamanda Veronica ambaye ametwishwa jukumu nzito la kumpeleleza mtukutu Zabroni ili mwisho wa siku atiwe katika mkono wa sheria baada kusumbua kwa kipindi kirefu sana.
Siku ya pili yake ilipo fika,siku ya nne sasa. Asubuhi mapema Zabroni alimuamsha Veronica ili ampe madini ajilie,lakini Veronica muda huo akajifanya kuamka kwa haraka haraka akidai kwamba kachelewa shule. "Baby unajua mimi nikadhani lao mapumziko.
Afadhali ulivyoniamsha acha niwahi ingawa leo nitatoka mapema ili nije nicheze na wewe mpaka pale hamu yako utakapo kata. Alisikika akisema hivyo Veronica akimwambia Zabroni ambaye yeye muda huo alimuamsha kwa niaba ya kutaka $$## lakini Vero akawa ameingizia mambo mengine tofauti na aliyo yatarajia Zabroni.
"Subiri atakuja kunielewa atakavyo nipa nafasi lazima aombe mchuzi wa supu",alijisemea Zabroni ndani ya nafsi yake akionekana kumkamia Veronica pindi atakapo mpa penzi lake. Na wakati Zabroni anajisemea hayo,Veronica alikuwa bafuni kuoga. Punde si punde alirejea akajiandaa haraka haraka kisha akamuaga mpenzi wake akawa ameondoka zake akiwa katika hali ya kujifanya mwanafunzi.
INAENDELEA
