SITAISAHAU TANGA 18:
Nikawa bado naiangalia ile damu na kuitafakari, bibi akaendelea kuniamuru kuwa ninywe.
BIBI: Uzima wako upo humo, ni bora unywe tu kwa hiyari yako.
Nikajaribu kunywa ile damu ila kinyaa kilizidi kunishika.
Bibi akaniangalia kwa jicho kali sana na kusome.
BIBI: Nimeshakwambia unapokula vitu hvyo weka kinyume chake utaona ni kawaida tu. Narudia tena, uzima wako upo humo.
Ikabidi nifanye kama alivyosema kuwa damu ni maziwa na mavi ya mbuzi ni karanga. Ila nikala kidogo tu na kumrudishia,
MIMI: Asante bibi nimeshiba.
BIBI: Hapana, hutakiwi kubakisha unatakiwa umalize vyote na kikombe ukilambe kuonyesha kuwa umeridhika na ladha yake.
MIMI: Bibi ila vimenishinda kwakweli.
BIBI: Hiyo ni lazima ule, yani utake usitake. Je ungependa nikwambie hiyo damu ni ya nini?
MIMI: Ndio niambie.
BIBI: Mwanamke akiwa kwenye siku zake huwa anatoa uchafu, na uchafu huo huwa kwenye mfumo wa nini?
MIMI: Huwa ni damu.
BIBI: Basi hiyo ni damu ya mwanamke akiwa kwenye siku zake.
MIMI: Aaargh mbona umenipa uchafu jamani?
BIBI: (Akacheka sana), haya kunywa sasa.
MIMI: Hapana, siwezi kunywa uchafu.
Mara yule bibi akanipulizia kitu, nikawa kama nimepumbazika nikajikuta nikiyala yale mavi ya mbuzi na kuinywa ile damu, ila nilipomaliza tu nikawa kawaida, nilitamani kutapika kabisa yani.
Mara akanipa glas nyingine na kuniambia,
BIBI: Chukua na maji ya kunywa ushushie.
MIMI: (Yani ile kuangalia hadi kichefuchefu), jamani bibi mbona ni mate tena yamechanganyika na makohozi.
BIBI: Inakupasa unywe na hapo utajifunza kuona kinyaa cha yale uliyoyafanya.
MIMI: Aaah bibi, siwezi kunywa mate kwakweli.
Akanifanyia kama mwanzo, nikajikuta nikinywa ile galsi yenye mate hadi kuimaliza, halafu nikawa kawaida. Yule bibi akawa ananiangalia na kusema,
BIBI: Kuna juice pia inapaswa unywe, ngoja nikupe.
Akachukua glasi na kunikabidhi.
MIMI: Loh bibi jamani ndio usaha kweli?
BIBI: Ndio, kunywa juisi hiyo.
MIMI: Siwezi bibi yani ninywe usaha kweli dah!
Akafanya kama mwanzo, na ule usaha nao nikanywa. Mara gafla nikaanza kuumwa na tumbo hadi nikawa nalia na kugalagala chini, yule bibi alikuwa akicheka sana, na mimi nilizidi kuugulia.
Wakati nalia vile, wakaja wasichana wazuri na kunizunguka mahali pale, kwakweli sikuona hata uzuri wao kwa maumivu yale ya tumbo, niliugulia sana na hakuna aliyenisaidia.
Baada ya kuugulia kwa muda mrefu, bibi akanipa glasi na kuniambia.
BIBI: Kunywa hii ni juisi ya machozi itapoza maumivu yako ya tumbo.
Kunywa machozi haikuwa shida kwangu kwani nilishakunywa vingi visivyonywewa, nikaichukua ile glasi ya machozi na kunywa, ilikuwa ina ladha kama ya chumvichumvi hivi. Nilipomaliza kunywa tu na yale maumivu yakakatika.
BIBI: Unajua kwanini umeumwa na tumbo?
MIMI: Sijui bibi.
BIBI: Kwasababu ulikuwa unakataa kula chakula chetu.
MIMI: Nahitaji kurudi kwenye maisha ya kawaida, nirudisheni tafadhari.
BIBI: Unadhani ni kazi rahisi?
MIMI: Sijui kwakweli.
BIBI: Je unaweza kuifanya jana kuwa leo?
MIMI: Siwezi.
BIBI: Lazima ifanyike kazi ya ziada ili uwe kawaida na si kinyume tena.
MIMI: Basi bibi nisaidie.
Bibi akaniangalia tu, mara akawaita tena wale mabinti wa tano.
BIBI: Chagua mmoja uwe nae kila utakapokwenda.
MIMI: Hapana bibi, sitaki mwanamke.
BIBI: Sasa wewe unataka nini?
MIMI: Nataka niwe kwenye maisha ya kawaida.
BIBI: Ngoja uone kwanza.
Akanionyesha mahali kwenye watoto wengi wakilia na mahali pengine wanawake wengi wakilia. Halafu akaniuliza.
BIBI: Upande upi unaonyesha huruma zaidi?
MIMI: Pande zote zaonyesha huruma ila zaidi Ni ule upande wa watoto.
BIBI: Umewaonea huruma watoto, ni sawa kabisa. Na kwanini hukupenda kuwahurumia wakiwa tumboni ili nao watoke wakiwa kama wewe?
Nikakaa kimya kwani sikuwa na la kujibu.
Bibi yule akanichukua na kunifungia kwenye chumba, kile chumba kilikuwa na sisimizi na siafu wengi nao wakaning'ata sana hadi vidonda vikanijaa. Baada ya muda akanifungulia na kuniuliza,
BIBI: Umejisikiaje wakati wale wadudu wanakung'ata?
MIMI: Nimeumia sana na maumivu yake hayaelezeki.
Akachukua majivu na kunipaka mwilini, huku akiniambia,
BIBI: Ukitaka tusiendelee kukufatilia fata kile watachokwambia.
MIMI: Nitafanya vyote bibi, sitapuuza hata kimoja.
Akachukua na damu nayo akanipaka mwili mzima, kisha akasema,
BIBI: Umependeza sana mjukuu wangu.
Nikabaki namtazama tu huku macho yangu yamejawa na huruma tupu na yakionyesha kuwa nahitaji msaada na kuhurumiwa.
Kufumba na kufumbua, sikuwa tena kwenye ile nyumba na wala yule bibi hakuwepo ila nilijikuta niko peke yangu chini ya mti, cha kushangaza ule mti ulikuwa na mdomo na macho. Nilitetemeka sana. Kila nilipouangalia nao ulinichekea, nikatetemeka sana mahali pale na kuanza kurudi kinyumenyume, wakati nafanya hivyo uli mti ulikuwa ukizidi kucheka huku nao ukinifata. Kwakweli mkojo ulinitoka, wakati narudi vile kinyumenyume kuna kitu nikakigonga kwa nyuma kwa haraka kabisa nikageuka na kuangalia, Mungu wangu, alikuwa mtu mrefu sana mbele yangu sikuweza hata kumtazama, akachukua mkono wake na kushika shingo yangu huku akinining'iniza juu juu nikawa natetemeka huku ninalia sana.
Alichokifanya sasa ni kunitupa toka kule juu hadi chini, na hapo hapo nikapoteza fahamu.
Kuja kushtuka, Mungu wangu sikutegemea nilichokiona mbele yangu.
ITAENDELEA
