Posts

Showing posts from April, 2025

Simulizi: Jina La Urithi 04.

Image
 SEHEMU YA NNE(04)                     ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ hatimae baba Laula akazaliwa,,,lakini aliishi na kufanikiwa kuoa  Lakini akaanza kuota magome ya miti katika mwili wake akapelekwa hospitali lakini haikufahamika anaumwa ugonjwa gani,,,ndugu zake wakaamua kumpeleka kwenye tiba mbadala wakampeleka kwa mganga wa kienyeji....mganga akasema,,mkitaka mtu huyu apone,,ni lazima akafukue kaburi la muanzilishi wa ukoo wake,,achukue jino la mbele katika fuvu la muanzilishi wa ukoo wake...ikalazimika afanye hivyo! siku hiyo akadamka usiku wa saa sita akaelekea makaburini! alipolikaribia kaburi hilo mara ghafla!!!!!                       ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ akahisi miguu yake imekuwa mizito kupiga hatua,,lakini akajipa moyo,,akalisogelea kaburi hilo,,punde si punde kaburi likafunguka akafanikiwa kuona mabaki ya mifupa ya muanzilishi wa ukoo wake,,akatumbukia ndani ya kaburi hilo,akachuk...

Simulizi; Jina la Urithi 03

Image
  SEHEMU YA TATU(03)                     ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ mwanzo nilihisi ni utani,,lakini kadri sekunde zilivyozidi kusonga akadondoka chini na kutulia tuli.. ghafla wakajitokeza wazee wawili,,ambao ni baba na mama yake..lakini wazee hao walishakufa miaka mingi iliyopita! wakati Njile anaendelea kusimulia,,ghafla yule mzee akajitokeza ndani ya nyumba ya msamalia huyo! Nje aliweza kumuona mzee huyo,,akasita kuendea kusimulia,,macho yakamtoka na hofu ikazidi kuongezeka,, Ye msamalia akastaajabu,,kumuona Njile amebaki kimya huku macho yake yakitazama uoande mwingine kwa muda mrefu...akaamua kugeuza shingo yake naye aone Njile anatazama kitu gani kilichomfanya akodoe macho. alipogeuza shingo yake,ghafla mlango ukafunguliwa kwa pupa!!! KIZAA ZAA!!!!!                         ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ akashtuka,,,akashika kifua chake upande wa moyo,,huku akipumua kwa haraka,,,kumbe Njile ali...

Simulizi: Jina la urithi 02

Image
  SEHEMU YA PILI (02)                      ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ ni sauti ya mwanaume mzee kati ya watu hao wawili waliojitokeza kimiujiza,,kisha akaisogelea maiti hiyo akachomoa kisu na kukata kipande cha nyama katika mwili wa maiti hiyo. Njile akatamani kutimua mbio,,lakini alishindwa kwa sababu mwili wake haukuwa na nguvu hata za kumuwezesha kutembea,,akastaajabu kumuona mzee huyo,,akimfuata,,na kumnyang'anya mtoto kwa nguvu! punde si punde yule bibi akazioiga hatua kumsogelea mzee huyo aliyekuwa kamshikilia mtoto mchanga,,Njile alipowatazama kwa makini wazee hao akashtuka kuona ni baba na mama wa mumewe,,kilichomshangaza zaidi wazee hao walikufa na wakazikwa miaka mingi iliyopita....wakati anatafakari nini cha kufanya mara ghafla!!!! TAHARUKI!!!!!!                        ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ Mzee huyo akachukua kile kipande cha nyama ya maiti ya baba wa mtoto huyo mchanga,,pam...

Simulizi: Jina la urithi 01

Image
  SEHEMU YA KWANZA(01) Njile alimlea mwanae kwa upendo wa hali ya juu,,japo hakuwa na uwezo mkubwa  kifedha....mumewe alifariki, siku ambayo alizaliwa mwanae wa pekee,,siku hiyo Mume wa Njile,,alidamka mapema na kumuaga mkewe kuwa anakwenda katika shughuli zake za kila siku kama ilivyo kawaida yake,,lakini Njile alishangazwa sana na kitendo hicho cha mumewe kudamka alfajiri, na sio kawaida yake! Njile hakuwa na kipingamizi,, mumewe akachukua kibuyu kilichokuwa na maziwa ya ng'ombe kabla hajatoka ndani ya nyumba akasema,,"nakupenda sana mke wangu,,mtoto utakayemzaa, kama ni wa kiume jina lake ataitwa  Laula,,na kama ni wa kiume ataitwa Minze....aliongea maneno hayo kwa msisitizo,,, Njile,,akaonekana kuyazoea maneno hayo,,haikuwa mara ya kwanza mumewe kumwambia maneno hayo,,tena huwa anaongea kwa msisitizo,,,Njile akaitikia kwa kutikisa kichwa,,kisha akavuta shuka na kuendelea kuuchapa usingizi. Mumewe akatoka nje ya nyumba akafunga mlango na safari ya ikaanza kuelekea kusi...

BINTI WA KAZI Sehemu ya (1-13)

Image
  Ep 01.... Mara nyingi sisi wasichana wa kazi huwa tunaonekana hatuna thamani na vile vile tunaonekana kana kwamba kwetu kuna njaa au masikini wa kutupwa.. Mara nyingi watoto wa kiume wa mabosi wetu huwa wanatuona sisi ni sehemu ya kujifunzia mapenzi,kila mtoto wa kiume atataka alale kwanza na sisi akishapata uzoefu ndo aende kuwatafuta hao wa nje. hata Mimi yamenikuta hayo,wa toto wa bosi wangu walikua wakirudi likizo kutoka chuo basi ilikua na mapigano wenyewe kwa wenyewe,kila kijana alitaka awe wa kwanza kunigusa kuna mda usiku mmoja wao akaja chumbani kwangu,alidhani atanipata kirahisi....akawa ananambia eti atamwambia mama ake aniongezee mshahara....nikamkatalia..akaanza kutumia nguvu..nikatoka nikaenda lala sebuleni. katika ule mtaa(mtaa wa kinondoni b)mimi ndo nilikua msichana wa kazi mdogo(miaka 14) ndo kwanza nilikua nimeanza kutoka maziwa.... Nilipokua chumbani nikasika baba(mume wa boss wangu) anaongea na mkewe(boss wangu sababu yeye ndo akionilipa mshahara)  baba ...

FULL STORI : DUDU KOJOLEA

  MTUNZI : GEOFREY MALWA Naitwa Maria, ni mwanamke mzuri na najikubali, ndio! Najikubali mwenyewe. Hakuna mwanaume niliyewahi kukutana naye akaniacha bila kunisifia hata kama ni kwa Dakika moja. Sifa nyingi kutoka mpaka kwa wanawake wenzangu zilinivimbishwa kichwa lakini hazikunisahaulisha utu wa mtu. Kwenye hilo nilikuwa tofauti na wanawake wengi waliolewa sifa, nilipenda kutengeneza urafiki na kila mtu, awe masikini au tajiri, heshima niliizingatia, labda pengine ndio sababu iliyonifanya nielewane na kila mtu aliyenizunguka. Maria mimi nilipenda sana maisha mazuri, nadhani hiyo ni ndoto ya kila mwanadamu, nilimaliza chuo kikuu na sikupata kazi ya kufanya, sio kwamba niliweka juhudi zangu kwenye kutafuta kazi, Hapana! Nililemazwa na kaka yangu Jastini aliyekuwa akifanya kazi katika shirika la reli, yeye alikuwa na maisha mazuri kwahiyo aliniwezesha kwa kila kitu nilichohitaji. Alinidekeza kupita kiasi mpaka nikawa sielewani na wifi yangu Nadia. Baada ya mwaka nikiwa namtegemea kak...